name
stringclasses 429
values | text
stringlengths 0
767k
⌀ |
|---|---|
Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba amesisitiza umuhimu wa kufanyika mambo matano kuelekea uchaguzi
|
Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba amesisitiza umuhimu wa kufanyika mambo matano kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, akiyataja kuwa nyenzo ya kuongeza ushiriki wa wananchi na imani yao kwa uchaguzi huo.
Miongoni mwa mambo hayo ni wananchi kuhakikishiwa dosari zilizotokea mwaka 2019 hazitokei tena, kupewa uhuru wa kuwachagua viongozi wanaowataka na meza ya mazungumzo kati ya Serikali na vyama vya siasa juu ya mambo yanayolalamikiwa.
Warioba anaibuka na mambo hayo, ikiwa umesalia mwezi mmoja na siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo, Novemba 27, mwaka huu.
Jaji Warioba alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mazungumzo
Katika mkutano wake huo, kiongozi huyo aliyewahi kuiongoza tume ya mabadiliko ya katiba mwaka 2014, alisema Serikali inapaswa kufanya jitihada za kukutana na vyama vya siasa kukubaliana namna nzuri ya kuuendea uchaguzi huo.
Umuhimu wa kufanyika hilo, unatokana na kile aliochofafanua, Serikali imefanya maandalizi lakini wakati wote vyama vya siasa havionyeshi kuamini kwamba uchaguzi wa mwaka huu utakuwa tofauti na zilizopita.
“Ni juu ya Serikali kufanya hatua za kuwahakikishia wananchi kwamba yaliyotokea hayatatokea. Serikali iandae mipango kuvikaribisha vyama vya siasa kuwaeleza kwamba hakitafanyika hivi na vile,” alisema.
Alikifananisha kinachoendelea sasa na mapambano, akisema kila upande kati ya Serikali na vyama vya siasa unazungumza lake, ilhali kulipaswa kuwa na mazungumzo ya pamoja.
“Inaonekana ni mapambano tu vyama vya upinzani vinasema tunaweza kuchukua hatua hizi wakati Serikali inasema tutalinda amani Polisi wapo,” alisema.
Pamoja na elimu ya mpigakura inayotolewa, alitaka wananchi wahakikishiwe kuwa wanakwenda kupiga kura ya wazi, huru na kuwachagua wale wanaowataka.
Hakikisho kwa wananchi
Kuelekea uchaguzi huo, Warioba alisema ni muhimu kuwahakikishia wananchi kuwa, dosari zilizoshuhudiwa katika uchaguzi kama huo mwaka 2019, hazijitokezi tena.
Dosari zinazozungumziwa na Warioba katika uchaguzi huo wa mwaka 2019, zinahusisha kuenguliwa kwa wagombea wa vyama vya upinzani, mawakala kuondolewa, jambo lililosababisha wagombea wengi wa chama tawala CCM kupita bila kupingwa.
“Tuepushe kabisa yale yaliyotokea huko nyuma na hili ni jukumu kubwa kwa Serikali kwa sababu ndiyo inayosimamia uchaguzi, hatua zichukuliwe kwa yaliyotokea nyuma ili kuwahakikishia wananchi kwamba mambo yako sawa,” alisema.
Umuhimu wa hakikisho hilo ni kile alichofafanua, aliyesimama uchaguzi wa mwaka 2019 ndiye anayesimamia huu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, hivyo bado watu wana wasiwasi kwamba atarudia yale au atafanya tofauti.
Uhuru kuchagua wanaowataka
Jaji Warioba alisema pamoja na kutolewa kwa elimu inayowapa uhuru wananchi kuwachagua viongozi wanaowataka la msingi ni maandalizi ya kuhakikisha raia wanawachagua viongozi kulingana na matakwa yao.
“Ukifika uchaguzi wananchi wana uhuru huo wa kusema sisi tunayemtaka ni huyu, au wanaletewa watu wa kuwachagua? Hili ni tatizo lingine lililopo,” alisema.
Aliijenga hoja hiyo akitolea mfano juhudi za zamani kuhakikisha wananchi wanawachagua viongozi wanaowataka, akisema kulikuwa na utaratibu wa kujua kuwa anayegombea anakubalika.
Kama ilivyokuwa wakati huo, alisema vyama vya siasa viwe na utaratibu unaozingatia kama wanaoteuliwa wanakubalika katika maeneo husika kinyume na hivyo watapatikana viongozi wasiostahili.
Mazingira hayo, alisema ndiyo yanayosababisha uongozi ngazi ya chini ukose nguvu, kiasi cha kila mwananchi anaona bora awasilishe lalamiko lake kwa ngazi ya taifa.
“Siku hizi kwa sababu ya haya yanayotokea unaona kama nguvu iliyokuwepo kule chini imepungua sana, wananchi hawatazami viongozi wao waliopo kule chini wanatazama juu. Ukiwauliza wananchi wanasema wanaomba Rais awatazame kutatua tatizo fulani,” alisema.
Demokrasia
Kwa mujibu wa Warioba, wengi wanaozungumzia demokrasia wamejikita katika madaraka, badala ya utawala bora ambao ndiyo msingi sahihi.
Alieleza hilo linaonyesha watu wanafikiria zaidi kuhusu madaraka, kwa kuwa demokrasia wanayoielezea inahusu tume ya uchaguzi, uchaguzi wa rais kupingwa mahakamani na ushindi wa kura za rais uwe kwa zaidi ya asilimia 50.
Akiijenga hoja hiyo aligusia suala la uchaguzi huo kusimamiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mi9koa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), akisema kilichobaki ni mazungumzo ya kukubaliana namna ya uchaguzi huu kufanyika kama ulivyopaswa kufanywa iwapo ungesimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Amani
Kuhusu amani, Warioba alisema polisi sio chombo cha kulinda amani, isipokuwa amani inalindwa na wananchi wenyewe.
“Amani haikuletwa na mtutu wa bunduki wala umoja, ni makubaliano ya wananchi kwamba tunapaswa kuwa na amani kwa mtindo huu,” alisema.
Katika mazingira hayo, alisema ni vigumu kulinda amani kwa kutumia bunduki na kuwafanya wananchi waamini.
“Kulinda amani yetu, umoja wetu, tusirudishe ukabila udini na sasa hivi ukanda unaanza kupata nguvu, nasema hivi kama tukivikataa tutaweza kulinda umoja wetu na amani yetu,” alisema.
Hata hivyo, alitumia jukwaa hilo, kueleza angalau kwa kiwango fulani Tanzania imefikia kiwango kizuri cha maridhiano, ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita.
“Katika kipindi hicho, hali ya siasa haikuwa nzuri. Rais Samia Suluhu Hassan alirithi matatizo mengi tu, mikutano ya siasa ilizuiwa, maandamano yalizuiwa,” alisema.
Alieleza kwa sasa nchi inaongozwa katika namna ambayo matatizo mengi yaliyokuwepo yameondolewa, akisisitiza ni kweli maridhiano hayajafikiwa kwa kiasi kikubwa, lakini msingi bado upo.
|
Mwanahabari wa kujitegemea, Erick Kabendera ametangaza uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya pingamizi lil
|
Mwanahabari wa kujitegemea, Erick Kabendera ametangaza uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya pingamizi lililozuia kuendelea kwa kesi yake anayokabiliana na Kampuni ya mtandao wa simu ya Vodacom Tanzania Ltd.
Kabendera aliifungua kesi hiyo, Julai mwaka huu, akiituhumu kampuni hiyo kuhusika na utoaji wa taarifa za mahali alipo hadi kukamatwa kwake Julai, mwaka 2019 nyumbani kwake Mbweni, jijini Dar es Salaam.
Baada ya kufungua kesi hiyo namba (12799/2024), iliwekewa pingamizi lililosababisha Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kuifuta.
Kabendera alitangaza uamuzi wa kukata rufaa juzi, alipozungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, akidokeza anafanya hivyo baada ya kushauriana na mawakili wake.
Alisema anatarajia kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa dhidi za pingamizi lililowekwa kwa kuwa wanaamini kesi hiyo ina mashiko na inastahili kusikilizwa ili wawasilishe ushahidi.
“Kutokana na ushahidi tulioukusanya baada ya miaka mitatu ya uchunguzi, tumeona kuwa ushahidi ni mkubwa kiasi kwamba unatosha kuishitaki Vodacom Tanzania na kampuni zake tanzu nchini Afrika ya Kusini na Uingereza,” alisema.
Sambamba na uamuzi huo, Kabendera alisema wanasheria wake kutoka Uingereza na Afrika ya Kusini wanakamilisha utaratibu wa kufungua kesi dhidi ya Vodacom Group South Africa na Vodafone Group PLC yenye makao yake makuu nchini Uingereza haraka iwezekanavyo.
Kwanini anaituhumu Vodacom
Katika maelekezo yake kwa wanahabari, Kabendera alisema kabla ya kukamatwa simu yake yenye laini ya mtandao wa kampuni hiyo ilizimwa na kila alipofanya juhudi za kuwasiliana na huduma kwa wateja alitakiwa kwenda makao makuu.
Katika juhudi hizo, alieleza ulifika wakati laini hiyo ilifunguliwa, lakini wahudumu kwa mteja walikuwa wakimpigia mara kwa mara kumuuliza alipo na zilisikika sauti za watu wakipanga kuizungumza nyumba yake.
“Muda mfupi baadae, nilipigiwa simu kutoka kwenye namba ya Vodacom Huduma kwa Wateja na sauti ya kiume ilijitambulisha kama mhudumu kutoka Huduma kwa Wateja. Alinitaka nijitambulishe na kumwambia eneo nilipokuwa.
Nikapata wasiwasi na kujizuia kusema jambo lolote. Hata, kunilikuwa na muungurumo mkubwa sana kwenye laini na muungurumo huo uliniumiza masikio. Nilisikia pia kikundi cha watu wakibishana kwenye laini na kusema kuwa nilikuwa nyumbani kwangu na kwamba wasogee na kuzunguka nyumba yangu,” alisema.
Alieleza baada ya kauli hiyo alishtuka na kuchungulia nje, ndipo alipogundua nyumba yake imezingirwa na watu waliovaa nguo za kiraia, wakiwa na silaha na magari kadhaa.
“Niliwapigia simu majirani na vijana kadhaa wanaofanya shughuli za kuendesha pikipiki ili wafike nyumbani. Baadhi ya watu waliofika nyumbani kwangu na kuanza kuchukua video za tukio zima walitishiwa na simu zao kuchukuliwa. Baadhi yao walifanikiwa kusambaza video kwa watu mbalimbali,” alisema.
Alisema kwa kuwa kulikuwepo na kundi kubwa nje ya nyumba na kampuni ya ulinzi iliyokuwa inalinda nyumba hiyo ilishatuma wawakilishi wake, aliamua kutoka nje.
“Watu waliovaa kiraia wakiwa na mitutu walinifunga pingu na kuniweka kwenye gari. Kutokana na taarifa za kutekwa kwangu kusambaa kwa kasi, walianza kupata wasiwasi na kuamua kunihimishia kwenye gari lingine baada ya kutembea kwa takribani kilomita tano kutoka nyumbani kwangu kwa kuhofia kuwa watu wangelitambua gari hilo ambalo lilikuwa limepigwa picha,” alieleza.
Kutokana na maelezo hayo, alisema kwa mtazamo wake kuwa kampuni ya Vodacom ilihusika moja kwa moja katika kufanikisha kutekwa kwake.
“Bila watumiaji wa mitandao ya kijamii, yombo vya habari kusambaza taarifa kwa kasi, ni wazi kwamba ningeweza kupotezwa na pengine kuuwawa,” alisema.
Hata hivyo, alisema kilichofanya achelewe kufungua kesi tangu alipotoka mahabusu ni ugonjwa uliomsumbua na juhudi za kutafuta fedha alizopaswa kulipa ili awe huru.
“Kutokana na hali hiyo kipaumbele hakikuwa kufungua kesi mahakamani bali kupata matibabu ya uhakika,” alisema.
|
Kama mara yako ya mwisho kufika Dar es Salaam ni miaka 10 iliyopita, pengine unahitaji mwenyeji wa k
|
Kama mara yako ya mwisho kufika Dar es Salaam ni miaka 10 iliyopita, pengine unahitaji mwenyeji wa kukupokea na kukuelekeza maeneo mbalimbali ya jiji hili.
Hilo linatokana na ukweli kwamba, karibu kila kitu kimebadilika kuanzia barabara, majengo marefu kwa mafupi na hata kuwapo kwa miji mipya kumeibadili Dar es Salaam kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya maeneo yaliyoonekana ya kawaida zamani sasa ni kivutio kiasi cha watu kuyatumia kupiga picha wakiambatanisha na maelezo kuwa, hii ni Tanzania si nchi za nje.
Ujumbe huo ni tafsiri inayobeba uhalisia wa mfanano wa baadhi ya maeneo ya Jiji hilo na miji mingine ya mataifa ya nje, ambayo aghalabu ilitumika kama mfano kwa uzuri.
Eneo la Barabara ya Bagamoyo kuanzia Sayansi hadi Morocco katika Wilaya ya Kinondoni ni kielelezo cha maeneo yaliyopitia mabadiliko ya mandhari kiasi cha kushangaza.
Mvuto wa eneo hilo, umetokana na nyumba za ghorofa, zilizopangwa zikapangika, nakshi za aina yake na barabara iliyonyooka, hakika Dar es Salaam ya leo sio ya jana.
Kama unastaajabu mwonekano wa mchana, utakachokiona usiku kitakushangaza, ni mvuto unaoambatana na mwangaza wa taa zenye mitindo mbalimbali katika kuta na baraza za maghorofa.
Badala ya Posta iliyozoeleka kama makao makuu ya ofisi mbalimbali, kwa sasa eneo hili ndiko yaliko makao makuu ya kampuni kadhaa za simu, ikiwemo Tigo, Halotel na Vodacom.
Migahawa yenye hadhi ya kipato cha kati na juu, ndizo ofisi nyingine zinazopatikana katika eneo hilo, ni tafsiri halisi ya mabadiliko ya Jiji.
Mabadiliko ya Dar es Salaam hayahusishi majengo peke yake, mawasiliano ya barabara za zege na lami katika mitaa mbalimbali ni jambo lingine litakalokupoteza kama hujakanyaga jiji hili kwa miaka kadhaa.
Kama hiyo haitoshi, madaraja na barabara za juu sio Afrika Kusini na Kenya pekee, hadi Dar es Salaam zinapatikana kwa sasa, lipo lile la Kijazi Interchange lililopo Ubungo, Daraja la juu la Mfugale, Daraja la Juu Kurasini na Uhasibu.
Unapoingia Dar es Salaam kwa njia ya Morogoro, unakaribishwa na makutano ya barabara ya Kijazi (Kijazi Interchange), lile eneo lililokuwa kitovu cha msongamano wa magari, sasa ni kuteleza tu.
Achilia mbali kuleta mandhari murua, ujenzi wa barabara hizo uliofanyika kwa vipindi tofauti, umesaidia kupunguza msongamano wa magari, hivyo kurahisisha maisha ya wananchi.
Ujenzi wa barabara za lami katika mitaa mbalimbali ulioambatanishwa na uwekwaji taa za barabarani ni moja ya vitu vilivyolifanya jiji hili libadilike.
Madaraja ya juu
Daraja la Mfugale ndiyo lililokuwa la kwanza kujengwa na kisha kuzinduliwa Septemba 28, 2018.
Ujenzi wa daraja hilo ulilenga kuondoa foleni kwa watumiaji wa barabara wanaotoka katikati ya jiji kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na wale wanaotoka Ubungo kwenda bandarini na Mbagala.
Siku ambayo daraja hilo linazinduliwa ndipo ujenzi wa daraja la juu la Chang’ombe ulitangazwa lengo ikiwa ni kuendelea kuboresha na kuondoa foleni baada ya awali kubainika kuwa tatizo hilo lilipotatuliwa Tazara shida ilihamia Chang'ombe.
Hata hivyo, changamoto imeendelea kubaki katika eneo la kutoka Buguruni kuvuka eneo hilo kwenda Temeke na Kurasini kwani bado foleni imeendelea kuwa kubwa katika baadhi ya siku na saa.
Mbali na ujenzi huo, pia mkakati wa kumaliza foleni katika jiji ulihamia katika mradi wa makutano ya barabara ya Ubungo maarufu Kijazi interchange na baadaye Kurasini.
Jitihada hizo zilienda mbali zaidi na sasa watu wanaotoka Posta kwenda Masaki hawalazimiki kupita Daraja la Selander na badala yake kuna Daraja jipya la Tanzanite.
Mbali na kupunguza msonganani pia limekuwa ni kivutio kipya cha utalii kutokana na jinsi lilivyojengwa likichuana kwa ubora na uzuri na lile la Julius Nyerere linalounganisha Kurasini na Kigamboni ambalo pia limekatisha baharini.
Haya yote yaliyofanyika yamebadilisha mandhari ya jiji la Dar es Salaam na kulifanya kuwa jipya.
Barabara za mitaa
Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP) nao umechangia kwa kiasi kikubwa kulifanya jiji hilo kuwa na mwonekano wa kuvutia.
Chini ya mradi huo, barabara za lami zimejengwa katika maeneo tofauti ambayo awali isingekuwa rahisi kupitika. Kwa sasa yamewekwa na taa na kuongeza mvuto na urahisi wa usafiri kwa wananchi.
Eneo kama Mtoni Kijichi, Mbagala Kuu ambalo linatajwa kuteuliwa kuwa la mfano, ni sehemu ambayo uwekaji wa barabara za lami umebadilisha asilimia 90 ya mwonekano wake na kwa kiasi kikubwa, hata aina ya maisha.
Miundombinu hiyo imeongeza sifa ya eneo hilo na mtazamo wa watu juu ya wenzao wanaoishi umebadilika na sasa wanaonekana kuwa ni wenye maisha bora tofauti na awali.
Uboreshaji huo ulikwenda sambamba na ujenzi wa daraja linalounganisha Vikunai na Kigamboni ambalo pia linatumika kama njia ya haraka kwa wale wanaotoka Mbagala kwenda maeneo ya karibu ikiwamo Toangoma.
Magomeni Kota
Sina shaka kama uliwahi kuishi Dar es Salaam, unakumbuka taswira ya Magomeni inayounganisha Mwembechai na Usalama, eneo lililokuwa na nyumba za watumishi wa umma wa enzi hizo Magomeni Kota.
Ninaposema watumishi wa umma wa enzi hizo na nyumba hizo ziliakisi enzi haswa, maana ni mithiri ya mabanda yanayotumika kama kambi za siku kadhaa na wakati wowote ungedhani zinaanguka.
Mambo hayako hivyo tena kwa sasa, eneo hilo limetapakaa nyumba zenye ngorofa sita na ndani yake kuna kila huduma kwa ajili ya kukidhi haja ya kaya 644.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Daud Kondoro anakaririwa akisema kuwa mradi huo wa nyumba za ghorofa una uwezo wa kuchukua kaya 644.
Kadhalika anasema kuna eneo la uwekezaji la Machinga Center ambalo lina vizimba 286, vyoo vya kulipia na uwekezaji wa sakafu juu na chini.
Barabara za mwendokasi
Ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka ni jambo lingine lililobadili sura ya jiji la Dar es Salaam. Huduma hiyo imekuwa kivutio sio kwa watu wa ndani pekee, bali hata mataifa mengine ya Afrika yamefika nchini kuona namna huduma hiyo inavyoendeshwa.
Baada ya kukamilika katika eneo hilo na kutoa huduma kwa miaka kadhaa, mradi huo umeanza kutanuka na hivi karibuni, wakazi wa Mbagala na maeneo ya jirani wataanza kunufaika.
Kwa mujibu wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, awamu ya pili ya ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka kutoka Gerezani hadi Mbagala Rangi tatu, utakamilika mwezi ujao.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 20.3, vituo 27, barabara za juu tatu na njia za maji za chini zenye urefu wa kilomita 40.
Mradi huo hauishii hapo, Profesa Mbarawa alisema hayo wakati akikagua ujenzi wa awamu ya tatu ya barabara ya kiwango cha zege ya mabasi yaendayo haraka kutoka Posta ya zamani hadi Gongo la Mboto yenye urefu wa kilomita 23.3 utakaogharimu Sh231 bilioni unaotarajiwa kukamilika Aprili mwakani.
Barabara za njia nane, nne
Moja ya vitu vilivyobadili mandhari ya Dar es Salam ni ujenzi wa barabara za njia nane wenye urefu wa kilomita 19.2 kuanzia Kimara hadi Kibaha.
Kati ya njia hizo, tatu zinatumiwa na magari yanayoelekea mikoani na tatu yanayoingia Jiji la Dar es Salaam na mbili za katikati ni mahsusi kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka.
Miundombinu hiyo iliyogharimu zaidi ya Sh161 bilioni imefanya maisha ya wakazi wa Kibaha wanaofanya shughuli zao jiji la Dar es Salaam kuwa rahisi kwani foleni ambayo ilikuwa mwiba hivi sasa haipo tena.
Hiyo haina tofauti na upanuzi wa barabara kuanzia Morocco hadi Mwenge ambao kujengwa kwake kulitokana na amri ya aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati John Magufuli baada ya kufuta shamrashamra za sherehe ya Uhuru, Desemba 2015 na kuamuru Sh4 billioni zilizokuwa zimetengwa zitumike kugharimia ujenzi huo.
Kwa hiyo kama unajijua kwamba hujafika Dar es Salam kwa miaka 10. Badili fikra zako, Manzese, Kijitonyama, Magomeni, Mbezi, Kigamboni na maeneo mengine mengi uliyokuwa na picha zake kichwani, zifute, fika upate picha na taswira mpya za jiji hili.
Bernard Kiluwa ambaye ni mkazi wa mkoa wa Katavi alisema mara ya mwisho kufika Dar es Salaam ni wakati kituo cha daladala kipo Ubungo nyuma ya Tanesco tofauti na sasa kuwa Mawasiliano.
“Nilipotea, nilipoambiwa hapa ndiyo Ubungo, daraja, kituo hakipo, barabara zilivyojengwa nilishindwa kujizuia kuuliza hapa ni wapi kila wakati,” anasema.
Alisema hata ujenzi wa barabara ya njia nane ya Kimara hadi Kibaha umefanya maeneo mengi kuwa na muonekano wa tofauti kuliko ilivyokuwa imezoeleka.
“Eneo kama Mbezi kwa Msuguri, Stop Over, Kimara Bucha, watu walikuwa wakipanga biashara zao hadi barabarani na ilikuwa ni alama kwetu tukiwaona tunajua hapa ni sehemu Fulani, sasa hivi kondakta asipotaja vituo unapotea,” alisema Bernard.
Bagamoyo road
Lakini siyo kusafiri tu na kurudi ndani ya jiji hili la Dar es Salaam ndiyo kumefanya baadhi ya watu kushangaa kubadilika kwa maeneo hayo, bali hata wale waliopo ndani ya jiji wakati mwingine hushangaa kilichofanyika.
“Hili eneo la Makumbusho hadi Morocco nilikuwa nina muda sijapita hiyo barabara, nilianza kwa kuona picha mtandaoni nikajua ni nje ya nchi nilipojaribu kufuatilia maoni nikagundua ni Tanzania tena Dar es Salaam ndipo niligundua nina siku nyingi sijatembea,” alisema Grace Richard.
Alisema mara nyingi amekuwa mtu wa kutoka nyumbani kwake Mbagala kwenda Posta kazini huku akieleza kuwa kupanuka kwa mji kumefanya huduma nyingi zilizokuwa zikifuatwa sehemu fulani kupatikana karibu kila eneo jambo linalofanya watu wasiende maeneo mengine.
“Kumebadilika, miaka sita nyuma na sasa kulivyo ukimuonyesha mtu hawezi kuamini,” alisema Richard.
Kurasini
“Kuna wakati ulikuwa unaweza kusubiri hadi saa zima ili upite hapa mataa ya Uhasibu, japokuwa ujenzi wa hili daraja la juu haujakamilika ila tumeshaanza kuona tofauti, magari yanayotoka Mbagala kwenda Posta hayakai foleni,” alisema Qauthar Alhamdu mkazi wa Kijichi.
“Ni hatua kubwa kwani hili limepunguza hata muda tunaotumia barabarani kwenda kazini tunaamini ujenzi ukikamilika itakuwa na faida,” alisema.
|
Kama uliwahi kujiuliza ni lini Tanzania itatekeleza miradi yake kwa makandarasi wake wa ndani, huu n
|
Kama uliwahi kujiuliza ni lini Tanzania itatekeleza miradi yake kwa makandarasi wake wa ndani, huu ni wakati sahihi na jawabu la swali hilo kupatikana.
Sababu ya maswali kama hayo ni uhalisia wa mwenendo wa utekelezwaji wa miradi mbalimbali nchini, ambayo aghalabu walipewa makandarasi kutoka nje ya nchi.
Kilichosababisha hali hiyo ni kile kilichowahi kuelezwa kuwa, kulikuwa na ombwe la utaalamu kwa makandarasi wazawa juu ya teknolojia za utekelezaji wa miradi hiyo.
Katika mazingira hayo, makandarasi wazawa walijiona kinachowastahili ni miradi midogomidogo ambayo hata thamani yake ni ndogo pia.
Lakini sasa mambo yamebadilika na hilo kinakwenda kuwa historia, baada ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuweka mpango wa kuhakikisha makandarasi wazawa wakiwemo wanawake wanapewa miradi.
Utekelezwaji wa adhma hiyo, umeanza kwa Serikali kutenga asilimia 10 ya bajeti ya kila mwaka ya maendeleo kwa ajili ya miradi ya mafunzo kwa vitendo.
Sambamba na hilo, angalau asilimia thelathini ya bajeti ya maendeleo imetengwa kwa ajili ya upendeleo kwa wazawa, huku asilimia tano ya bajeti ya miradi ya maendeleo ikitengwa kwa ajili ya makundi maalumu.
Hayo yote yanakwenda sambamba na ushiriki wa wanafunzi na wahitimu katika miradi mbalimbali ya ujenzi.
Mageuzi hayo ni matokeo ya marekebisho ya Sera ya Ujenzi ya Mwaka 2003, yaliyosababisha kutengwa kwa nafasi maalumu kwa wakandarasi wa ndani kushiriki katika miradi ya umma, ikiwemo barabara, maji na miundombinu.
Kwa mujibu wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB), kufikia mwaka 2023, kulikuwa na wahandisi 23,000 waliosajiliwa nchini.
Kati yao, karibu 4,000 walikuwa wanawake, ikiwa ni takriban asilimia 17 ya wahandisi wote.
Makandarasi hao sio tu wanachangia moja kwa moja katika ujenzi wa miundombinu, bali pia wanasaidia kukuza uchumi wa ndani kwa kutoa ajira na kuimarisha sekta ya ujenzi.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, sekta ya ujenzi inachangia takriban asilimia 13 ya Pato la Taifa (GDP) la Tanzania na sehemu kubwa ya ukuaji huo inatokana na ushiriki wa makandarasi wazawa.
Zaidi ya hayo, makandarasi wazawa wanahamasisha matumizi ya malighafi za ndani kama vile saruji, nondo na mbao, jambo ambalo linasaidia kukuza viwanda vya ndani.
Pia, inakadiriwa makandarasi wazawa wanazalisha takriban ajira 700,000 kila mwaka, idadi ambayo inatoa mchango mkubwa katika kupunguza tatizo la ajira nchini.
Juhudi zinaendelea kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye sekta hii kupitia programu maalumu za mafunzo, ruzuku na usaidizi wa kifedha unaotolewa na Serikali pamoja na mashirika binafsi.
Kupitia uwezeshaji huo, Tanzania inaweza kujenga uchumi imara zaidi na miundombinu inayokidhi viwango vya kimataifa huku ikiwanufaisha raia wake moja kwa moja.
Wahandishi wanawake
Rais wa Chama cha Makandarasi Wanawake Tanzania, Judith Odunga anautazama mpango huo kama fursa kwa wakandarasi wazawa.
Anasema fursa hiyo itawaondoa kwenye mazoea ya kufanya kazi ndogondogo na zenye maslahi madogo, wakati zile kubwa zinafanywa na wakandarasi wa nje.
“Ni miaka mingi imepita tukiwa tunafanya miradi midogo ambayo thamani yake pia ni ndogo, lakini sasa hivi tumeambiwa tutaweza kufanya miradi mikubwa, fedha nyingi zilikuwa zinachukuliwa na wageni kwenda kwenye nchi zao,” anasema.
Anasema ni jambo jema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia imeona umuhimu wa kuwakomboa wakandarasi wa ndani kwa kuwawezesha kutekeleza miradi mikubwa.
Kwa mujibu wa Judith, hatua hiyo ni furaha kwa mkandarasi, huku akiisihi Serikali kuharakisha mpango huo ili kuwanufaisha wanataaluma hiyo.
“Sisi tutakapoiona fursa naomba wakandarasi wenzangu tuichangamkie kwa kuomba kazi ili tuweze kuingia katika ulingo wa kupambania miradi hii,” anasema Judith.
Judith anasema ni imani yake wakandarasi wa ndani hasa wanawake wanafanya vizuri katika miradi hiyo na kwamba utaratibu huo utawahamasisha watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi.
Wakandarasi wazawa wanasemaje
Mkandarasi mzawa ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Lazafa Co. Ltd, Magira Magira anasema kilichofanyika kitawakwamua makandarasi kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kukua zaidi kitaaluma kama walivyo wa nje.
“Namshukuru Rais Dkt. Samia kwa namna alivyojipambanua kwamba sio mtu wa maneno mengi bali mtu wa vitendo pia namshukuru kwa namna ambavyo ameamua kuwainua makandarasi wa ndani,” anasema.
Anasema hatua hiyo, itawezesha miradi yote inayotekelezwa nchini ifanywe na wakandarasi wa ndani na hivyo kuifaidisha nchi kiuchumi.
“Nikuhakikishie kwamba tunakwenda kusimamia ujenzi wa daraja hili kuhakikisha kila kazi inakamilika kwa viwango vinavyokubalika, kulingana na mkataba,” anasema.
Anachosema Bashungwa
Akiwa katika mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, makandarasi wazawa na washauri elekezi wa ndani jijini Dodoma, Novemba 21, 2023, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa anasema Serikali inaendelea kutenga miradi mingi kwa ajili ya makandarasi wazawa.
"Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita ni kusaidia kujenga uwezo wa makandarasi wazawa, ili wakue na kupata uzoefu," anasema.
Katika mwaka wa fedha 2023/2024, anasema jumla ya miradi minne ya barabara yenye urefu wa Kilomita 50, imetengwa kwa ajili ya makandarasi wa ndani.
Si hivyo tu, anasema katika mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya Kilomita 20 za barabara zimetengwa kwa ajili ya makandarasi wanawake.
Anasema kazi hizo zitakazogawanywa katika vipande vya kilomita tano na kushindanishwa kwa kampuni za wanawake pekee.
"Hii inafanya jumla ya Kilomita 220 zijengwe na makandarasi wazawa kwa mwaka 2023/2024," anasema.
Pia, Bashungwa anasema kazi za matengenezo ya barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara zenye thamani ya Shilingi Bilioni 600 zitatekelezwa na makandarasi wa ndani katika mikoa yote 26 nchini.
“Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Rais Dkt Samia ameamua kazi zote za matengenezo ya barabara Kwa mikoa yote 26 nchini, zitekelezwe na makadarasi wa ndani,” anaeleza.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, Sheria ya Ununuzi wa Umma imefanyiwa marekebisho kwa kuongeza kiwango cha thamani ya mradi utakaotekelezwa na makandarasi wa ndani, bila kushindanishwa na makandarasi wa nje.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta anasema daraja hilo linajengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia 100.
Anasema litakapokamilika litarahisisha usafiri kwa majira yote ya mwaka, kwa saa 24 za siku.
|
Moja ya alama kuu za juhudi za Serikali katika kuimarisha miundombinu na kukuza uchumi, ni ujenzi wa
|
Moja ya alama kuu za juhudi za Serikali katika kuimarisha miundombinu na kukuza uchumi, ni ujenzi wa Daraja la JP Magufuli, ambalo awali liliitwa Kigongo Busisi.
Mabadiliko ya jina la daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3.2 yana uhusiano wa moja kwa moja na historia ya Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli.
Mitazamo ya wengi ilikuwa kufariki kwa Hayati Dkt. Magufuli, kungezima ndoto ya kukamilika kwa mradi huo, unaogharimiwa kwa Shilingi bilioni 716.3 zote zikitolewa na Serikali.
Aliyeipa uhai ndoto hiyo ni Rais wa Serikali ya awamu ya sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye muda mchache baada ya kuapa kuwa Rais, alijipambanua kuiendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake, huku akianzisha mipya pia.
Daraja la JP Magufuli ni miongoni mwa miradi hiyo, ambayo mkuu huyo wa nchi sio tu anaiendelea mradi huo kuakisi ndoto ya Hayati Magufuli, bali pia analenga kuwaondolea changamoto wakazi wa Busisi na Kigongo mkoani Mwanza za kuvuka kutoka eneo moja kwenda lingine.
Ujenzi wa daraja hili ulianza rasmi mwaka 2019 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2024.
Historia ya daraja na Hayati Magufuli
Katika ziara yake Desemba 31, mwaka 2020 kutembelea mradi huo, Dkt. Magufuli, aliwaambia wakazi wa eneo hilo kuwa anayo historia na daraja hilo, tangu wakati ambao hakuwa na wadhifa wa Urais.
“Siku moja niliondoka Mwanza kwenda Busisi kuposa, nimefika pale kwa Mzee mmoja ni Askari Magereza anaitwa Mathias Mbiza, nikamaliza kuposa na mahali tukapatana, wakati wa kurudi Kivuko kilikuwa MV Geita au Sengerema.”
Anaongeza, “Kikawa kimeharibika na kilikuwa kinafanya hivyo kila siku, nilikuwa na pikipiki yangu XL 125 Honda, kwahiyo kulikuwa na mitumbwi walikuwa wanavusha kwa pesa, kila mara kivuko kilipoharibika watu walipakiwa kwenye mitumbwi”.
Anasema alisogea karibu na eneo hilo na wavushaji walimtaka kuingia kwenye Mtumbwi na pikipiki yake, alipofikiria moyo ulikataa, wakati huo kulikuwepo na familia na baskeli yao walipakiwa.
“Mimi nikazunguka Kamanga, nilipofika Mwanza ule Mtumbwi ukawa umezama na ukaua watu 11, kwahiyo ninaifahamu na ndiyo maana nilipofanikiwa kuwa Waziri wa ujenzi mawazo yangu yalikuwa niokoe maisha ya watu wa hapa,” anasema.
Lafikia asilimia 90.5
Rais Dkt. Samia aliingia madarakani pamoja na mambo mengine, mradi huo ulikuwa sehemu ya ile aliyoiangazia kuhakikisha inakamilika.
Juhudi zilizofanywa na Serikali, zimewezesha kazi ziendelee kufanyika usiku na mchana na hatimaye, daraja hilo kufikia sasa ujenzi wa daraja hilo, umefikia asilimia 90.5.
Hilo, linathibitishwa na Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa daraja hilo, Abdulkarim Majuto Septemba 17, mwaka 2024.
Kwa mujibu wa Majuto, kazi zinaendelea kufanyika usiku na mchana na kwamba matarajio hadi kufikia mwanzoni mwa Oktoba 2024, daraja hilo liwe limeunganishwa.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Innocent Bashungwa anasema daraja hilo linaunganisha barabara kuu ya Usagara - Sengerema - Geita katika Ziwa Victoria na sasa lipo mbioni kukamilika, kwani kimebaki kipande cha mita mbili kuunganishwa.
Anasema ujenzi wa daraja hilo unaenda sambamba na ujenzi wa barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 1.66 upande wa Kigongo na Busisi.
“Nimetembea kilometa tatu za Daraja la J.P Magufuli kujionea kazi, nimejiridhisha tumebakiza mita mbili ndicho kipande kilichobaki kukamilisha ujenzi wa kilometa tatu za daraja hili pamoja na barabara za maungio kiliometa 1.66 ambazo pia ujenzi unaendelea,” anasema Bashungwa.
Bashungwa aliyetembelea mradi huo Septemba 17, 2024 anamshukuru Rais Dkt. Samia kwa kusimamia maono yake na kuendeleza miradi yote iliyoasisiwa na mtangulizi wake.
Anasema Rais Dkt. Samia ameendelea kutoa fedha, ili ujenzi wa daraja ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma.
Anaeleza Serikali inaendelea kuhakikisha mkandarasi analipwa malipo yake, hivi karibuni amepokea Shilingi bilioni 18 zitakazomwezesha kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ifikapo Desemba 2024.
Aidha, Bashungwa anampongeza Meneja wa Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoa wa Mwanza, mhandisi mshauri kampuni ya Yooshin Engineering Corporation (Korea) na mkandarasi wa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Bashungwa anaeleza ujenzi wa daraja hilo umetoa fursa kwa wataalamu wa ndani na wahitimu wa kada ya ujenzi kupata ujuzi na uzoefu, utakaosaidia kupunguza utegemezi wa wataalamu kutoka nje ya nchi.
La sita kwa urefu Afrika
Daraja la JP Magufuli limetajwa kuwa refu zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati, huku likishika nafasi ya sita kwa bara la Afrika.
Hilo lilithibitishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara, Joseph Haule Julai mwaka juzi, alipokagua ujenzi wa mradi huo mkoani Mwanza.
Katika orodha ya madaraja marefu, linaloongoza ni 6th October lililopo nchini Misri lenye urefu wa kilomita 20.5.
“Kama mnavyoona Tanzania sasa tunazidi kupaa, tumeona madaraja mengine mengi makubwa na mazuri yakichukua rekodi lakini sasa daraja hili ndilo litakalovunja rekodi nchini, Afrika Mashariki na Kati,” anasema.
Mengine marefu ni Third Mainland la Nigeria (kilomita 11.8), Suez Canal la Misri (kilomita 3.9), Kisiwa cha Msumbiji (kilomita 3.8), na Dona Ana la Msumbiji (kilomita 3.67), kisha JP Magufuli linafuata.
Manufaa kiuchumi
Utekelezwaji wa mradi huo, siyo tu utaunganisha pande mbili za wakazi wa maeneo ya jirani, bali pia linafungua fursa nyingi za kiuchumi na kijamii.
Mradi huo pia, utapunguza gharama za usafirishaji kwa kuwa kwa sasa, kivuko cha Kigongo-Busisi kinabeba abiria na bidhaa kuvuka Ziwa Victoria, jambo linalosababisha msongamano mrefu na ucheleweshaji.
Kwa mujibu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, takriban magari 1,600 huvuka kwa kivuko hicho kila siku, huku abiria zaidi ya 2,000 wakikabiliwa na changamoto ya kungoja kwa muda mrefu.
Kwa kukamilika kwa daraja hilo, gharama za usafirishaji zinatarajiwa kupungua kwa asilimia 25 hadi 30, huku muda wa kusafiri kati ya mikoa hiyo ukipungua kutoka zaidi ya saa mbili hadi dakika chache.
Daraja hilo pia litaunganisha maeneo ya uzalishaji wa mazao kama dhahabu, pamba na samaki kutoka mkoa wa Geita na masoko ya Mwanza, ambayo ni kitovu cha biashara cha Kanda ya Ziwa.
Takwimu za Benki ya Dunia mwaka 2023, zinaonesha mradi huu unatarajiwa kuongeza thamani ya biashara kati ya mikoa hii kwa zaidi ya asilimia 40 katika kipindi cha miaka mitano baada ya kukamilika.
Ujenzi wa daraja hilo, umeajiri zaidi ya wafanyakazi 700 wa ndani, wengi wao wakiwa vijana wa kitanzania. Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2022 ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), ajira hizo zimechangia kuboresha hali ya maisha ya wakazi wa maeneo ya Kigongo na Busisi.
Pia, ripoti inakadiria kwamba ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zitokanazo na mradi huo zinaweza kufikia zaidi ya 5,000 baada ya kukamilika, kutokana na kuanzishwa kwa shughuli za kibiashara kama migahawa, huduma za usafiri na biashara ndogondogo.
Utalii ni faida nyingine ya daraja hilo kwa kuwa Ziwa Victoria ni kivutio kikubwa cha watalii, mradi huo unatarajiwa pia kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea mkoa wa Mwanza na maeneo mengine ya Kanda ya Ziwa.
Kwa mujibu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), takwimu za mwaka 2022 zinaonyesha idadi ya watalii katika Kanda ya Ziwa iliongezeka kwa asilimia 10, huku matarajio ya ongezeko zaidi yakiwa ni asilimia 20 baada ya daraja kukamilika, kutokana na urahisi wa usafiri wa barabara.
|
Licha ya uwepo wa vivuko vya watembea kwa miguu kutazamwa kama muarobaini wa ajali barabarani, kwa b
|
Licha ya uwepo wa vivuko vya watembea kwa miguu kutazamwa kama muarobaini wa ajali barabarani, kwa baadhi ya wananchi vimekuwa kama vikwazo.
Hatua ya kuviona vikwazo inatokana na kile kinachoelezwa na baadhi yao kuwa, urefu wake, uvivu wa kupanda unawalazimu wakatize barabara badala ya kutumia vivuko hivyo.
Hata hivyo, uwepo wa vivuko hivyo kwa mujibu wa wananchi hao hao, umepunguza kwa kiwango kikubwa matukio ya ajali za barabarani zinazowahisisha watembea kwa miguu.
Mathalan, kwa kipindi cha mwaka huu eneo la Buguruni lilipo kimoja ya vivuko hivyo, zimetokea ajali tano pekee ukilinganisha na 12 za mwaka uliopita.
Hata hivyo, idadi hiyo ni pungufu ya ajali kwa asilimia 70, ukilinganisha na zile zilizokuwa zinatokea kabla ya kujengwa kwa kivuko hicho.
Mitazamo ya wananchi
Uwepo wa vivuko hivyo, umewapa wazazi uhakika wa usalama wa watoto wao ambao kila siku hulazimika kuvuka barabara wanapotoka na kwenda shuleni.
Rehema Mapande, anayeishi Mbagala jijini Dar es Salaam analithibitisha hilo, akisema awali walilazimika ama kuwasubiri watoto wawavushe, au wapate usaidizi kutoka kwa watu wazima.
“Kwa watoto wetu wanaosoma Chamazi kutokea Mbagala Rangitatu, kila siku walikuwa wanapata shida. Wakifika eneo hili lazima wamwombe mtu mzima awavushe,” anasema.
Anaeleza kwa kiasi kikubwa uwepo wa daraja hilo, umewasaidia watoto hao kuepuka ajali ingawa wapo wanaolitazama kama kero.
Kwa mujibu wa Rehema, kero hiyo inatokana na urefu wa daraja husika unaosababisha mvukaji kutumia muda mrefu, kuliko yule anayeamua kukatisha barabara.
“Daraja ni refu mtu anaona anazunguka anapopanda, kwa hiyo anaona afadhali akatishe barabara ambayo ni hatari kwake,” anasema.
Kwa mtazamo wa Rehema anayefanya biashara ya chakula lilipo daraja hilo, idadi ya ajali za watembea kwa miguu zimepungua kwa kuwa awali zilishuhudiwa mara kwa mara.
“Sisi wenzangu na mie waoga wa barabara tunapita juu kwenye daraja, wachache ndiyo wanalazimisha kupita chini,” anasema.
Pamoja na urefu wa daraja unaolalamikiwa na baadhi ya wananchi, Nas Everist dereva wa bodaboda anayeegesha karibu na kivuko hicho Mbagala anasema bora njia ndefu itakayokuepusha na ajali kuliko kukatisha na ukagongwa.
“Bora upite njia ndefu ya kupanda kivuko, kuliko ukatishe alafu ukapatwa na ajali. Sasa kipi bora upite hapo juu uende sokoni na kurudi au upite chini ugongwe na gari au bodaboda,” anaeleza.
Hata hivyo, anaibua changamoto nyingine ya baadhi ya watembea kwa miguu kupenya katika kingo za daraja hilo ili wakatishe barabara, kwa uvivu wa kupanda daraja.
Wingi wa ajali za watembea kwa miguu kabla ya uwepo wa daraja hilo, unathibitishwa pia na Everist, akisema kwa sasa zimepungua.
“Watu waliokuwa wanavuka kwenda sokoni hasa ndiyo waliokuwa wanagongwa, lakini kwa sasa wanapita juu hawakutani na shida hizo,” anaeleza.
Daniel Mgala Machinga katika daraja la watembea kwa miguu Buguruni jijini Dar es Salaam, anasema idadi ya ajali alizokuwa akizishuhudia kwa siku katika eneo hilo ni tofauti na sasa baada ya kuwepo kwa daraja.
Ingawa ajali zimepungua, Daniel anasema bado zinaendelea kutokea kutokana na uzembe wa baadhi ya watembea kwa miguu wanaoamua kuvuka barabara bila kupitia darajani.
“Lakini sasa wamepunguza sana ajali kupitia hili daraja, nashukuru Serikali kwa kuamua kujenga daraja hili,” anasema.
Anasema wanaopuuzia kutumia daraja hilo, wameamua kwa makusudi kuvunja utaratibu ilhali Serikali ilishauweka ili kuwaepusha na ajali.
“Uelewa ndiyo tatizo kwa hawa wanaopita chini kuvuka barabara, ningependa waendelee kuelimishwa na kuonywa ili waache tabia hiyo,” anasisitiza.
Pamoja na uwepo wa daraja hilo kuwa matumaini kwa wananchi wengi, Lilian Patrick anasema ni changamoto kwa wajawazito ambao kwa hali zao inakuwa vigumu kupanda daraja.
“Kwa wanawake hasa wajawazito inakuwa vigumu kupandisha daraja kwa hiyo, hawa mara nyingi ndiyo wanakatisha barabara,” anasema.
Anapendekeza watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo wajawazito kuwekewa utaratibu maalumu ili kuwarahisishia kuvuka.
Hata hivyo, anasema daraja limesaidia kupunguza matukio ya ajali katika eneo hilo, ambayo kila siku alikuwa akiyashuhudia.
Dereva bodaboda anayeegesha katika daraja hilo la Buguruni, Hamisi Ally anaibua changamoto mpya baada ya uwepo wa daraja hilo, akisema linatumika kama hifadhi ya wahalifu.
“Hili ni daraja la waenda kwa miguu lakini unakuta hadi usiku mtu amekaa hajui kwamba hafanyi shughuli yoyote anaishia kuwaibia watu na kufanya vitendo vingine vya kihalifu,” anasema.
Hata hivyo, anasema uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Maruzuku lilipo daraja hilo unaendelea kuwadhibiti wahalifu hao kwa kuwafanya bodaboda wawe walinzi.
“Sisi bodaboda wa hapa ndiyo tumepewa jukumu la ulinzi wa usalama wa eneo hili, kwa hiyo angalau matukio haya yamepungua kwa kiasi kikubwa,” anasema.
Anasema ajali hazikwisha isipokuwa zimepungua kwa kuwa wapo baadhi ya watembea kwa miguu wanaokatisha barabara badala ya kupanda darajani.
Kauli ya Serikali
Godfrey Malinda ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Maruzuku anayesimamia masuala ya ulinzi na usalama, anasema kabla ya daraja hilo, ajali zaidi ziliwahusisha wanafunzi wanaovuka kutoka na kwenda shuleni.
Hali hiyo, anasema imepungua maradufu kwa sasa kwa kuwa kuna daraja linalotumika na wananchi kuvuka, ingawa baadhi yao wanapuuzia.
Kuhusu wanaopuuzia, anasema wanatumia mianya iliyotokana na kuvunjwa kwa kingo za barabara kukatisha na kuacha kutumia daraja.
Anaeleza hao ndiyo wanaendelea kusababisha ajali za watembea kwa miguu ziendelee katika eneo hilo.
Akizungumza matukio ya uhalifu, anakiri yalikuwepo lakini ilipogundulika walianzisha utaratibu wa kuweka walinzi shirikishi.
“Kwa siku za sikukuu, walinzi hawa wanakaa kuanzia asubuhi hadi usiku na tumeweka marufuku ya mtu kufika katika eneo lile na kuzurura tu.
“Mara nyingi tukiwakuta tunawapeleka Polisi wanahojiwa waeleze kama wana sababu za msingi za kukaa katika eneo hilo usiku,” anasema.
Malinda anapendekeza kuboreshwa zaidi kwa daraja hilo, kutoka kuwa la kuhamisha sasa lijengwe la zege litakalokuwa inara zaidi na kutumika na wananchi wengi.
Takwimu
Mjumbe huyo, anasema mwaka huu pekee katika eneo hilo zimetokea jumla ya ajali tano zinazohusisha bodaboda na watembea kwa miguu.
Idadi hiyo imepungua ukilinganisha na ajali 12, zilizotokea katika eneo hilo mwaka 2023.
“Kuna wengine wamekufa kabisa, wengine wamepata ulemavu wa kudumu. Lakini ajali nyingi zinatokea kwa wale wazembe wanaotaka kuvuka barabara bila kutumia daraja,” anasema.
Hata hivyo, anasema idadi hiyo ya ajali ni upungufu wa asilimia 70 ya zile zilizokuwa zinatokea kabla ya uwepo wa daraja hilo.
Kauli ya Polisi
Ofisa kutoka Dawati la Elimu ya Usalama Barabara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Usalama Barabarani jijini Dar es Salaam, Edwin Mtenga anasema kujengwa kwa vivuko hivyo ni matokeo ya mapendekezo ya askari hao.
“Vivuko hivi vilijengwa katika maeneo tete ili kusaidka kuwavusha watu, lakini kusaidia kupunguza msongamano kwenye maeneo hayo,” anasema.
Anasema vivuko hivyo vimejengwa hasa kwenye maeneo yenye makutano ya barabara kubwa ili kupunguza uwezekano wa ajali.
Kwa Dar es Salaam anasema vivuko hivyo vipo Buguruni, Manzese, Kimara, Mbagala, Mbezi na maeneo mengine.
“Vimetusaidia kupunguza ajali katika maeneo hayo. Lakini tuliyabainisha hayo maeneo kama ni tete. Kulikuwa na matukio mengi a watu kugongwa na gari au pikipiki, baada ya kujengwa kwa vivuko vimesaidia kupunguza matukio hayo,” anasema.
Kuhusu wanaolazimisha kupita chini, anasema jeshi hilo linaendelea kutoa elimu kwa wananchi hao kuhakikisha wanavitumia vivuko hivyo badala ya kupuuzia.
|
Ni saa 144 zinazounda siku sita, ndio jumla ya muda ambao Rais Samia Suluhu Hassan ameutumia mkoani
|
Ni saa 144 zinazounda siku sita, ndio jumla ya muda ambao Rais Samia Suluhu Hassan ameutumia mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi.
Kwa mtazamo wa wanazuoni, ziara hiyo kwa maneno machache inatafsiriwa kuwa ya maelekezo, utatuzi kero, fursa na matumaini kwa wakulima.
Mtazamo huo wa wanazuoni, unaakisi uhalisia wa mlolongo wa matukio na kauli za Rais Samia akiwa katika ziara hiyo iliyoanza Septemba 23 na kuihitimisha Septemba 28, mwaka huu.
Ukiachana na zawadi nyingi ambazo aghalabu mkuu huyo wa nchi huzawadiwa anapotembelea maeneo mbalimbali, katika ziara hii alipokea zawadi ya Sh1,800 kutoka kwa wanafunzi wa shule ya awali na msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Chief Zulu, jambo alilosema limeugusa moyo wake.
Awajibu wanaomwita muuaji
Ni ziara hiyo mkoani Ruvuma, ndiyo iliyoibua kauli ya Rais Samia dhidi ya shutuma zinazotolewa na wanasiasa hasa wa upinzani, wakimhusisha na matukio ya kutekwa, kutoweka na kuuawa kwa watu.
Rais Samia alitumia hotuba yake katika hafla ya kufunga Kikao cha Mafunzo cha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa CCM, kuweka wazi kuwa, hakuwahi kuua mtu, labda umasikini na giza.
Katika hotuba yake hiyo ya takriban nusu saa, aliipa UWT jukumu la kuwajibu wanaotoa kauli hizo dhidi yake, akiwasisitiza wasihofu kujibu.
“Ombi langu kwenu (UWT) ni kusimama imara ukweli mnaujua, mdomo wa Mwenyekiti mmoja kujibu hoja zile hautoshelezi na Pengine Mwenyekiti wakati mambo yale yanatoka nipo kwenye majukumu mengine, msimame tu mjibu mnahofia nini,” alisema.
Alikwenda mbali zaidi na kuwaeleza, wakiambiwa Mwenyekiti wao ni muuaji wanapaswa kujibu ameuwa njia zote za kuzidisha umasikini katika nchi na amekuza uchumi.
Kadhalika, katika hoja hiyo hiyo ya kuitwa muuaji, amewataka wajibu kwa kusema ni kweli ameua giza lililokuwa limegubika Tanzania na sasa nchi ipo katika kiwango cha kimataifa cha kung’aa.
“Hayo ndiyo niliyouwa Rais wenu na Mwenyekiti wenu, sijawahi kuua mtu labda sisimizi nimeuwa, lakini sio mtu. Kwa hiyo ndugu zangu simameni tu mjibu,” amesema.
Akizungumzia hilo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Dk Conrad Masabo alisema ingawa ni sahihi kutoa majibu kwa wanaojenga hoja hizo, pia alisisitiza umuhumu wa changamoto za utekaji kushughulikiwa.
Alieleza kauli dhidi ya Rais zisiaminiwe kuwa yeye ndiye anayehusika moja kwa moja na vitendo hivyo, isipokuwa mamlaka aliyonayo yanafanya baadhi ya watu watupe lawama kwake, akifananisha na msemo 'ukubwa kalala.'
Katika mazingira hayo, alisema kuwataka UWT wajibu ni sahihi kisiasa, lakini naye anapaswa kuzungumza asiwaache waendelee kumchafua.
"Ninaona hatari ya watu kimesema vibaya zaidi Rais, maana wakati UWT wanajibu naamini na upande mwingine utajibu, sasa atakayeathirika zaidi ni mwenye dhamana ya uongozi," alifafanua.
Matumaini kwa wakulima
Ziara hiyo ilihitimishwa na kauli ya matumaini kwa wakulima hasa wa Kahawa kwa kile alichoeleza Rais Samia kuwa, kuanzia mwakani Serikali inafanya mageuzi ya mfumo wa mauzo ya kahawa.
Mageuzi hayo kwa mujibu wa Rais Samia, yanahusisha kuondoa utaratibu wa malipo ya wakulima, kupitia Vyama Vikuu vya Ushirika, kisha vyama vya msingi ndipo yawafikie.
Alisema mwakani, mkulima atkayeuza kahawa yake na mazao mengine, fedha zake atazipokea kutoka kwenye chama chake kikuu cha ushirika na haitapita kwingine kokote.
Msingi wa maelekezo yake hayo ni kile alichobinisha, kuna harufu ya kukatwakatwa kwa fedha hizo za wakulima, pia mfumo huo unatengeneza urasimu na kuwachelewesha wakulima kupata haki zao.
Baadhi ya wakulima wanasema hatua hiyo itawafaidisha zaidi na shughuli zao, wakisisitiza utekelezwaji wa hilo ungepaswa kuanza sasa.
“Kwa kuwa wameambiwa mwakani wanatumia muda uliobaki kutukata malipo yetu ili wafaidishe matumbo yao.
“Yote haya wanayafanya kwa sababu hawajui uchungu wa kulima. Wengi sio wakulima wa jembe la mkono, wanakaa ofisini tu kuelekeza,” alisema Mtutula Mtutula mkulima mkoani Ruvuma.
Wakulima wawaepuke walanguzi
Vitendo vya baadhi ya wakulima kuendelea kuwauzia mahindi walanguzi wanaonunua kwa bei ya chini, ilhali Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inanunua kwa bei nzuri, ni jambo lingine lililomwibua mkuu huyo wa nchi katika ziara yake hiyo.
Akiwasalimia wananchi wa Mbinga Sokoni, Septemba 25, mwaka huu, Rais Samia aliwataka wakulika wabadilike na kuacha kuwauzia mazao walanguzi.
Aliijenga hoja yake hiyo kwa ufafanuzi kuwa, walanguzi hununua kilo moja ya mahindi chini ya Sh400, huku NFRA imewekwa kununua kuanzia Sh400 na kuendelea, ni vema wakulima wawaepuke walanguzi.
Alisema kuwauzia walanguzi kunawafanya wakulima wasinufaike na shughuli zao, huku akiitaka NFRA kuendelea kusalia eneo hilo, hadi mahindi yote ya wakulima yatkaponunuliwa.
“Serikali inataka vizuri na imejitahidi kila inapoona kuna changamoto za wakulima inazitatua, lakini wakulima wenyewe nanyi mnapaswa kubadilika,” alisema.
Maagizo kwa Bashe, Aweso, Pindi
Baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa mradi wa maji Mtyangimbole katika Halmashauri ya Madaba mkoani Songea, Rais Samia alimtaka Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ahakikishe mradi huo unatoa huduma hiyo baada ya miezi mitatu.
Hatua ya kuelekea hivyo, inatokana na uhalisia wa changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo, inayowakabili wakazi wa eneo hilo, waliosema aghalabu hutegemea maji ya visima na mabwawa ambayo si salama.
“Tunachota maji kwenye visima vya watu binafsi, lakini huwa vinakauka kwa hiyo tutakwenda kuchota mabondeni. Hayo ya mabondeni ni machafu na wanatumia wanyama wengine pia,” amesema Zainab Kanyale mkazi wa Madaba.
Rais Samia alisema kwa kuwa wananchi wameona jiwe la msingi zimewekwa, wamepata matumaini, hivyo kufikia Desemba Aweso ahakikishe mradi huo unatoa maji.
“Hakikisheni kufikia Desemba mwaka huu maji yanatoka hapa wananchi wale krismas huku wanaoga, kwa sababu tumeweka Jiwe la Msingi tumewapa matumaini,” amesema.
Agizo lingine ni kwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliyemtaka ahakikishe kufikia mwakani malipo ya wakulima katika zao la kahawa yanafanywa kupitia Chama Kikuu cha Ushirika kisha mkulima moja kwa moja.
Sambamba na hilo, agizo lingine lilimlenga Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana aliyetakiwa kuongeza ndegenyuki, vituo na askari wa kudhibiti wanyama waharibifu kwenye mazao ya wakulima wilayani Tunduru.
Akerwa wanaonyamazia uzushi
Katika ziara yake hiyo, alipotembelea Wilaya ya Tunduru, kuliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii zinazomwonyesha mgonjwa akibebwa katika tenga kupelekwa hospitali kutoka Kituo cha Afya cha Mchoteka.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua ya wagonjwa kubebwa kwenye matenga, inatokana na kushindwa kumudu gharama za kukodi gari la kubebea wagonjwa ambazo ni Sh80,000 hadi Sh100,000.
Taarifa hizo zilianza kujibiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa aliyasema ni uzushi.
Ameijenga hoja yake hiyo kwa kufafanua, Tunduru ni moja ya wanufaika wa magari ya kubebea wagonjwa manne kati ya zaidi ya 500 yaliyonunuliwa hivi karibuni.
Si hivyo tu, alisema Wilaya hiyo pia, ni mnufaika wa programu ya M-mama inayowaaniri madereva wa magari binafsi kubeba wagonjwa pale inapotokea gari la kubebea wagonjwa halipo.
Alisema takriban madereva 20 wamesajiliwa na kulipwa fedha kuifanya kazi hiyo, hivyo hakuna uhaba wa gari za kubebea wagonjwa kama ilivyozushwa.
Alipozungumza Rais Samia alionyesha kukerwa na hatua ya viongozi katika eneo hilo, kunyamazia uzushi huo na kusubiri viongozi wa kitaifa wakanushe.
“Kama kunarushwa picha ya uongo katika mitandao, katika maeneo yetu kuna wakuu mbalimbali wapo, lakini hakuna anayekanusha, kwamba hiyo picha sio ya leo.
“Kwamba hii hospitali au hilo eneo sasa hivi ipo katika hali hii na ikapigwa picha ikiwa katika hali hii kuondoa ule upotofu uliofanywa, sijui tunaelekea wapi,” alisema.
Alisema sio sawa kusubiri Rais au Waziri aende katika eneo husika akanushe uzushi, ilhali kuna viongozi ambao uzushi huo unawahusu moja kwa moja.
“Hii ni sawa mwanaume kaingia nyoka nyumbani kwako, unakwenda kumwita mwanaume mwenzio njoo nitolee nyoka nyumbani kwangu,” alisisitiza.
Alieleza kama wanazushiwa kwenye maeneo yao, ilhali maendeleo yanafanyika na fedha zinapelekwa, hiyo sio sawa.
“Kama kwenye nyuma yako unazushiwa, maendeleo yanakuja, fedha zinatoka, alafu anatokea mpuuzi mmoja anaweka picha za ajabu ajabu, lakini viongozi mmenyamaza kimya, mpaka Waziri aje awakanushie, mnatutia wasiwasi ndugu zangu,” alisema.
Hakikisho la kulipwa fidia
Hata hivyo, Rais Samia katika ziara yake hiyo, aliwahakikishia wananchi wanaopisha miradi ya maendeleo, kulipwa fidia zao.
Ingawa inaweza kuchelewa, amesema Serikali itahakikisha inampa kila mwananchi haki yake anayoistahiki.
Aliitoa kauli hiyo, akijibu ombi la Mbunge wa Madaba, Dk Joseph Mhagama aliyeomba wananchi watakaopitiwa na ujenzi wa barabara ya Makambako walipwe fidia.
“Hakuna mradi utakaopita kwa wananchi, Serikali ichukue ardhi bila kulipa fidia za watu. Inaweza ikachekewa lakini sio kwamba Serikali itaacha kabisa kulipa fidia,” alisema Rais Samia.
Ni ziara ya fursa Songea
Siku sita za ziara hiyo, zilitosha kujaza vyumba vya nyumba za kulala wageni hasa wilayani Songea, baada ya watu mbalimbali kufurika mkoani humo na hivyo kuibua fursa kwa wananchi.
Sakina Issihaka ni mmoja wa wahudumu katika nyumba ya kulala wageni Songea, alisema wateja walizuia vyumba tangu Septemba 20 na wengi wanahisi kuviachia Septemba 29, mwaka huu.
“Hapa vyumba vimejaa, hata nyumba nyingine ya jirani hapo nako vyumba vimejaa, huwezi kupata chumba kwa ugeni huu walivizuia mapema,” amesema Sakina.
Hali ilivyo kwa Sakina ndivyo ilivyo kwa Modesta Zullu aliyasema tayari vyumba vilizuiwa na karibu kila siku wanakwenda wateja kuulizia nafasi lakini zimejaa.
“Tofauti na ugeni huu, huwa vyumba vinakuwepo. Mimi napata wastani wa wateja watano Kati ya vyumba 10 vilivyopo, lakini kwa sasa vyote vimejaa,” amesema.
Hata hivyo, pamoja na ziara hiyo ya Rais Samia, katika Mji wa Songea kulifanywa Tamasha la tatu la Taifa la Utamaduni, ambalo pia lilichochea ongezeko la watu.
Kufungwa kwa tamasha hilo, ndiyo iliyokuwa shughuli ya kwanza ya Rais Samia katika ziara yake hiyo.
Mtazamo wa jumla
Akizungumzia ziara hiyo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk Revocatus Kabobe alisema mbali na uzinduzi na ukaguzi wa miradi, kilichofanyika ni muhimu kwa wananchi na Serikali kwa ujumla.
Umuhimu kwa wananchi unatokana na kile alichoeleza, watanufaika na huduma kutoka katika miradi husika, lakini kwa Serikali imejionea na kujipima nguvu inazotumia katika kuleta maendeleo.
Lakini kwa mtazamo mwingine, Dk Kabobe alisema ziara hiyo imekuwa muhimu hata kwa CCM kujiimarisha kwa kuwavutia wananchi.
“Ziara hii ni muhimu sana kwa CCM pia, sababu imekuwa ni sehemu ya kuendelea kuonesha yale yaliyoyafanywa kwa wananchi na kuhamaisha kuungwa mkono kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa,” alieleza.
|
Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya viongozi wanaoacha taarifa za uzus
|
Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya viongozi wanaoacha taarifa za uzushi zisambae bila kuzikanusha.
Kinachomkera zaidi ni kile alichofafanua, pamoja na uzushi huo aghalabu hutokea na kuyahusu maeneo yenye wawakilishi wa Serikali, lakini wanasubiri viongozi wa kitaifa waje kukanusha.
Kauli hiyo ya Rais Samia inakuja kufuatia taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, zikionyesha picha ya mtu anayedaiwa kuwa mgonjwa aliyebebwa kwenye tenga kupelekwa hospitali.
Taarifa hiyo inadai, mgonjwa huyo mkazi wa Mchoteka wilayani Tunduru amebebwa katika tenga hilo, baada ya kushindwa kulipa gharama za kukodi gari la kubebea wagonjwa.
Kutokana na taarifa hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa alieleza kinachosambazwa ni uzushi.
Ameeleza kwa sasa hakuna changamoto ya gari za kubebea wagonjwa kwa kuwa Serikali ilinunua magari ya kubebea wagonjwa 530 yaliyosambazwa kwenye halmashauri mbalimbali.
Katika mgawo huo, amesema halmashauri ya Tunduru imepokea magari manne kwa ajili ya kusambazwa kwenye vituo mbalimbali vya afya.
Mchengerwa alisema magari hayo yaliyoenda
katika vituo vya afya vya Nakapanya, Matemanga, Tunduru Kusini na Nalasi.
Si hivyo tu, amesema Tamisemi ina programu ya M-MAMA inayolipa fedha kwa madereva wa kijamii kuwabeba wagonjwa pale inapotokea gari la wagonjwa halipo.
Ameeleza kwa Tunduru, Sh19 milioni imetolewa kwa ajili ya kuwapa madereva 20 kwa ajili ya kutekeleza kazi hiyo.
“Picha hizi zinazosambaa zinalenga kuwachanganya Watanzania, kazi unayoifanya (Rais Samia) ni kubwa. Picha hizo za zamani,” amesema.
Ufafanuzi wa Mchengerwa, ndiyo uliomuibua Rais Samia akionyesha kukerwa na hatua ya kusubiriwa viongozi wa kitaifa wakanushe uzushi unaoyahusu maeneo yenye viongozi wa ngazi husika.
Kauli ya Rais Samia
Rais Samia aliyasema hayo jana, alipozungumza na wananchi wa Tunduru, ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Ruvuma.
“Kama kunarushwa picha ya uongo katika mitandao, katika maeneo yetu kuna wakuu mbalimbali wapo, lakini hakuna anayekanusha, kwamba hiyo picha sio ya leo.
“Kwamba hii hospitali au hilo eneo sasa hivi ipo katika hali hii na ikapigwa picha ikiwa katika hali hii kuondoa ule upotofu uliofanywa, sijui tunaelekea wapi,” alisema.
Alisema sio sawa kusubiri Rais au Waziri aende katika eneo husika akanushe uzushi, ilhali kuna viongozi ambao uzushi huo unawahusu moja kwa moja.
“Hii ni sawa mwanaume kaingia nyoka nyumbani kwako, unakwenda kumwita mwanaume mwenzio njoo nitolee nyoka nyumbani kwangu,” alisisitiza.
Alieleza kama wanazushiwa kwenye maeneo yao, ilhali maendeleo yanafanyika na fedha zinapelekwa, hiyo sio sawa.
“Kama kwenye nyuma yako unazushiwa, maendeleo yanakuja, fedha zinatoka, alafu anatokea mpuuzi mmoja anaweka picha za ajabu ajabu, lakini viongozi mmenyamaza kimya, mpaka Waziri aje awakanushie, mnatutia wasiwasi ndugu zangu,” alisema.
Alieleza kitendo hicho kinaonyesha tafsiri kuwa, katika eneo husika hakuna viongozi.
Mbali na hilo, Rais Samia alitumia mkutano huo kueleza uwepo wa soko la madini na ushindani unawahakikisha wachimbaji na wauzaji bei na mapato zaidi.
Kauli hiyo ni baada ya kuzindua soko la madini katika Wilaya ya Tunduru.
Alieleza kati ya Julai na Agosti mwaka huu, Serikali ilipokea Sh6.3 bilioni kama maduhuri ya Serikali kutokana na madini katika Mkoani Ruvuma.
“Ni mapato hayo ambayo yanatuwezesha kuja kufanya shughuli za maendeleo kama walivyosema wabunge wenu,” alisema.
Kadhalika, alieleza katika eneo hilo kuna masoko mawili ya zamani, akimtaka Waziri wa Madini, Anthon Mavunde kukaa na wachimbaji wadogo na sekta binafsi wazungumze kuona wanashirikianaje kufanikisha ujenzi.
Hata hivyo, aliahidi kufufua kiwanda cha Korosho katika eneo hilo, kwa kuwaagiza Waziri wa Viwanda na Biashara (Seleman Jaffo) kwa kushirikiana na Msajili wa Hazina (Nehemiah Mchechu) kukifufua kiwanda hicho kwa kumtafuta mwekezaji mwingine mwenye uwezo stahiki.
Kuhusu ndovu, alisema Serikali imeanza kuchukua hatua kwa kuongeza askari hadi ngazi za vijiji wanaoshirikiana na wengine.
Alisema magari ya doria yapo katika Wilaya husika na sasa kuna ndege nyuki zinazokimbiza tembo.
“Tunajua kuna tatizo la tembo lakini tumeanza kuchukua jitihada hizo, lengo letu ni kuongeza ndege nyuki na askari,” alisema.
Mapato madini kwa siku 84
Awali, akizungumza katika uzinduzi wa soko la madini Tunduru, Waziri Mavunde alisema katika siku 84 za mwanzo wa mwaka huu wa fedha, mauzo ya madini yameingiza Sh225 bilioni katika Mfuko Mkuu wa Serikali.
Kiwango hicho cha fedha kilichoingizwa, alisema ni matokeo ya uwepo wa masoko 43 ya madini na vituo 102 vya ununuzi wa rasilimali hiyo.
Kwa mujibu wa Mavunde, kiasi hicho cha fedha kilichoingizwa kinaonyesha matumaini katika kulifikia lengo la mwaka huu wa fedha, ambalo ni kuingiza Sh1 trilioni katika mfuko mkuu wa Serikali.
“Miradi ni ile ile, tumeongeza ufanisi, ufuatiliaji wa utoroshaji madini na kusimamia sheria,” alisema.
Hata hivyo, Mavunde alisema katika mwaka wa fedha uliopita, kiasi cha Sh1.7 trilioni kilizunguka kama sehemu ya biashara katika masoko yote 43 ya madini.
Hatua hiyo kwa mujibu wa waziri huyo, ilisaidia kuongeza wastani wa mapato yaliyoingia katika mfuko huo kufikia Sh753 bilioni kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Alisema kiasi hicho ni kikubwa zaidi ya kile kilichoingizwa katika mwaka wa fedha 2015/16 ambacho ni Sh151 bilioni.
“Kabla ya mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017, Tanzania haikunufaika na sekta hii na baada ya sheria, masoko na vituo vya ununuzi wa madini vilianzishwa,” amesema.
Akizungumzia mradi wa soko la madini Tunduru, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Chizya Marando amesema ujenzi wake umetekelezwa kwa ushirikiano na wafanyabiashara.
Ujenzi huo ulioanza Desemba mwaka jana, amesema umegharimu Sh1.4 bilioni na kati ya hizo, Sh1.37 bilioni zimetokewa na wafanyabiashara na Sh300 milioni ni halmashauri.
‘Mradi wa Uranium uharakishwe’
Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa aliiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa madini ya uranium ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo.
Hoja hiyo aliibua mbele ya Rais Samia aliyesimama katika eneo hilo kuzungumza na wananchi, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Ruvuma.
Kawawa aliijenga hoja hiyo kwa kueleza uwepo wa hofu kwa wananchi wa Namtumbo, juu ya ucheleweshwaji wa mradi huo.
Hata hivyo, kinachoelezwa na Mbunge huyo kinashinikiza kuharakishwa kwa tathmini ya kimkakati ya mazingira (SEA) inayoendelea ili kuchunguza uwezekano wa uchimbaji na masharti kabla ya shughuli hizo katika eneo hilo.
Mapema mwezi huu, Naibu Waziri wa Madini, Dk Stephen Kiruswa alisema mchakato wa kuchagua kampuni itakayofanya SEA uko ukingoni na tayari zabuni imetangazwa.
Inakadiriwa Tanzania ina tani 55,000 za akiba ya madini ya uranium iliyothibitishwa hadi mwaka 2022, ingawa uchimbaji wa kibiashara bado haujaanza rasmi.
Eneo la Mto Mkuju wilayani Namtumbo linaaminika kuwa na akiba kubwa zaidi ya uranium nchini, ikiwa na tani milioni 182.1 za mabaki ya madini hayo na kiwango cha uranium kinachofikia asilimia 0.025.
Mbunge Kawawa alisisitiza umuhimu wa kuharakishwa mradi huo, “Mradi huu wa muda mrefu umewaacha wananchi wakiwa na maswali kuhusu lini utaanza.
“Tunaomba mara tu matokeo ya awali ya utafiti yanapopatikana, ruhusa ya uchimbaji itolewe haraka,” amesema Kawawa.
Alibainisha kuwa wilaya hiyo haina viwanda vya kutosha, huku akitaja faida za kiuchumi zilizopatikana wakati wa utafiti, ikiwemo ajira kwa vijana na kuongezeka kwa mzunguko wa fedha.
Katika hatua nyingine, alitumia jukwaa hilo kueleza uwepo wa changamoto ya uvamizi wa tembo, akisema zaidi ya kaya 400 zimeathirika.
Akijibu malalamiko hayo, Rais Samia aliwahakikishia wakazi kuwa Serikali inashughulikia kila ombi la Mbunge na wananchi kwa ujumla kwa njia zinazostahili.
|
Rais Samia Suluhu Hassan amesema sambamba na Serikali kuanza ujenzi wa bandari ya Mbambabay, pia ina
|
Rais Samia Suluhu Hassan amesema sambamba na Serikali kuanza ujenzi wa bandari ya Mbambabay, pia inatarajia kuzungumza na Serikali ya Malawi juu ya ushirikiano katika huduma za bandari hiyo.
Hatua hiyo kwa mujibu wa Rais Samia, inalenga kufungua milango ya ushirikiano wa kibiashara kupitia bandari hiyo kwa mataifa hayo, kwa kuwa bandari ya Mbambabay itahudumia mizigo inayotoka Malawi.
Mkuu huyo wa nchi anaeleza hayo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa bandari hiyo unaotarajiwa kufanyika kwa kipindi cha miezi 24, ukigharimu Sh70 bilioni.
Kujengwa kwa bandari hiyo, pamoja na mambo mengine, kunalenga kuimarisha ushoroba wa maendeleo ya Mtwara na kurahisisha uhudumiaji wa mzigo kutoka nchini Malawi kwa kuwa ndiyo njia fupi kutoka bandari ya Mtwara.
Rais Samia ameyasema hayo leo, Septemba 25, 2024 katika mkutano wake na wananchi uliofanyika Viwanja vya Maegesho ya Bandari ya Mbambabay, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku sita mkoani Ruvuma.
Amesema uwepo wa bandari hiyo pekee hautatosha kuleta mafanikio yanayotarajiwa, isipokuwa kunahitajika kuwepo huduma nzuri za usafirishaji wa mizigo.
Katika hilo, ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia kamati za pamoja, kuzungumza na Serikali ya Malawi.
Mazungumzo hayo, amesema yajikite katika kuisihi Serikali ya Taifa hilo, ijengwe miundombinu ya kupokea na kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Mbambabay.
“Hii ndiyo diplomasia ya uchumi, nchi moja inaanza lakini mnazungumza na nchi ya pili ili muungane muelewane na wao waweke miundombinu inayofaa kupokea mizigo itakayotokea Tanzania na hivi ndivyo biashara inavyofanyika,” amesema.
Ushirikiano wa namna hiyo, amesema haufanyiki kwenye bandari hiyo pekee, tayari unafanyika katika miradi mbalimbali ukiwemo wa Reli ya Kisasa itakayounganisha Tanzania na Burundi.
Amesema hata barabara kubwa zinazoiunganisha Tanzania Kenya, Msumbiji na Uganda ni sehemu ya miradi inayotekeleza diplomasia ya uchumi na itifaki za biashara huru katika eneo la Afrika.
Hata hivyo, amesema tangu mwaka 2019 akiwa bungeni, amekuwa akimsikia Mbunge wa Nyasa, Stella Manyanya aliomba kujengwa Kwa bandari hiyo.
Amesema hatimaye miaka 10 baadaye, ujenzi wa bandari hiyo umeanza kwa kuwekwa Jiwe la Msingi na kwamba adhma inatimia.
Amesisitiza bandari hiyo itarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa kutoka na kwenda Malawi na inatarajiwa kuongeza fursa hasa kwa wananchi.
Ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kukamilisha mradi huo kwa wakati, viwango na ubora kama uliokubaliwa katika mikataba.
Aidha, akiwa wilayani Nyasa, Rais Samia amezindua barabara ya Mbinga-Mbambabay yenye urefu wa kilomita 66.
Kuhusu barabara hiyo, amesema ujenzi wake umetokana na ufadhili wa Sh630 bilioni kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Mbali na mradi huo, amesema kwa mara ya kwanza benki hiyo itasaidia mkopo wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) eneo la Kigoma inayounganisha na nchi ya Burundi.
Amewataka madereva wanaotumia barabara hiyo wahakikishe haileti masikitiko kwa ajali, badala yake inawapa furaha.
Uvuvi wa vizimba
Katika mkutano huo, Rais Samia amewataka wavuvi wilayani humo kuhakikisha wanakuwa na vizimba, huku akiisisitiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenda kutoa elimu ya uvuvi huo.
Sababu ya hilo ni kile alichoeleza, uvuvi wa vizimba unawapa wavuvi fursa ya kufnya shughuli zao hata Serikali inapofungia maziwa.
“Pale tunapobaini kwamba rasilimali zilizomo ndani ya maziwa zinapungua, huwa tunafunga kwa miezi kadhaa ili rasilimali hizo zijizalishe tena. Kwa hiyo uvuvi wa vizimba unasaidia msikose kuvua nyakati hizo,” amesema.
Kuhusu zao la kahawa, amesema pamoja na mambo mzuri yaliyofanywa na Serikali, kuna changamoto ya makato ya malipo ya wakulima ambayo kwa sasa yanashughulikiwa.
Sambamba na hilo, amewataka wakulima wote, waendelee kuzingatia kanuni za kilimo bora na wavune pale inapokuwa imeiva na hata uzalishaji usiathiri soko la Kimataifa.
Kwa kuwa katika eneo hilo wanachimba madini, amesema Serikali itahakikisha inawasaidia wachimbaji hasa wadogo ili wanufaike huku nchi nayo ikinufaika.
Amewataka wachimbaji hao kutouza nje ya nchi madini bila kufuata njia halali, kwani kufanya hivyo kunaathiri mapato ya Serikali.
Ametumia fursa hiyo kueleza kuwa, anatambua uwepo wa baadhi ya vijiji visivyopata umeme, lakini kupitia mradi wa ujazilizi vyote vitapata nishati hiyo.
Uchaguzi Serikali za Mitaa
Amesema hana mashaka kwamba Wilaya hiyo ni ya kijani na njano ingawa ameona rangi nyingine.
Amesema kila mwenye sifa ya kuchaguliwa ahakikishe anaomba nafasi na kwamba mwenye haki ya kupiga kura ajitokeze kufanya hivyo.
Kuanza Oktoba 11, mwaka huu, amesema wananchi wajitokeze kujiandikisha katika daftari la uboreshaji wa taarifa za mpigakura.
Ametaka wananchi wote wanaotaka kuleta fujo kuelekea uchaguzi wanapaswa wakemewe.
“Tusikubali kurudisha nyuma kwa siasa zisizojami maslahi ya nchi wala sisi wananchi,” amesema.
Awali, akimkaribisha Mkuu wa Nchi, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema hatua ya kukamilika kwa miundombinu hasa ya barabara ya Mbinga-Mbambabay inaufungua Mkoa wa Ruvuma ambao awali ulijifunga kwa kushindwa kuingiliana na mikoa mingine.
Amesema Tanroads imejenga mtandao wa barabara za kiwango cha lami kilomita 12,209, kati hizo, kilomita 2,384 sawa na asilimia 20 ya mtandao wote zimejengwa kwa ufadhili wa Benki ya AfDB.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Patricia Laverley amesema kujengwa kwa barabara hiyo ni sehemu ya mchango na ushirikiano wa benki hiyo na Serikali ya Tanzania.
Ameeleza kukamilika kwake, hakutaishia kupunguza gharama za safari bali hata matengenezo ya magari yanayopita katika barabara hiyo.
“Mwaka jana zaidi ya magari 4,000 yanafanya safari katika barabara hii na kusafirisha abiria na mizigo, lakini mwaka 2015 tulivyokuja ni chini ya magari 150 ndiyo yaliyokuwa yanapita,” amesema.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mohamed Besta amesema barabara hiyo inaunganisha Mikoa ya Ruvuma na Mtwara.
“Ujenzi wa barabara hii umefadhiliwa na benki ya AfDB kupitia mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa Sh670 bilioni na kati ya hizo Serikali imetoa Sh70 bilioni,” amesema.
Kwa mujibu wa Besta, ujenzi wake umefanywa na kampuni ya uhandisi ya Chico kutoka nchini China na ulikamilika mwaka 2021.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Miundombinu, Suleiman Kakoso amesema bandari hiyo inaunganisha ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia nchi ya Malawi na itaifanya Bandari ya Dar es Salaam ifanyie kazi vizuri.
Amesema zaidi ya kilomita 3,000 za barabara zimejengwa kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia.
“Tunashukuru na tunakuahidi tutaendelea kuiunga mkono Serikali yako,” amesema.
|
Kama ulidhani kuzaliwa kwako na baba na mama kunakupa uhalali usio na shaka wa kurithi mali walizona
|
Kama ulidhani kuzaliwa kwako na baba na mama kunakupa uhalali usio na shaka wa kurithi mali walizonazo unakosea, lipo takwa la kisheria linalokuondolea haki hiyo, ingawa mwenye mali ni baba au mama yako wa damu.
Pengine huu unaweza kuwa ukweli mchungu kwa baadhi ya warithi, kutokana na uhalisia wa matukio kadhaa ya ugomvi wa mali za urithi yanayozikabili familia mbalimbali na wengine wanafikia hatua ya kukatizana uhai.
Mfano wa hayo ni familia ya Bwire Mathayo wa Kibaha mkoani Pwani, iliyoingia kwenye mzozo wa miradi baada ya mama yao kufariki na kuacha mali.
Mzozo huo umetokana na wakubwa kugoma kuwaingiza wadogo zao kwenye mirathi, wakidai hawastahili kwa kuwa mali hizo zilichumwa na baba yao.
Kaka katika familia hiyo, Justine Zuberi alidai baba aliyefariki, ndiye mmiliki wa mali hizo na si baba yao wa kambo (Bwire Mathayo) aliyemuoa mama yao na kumkuta na mali alizoachiwa na baba yao.
Mama yao huyo alifariki dunia Desemba mwaka jana na kuacha watoto wanne lakini kwa baba wawili tofauti.
Binti mdogo, Sabrina Mathayo anasema mgogoro huo umeigawa kwenye familia, haina maelewano, baadhi ya wanandugu wanaamini watoto wote wana haki ya kupata urithi kwa mama yao kwani wote ni watoto wa marehemu na wengine wanapinga.
Mkasa mwingine unaikabili familia mjini Morogoro, baada ya baba kufariki mmoja wa watoto wake aliingia kwenye mgogoro na wenzake akipinga kuenguliwa kwenye mirathi.
Kijana huyo Deniss Joachim (sio jina lake halisi) anataka kuwa mmoja wa warithi, ndugu zake wanagoma wakisisitiza baba yao akiwa hai alimuengua kwenye warithi wake na wosia aliouacha umebainisha hilo.
Kama hiyo haitoshi, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka alieleza mgogoro wa mirathi wa watoto wa familia moja mkoani humo ambao walikwenda ofisini kwake kutaka usuluhishi.
Katika mgogoro huo, watoto wadogo watatu walipinga wakubwa zao wawili kuwa wasimamizi wa mirathi, wakitoa hoja kwamba ndugu zao hawakutaka baba yao apelekwe hospitali alipokuwa anaumwa, iweje afariki ndiyo wawe wasiwamizi wa mirathi yake.
Katika simulizi hiyo, Mtaka alisema wale wadogo walipoulizwa kwanini hawataki, kaka zao wasimamie mirathi, wakasema baba yao alipata kiharusi, waliposhauri apelekwe Muhimbili (Hospital ya rufaa ya Taifa, Dar es Salaam), wale wakubwa walikataa wakidai mzazi wao huyo anaweza kufa muda wowote.
“Alikaa kwenye ari ya ugonjwa mwaka mmoja na miezi minne na kufariki, mvutano ulikuwa wadogo hawataki kaka zao kuwa wasimamizi wa mirathi, wakitoa hoja kwamba ndugu zao walikataa baba yao asipelekwe Muhimbili kwa matibabu zaidi wakati pesa ambazo zingetumika zilikuwa na zake, wakidai walitaka afe ili wagawane fedha za baba yao zikiwa nyingi.
“Wakubwa nilipowauliza wakasema mzee wao alikuwa amefikia kwenye koma, hivyo huenda angefia njiani, lakini swali la kujiuliza hata kama wangechukua ambulance wakalipa milioni 80, hela ni ya mgonjwa mwenyewe,” alisema Mtaka.
Ufafanuzi wa kisheria
Akizungumzia sintofahamu hiyo, Ofisa Usajili wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) Joseph Mwakatobe anasema kuna vigezo vinavyomuondoa mtoto kwenye mirathi iwe baba/mama yake aliacha wosia au la.
“Kwa aliyeacha wosia, mwenye mali anaweza asimrithishe mtoto wake, lakini ni lazima amtaje kuwa ni miongoni mwa watoto wake na sababu za kutomuweka kwenye orodha ya warithi wake na ziwe na ushahidi,” anasema.
Kwa ambaye hakuacha wosia, anasema lazima kuwepo na mashahidi wasiopungua wanne kuthibitisha hilo kuwa mtoto husika hastahili kurithi na Mahakama itaviangalia kama vya msingi.
Kinachomuondolea mtoto uhalali wa kurithi
Pamoja na sababu nyingine, hatua ya kuzini na mke au mume na muandika wosia ni moja ya vigezo vinavyomwondolea mtoto haki ya kurithi.
“Hilo likithibitika, linamuondoa mtoto huyo katika haki hiyo kwa kuwa ni mkosefu wa maadili,” anasema.
Kama wewe ni mtoto na unaharibu mali za mzazi wako, hesabu hiyo ni moja ya sababu zinazokuondolea sifa ya kurithi kwa mujibu wa Mwakatobe.
“Mali aliyoharibu ndiyo itahesabika kuwa ni urithi wake, mzazi akiandika au hata kutamka na ndugu jamaa wakawa wanafahamu, hiyo ni moja ya vigezo vinavyomuondoa huyo mtoto katika mirathi,” anasema.
Lakini, ukishindwa kutoa huduma kwa mzazi wao angali hai, anasema ni sababu nyingine inayokuondolea sifa ya kumrithi.
“Ni kweli huyo mwanao ni mrithi wako, lakini hakukujali labda wakati unaumwa, hiyo inapelekea dhana kwamba pengine anataka ufe ili arithi, na baadhi ya mifano ipo watoto wengine huwaombea mabaya wazazi wao ili tu warithi mali, kigezo hicho kikiwa na ushahidi kinakuondoa kwenye mirithi,” anasema.
Lakini, anasema mtoto anaweza kupinga Mahakamani kama mzazi ameacha wosia na Mahakama itaangalia kama vigezo vilizingatiwa.
Mama mwenye watoto wa baba tofauti
Akifafanua mirathi ya watoto waliochangia mama, Mwakatobe anasema kama mume wa kwanza wa mama huyo alipofariki ulifanyika mgao na kila mmoja (mke na watoto), mama huyo akifariki watoto na mume wake mpya atakuwa na haki ya kumrithi.
“Kama mgao ulifanyika mume wake wa kwanza alipofariki, inamaanisha watoto wakubwa tayari walishapata mgao wao, na kama haukufanyika mali zote zikaenda kwa mama hiyo ni utaratibu anapaswa kufanya mgao bila kuangalia alizaa na nani.
“Mwakatobe anasema kuna migogoro watoto wakubwa wanadai mali alichuma baba yao, lakini kama mali hizo ziligawanywa baba wa kwanza alipofariki, kisha baadae mama akaolewa na kuzaa, ikitokea huyo mama amefariki wote ni uzao wa tumbo lake na kila mtoto anastahili kurithi na hata huyo mume aliyekuwa amemuoa naye anastahili,” anasema.
Anasema huyo mama akiwa na hekima atawaweka wazi mapema kuhusu mali zake na kueleza hizo mali alichuma na baba gani na warithi wake ni watoto wake na wale wa baba mwingine ataangalia baba yao na mali zao.
“Kama hakufanya hivyo, hakuacha wosia na hakuna maandishi na nyaraka, basi vyote vinakwenda kwa wale warithi wake hata mume aliyekuwa amemuoa anaweza kurithi, kwani anapofariki mwenye mali zake, mali zitangukia kwa warithi wake,” anasema.
Wajukuu wanaweza kurithi?
Mwakatobe anasema katika sheria wanaopaswa kurithi ni wale walioachwa na marehemu, mke, mume, wazazi au watoto.
"Kama watoto wa huyo marehemu walitangulia kabla ya baba yao, lakini nao wameacha watoto (wajukuu wa marehemu) hao hawana nafasi labda kama awe aliacha wosia na kuwaandika kwenye mirathi.
"Kinyume na hapo, hao wajukuu tunasema baba au mama yao alikimbia urithi, kwa sababu walifariki kabla ya mwenye mali, na ikitokea wamepata basi ni busara tu inatumika kwenye familia,” anasema.
Unavyoweza kuandika Wosia
Mwakatobe anasema, ili kuandika wosia unakwenda Rita kwanza ukiwa peke yako.
"Haihitaji kitu kingine zaidi ya kuja wewe kama wewe, tutakuelekeza, utaandika mali zako na sisu tutakupangia tarehe ambayo utakuja na mashahidi wawili ili kuandika wosia," anasema.
Hata hivyo, Mwakatobe anasema kitu cha muhimu ambacho watu wanapaswa kukifahamu ni kwamba kuandika wosia inaweza isiwe kigezo cha usimamizi wa mirathi yako pale unapokuwa umefariki endapo wosia utakosa vigezo.
"Hii imekua ikileta shida, unaweza kujiuliza inakuwaje Mahakama imekataa wosia na marehemu aliuandika akiwa hai? ndiyo anaweza kuwa ameandika lakini haujakidhi vigezo, sisi Rita kabla ya kuandika tunakupa elimu kwanza," anasema.
Anasema kwenye wosia mbali na mali, unaandika pia madeni na lazima uwaorodheshe watoto wako na kama miongoni mwao yupo ambaye humpi urithi na ueleze sababu na umtaje msimamizi wa mirathi.
"Unapokuja kuandika wosia uthibitisho wa mali zako unao mwenyewe, Rita tunachohitaji ni taarifa na taarifa yako anakua nayo kichwani, kama una vitu vingi, tunakwambia kaa tulia andika summary ya vitu vyako.
"Wosia unaweza kukosa vigezo, kama muandikaji ameandika si kwa hiari yake, kwani kuna watoto huwa wanazimisha baba aandike kisa labda kaoa mke mwingine halafu wanaona hizo mali zilichumwa na mama yao," alieleza.
Anasema kigezo cha kwanza katika kuandika wosia lazima uwe na hiari nao, pili ni utimilifu wa akili ukijua kile unachoandika na unakikumbuka.
"Pia uwe na mashahidi wasiopungua wawili na lazima uchapwe, usifutwe futwe na kilichoandikwa kisilete utata na usainiwe na muandikaji na mashahidi siku moja na uthibitishwe,” anasema.
Anasema kwenye wosia shahidi anaweza kufariki kabla ya mwenye mali, hivyo wosia unaweza kubadilika mara kwa mara kulingana na uhitaji uliopo.
Kwa mujibu wa Mwakatobe, gharama za kuandika wosia zinaanzia Sh30,000 na kuuhifadhi ni Sh30,000 kwa mali isiyozidi Sh50 milioni.
Kuanzia mali za Sh50 milioni hadi Sh500 milioni kuandika ni Sh100,000 na kuuhifadhi ni Sh100,000.
Na kwa mali ya kuanzia Sh500 milioni na zaidi kuandika ni Sh150,000 na kuuhifadhi ni Sh150,000.
"Mali hizo huwa tunazifanyia makadirio na kutathimini kulingana na mazingira," anasema.
|
Baada ya kusuasua kiuendeshaji, hatimaye Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), imebadili mfum
|
Baada ya kusuasua kiuendeshaji, hatimaye Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), imebadili mfumo wa utendaji wake, ikitangaza kubadili mfumo wa utekelezaji wa majukumu yake, kwa kushirikiana na sekta binafsi kupitia ubia (PPP).
Kutokana na mabadiliko hayo, Temesa imewaita wawekezaji wa sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi kuwasilisha mapendekezo ya ushirikiano nayo katika huduma za vivuko, karakana za ufundi magari na ufundi umeme.
Temesa inakuja na mpango huu ikiwa ni miezi mitatu tangu gazeti hili lichapishe mfululizo wa ripoti maalumu zinazoonyesha wakala huo kuhelemewa na majukumu, kuathiriwa na mifumo na hata kujikuta ikiangukia katika madeni.
Ripoti hiyo iliyotokana na uchunguzi uliofanywa kwa takriban miezi mitatu, iliweka wazi juu ya Temesa kukiuka mpango wa matengenezo ya vivuko na kudaiwa zaidi ya Sh30 bilioni na wasambazaji wa vipuli kwenye karakana zake za ufundi magari.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ubia wa sekta ya umma na binafsi ndiyo ulioonekana kama suluhu ya changamoto zote zinazoukabili wakala huo na sasa hatimaye umeanza kulitekeleza hilo kwa kushirikiana na Kamishna wa Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi, David Kafulila.
Hata hivyo, pamoja na ubia huo kuwa fursa kwa sekta binafsi, wadau hao wanasema kunahitajika uhuru wa kuamua baadhi ya mambo ili kuzalisha faida kwa pande mbili.
Ushirikiano katika vivuko
Katika taarifa hiyo, Temesa imewaalika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya kuwekeza kwenye uendeshaji wa vivuko kupitia mpango wa PPP.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwekezaji ana fursa ya kuwekeza kwa njia ya kukodisha vivuko vyote, kuunda ubia wa pamoja au kuendesha vivuko vyake sambamba na vile vya Temesa.
Mwekezaji huyo anayeonyesha nia, anapaswa kuwasilisha nakala zilizothibitishwa za hati za kisheria za taasisi husika na muhtasari wa maelezo ya awali ya uwekezaji.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwekezaji huyo pia anapaswa kuwasilisha maelezo ya awali ya uwekezaji, kutoa muhtasari wa mradi uliopendekezwa na uwezo wake wa kufikia ufanisi, unafuu wa kifedha na thamani.
Katika pendekezo hilo, mwekezaji anatakiwa kutuma idadi ya vivuko atakavyoendesha na idadi ya abiria na magari yatakayohudumiwa kwa mwaka.
Kwa mujibu wa Temesa katika tangazo hilo, mradi uliopitishwa utapaswa kuanza ndani ya miezi 24 kwa kusaini mkataba wa utendaji na kuwasilisha dhamana ya benki, kiasi kitakachokubaliwa kati ya Temesa na mwekezaji mtarajiwa.
Pia, taarifa hiyo inataka ulinganifu na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Tanzania 2025 na mipango ya kitaifa ya maendele.
“Thamani ya fedha kwa manufaa kwa Serikali, ikihusisha kuchochea maendeleo ya kiuchumi, kuongeza huduma, ajira na ukuaji wa uchumi, mageuzi ya teknolojia na kuongeza mapato ya taifa,” imeeleza.
Ushahidi wa uwezo wa kifedha wa wawekezaji kwa kuwasilisha ripoti za fedha zilizokaguliwa kwa miaka mitatu, uzoefu wa mwekezaji katika kutekeleza miradi kama hiyo ni vigezo vingine vilivyobainishwa.
Kadhalika, uwezo wa kuboresha na kuendesha vivuko kwa kutumia teknolojia ya kisasa, makadirio ya gharama za mitaji ya uwekezaji, faida zinazopendekezwa kulipwa kwa Temesa na faida za kijamii zinazopendekezwa kwa jamii inayozunguka mradi huo.
Karakana
Kwa upande wa karakana, Temesa imetawatangazia wawekezaji kushirikiana nayo katika uendeshaji wa karakana 13 kupitia mpango wa PPP
Limesema baada ya hatua hiyo, Temesa itachagua wawekezaji watakaokidhi vigezo vya tathmini na baadaye kuwaalika waombaji waliofanikiwa.
Tangazo hilo hilo pia limetolewa kwa sekta binafsi itakayoshirikiana nayo katika ufundi wa umeme.
Alichosema Kamishna wa PPP
Kamishna wa Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi, David Kafulila alisema ushirikiano huo unalenga kufanywa katika uendeshaji wa karakana 13 kati ya 30 za wakala huo, sambamba na majukumu mengine kama vivuko na ufundi.
Kwa upande wa magari Kamishna huyo alisema karakana hizo 13 zipo katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Shinyanga, Kagera, Singida, Iringa, Mara, Manyara, Pwani, Lindi, Ruvuma, Njombe na Simiyu.
Hata hivyo, Kafulila alisema hatua hiyo ya Temesa inaakisi matakwa ya Kanuni ya 36 (b) na (d) ya Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi ya mwaka 2020 na marekebisho yake ya mwaka 2023.
Kanuni hiyo, kwa mujibu wa Kamishna huyo, inairuhusu Temesa kuwaalika wawekezaji katika utekelezaji wa miradi yake kwa njia ya ubia.
“Mpango wa Temesa kuboresha karakana zake na kutoa huduma kwa njia ya ubia unatoa matumaini ya kukidhi mahitaji ya huduma za matengenezo kwa aina mbalimbali za magari na mitambo,” alisema.
Kwa mtazamo wa Kafulila, hatua hiyo itawezesha kuvutia teknolojia za kisasa, kuchochea ufanisi wa uendeshaji na kuboresha ubora wa huduma.
“Mageuzi makubwa yatazidi kutokea katika miradi ya ubia baada ya Kituo cha Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi kufikia adhma yake ya kutoa huduma zote za ubia ndani ya kituo (one-stop centre),” alieleza Kafulila.
Maoni ya wadau
Akizungumza kuhusu ushirikiano katika uendeshaji wa vivuko, mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu kutoka moja ya kampuni binafsi zinazoendesha huduma za vivuko nchini (jina lake limehifadhiwa), alisema hiyo ni fursa kwa upande mmoja lakini inahitaji maelewano kwa upande mwingine.
Kwa upande wa fursa, alieleza kwa sababu kuna mahitaji makubwa ya abiria kutumia usafiri huo, bila shaka ni biashara nzuri na yenye faida.
Lakini, fursa hiyo alisema haitakuwa kama inavyotarajiwa iwapo Temesa haitatoa uhuru kwa mwekezaji huyo kutoka sekta binafsi wa kupanga baadhi ya mambo kwa maslahi ya pande zote.
Miongoni mwa mambo hayo, alitaja ni nauli kwa abiria, utaratibu wa uendeshaji, mbinu za ukusanyaji nauli na hata mageuzi ya huduma kwa ujumla wake.
“Kiufupi isiwe huduma iwe biashara, sekta binafsi inatafuta faida, wenzetu serikali wanahudumia. Kama wanataka ubia wakubali kukaa pembeni washuhudie biashara ikifanyika wabaki kusimamia ili wachungulie mapato,” alisisitiza.
Mkuu wa Idara ya Usafirishaji na Biashara wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Dk Prosper Nyaki alieleza ushirikiano huo utawezekana iwapo Serikali itaendelea kukusanya nauli na kumlipa mwekezaji kulingana na gharama zake za uendeshaji.
Ikitoa ruhusa kwa mwekezaji kukusanya, alisema itakuwa vigumu kuilipa Serikali kwa kuwa inaonekana gharama za uendeshaji wa vivuko ni kubwa ukilinganisha na nauli inayotozwa.
“Kwa nauli sekta binafsi haitaweza kulipa labda Serikali ije na mbinu ya mwekezaji atoe huduma na Serikali iwe inawalipa,” alieleza.
Hata hivyo, mwanazuoni huyo alisema kwa kawaida usafiri wa umma huwa ni huduma na sio biashara na unapoishirikisha sekta binafsi unalenga kupata faida.
“Napata shida kujua itawezekanaje ukizingatia nauli wanayolipa abiria hailingani na gharama halisi za uendeshaji wa vivuko, sijui mwekezaji atapataje faida,” alisema.
Lakini, alisema ushirikiano utakuwa na tija iwapo mwekezaji huyo ataamua kuja na vivuko vyake.
Kuhusu karakana, Mtaalamu wa Ufundi, Salim Msami alisema itakuwa vema kwa sekta binafsi kuunda ubia na Temesa kwa kuwa wadau hao binafsi watajihakikishia upatikanaji wa soko.
“Serikali ina magari mengi kwa hiyo ukishirikiana nao moja kwa moja unakuwa na uhakika wa wateja,” alisema Msami ambaye pia ni ofisa katika kampuni binafsi ya Hyundai.
Ili ushirikiano huo uwezekane, alisema kunahitajika kuwepo na sharti la wadau wote wawili kuwa sehemu ya uongozi na mgawanyo wa majukumu na mapato ueleweke vema.
Alisisitiza sekta binafsi imejikita katika faida zaidi na sio kutoa huduma, ili Temesa ishirikiane nayo vema inahitaji kubadili mfumo wa utendaji wake na kuweka wazi makubaliano ya uendeshaji wa karakana hizo.
Kwa mujibu wa Msami, kunahitajika uhuru wa uendeshaji wa karakana hizo kwa sekta binafsi iwapo itapewa kazi hiyo.
|
Katika jitihada za kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na gharama za uzalishaji wa
|
Katika jitihada za kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na gharama za uzalishaji wa kilimo, matumizi ya nishati ya umeme jua hasa kwenye umwagiliaji yanatazamwa kama suluhisho.
Teknolojia hiyo sio tu inapunguza gharama za kilimo, bali inachangia kuongeza uzalishaji wa mazao, hasa katika maeneo yenye ukame na upatikanaji mdogo wa maji.
Pamoja na uhalisia huo, matumizi ya nishati ya umeme jua katika kilimo cha umwagiliaji nchini, bado hayaridhishi kama inavyoonyeshwa katika utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Kilimo Tanzania (Tari) mwaka 2020.
Kwa mujibu wa Tari, kwa mwaka huo takriban asilimia 85 ya wakulima wanaotumia mifumo ya umwagiliaji wanategemea pampu zinazotumia dizeli.
Takwimu za Tari, zinaakisi matokeo ya ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2021, iliyoonyesha wakulima wengi wadogo nchini wanaendelea kutumia pampu za dizeli kutokana na gharama ndogo za awali za ununuzi wake, ingawa gharama za uendeshaji kwa muda mrefu huwa kubwa zaidi.
Mwaka mmoja baadaye 2022, Benki ya Dunia ilitoa ripoti yake ikionyesha wakulima wanaotumia nishati ya umeme jua katika umwagiliaji ni asilimia 15 pekee nchini.
Ingawa hali iko hivyo, matokeo ya tafiti na ushuhuda wa wakulima unaonyesha matumizi ya nishati ya umeme jua katika kilimo cha umwagiliaji yana tija zaidi kuliko nishati nyingine.
Tija ya umeme jua kwenye umwagiliaji
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) mwaka 2021, liliweka wazi kuwa kwa kutumia pampu za umeme jua, wakulima wanaweza kupunguza gharama za nishati kwa asilimia 70 hadi 90.
Shirika hilo, kupitia mradi wake wa kilimo cha umwagiliaji wa pampu za umeme jua kwa kilimo endelevu, uliofanywa mkoani Dodoma, ulionyesha wakulima walipunguza gharama za nishati kwa asilimia 80 baada ya kubadili matumizi ya dizeli kwenda kwenye umeme wa jua.
Katika hatua nyingine, Ripoti ya Benki ya Dunia kuhusu nishati mbadala ya mwaka 2022, inakadiria matumizi ya umeme jua kwenye kilimo cha umwagiliaji yanaweza kuongeza uzalishaji wa mazao kwa wastani wa asilimia 30 hadi 50.
Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) nalo linaonyesha matumizi ya nishati ya jua katika kilimo cha umwagiliaji yameongeza uwezo wa wakulima kukabiliana na majanga ya hali ya hewa kwa kuboresha upatikanaji wa maji.
Unafuu wa gharama
Kwa mujibu wa Chama cha Nishati Jadidifu Tanzania (Tarea), mkulima atagharimika Sh3.81 milioni kwa mwaka, kumiliki jenereta linalotumia mafuta kwa ajili ya umwagiliaji katika shughuli za kilimo na litadumu kwa miaka mitatu.
Lakini kwa mtambo wa umeme jua kwa ajili ya umwagiliaji, unagharimu Sh10 milioni, ambao kiuhalisia unadumu kwa miaka 20.
Tarea inaeleza licha ya gharama kubwa za mwanzo katika usimikaji wa mtambo wa nishati ya umeme jua katika kilimo cha umwagiliaji, kuna unafuu mkubwa baadaye.
Unafuu huo kwa mujibu wa Tarea, unatokana na muda mrefu ambao mtambo wa nishati ya umeme jua unadumu, kadhalika hauhusishi gharama yoyote ya uendeshaji, wakati jenereta linahitaji mafuta kila siku.
Chama hicho kimekwenda mbali zaidi na kueleza, jenereta linalotumia mafuta katika shughuli za kilimo cha umwagiliaji linazalisha kilo 487 za hewa ya ukaa, ambayo ni hatari kwa mazingira kila siku.
Ushuhuda wa mkulima
Mbali na tathmini ya Tarea, Anthony Machai mkulima anayetumia nishati hiyo mkoani Dodoma, anasisitiza unafuu wa nishati hiyo katika kilimo, ukilinganisha na mtambo unaotumia mafuta.
Kwa mujibu wa Machai, katika shamba la ekari tatu kwa jenereta utalazimika kununua mafuta ya Sh50,000 kila siku kuwezesha kuvuta maji kutoka kisimani hadi kwenye mazao kwa ajili ya umwagiliaji.
Gharama hizo, anasema kwa mwezi ni sawa na kutumia Sh1.5 milioni, kiasi ambacho ni maumivu kwa mkulima.
Lakini unapotumia mitambo ya umeme jua, anasema gharama ni kuifunga tu, baada ya hapo mkulima hatagharimika na chochote.
“Pamoja na mazingira hayo, ni wakulima wachache ndiyo tunaotumia nishati ya umeme jua kwenye kilimo, wengi wanaona afadhali watumie majenereta na mafuta,” anaeleza.
Kinachochochea wakulima wengi wachague majenereta licha ya faida ndogo wanayopata ni kile kilichoelezwa na Machai kuwa, hawana uwezo wa kufunga mitambo ya umeme jua.
Machai anasema mtambo wa umeme jua unaomudu huduma za shamba la ekari nne hadi tano, unagharimu Sh9 hadi 15 milioni.
Anasema ni wakulima wachache wenye uwezo wa kuwa na viwango hicho cha fedha kwa mara moja, ndiyo maana wanachagua kuingia gharama kidogokidogo kwenye mafuta.
“Ni kweli ukifunga mtambo kwa gharama hizo hautahitajika kutoa gharama nyingine yoyote, lakini ni wakulima wachache wenye uwezo wa kupata kiasi hicho cha fedha kwa mkupuo wafunge nishati hiyo,” anasema.
Kinachopaswa kufanywa, anasema ni Serikali iangalie utaratibu wa kuwawezesha wakulima kukopeshwa mitambo hiyo ili wawe wanalipa kidogo kidogo hadi watakapomaliza
Kwa sababu anasema gharama za mitambo huo, zinarudishwa kwa awamu moja ya kilimo.
“Mimi mwaka huu nimelima ekari moja ya nyanya kwa kutumia solar nimeingiza Sh12 milioni, kwa hiyo ni msimu mmoja unakuwezesha kurudisha gharama za mtambo lakini si kila mkulima ana uwezo wa kupata fedha ya kununua mtambo kwa mara moja, wakopeshwe,” anaeleza.
Gharama kubwa za mtambo anasema zinasababishwa na kodi zilizopo katika uingizaji wa bidhaa hizo nchini.
Anapendekeza kuwepo msamaha wa kikodi katika uingizaji wa bidhaa za sola nchini ili kuwarahisishia wakulima na kuendana na mpango wa Serikali wa matumizi ya nishati safi.
Mikakati ya Serikali
Akizungumzia hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa anasema kinachofanywa na mamlaka hiyo ni kutoa elimu kwa wakulima kutumia nishati ya umeme jua katika shughuli za umwagiliaji.
Sambamba na hilo, anasema mamlaka hiyo imeshaanza mkakati wa matumizi ya nishati hiyo kwa kupendekeza nishati ya umeme jua.
Kwa hatua za awali, anaeleza wameanza kuingiza visima 60 kati ya 1,000 mwaka huu vitakavyotumia nishati ya umeme jua katika umwagiliaji.
“Tumeanza na visima 60 kati ya 1,000 mwaka huu. Tumeyabainisha maeneo tutakayoanza nayo lakini kuna uwezekano wa visima hivyo kuongezeka zaidi,” anasema.
Anasema tayari kazi hiyo imeshaanza na kwamba anaamini itakwenda kukamilika.
|
Rais Samia Suluhu Hassan ameyajibu matamko ya balozi zinazoyawakilisha mataifa mbalimbali nchini, ya
|
Rais Samia Suluhu Hassan ameyajibu matamko ya balozi zinazoyawakilisha mataifa mbalimbali nchini, yaliyotaka uchunguzi wa haraka wa matukio ya utekaji na mauaji ya watu, akisema Tanzania ni nchi huru haipaswi kuelekezwa cha kufanya kwenye mambo yake.
Katika majibu yake hayo, amewashutumu mabalozi hao akisema walichokitamka haamini kama ni maelekezo ya wakuu wa nchi zao, huku akiahidi kuwachongea kwa marais wa mataifa husika kwa kuiingilia Tanzania.
Chimbuko la majibu ya mkuu huyo wa nchi ni tamko la pamoja la balozi za mataifa 15 yanayowakilisha Umoja wa Ulaya (EU) nchini, yakilaani na kutaka uchunguzi wa haraka na huru wa matukio ya mauaji.
Balozi zilizotoa tamko hilo la pamoja ni Ubelgiji, Uingereza, Canada, Denmark, Ufaransa, Finland, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Poland, Hispania, Sweeden na Uswisi.
Katika tamko hilo, balozi hizo zilisema; “Tunakaribisha wito wa Rais wa kuanzisha uchunguzi wa haraka ili kubaini wahalifu waliohusika na kuhakikisha kuna uwajibikaji.”
Kadhalika wametaka ulinzi wa upinzani, ili kuakisi falsafa ya R4 ya Rais Samia na kusisitiza; “Tunatambua kwa wasiwasi mkubwa kwamba matukio haya ya hivi karibuni yanatishia misingi ya kidemokrasia na haki za wananchi wa Tanzania.
Hata hivyo, mabalozi hao walitoa tamko hilo, muda mchache baada ya taarifa ya kifo cha kada wa Chadema, Ali Kibao aliyechukuliwa akiwa katika usafiri wa umma Septemba 6, mwaka huu na siku moja baadaye amekutwa ameuawa.
Rais Samia aliyasema hayo mkoani Moshi jana, alipohutubia hafla ya kufunga mafunzo ya Maofisa wa Jeshi la Polisi yaliyofanyika kuadhimisha miaka 60 ya jeshi hilo katika Chuo cha Polisi.
“Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya ndani ya nchi yetu, tuna Katiba sheria, miongozo, mila na desturi zetu zinazotuongoza nini cha kufanya kwenye nchi zetu,” alisema.
Rais Samia alisema ameapa kuilinda na kuitetea nchi na kwamba atafanya kila linalowezekana kuimarisha ulinzi wa maisha na uhai wa watanzania kwa kuwa ni jukumu lake.
Katika wajibu huo, alisema hahitaji kuelekezwa na mtu yeyote cha kufanya kwa sababu Katiba ya Tanzania ina maelekezo ya jinsi ya kuendesha Serikali.
“Wengine wanapotaka kuonyesha huruma yao basi tunawasihi wafanye hivyo kwa kufuata makubaliano ya mahusiano kidiplomasia ya kimataifa kama ilivyoelezwa kwenye Vienna Convention on Diplomatic Relation la 1961.
“Lile tamko lililotoka na kuambiwa tufanye moja mbili tatu, sisi tunajua cha kufanya kama Tanzania kama nchi yetu. Na ni imani yangu kwamba tamko lile lililotolewa si maelekezo ya wakuu wa nchi huko walikotoka,” alisema.
Kwa sababu ana namna ya kujua, mkuu huyo wa nchi alisema atawasiliana na wakuu wenzake wa nchi za balozi hizo kujua iwapo tamko hilo ni maelekezo yao na kama sivyo atawasilisha malalamiko yake.
Katika maelekezo yake hayo, alisema mauaji yanatokea katika kila nchi, lakini Tanzania haikuwahi kuwatuma mabalozi wake wakaelekeze nchi hizo cha kufanya.
Atoa onyo
Katika hotuba yake hiyo, alisema ingawa Serikali yake inaongozwa kwa falsafa ya R4, haimaanishi kuruhusu uvunjwaji wa sheria, mila, desturi na kuruhusu utovu wa nidhamu.
“Hatutavumilia vitendo vyovyote vya kuleta machafuko na mifarakano nchini. Sasa ni vizuri tusisahau au wale wanaojiandaa na machafuko wasisahau mapito waliyopita. Ni falsafa hii hii ndiyo imewapa ruhusa ya kurudi nchini, tukafumbia macho mengine yote, sasa kama wameshaota mikia sasa sheria zile zile bado zipo.
Alieleza Serikali imefanya juhudi za kurudisha uhuru wa vyama vya siasa, vyombo vya habari, waliokuwa jela walitolewa na waliokuwa na jinai zilifumbiwa macho kwa lengo la kuwa pamoja kujenga nchi.
Alieleza inakuwa mbaya watu hao hao wanasimama kutoa kauli zinazoirudisha nyuma nchi, akisisitiza atailinda amani ya nchi kwa gharama yoyote.
“Ukimya wangu sio ujinga na wala kuzungumza sana sio werevu hata kidogo, kuzungumza sana ni udebetupu tu haliachi kuvuma lazima litavuma.
“Na anayenyamaza kimya si mjinga ni mtu anayetafakari mambo si mjinga. Kwa hiyo ukimya wangu sio ujinga na kuropoka kwao sio werevu,” alieleza.
Kwa kuwa aliapa kuilinda na kutetea Katiba, alisema hatakuwa na muhali kwa atakayetaka kuivuruga amani.
“Tumevumiliana sana kwa mambo mengi, lakini kwenye kulinda tunu ya amani na utulivu nieleze, sitakuwa na muhari kwa yeyote atakayejikaribisha katika mambo haya, anayeratibui, anayeshiriki na hata anayetekeleza mipango hiyo miovu,” alisema.
Mauaji ya Kibao
Mkuu huyo wa nchi, pamoja na kueleza kuhuzunishwa na kulaani tukio la kifo cha Kibao, lakini ameshangazwa namna wananchi walivyoponyesha hisia kali ilhali kwenye mauaji ambayo aghalabu hutokea yakiwemo ya albino hawaonyeshi hali hiyo.
“Katika hali ya kushangaza kifo hicho kimeleta hisia kali pia kwa wawakilishi wa baadhi ya mataifa ya nje wanaoiwakilisha nchi zao hapa kwetu. Nataka niungane nao na niseme kwamba kwa sababu yoyote ile mauaji haya hayakubaliki,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, alisema ndiyo maana Serikali ililaani na kutaka vyombo vya uchunguzi vifanye uchunguzi kama inavyofanyika katika mataifa yote duniani.
“Lakini kuna vifo vinasemwa muda baada ya muda, watoto maalbino wanakatwa mikono, watoto wadogo wanauliwa wanakatwa sehemu nyeti wanatupwa sijui huyu kamuua huyu.
“Hadi leo asubuhi IGP (Camilius Wambura) kanipa ripoti huko Dodoma watu watatu wameuliwa lakini yanapotokea haya yanatokea kwenye maeneo yetu lakini kimya mpaka polisi iibuke iseme wengine hawasemi.
“Lakini inashangaza kifo cha ndugu yetu Kibao kimeibua wimbi kubwa kulaani, kusikitika, kulaumu, kuita Serikali ya wauaji hii si sawa, kifo ni kifo. Tunachopaswa kufanya Watanzajia wote tukemmeane tusimame imara kukemea mambo haya,” alisema.
Wavunjifu wa amani
Katika hotuba yake hiyo, alisema alisikiliza sauti za wanasiasa mbalimbali wote wakitoa taswira ya mipango ya uvunjifu wa amani inayopangwa na baadhi ya vyama vya siasa.
“Nayaunganisha haya na kikao cha Septemba 11, mwaka huu kilichofanywa na chama kimoja cha siasa kule Nguleli mkoani Arusha. Kikao ambacho kimeazimia kuwatumia na kuwachochea vijana kwa kuzusha tuhuma dhidi ya jeshi la polisi, kufanya siasa chonganishi kwenye misiba na kushusha molari kwa jeshi la polisi ili washindwe kufanya kazi yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao,” alisema.
Alieleza kwa sababu ya ukubwa wa intelejensia ya nchi, ndiyo maana imewezekana kupata taarifa za kikao hicho, akisisitiza naye anayo.
“Kwa hiyo nataka niwaambie vikao vyote vinavyokwenda kupanga uovu huu, uovu tutaupata. Kumepangwa sijui kushusha moto mpaka Samia aseme sijui basi nime-surrender naondoka, hiyo Serikali Serikali ya samaki?” alihoji.
Matukio mengine aliyoyazungumzia, ni mauaji yanayohusisha upigaji ramli na vuguvugu la uchaguzi, akisema yanapaswa yakome.
“Wananchi wanakata tamaa kuona matukio haya yanahusishwa sio tu na waganga wa kienyeji bali hata watu mashuhuri kama viongozi wa dini na hata wazazi na watoto.
“Lakini yanapotokea kule chini jamii ipo kimya kama Tanzania haitokei kitu, lakini vyombo vya ulinzi wakiibua ndiyo sasa watu wanaibuka eeeyeye yeye… lakini kabla ya kuibuka hakuna anayelaani,” alisema.
Mafunzo kwa askari
Alisema askari wanatakiwa kupatiwa mafunzo kazini, ndani na nje ya nchi, huku akisisitiza nchi nyingine ziongezwe ili wakajifunze wenzao wanavyofanya.
Sambamba na hayo alitaka mafunzo ya ndani pia yaendelee, akisisitiza mabadiliko ya fikra yanategemea mafunzo ya mara kwa mara.
Hata hivyo, alieleza bado kuna changamoto katika utendaji wa jeshi hilo na kwamba Tume ya Haki Jinai imeshapendekeza namna ya kufanyia kazi.
Mambo mengine aliyozungumzia ni ajali za barabarani akisema zinasababisha vifo vya wananchi wengi na kwamba zinapaswa kudhibitiwa.
Kadhalika, alilitaka jeshi hilo kuendana na teknolojia za sasa ili kudhibiti uhalifu wa mtandaoni hasa kuelekea chaguzi na wizi kwa njia ya mtandao.
“Miongoni mwa uhalifu unaongezeka kwa kasi ni kutoa taarifa za uzushi na uongo na kutuma picha za utupu na unyanyasaji. Kutokana na kukua kwa teknolojia ya akili bandia taarifa za uzushi zinatarajiwa kuongezeka,” alisema.
“Hatusemi tufungie mitandao ya kijamii au tuwafunge midomo wananchi kuto maoni yao, lakini haijuzu kufumbia macho uhalifu unaofanywa kwenye mitandao ya kijamii. Uhalifu ni uhalifu.
“Kama ambavyo mhalifu angekamatwa kufanya uhalifu nje ya mitandao ya kijamii, vivyo hivyo afanywe yule atakayefanya hivyo kupitia mitandao ya kijamii,” alisema.
Kadhalika, mkuu huyo wa nchi alisisitiza kuongezwa uwezo na ujuzi wa kuwabaini wahalifu wanaotumia majina bandia au anga la nje ya Tanzania.
Kuhusu utapeli, alitaka liangaziwe kwa karibu zaidi kwani kwa kadri wananchi wanavyohamasika kufanya miamala kwa njia ya mtandao na ndivyo wahalifu nao wanavyobuni mbinu za kuiba.
Kwa kuwa mwelekeo wa Serikali ni kuongeza matumizi ya fedha kidigitali, alisema ni vema jeshi hilo kuhakikisha linaimarisha mbinu za kudhibiti uhalifui huo.
Alilitaka jeshi hilo, liwasilishe mkakati na bajeti ya kukabili uhalifu wa mtandao ili Serikali ione namna itakavyowezesha kukomesha hilo.
Kuelekea uchaguzi, alisema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha nchi inabaki kuwa moja na salama kwa kuwa uchaguzi utapita na taifa litabaki.
“Jeshi la polisi liwe macho katika kipindi chote cha kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Jeshi la Polisi lihakikishe yeyote anayejaribu kuhatarisha amani ya nchi yetu kwa kisingizio cha chaguzi hizo anachukuliwa hatua haraka na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema.
Rais Samia alisema jeshi la polisi halipaswi kuhusishwa au kuhisiwa kuhusika na ukiukwaji wa sheria na haki inazozisimamia.
“Nilikuwa naona leo kuna clip kule Mwanza, kuna mhalifu kakamatwa polisi wanataka kuondoka naye, raia wamezuia gari wanasema haliondoki mpaka OCS aje ndiyo aondoke na huyu mtuhumiwa sasa hiyo ifanyieni kazi vizuri,” alisema.
Alilitaka lisimamie maadili ya askari ili jeshi litoe huduma stahiki na kuongeza imani ya wananchi kwa chombo hicho.
Alitaka kasi ya kuikumbatia Tehama katika jeshi hilo iwe kubwa na anasubiri bajeti ilia one namna atakavyosaidia.
Alisisitiza askari kujengewa uwezo stahiki ili wasipitwe na teknolojia, huku akidokeza juu ya umuhimu wa mifumo kusomana.
|
Tofauti na ilivyo katika maeneo mengi, kila jina la mtaa unaounda Kata ya Kimara ni simulizi yenye h
|
Tofauti na ilivyo katika maeneo mengi, kila jina la mtaa unaounda Kata ya Kimara ni simulizi yenye historia maridhawa.
Uwepo wa viwanda, shughuli za kiuchumi na miradi mbalimbali, ndiyo msingi wa ubatizo wa majina hayo, yanayoendelea kutumika hadi sasa.
Unapotokea mjini kati Dar es Salaam, Mtaa wa Kibo ndilo lango la kuingia Kimara. Ingawa Kibo inahusishwa na Kata ya Ubungo, kwa sehemu fulani imeigusa Kimara.
Kwanini Kibo
Historia ya jina Kibo inahusishwa na Mlima wenye jina hilo, mkoani Kilimanjaro, kama inavyosimuliwa na Meya mstaafu wa Ubungo, Boniface Jacob kupitia mtandao wake wa X.
Mzee Naumu ndiye mwasisi wa jina hilo, aliyeamua kuipa jina baa yake aliyoijenga katika eneo hilo, Kibo Bar na umaarufu wake ukazaa jina la mtaa hadi sasa panaitwa Kibo kwa mujibu wa Jacob.
Kwa mujibu wa Jacob, Mazee Naumu aliamua kuiita baa yake kwa jina hilo kwa kuwa eneo hilo lilikuwa na mlima na hivyo aliufananisha na ule wa Kibo, Kilimanjaro.
Kabla ya jina hilo, Jacob anasema eneo hilo liliitwa kilima cha kwanza kwa anayetoka mjini kati na kilima cha mwisho kwa anayetokea Mbezi. Hivyo hakukuwa na jina rasmi.
Kwa bahati nzuri Kibo Bar ipo hadi sasa, lakini si kwa umaarufu kama ilivyokuwa zamani. Hata hivyo ni vigumu kuiona unapopita barabarani kwa kuwa mbele yake kuna flemu za maduka na mti ambao ni kijiwe cha madalali.
Kimara Baruti
Ukistaajabu ya Kibo, ya Kimara Baruti yatakusangaza. Asili ya jina hilo ni shughuli za uhifadhi baruti zilizokuwa zinafanywa katika eneo la kiwacha cha Saruji cha Twiga Chemical.
Baruti hizo, zilitumika kupasulia mawe yanayotumika katika kutengenezea saruji.
Katika eneo hilo pia, Jacob anasema kulikuwa na maghala ya kuhifadhi baruti na kambi kubwa ya wafanyakazi wa kiwanda cha saruji.
Haikuwawia vigumu waswahili, kushabihisha shughuli maarufu katika eneo hilo na jina la mtaa na ndilo chimbuko la Kimara Baruti.
Mwanasiasa huyo anasema kwa sasa eneo hilo imejengwa Hospitali ya Wilaya ya Ubungo na shughuli za uhifadhi baruti zilihamishwa tangu miaka ya 1990.
Kimara Bucha
Kama lilivyo jina lake, asili ya jina la mtaa huu ni bucha la nyama ya kitimoto, lililojengwa kwa nakshi za aina yake kulingana na nyakati hizo, inadaiwa miaka ya 1980, kwa mujibu wa Jacob.
Bucha hilo lililokuwa mali ya Thomas Lyimo ambaye pia alimiliki kiwanda cha maziwa cha Thom Dairy, yaliyokuwa yakigawiwa bure katika shule za msingi.
Jamaa alianza kwa kujenga banda la chuma tupu, kwa namna lilivyopambwa kila mmoja alikuwa na shauku ya kujua nini kinalengwa kuwekwa ndani yake. Hatimaye likawa duka la nyama ya nguruwe na ndiyo asili ya jina la Kimara Bucha.
Kimara Korogwe
Hili sio la muda mrefu kama yalivyo majina mengine. Liliibuka mwanzoni mwa miaka ya 1990 kama inavyosimuliwa na Jacob kupitia mtandao huo.
Kabla ya Korogwe, eneo hilo liliitwa Kimara Resort kutokana na uwepo wa kiwanja cha starehe, mithiri ya vile maarufu hapa mjini kwa sasa.
Watu wa nyakati hizo, kabla ya kwenda kwenye kumbi hiyo, walivalia suti ya kitambaa cha Asante Urafiki, lililokuwa vazi maarufu kipindi hicho.
Mbwembwe na umaarufu wa jina hilo, ulivurugwa na Msambaa aliyetoka Korogwe mkoani Tanga na kuanzia banda la chipsi, msosi pendwa kwa mabinti.
Haikuwa kawaida, kwa kuwa banda hilo lilipanga magari ya Serikali na msululu wa wananchi wakisubiri chipsi za msambaa, pengine kwa sababu ya ladha yake.
Hakuwa peke yake, kama ulivyo utamaduni wa wasambaa, alikuwa na vijana zaidi ya 100 wanaotumikia ofisi hiyo kwa kumenya viazi kukidhi mahitaji ya wateja.
Kwa mujibu wa simulizi ya Jacob, isingekuwa rahisi upite eneo hilo na una fedha mfukoni, usinunue chipi kwa namna zilivyonukia na kuvutia.
Basi bwana, jamaa akapata aidia ‘idea’ akaandika bonge la bango kwa mkono ‘KOROGWE’ kuanzia hapo jina la Resort likajifia na Korogwe likaibuka.
|
Licha ya mtazamo kuwa, kuimarika kwa usafiri wa reli ya kisasa (SGR) kutaathiri usafiri wa anga kwa
|
Licha ya mtazamo kuwa, kuimarika kwa usafiri wa reli ya kisasa (SGR) kutaathiri usafiri wa anga kwa upande mmoja, wadau wa usafiri huo, wamesema reli hiyo ya kisasa inaweza kuimarisha sekta ya anga pia.
Matumaini ya wadau hao yanatokana na mtazamo kuwa, kuna uwezekano wa vyanzo hivyo vya usafiri kushirikiana na kuwapa fursa wananchi kuchagua aina gani wanayopenda kulingana na mahitaji yao.
Hoja hizo za wadau zinakuja katika kipindi ambacho, treni za SGR zimeteka soko la sekta ya usafiri kutokana na gharama nafuu, ufanisi na ratiba za kuaminika, jambo linalovutia abiria wengi.
Katika siku za karibuni, Shirika la Reli Tanzania (TRC) liliripoti kuhudumia abiria 366,000 tangu treni hiyo ilipoanza kutoa huduma kwa njia za Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.
Idadi hii imezidi matarajio ya awali na makadirio yanaonesha idadi ya abiria inaweza kufikia au kuzidi milioni moja katika miezi ijayo.
Uimara na ushawishi huo wa usafiri wa njia ya reli ya kisasa, haujawa tishio kwa wadau wa usafiri wa anga, wanaoonyesha matumaini ya kuimarika pia na kuwapa abiria fursa ya kuwa na machaguo ya aina ya usafiri.
Tishio la athari katika usafiri wa anga kama matokeo ya uimara wa SGR, linathibitishwa na mmoja wa abiria aliyeomba hifadhi ya jina lake, anayesema ndege aliyopanda Jumamosi usiku kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, kulikuwa na abiria 10 pekee.
Hilo lilimpa wasiwasi kwa kile alichoeleza, kuna uwezekano safari hizo zikapotea, kwa kuwa, kwa kawaida ni hasara kwa ndege kupakia abiria chini ya 50.
“Ingawa SGR inaweza kutoa changamoto, hasa kwa abiria wa daraja la juu ambao kwa kawaida hushika nafasi zao mapema, haipaswi kuonekana kama mbadala wa moja kwa moja wa safari za anga,” alisema.
Aliongeza kuwa mashirika ya ndege yanayohudumia maeneo kama Dodoma yanapaswa kufikiria kuratibu ratiba zao na huduma za treni ili kudumisha faida.
Wasiwasi wake unaakisi suala pana zaidi, hasa mabadiliko yanayoweza kutokea ya abiria wa daraja la juu kutoka kwenye ndege kwenda kwenye treni.
Mabadiliko haya yanaweza kuwa changamoto kwa mashirika ya ndege, hasa katika njia maarufu kama ya Dodoma-Dar es Salaam, ambapo ndege huwa zimejaa lakini sasa zinakabiliwa na ushindani kutoka kwa huduma ya treni.
“Iwapo SGR itaendelea kuwa na ufanisi wa hali ya juu, huenda kukawa na kupungua kwa safari za ndege kwenda Dodoma kwani abiria wengi watapendelea kutumia treni. Tofauti kati ya kusafiri kwa treni na ndege ni ndogo, na urahisi unaotolewa na treni za umeme unaweza kuathiri usafiri wa anga,” aliongeza.
Ingawa kwa abiria huyo ni wasiwasi, mtaalamu wa usafiri wa anga, John Njawa kwake ni matumaini, akipendekeza SGR inapaswa kuangaliwa kama nyongeza ya safari za anga badala ya kuwa mshindani wa moja kwa moja.
Hata hivyo, anasema kuanzishwa kwa SGR kunaweza kubadilisha mwamko wa abiria kwa muda, lakini haiwezekani kuathiri moja kwa moja usafiri wa anga, akisisitiza njia zote za usafiri zinaweza kuishi pamoja.
“Watu wana ladha tofauti na inahusu tabia ya wateja. Kitu kipya kinapotokea, watu wanataka kukijaribu,” alisema.
Njawa alikubali kuwa sekta ya usafiri wa anga hatimaye itaweza kuendana na kuwepo kwa SGR.
“Patakuwa na athari, hasa kwa muda mfupi, lakini hazitakuwa endelevu kwa muda mrefu. Ninaona huduma ya SGR kama nyongeza ya sekta ya usafiri wa anga badala ya mshindani wa moja kwa moja,” alisema.
Mtaalamu mwingine wa usafiri wa anga na mkufunzi, Juma Fimbo anaamini SGR ambayo bado iko katika hatua za mwanzo, haijawa changamoto kwa mashirika ya ndege.
Anaeleza huduma za reli hazina sera kamili za kushughulikia ucheleweshaji na usumbufu mwingine mdogo, maeneo ambayo mashirika ya ndege yameanzisha mikakati thabiti ya huduma kwa wateja.
“Kwa sasa hakuna ushindani halisi kati ya SGR na ndege; wako kama marafiki. Kuna uwezekano wa abiria kuchanganya safari za ndege na safari za SGR kwa usafiri wa ndani. Sekta zote mbili zinaweza kushirikiana kuboresha uzoefu wa usafiri,” alisema Fimbo.
Anaona uwezekano wa ushirikiano wa baadaye mashirika ya ndege na SGR yanaweza kuwa na huduma za pamoja za tiketi na kugawana mapato, hivyo kuzinufaisha sekta zote mbili.
Mtazamo huo, unaungwa mkono na Nahodha wa ndege, Philemon Kisamo anayesema abiria wengi kwa sasa wanapendelea SGR kwa sababu ya bei nafuu ukilinganisha na tiketi za ndege.
Mara kwa mara za safari za SGR kila siku zinatoa urahisi kwa wasafiri wa muda mfupi, kama wale wanaosafiri kibiashara.
“Ingawa mabasi yaendayo mikoani yanaweza kutoa nauli za chini zaidi, SGR ni ya kasi zaidi na abiria wanathamini uratibu wake wa muda. Ningeshauri SGR kudumisha kiwango hiki cha huduma,” alisema.
Meneja wa masoko na mawasiliano ya ushirika wa Precision Air Tanzania, Hilary Mremi anasema badala ya kuiona SGR kama tishio vema itazamwe kuwa fursa.
Anasema itazamwe kama fursa itakayoyafanya mashirika ya ndege kuboresha huduma zao; “Kwa kuboresha ubora wa usafiri wa anga, mashirika ya ndege yanaweza kuendelea kutoa sababu zinazovutia kwa abiria kuchagua ndege badala ya treni.”
“Tunaona SGR kama changamoto chanya ambayo itatusukuma kuboresha huduma zetu, na kuzifanya kuvutia zaidi kwa abiria, hasa ukizingatia muda mfupi wa safari za ndege ukilinganisha na treni,” alisema Mremi.
Aliongeza athari za SGR ni ndogo kwa sasa na idadi ya abiria bado inabadilika akitoa mfano; “Safari za ndege kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam huwa zimejaa siku za Ijumaa, na kupungua kwa abiria siku za Jumamosi si jambo geni.”
Kama sehemu ya kukabiliana na athari za SGR, Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) kimetangaza mipango ya kuendeleza mikakati ili kuendelea kushindana, ikihusisha kuhamisha mitaji yao katika maeneo mengine ya uwekezaji.
Katibu Mkuu wa Taboa, Joseph Prisicus alibainisha chama hicho kinaangalia namna ya kukabiliana na changamoto hiyo, ikiwemo kuomba msamaha wa kikodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na kupungua kwa shughuli za mabasi.
“Hatuwezi kupinga maendeleo ya reli. Kuna faida nyingi kama abiria wataishia Dodoma na kuna mabasi ambayo yatawachukua kwenda maeneo mengine. Kwa kuwa sisi sote ni walipakodi, Serikali inapaswa kuangalia jinsi ya kuwasaidia wamiliki ili wote wanufaike,” alisema.
Prisicus aliongeza Taboa inachunguza athari kwenye ajira na mitaji ya wawekezaji na inaweza kurekebisha shughuli zao kulingana na matokeo ya uchunguzi.
Kuanzishwa kwa SGR kumesababisha baadhi ya wamiliki wa mabasi kupunguza safari zao.
Kwa mfano, kampuni iliyokuwa ikifanya safari 20 kwa siku kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro sasa imepunguza hadi safari tisa au 10 kwa siku. Kupungua huku kwa huduma kuna athari kwa malipo ya kodi na uendelevu wa uendeshaji.
Kadiri SGR inavyoendelea kuimarika na kupanuka, uhusiano wake na sekta ya usafiri wa anga unaweza kubadilika.
Ingawa kuna wasiwasi kuhusu ushindani, wataalamu wanakubaliana kwamba kuna fursa ndani yake.
|
Wakati Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na wadau wengine wakisisitiza uchunguzi huru dhidi ya m
|
Wakati Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na wadau wengine wakisisitiza uchunguzi huru dhidi ya matukio ya utekaji na mauaji, Serikali imesema kwanza jamii inapaswa kujiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila unapokaribia uchaguzi.
Katika hoja yake hiyo, Serikali imesema ni rahisi kutupa lawama kwa Jeshi la Polisi juu ya matukio hayo, huku ikieleza badala ya kufanya hivyo ni vema wananchi waanze kutafuta jawabu la kwanini yanatokea kila unapokaribia uchaguzi.
Wito wa uchunguzi ndiyo unaoonekana kubeba matamanio ya wadau wengi juu ya matukio hayo, wengine wakitaka ufanywe na tume ya kijaji, wapo wanaopendekeza mamlaka za nje ya Tanzania, kadhalika kuna lile kundi linalotaka polisi waifanye kazi hiyo.
Kila aina ya uchunguzi unaopendekezwa na wadau, unajengwa kwa msingi wa hoja, wanaotaka uchunguzi kutoka mamlaka ya nje wanadai hawana imani na vyombo vya ndani kuifanya kazi hiyo.
Lakini wale wanaotaka tume ya kijaji, wanaijengea hoja kuwa, ina uhuru zaidi wa kutekeleza jukumu hilo, hivyo watakaobainika watakuwa wahusika halisi, huku wale wanaotaka Polisi wakisema bado jeshi hilo halina udhaifu katika kuifanya kazi hiyo hivyo lipewe uhuru wa kuifanya.
Chumbuko la yote hayo ni mfululizo wa matukio ya kupotea, kutekwa na kuuawa kwa raia kulikotokea katika siku za karibuni na hivyo kuibua taharuki.
Tukio la mwisho lililoamsha hisia za wengi ni la kada wa Chadema, Ali Kibao aliyekamatwa Septemba 6, mwaka huu akiwa katika usafiri wa umma na siku moja baadaye mwili wake ukaokotwa Ununio jijini Dar es Salaam akiwa amefariki.
Hatua hiyo ilisababisha Chadema itake Serikali kuwatoa watu wote waliopotea kufikia Septemba 21 na isipofanya hivyo wataandamana kuanzia Septemba 23, katika Jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo, tayati Jeshi la Polisi limeshapiga marufuku juu ya maandamano hayo.
Kauli hizo za Bakwata na Serikali zimetolewa leo, Septemba 16, 2024 na Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Nuhu Mruma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa walipohutubia Baraza la Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) mkoani Geita.
Msimamo wa Bakwata
Katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa Bakwata, Nuhu Mruma amesema baraza hilo linaungana na Rais Samia Suluhu Hassan kulaani vitendo hivyo na wanavitaka vyombo vya ulinzi na usalama vifanye uchunguzi huru kubaini wale wote waliojitokeza kufanya uhalifu huo.
“Viende mbali zaidi (vyombo vya ulinzi na usalama) na kujua dhamira yao ni nini ili kutafuta ufumbuzi na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria,” amesema.
Amewasihi wanaofanya uchunguzi huo kutofanya upendeleo au kumkandamiza yeyote bali haki itendeke bila kujali itikadi za wanaofanya unyama huo.
“Tunaomba wananchi kuwa mabalozi wazuri wa kulinda na kutunza amani yetu na kutokubali kutumika na yeyote kwa maslahi binafsi katika kuvuruga amani yetu,” ameeleza.
Waziri Mkuu
Kwa upande wa Majaliwa amesema badala ya kutupa lawama kwa jeshi la polisi ni vema kujiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia uchaguzi.
Kwa mujibu wa mtendaji mkuu huyo wa Serikali, tangu awamu ya tatu hadi ya sasa ya serikali matukio kama hayo hutokea, lakini swali linabaki kuwa kwanini kila unapokaribia uchaguzi.
“Rais alitoa karipio juu ya yanayotokea matukio haya ambayo yanatokea kila kipindi fulani lazima tujiulize kwanini yanajitokeza hasa inapokaribia chaguzi nani anafanaya ni rahisi kusema polisi, lakini muhimu tukatafakari kwanini wakati huu na nani anafanya,” amesema Majaliwa.
Katika mazingira hayo, amesema mafanikio ya ulinzi wa taifa hayatfanikiwa kwa kuwategemea polisi pekee, badala yake kila mwananchi awajibike kuifanya kazi hiyo.
Ameijenga hoja yake hiyo kwa kurejea mwaka 2021, akisema kulikithiri matukio hayo mkoani Mtwara na Rais Samia aliunda tume ambayo matokeo yake ikawa ni kuundwa kwa Tume ya Haki Jinai.
Kwa sababu mkuu wa nchi ameshaelekeza, Majaliwa amesema Watanzania wanapaswa kuiamini Serikali kwa kuwa iko macho na imara.
Amesisitiza Serikali haitafumbia macho wanaochokoza taifa kwa matukio ya utekaji na mauaji, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao, huku akiwataka wananchi waendelee kuwa na imani.
Katika nyakati hizo, amesema yeyote atakayeona viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo awe mstari wa mbele kutoa taarifa, kwani kinachohitajika sasa ni ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, amewataka wazazi na viongozi wa dini kutimiza wajibu wao katika malezi ya watoto ili taifa liwe sehemu salama.
“kila mmoja anao wajibu iwe taasisi za elimu au dini moja kati ya ajenda muhimu ni kuhamasisha Watanznaia kulea jamii katika maadili mema ili kuepuka maovu yote,” amesema Majaliwa.
Amesema viongozi wa dini wana jukumu la kuhamasisha maadili kwa jamii, huku wazazi wakiwa na wajibu wa kulea watoto kuanzia ngazi ya familia ili wawe na maadili.
Mufti wa Tanzania, Abubakar Zuber amewataka Waislamu kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa, huku wakiweka elimu mbele na kuilinda amani.
Katika hotuba yake hiyo, amesisitiza umuhimu wa maadili kwa mtu mmoja mmoja, akisema mwonekano wako unatosha kutafsiri wewe ni muadilifu kiasi gani.
“Unakut mtu mzima mwanaume anavaa bukta anazurura huku na kule anashangaa tunamcheka. Tunamcheka kwa sababu amevaa vazi lisilopaswa kuvaliwa naye,” amesema.
Sambamba na hayo, amesisitiza tabia za kujidhuru na kudhuru wengine ni kinyume na matakwa ya dini ya Kiislamu na maelekezo ya Mtume Muhammad.
Amesema yeyote anayefanya hivyo kwa mujibu wa vitabu vitakatifu anakuwa amekiuka maelekezo ya Mungu na Uislamu unamkataa.
Baadhi ya waumini wakizungumzia matukio ya utekaji nchini wamesema yanayotokea sasa ni ishara ya kuwa watu wameacha kumwamini Mungu na kuamini ushirikina.
Wamesema ni jukumu la viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu ya dini ili watu wamrudie Mungu.
Jumapili Hussein amesema watu wamehamisha imani zao kutoka kwenye imani ya dini na kuamini ushirikina, ndio chanzo cha mauji na matukio mabaya yanayoshamiri nchini kwa sasa.
|
Hisia na mitazamo tofauti imeibuka juu ya sheria inayomtaka mama kuacha wazi eneo linalopaswa kuandi
|
Hisia na mitazamo tofauti imeibuka juu ya sheria inayomtaka mama kuacha wazi eneo linalopaswa kuandikwa jina la baba wa mtoto katika cheti cha kuzaliwa, iwapo mzazi huyo wa kiume hajulikani au kuna sababu za kutoandikwa.
Mitazamo hiyo inakuja ikiwa ni siku moja tangu Mwananchi Digital iliporipoti kuhusu takwa la mama kuacha eneo la jina la baba huyo au aandike ‘hajulikani’ badala ya kutumia ubini wa mzazi asiye asilia wa mtoto.
Msingi wa habari iliyoripotiwa na Mwananchi Digital ni maneno ya Ofisa Usajili wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Joseph Mwakatobe aliyesema ni vema kuacha wazi kuliko kuandika jina la baba bandia, akisisitiza ni kosa kisheria.
Wakili Kiongozi wa kampuni ya Uwakili ya Haki kwanza, Alloyce Komba ni miongoni mwa walioibukia kwenye mjadala huo, akiunga mkono kauli ya Rita kwa kueleza aliyetoa jina bandia na mwenye jina hilo wanaweza kuingia matatani kama baba asilia wa mtoto ataamua kufuata sheria.
Kwa mujibu wa Komba, sheria pia itamlinda mama, endapo ataamua kudai matunzo ya mtoto kwa baba asilia ambayo aliyatoa kwa mtoto katika kipindi chote ambacho alimlea peke yake.
"Itaandikwa baba hajulikani hadi pale wazazi watakapomaliza tofauti zao watakwenda kubadilisha au mama atumie busara kuandika ubini asilia wa baba mzazi wa mtoto tangu mwanzo hata kama hamtunzi, kisha akamshatiki kwa kutomtunza mtoto wake lakini akibainika ameandika jina tofauti na la baba mzazi ni kosa kisheria na ataingia matatani yeye (mama) na huyo baba bandia," anasema wakili Komba.
Anasema wapo watoto wengine pia anapokuwa mkubwa na kufahamu ubini anaotumia si wa baba yake asilia, anakwenda kubadilisha kwa kiapo ili kuwa na utambulisho wake sahihi.
"Hivi vitu vinafanyika sema watu huwa hawavizingatii tu, mama anapoandika ubini tofauti na wa baba mzazi, baba halisi asijue au asifuatile hilo si tatizo, lakini akijua na kwenda kushtaki Mahakama akijiridhisha ni kweli, anashinda hata kama hakuwa akimhudumia mtoto wake," anasema.
Hata ukimbadilishia mtoto ubini, Wakili Komba anasema haimuondolei baba halali uhalali wa kumchukua mwanawe atakapohitaji, sheria inamlinda.
"Suala sio huduma, baba mzazi ni yupi? mama anatakiwa amshtaki baba ambaye hatunzi mtoto mapema, sio kuamua kubadili ubini wa mtoto, hilo ni kosa kisheria,” anasema.
Anasema baba kumtunza mtoto wake ni suala la kisheria na sheria ya mtoto ya mwaka 2019 imeeleza wazi kuwa baba mzazi ana wajibu wa kutoa matunzo.
"Ikitokea hamtunzi na wewe mama umekaa kimya na ukampa ubini wa baba wa kufikia, fanya hivyo baba mzazi asijue, ikitokea amejua wewe mama na huyo baba wa kufikia wote mtakuwa matatani.
"Hata ukimpa ubini wa ujombani, bado utakuwa matatani kwani huwezi kuzaa na ndugu yako, hiyo sio sawa, kisheria baba mzazi ndiyo baba asilia anayetambulika bila kujali hamtunzi mtoto na akienda Mahakamani akamdai mtoto wake, Mahakama ikithibitisha atamchukua mtoto wake,” anasema.
Anasema baba huyo anaweza kunyimwa mtoto huyo kulingana na mazingira, Mahakama itaangalia yupo katika mazingira mazuri ya kumlea huyo mtoto au la?.
"Ikionekana mazingira ya mama yako vizuri zaidi, Mahakama ndiyo itasema kweli mtoto ni wako, lakini mazingira yako ya kumlea si rafiki hivyo ataendelea kulelewa na mama," anasema.
Wakili Komba anasema kinachozingatiwa ni maslahi ya mtoto, ambaye atapewa haki ya kuzungumza iwapo hamfahamu yule baba (mzazi) alilelewa na mama pekee au vinginevyo.
“Mashauri yoyote kuhusu mtoto kipimo kikubwa ambacho Mahakama huwa inakizingatia ni maslahi ya mtoto, kama mwisho wa siku baba mzazi atapewa mtoto, mama ana uwezo wa kudai gharama zote ambazo amezitumia kwenye matunzo na baba atazilipa ili achukue mtoto wake. lakini yote hayo hayamuondolei haki ya ubini kwa mtoto, kama ndiye baba mzazi ana haki bila kujali malezi," anasema wakili Komba.
Viongozi wa dini
Matumizi ya majina bandia ya baba si Rita pekee, hata katika Kitabu cha Quran inakataza hilo, kama inavyoelezwa na Kadhi wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Ramadhan Kitogo.
"Haitakiwi kumpa jina la ujombani, babu au baba wa kufikia mtoto, ikitokea baba na mama mmetengana. Quran inasema mwanamke akaichana na mumewe na ndani ya tumbo lake ana ujauzito wa mwezi mtu hawezi mjua, asifiche kile kilichomo ndani tumbo lake hata kama yule aliyekuwa amemuoa hampendi na anamchukia,” anasema.
Anasema haipaswi kumuunganisha mtoto na nasaba isiyo yake, na Mtume ametamka Mwenyezi Mungu umlaani afanyaye hivyo, Uisilamu ukielekeza watoto waitwe kwa majina ya wazazi wao.
"Kufanya kinyume ni jambo baya na tunalikemea na mwenye maadili mazuri hawezi fanya kitu kama hicho," anasema Sheikh Kitogo.
Mchungaji Daniel Sendoro wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Daniel Sendoro anasema suala la majina japo halina nguvu katika dini, lakini kuna athari pale mtu anapopewa jina tofauti na la baba yake.
"Kwa mtoto atakapokuwa mkubwa inaweza kumharibu kisaikolojia, jina ndilo limebeba utambulisho wake, kama ni Sendoro wewe ukamuita Makongoro akiwa mkubwa utamletea shida huyu mtoto na ataanza kutafuta utambulisho wake," anasema mchungaji Sendoro ambaye pia ni mwanasaikolojia.
Anasema huyo mtoto ipo siku ataambiwa baba yako sio yule, hao waliokupa hilo jina ni wajinga tu na mambo kama hayo, moja kwa moja ataanza kujiona asiyemkamilifu kwani moja ya vituvinafanya mtu kuwa mkamilifu ni utambulisho wake.
"Akijua jina alilonalo sio la utambulisho wake, ataanza kujioa sio wa huku ni wa kule, itamvuruga kisaikolojia na kutaka kumjua baba yake.
"Hivyo tuwaombe wazazi kina mama wawape majina ya utambulisho halisi watoto wao, labda kuwe na sababu za kiusalama uenda umezaa na askofu au padri, uliamua kuutoa mwili wako sadaka ukabeba mimba ndipo utandika ubini tofauti, lakini huko mbele ya safari mtoto aambiwe ukweli," anasema.
Mitazamo ya wengine
Katika mtandao wa kijamii wa Instagram ya Mwananchi, suala hilo liliibua mjadala mkali huku baadhi ya watu wakipinga na wengine wakitaka watoto wasiingizwe kwenye ugomvi wa wazazi.
Segito Mgonanzi alisema maumivu ya mtoto kukataliwa na baba yake ni makali mno na mama mzazi ndiye anayafahamu.
"Watuache tu tuandike tunavyojua, lakini hamjui maumivu ya kuandika un known yapoje kwa mtoto,” aliandika.
Shayo Luicensi yeye alisema kuandika jina la babu wa mtoto haisaidii akisema ni bora kuandika jina la baba halisi hata kama hamhudumii.
sibuma_binadamu anaona ni vema ugomvi wa wazazi ubaki baina yao, lakini usiathiri jina na ubini wa mtoto kwa namna yoyote.
Kwa mtazamo wa mgendison, Rita iishirikiane na madawati ya jinsia kutoa elimu na kuwakumbusha wazazi wajibu.
Ingawa Rita imeweka wazi kuhusu hilo, lakini ilikuwa vigumu kwa nely_qeuty yeye kukubali kuweka ubini wa baba asiyehudumia mimba.
|
Kutokana na kuongezeka kwa mwamko wa abiria kutumia usafiri wa treni ya umeme (SGR), wamiliki wa mab
|
Kutokana na kuongezeka kwa mwamko wa abiria kutumia usafiri wa treni ya umeme (SGR), wamiliki wa mabasi nchini wamekuja na mikakati mipya kuhakikisha wanaendelea kuwa sokoni bila biashara zao kuathirika.
Tangu kuanza kwa usafiri huo, wamiliki wa mabasi wamekuwa wakilalamikia changamoto katika soko na tayari wengine wameanzisha safari mpya katika njia zisizo na reli ya kisasa.
Makampuni kama Kimbinyiko, BM Coach, Abood na Shabiby tayari zimeanza kupanua huduma katika maeneo mapya, ikiwemo Sumbawanga, Bukoba, Musoma na hata nchi jirani ya Kenya.
Hatua hizi zinalenga kurejesha sehemu ya soko na kudumisha shughuli zao za usafirishaji licha ya mabadiliko makubwa katika sekta ya usafiri.
SGR, ambayo ilianza kutoa huduma hivi karibuni, imevutia wananchi zaidi, ikiwa na zaidi ya abiria 7,000 wanaosafiri kwa siku kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.
Ufanisi na mvuto wa mtandao huo wa reli umesababisha kupungua kwa idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi kwa njia ya barabara.
Hata hivyo, wamiliki wa mabasi wamesema, licha ya treni kuchukua soko katika njia zilizozoeleka, haitakuwa shida kwao, kwa kuwa Tanzania ni kubwa.
Tanzania ina eneo la kilomita za mraba 945,087, ikiwa ni kubwa zaidi kuliko Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda kwa pamoja.
Eneo la nchi hizo nne lina ukubwa wa kilomita za mraba 877,852, huku Kenya na Uganda zikichukua sehemu kubwa zaidi ya kilomita za mraba 582,646 na 241,038, mtawalia.
Kuwepo kwa mipaka na nchi saba, ambapo nchi mbili kati ya hizo hazina bahari na zinategemea bandari za Tanzania kwa biashara za kimataifa, kunatoa fursa kwa wamiliki wa mabasi kutumia fursa hiyo.
Akizungumza na gazeti hilo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Kimbinyiko, Ferdinand Mabumo alisema tayari kampuni yake ilishaanzisha njia nne mpya ili kuendana na soko linalobadilika.
"Tumepunguza safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma kutoka safari 10 hadi nne kwa siku," alisema.
Njia mpya sasa ni Dodoma-Arusha, Arusha-Mbeya, Dodoma-Njombe na Moshi-Mbeya. Mipango ya baadaye ya kampuni hiyo ni kupanua huduma hadi Nairobi, Kenya.
Meneja wa Kampuni ya Mabasi ya Shabiby, Edward Magawa alisisitiza umuhimu wa kupanua maeneo ya huduma.
“Tanzania ni kubwa ingawa bado kuna mahitaji ya safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma, tumejikita katika njia mpya kama vile Dodoma-Sumbawanga, Dodoma-Bukoba na Dodoma-Musoma,” alisema.
Shabiby pia imeagiza mabasi mapya yanayotarajiwa kufika katikati ya Oktoba ili kutumika katika njia hizo mpya.
BM Coach imeanzisha huduma za kuvuka mipaka, ikizindua njia mpya kati ya Dar es Salaam na Nairobi tangu Septemba 4, mwaka huu.
"Kwa sasa tupo kwenye majaribio na tuna mipango ya kupanua hadi Kampala na Rwanda," alisema Meneja wa Operesheni wa BM Coach, Gabriel Makundi.
Kampuni hiyo itaendesha safari nne kwa siku kwenye njia hiyo na inafikiria kuongeza njia ya Dar es Salaam-Tunduma hivi karibuni.
Kabla ya kuanza kwa SGR, BM Coach ilikuwa ikiendesha hadi mabasi 22 kwa siku kwenye njia ya Dar es Salaam-Morogoro na mabasi 10 kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa usafiri wa reli, sasa ni mabasi sita tu yanayofanya safari kati ya Dar es Salaam na Morogoro na manne kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
Licha ya changamoto zinazotokana na SGR, wamiliki wa mabasi nchini wanatumia uwezo wao wa kubadilika na kupanua njia zao ili kuhakikisha wanaendelea kuwa sehemu muhimu ya mtandao wa usafiri nchini.
BRT kama mbadala
Wamiliki wa mabasi wamesema wako tayari kuwekeza kwenye mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) endapo maboresho yatafanywa katika ukusanyaji wa nauli na mikataba ya uendeshaji.
Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) kinahimiza ushiriki zaidi katika mfumo wa BRT ili kuendeleza biashara zao huku mtandao wa reli ukiendelea kubadilisha sekta ya usafiri.
Katibu Mkuu wa Taboa, Priscus Joseph aliliambia gazeti hili kuwa, mazungumzo na Wakala wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart) yalifanyika mwaka 2022.
Katika mazungumzo hayo, wamiliki wa mabasi walipendekeza kununua mabasi ya kuendesha ndani ya mfumo wa BRT lakini bado hawajapata mrejesho.
“Tulipendekeza turuhusiwe kuwekeza kwenye mabasi huku serikali ikibaki na miundombinu, lakini bado hatujapata majibu,” alisema.
Mradi wa BRT, unaotekelezwa kwa awamu sita, umekumbwa na changamoto za kimuundo.
Awamu ya Kwanza ya BRT, iliyoanza mwaka 2016, ilikusudiwa kuendeshwa kwa mabasi 305 lakini kwa sasa yanafanya kazi mabasi 210 tu, huku mengi yakiwa yameharibika.
Awamu ya Pili ya BRT, iliyokamilika Oktoba mwaka jana, inasubiri kuwasili kwa mabasi mapya.
Mapema mwezi huu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa aliitaka Dart na Udart kushirikiana kuwaingiza waendeshaji wa mabasi ya mikoani kwenye mfumo wa BRT ili kuboresha huduma za abiria badala ya kusubiri wawekezaji kutoka nje.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi na mageti ya kisasa kwenye vituo vya BRT Dar es Salaam, Mchengerwa alisema kuanza kwa huduma za treni za umeme kwenye SGR kumeathiri baadhi ya waendeshaji wa mabasi ya mikoani.
Kwa hivyo, ingefaa kuangalia uwezekano wa mabasi hayo kufanya kazi ndani ya mfumo wa BRT.
“Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu suala la mabasi. Awamu ya Kwanza ya BRT bado inahitaji mabasi 170 ili ifanye kazi kwa ufanisi, na mabasi 500 yanahitajika ili kuanza kazi kwa Awamu ya Pili ya BRT kwenye njia ya Mbagala. Hakikisheni mabasi yananunuliwa kufikia Desemba mwaka huu,” alisema.
Mchengerwa alisema; “Wamiliki wa mabasi ya mikoani, ambao wamekuwa wakisafirisha abiria kwa miaka mingi, wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi katika njia za BRT. Kwa hivyo, wito unatolewa kwa waendeshaji wa ndani kuwekeza kwenye BRT badala ya kusubiri wawekezaji wa kigeni.”
Kwa upande wake, Makundi alisema ingawa wamiliki wa mabasi wako tayari na wanataka kutumia fursa hiyo, kuna haja ya uwazi zaidi kwenye mchakato wa zabuni kwa ajili ya uendeshaji wa mabasi ya BRT.
“Tangazo rasmi la zabuni linapaswa kutolewa ili kuainisha vigezo vinavyohitajika kwa mabasi ya mikoani kushiriki kwenye mfumo wa BRT,” alisisitiza.
Magawa wa Shabiby alisema kampuni yake iko tayari kuwekeza kwenye BRT lakini akatoa wito wa kufanyika mapitio ya nauli na mazingira bora ya uwekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Dart, Athumani Kihamia alikiri mazungumzo ya mwaka 2022 na wamiliki wa mabasi lakini alieleza kuwa hawakuafikiana.
“Tuna mpango wa kushirikisha waendeshaji zaidi ili kuelezea maendeleo yetu na kushughulikia masuala yanayowakabili,” alisema.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Taboa, Mustapha Mwalango alibainisha kupungua kwa idadi ya abiria na kuongezeka kwa mabasi yasiyo na kazi.
“SGR imeathiri shughuli zetu kuliko tulivyotarajia awali,” alisema.
Mkuu wa Mawasiliano wa Latra, Salum Pazzy alishauri wamiliki wa mabasi kuiona SGR kama fursa badala ya tishio.
Alibainisha SGR ikitumika vema, kutakuwa na ongezeko la mahitaji ya mabasi kusafirisha abiria kutoka Dodoma kwenda mikoa mingine.
Mkurugenzi wa Usafiri wa Barabara wa Latra, Johansen Kahatano alithibitisha kupungua kwa huduma za mabasi.
“Tafiti zetu zinaonyesha kupungua kwa safari za mabasi na idadi ya abiria tangu SGR ilipoanza. Tunafanyia kazi kutatua athari hizi,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, Latra inapanga kuandaa mkutano wa wadau wa usafiri, waendeshaji wa mabasi na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili kuchunguza njia za kuboresha muunganiko wa usafiri na kupunguza gharama za nauli kwa abiria.
Mkutano huo utalenga kutafuta suluhisho na kuboresha ushirikiano kati ya huduma za mabasi na treni, hususan karibu na vituo vya SGR.
Kadri sekta ya usafiri inavyoendelea kubadilika, wamiliki wa mabasi wana matumaini kwamba ushirikiano zaidi na mipango madhubuti itawezesha kuendelea kutoa huduma muhimu za usafiri nchini.
|
Licha ya Jeshi la Polisi kupiga marufuku maandamano ya Chadema, chama hicho kimesema kitu pekee kita
|
Licha ya Jeshi la Polisi kupiga marufuku maandamano ya Chadema, chama hicho kimesema kitu pekee kitakachositisha mpango huo ni jeshi hilo kuwarejesha viongozi wote waliotekwa wakiwa hai au wafu.
Mpango wa maandamano ulitangazwa Septemba 12 na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kushinikiza kurudishwa kwa viongozi wake waliotekwa.
Kabla ya maandamano hayo, Mbowe alitoa hadi Septemba 21, mwaka huu, Serikali iwe imeshawarejesha viongozi hao na kinyume na kulitekeleza hilo, Septemba 23, wataandamana jijini Dar es Salaam.
Siku moja baada ya tangazo hilo la Chadema, jeshi la polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilipiga marufuku maandamano hayo, likizuia wanachama na wafuasi kusafiri kutoka maeneo mbalimbali kwenda kushiriki tukio hilo.
Kutokana na hali inayoendelea, wadau wameikosoa marufuku ya polisi wakisema ni mapema sana kuzuia, walipaswa kuacha ili waone iwapo chama hicho kitafuata utaratibu au vinginevyo.
Lakini, wengine wameonyesha mashaka na marufuku hiyo, wakisema inawezekanaje Chadema hao hao waliruhusiwa kuandamana katika majiji makubwa nchini na sasa wanazuiwa.
Kauli ya wadau
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fulgence Massawe amesema kwa sasa jeshi la polisi linapaswa kusubiri hadi tarehe ya maandamano ndipo litoe kauli.
Sababu ya kusubiri huko, amesema ni kuona iwapo Chadema itafuata utaratibu kabla ya kufanya maandamano au hapana.
Lakini, ameeleza kilichofanywa na jeshi la polisi kupiga marufuku kabla hata ya kujua iwapo Chadema watafuata utaratibu wa kutoa taarifa kwa mamlaka husika, si sawa.
“Jeshi la polisi lilipaswa kusubiri hadi muda ufike ndipo waseme lolote, hawakupaswa kuingilia kati kabla hawajajua kama Chadema watakiuka utaratibu au hapana,” amesema.
Kwa sababu kuandamana na haki ya kikatiba kwa kila mtu, ameeleza hakukuwa na sababu ya kupiga marufuku hasa ukizingatia chama hicho kinazo hoja kinazozishinikiza kupitia maandamano hayo.
“Chadema wana haki ya kuandamana hasa kwa hoja waliyonayo na ukizingatia Katiba inaruhusu kuandamana. Chadema walifanya maandamano ya amani na yalikwenda vema haijulikani kwa sasa nini kimebadilika hadi polisi wanapiga marufuku,” amesema.
Wote wafuate sheria
Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki Taarifa, John Kitoka amesema pande zote mbili kwa Chadema na Jeshi la Polisi wanapaswa kuheshimu sheria na Katiba ya nchi.
“Maamuzi ya Chadema yako ndani ya Katiba na maandamano yao yanatakiwa kulindwa na kuhakikishiwa usalama na kama kutakuwa na vihatarishi vya uvunjivu wa amani kama wanavyodai Polisi wanapaswa kushughulika navyo na si kuzuia haki ya watu kuandamana,” alisema
Kitoka katika maelezo yake amedai iwapo Polisi wataenda nje kwa kuzuia maandamano hayo watakuwa wanavunja haki ya watu ya kukusanyika na kupashana habari.
“Chadema wanahaki ya kufanya hivyo kutokana na matukio kadha wa kadha yaliyojitokeza ya watu kutekwa,utesaji na uaji wa raia wasiokuwa na hatia,”alisema
Alisema sababu walizotoa Polisi kuzuia maandamano ni kuibua hasira kwani bado hazina mashiko na kwa nyakati tofauti wamekuwa wakidai hali ni shwari.
“Ukirejea maamuzi ya Rais kupitia mtandao wake wa kijamii wa X ni kwamba hali ya usalama si shwari na akaagiza uchunguzi ufanyike ili apate ukweli kuhusu yanayotokea," alisema
Kitoka alisema hata Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi alitoka hadharani hawakubaliani na matukio ya utekaji na mauaji yanayojitokeza.
“Polisi wanaonyesha hakuna shida lakini wakati huohuo wanaona kuandamana kama ni uvunjivu wa amani, chadema wanaandama kwakuwa matukio yanayojitokeza Polisi walipaswa kuzuia,” alisema.
Mwanaharakati, Gemma Akilimali alisema jeshi la Polisi linapaswa kujisahihisha.
“Katika kujisahisha wanapaswa kuangalia watendaji wao inawezekana walioingia ni majangili lakini wameingizwa kama walikuwa na hiyo tabia hawawezi kuacha ya kumtisha mwananchi," alisema
Alisema sheria inalitaka jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi na usalama wa mali za raia na maandamano wanayotaka kufanya Chadema yanapaswa kulindwa ili kuondoa dhana tofauti kwa wananchi.
“Jeshi la Polisi kupinga inaibua maswali mengi, kwanini unapinga inawezekana kuna ukweli ndiyo maana wanataka wasiandamane kama ndivyo kwanini wazuie basi wanajua makosa yao na wanaona kama yanalipuliwa,”alisema
Alisema maandamano ni haki ya wananchi huku akieleza kinachoendelea nchini Polisi hawataki hata kujenga utamaduni wa kujielimisha ni kiasi cha kusema kama wanataka kuandamana basi wataimarisha ulinzi.
“Polisi hawana haki ya kuzuia maandamano kwa sababu wenzao wanasababu na si shida za wanachadema pekee bali ni tatizo lilolifika Taifa nzima sasa wanataka wananchi wote wanyanyuke,” alisema
Alisema maandamano hayo hayapaswi kuzuiwa kwa sababu yanalenga kuwabeba wale wote walioumia na matatizo yanayolikumba taifa kwa waliotekwa,kuteswa na kuawa na ndugu au watu wao wa karibu.
Msimamo wa Chadema
Kitu pekee kitakachosimamisha maandamano ya Chadema ni Serikali kuwarudisha viongozi wao waliotekwa wakiwa hai au wafu na si kingine chochote, kama inavyoelezwa na Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema.
Amesema kitakachofanywa nao ni kufuata utaratibu wa kisheria unaowataka kutoa taarifa ndani ya saa 48 juu ya maandamano hayo, eneo yatakapofanyika na njia watakazopita.
“Wataosababisha maafa ni polisi sio sisi. Sisi tutafuata sheria na ikifika Septemba 21 kama polisi hawajawarejesha viongozi wetu tutaanza kuchukua hatua,” amesema.
Anasisitiza hawataogopa kutekeleza hilo kwa sababu wakiendelea kufanya hivyo, vitendo hivyo havitafika mwisho.
Hata hivyo, ameeleza hadhani kuwa chama hicho kinahitaji meza ya mazungumzo na jeshi la polisi, isipokuwa kila upande unapaswa kufuata sheria.
“Sisi kama chama hatuhitaji kupatanishwa na jeshi la polisi wao wafuate sheria na sisi tutafuata sheria hapo ndipo tutaenda vema,” amesema.
|
Usisubiri hadi kumbukumbu yake ya kuzaliwa au kumbukizi ya siku ya ndoa ‘anniversary’ kumwonyesha mk
|
Usisubiri hadi kumbukumbu yake ya kuzaliwa au kumbukizi ya siku ya ndoa ‘anniversary’ kumwonyesha mkeo thamani yake maisha mwako, unajua ipo siku rasmi ya kuadhimisha kumuenzi mke. Kwa lugha ya kimombo inaitwa ‘Wife Appreciation Day’.
Siku hiyo inayoadhimishwa Septemba 15 (leo), kila mwaka imeteuliwa kuwa maalumu kwa ajili ya kuhakikisha unamshukuru, kumsifu na kumpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya kama mke.
Andiko hili halihalalishi kumpitisha mkeo katika mitihani kwa siku zote usubiri Septemba 15 ndiyo umwonyeshe thamani yake hapana, muktadha ni kuitumia siku hii maalumu kama nyenzo ya kustawisha upendo, furaha na hali ya kuaminiana na mkeo.
Katika maisha ya ndoa ni muhimu kuonyesha thamani kwa mke wako. Hii si tu inadhihirisha kwamba unamwona na kumthamini, bali pia inaimarisha mahusiano yenu na kukuza upendo wa kweli. Haijalishi umekuwa na ndoa kwa mwaka mmoja, miaka 10 au hata 50, lazima uonyeshe mke wako jinsi alivyo na thamani kwako.
Umuhimu wa kulifanya hilo, unathibitishwa na takwimu za Taasisi ya Maendeleo ya Familia ya Afrika Mashariki za mwaka 2021, zinaoonyesha asilimia 65 ya familia zilizo na msingi wa uaminifu na kuthaminiana huwa na utulivu wa ndoa kwa kipindi kirefu zaidi kuliko zile zisizo na utaratibu huo.
Kama hiyo haitoshi, utafiti wa Chuo Kikuu cha Stanford mwaka 2018, ulibaini wanandoa walioonyesha kuthaminiana waliripoti kiwango cha juu cha furaha na kuridhika kwenye ndoa zao. Asilimia 80 ya wanandoa walioshiriki kwenye utafiti huo walisema kuthaminiana ni kiungo muhimu cha kudumisha uhusiano wa furaha.
Benki ya Dunia nayo mwaka 2020, iliweka wazi kuwa, familia zenye wanandoa wanaoheshimiana na kuthaminiana zina uwezo mkubwa wa kushirikiana kwenye maamuzi ya kifedha, jambo linalowasaidia kujenga uchumi imara.
Kwa baadhi ya wanaume, kuonyesha hisia za upendo inaweza kuwa jambo la kawaida. Lakini kwa wengine, inaweza kuwa changamoto. Si kwa sababu ya dosari ya tabia au makosa yako, bali kwa sababu baadhi ya wanaume hawapendi kuonyesha hisia zao au wanapata shida kuziwasilisha.
Tunajua hali hiyo, lakini siku ya kumuenzi mke wako inatoa nafasi bora ya kuhakikisha mke wako anajua jinsi anavyothaminiwa.
Unaweza kujifunza kuadhimisha siku hii
Kwanza kabisa mwanaume wa kweli na anayejali ndoa yake huhitaji kujua miaka ya ndoa. Badala yake anapaswa kufungua milango kwa mke wake, kumpongeza kwa busu la ghafla, kumletea maua au kutumia muda mzuri pamoja ili kumfanya ajue jinsi anavyothaminika kwake.
Siku hii inahusu kuonyesha upendo wako kwa mke wako na kuthibitisha thamani yake kwako. Mara nyingi hatutoi shukurani ya kutosha kwa wale tunaoishi nao kwa karibu, hususan wake.
Wakati umekaa na mtu kwa muda mrefu, inaweza kuwa rahisi kupuuza mambo yote wanayofanya kwa ajili yako. Iwe ni kupika chakula cha jioni au kukufanya uache tabasamu kila siku, ni muhimu kutafakari jinsi mke wako anavyochangia maisha yako na kumfanya ajue kuhusu hili.
Kununua pete kwa mke wako ni mila ya zamani sio kwa ndoa tu au uchumba, bali pia kwa maadhimisho ya miaka yenu ya ndoa. Unaweza kutumia siku hii kuhuisha ndoa yenu kwa kumnunulia pete nyingine.
Kitendo cha kutoa pete kama ishara ya upendo kilifanywa na mshairi wa Kirumi wa vichekesho aitwaye Plautus. Miaka michache baadaye, katika karne ya nne, kitendo hiki kilibadilishwa kuwa cha Kikristo.
Historia ya siku hii
Siku ya kumuenzi mke wako ni tukio la kupendeza linalowapa waume nafasi ya kuonyesha jinsi wanavyopenda na kuthamini wake zao. Tangu ilipoanzishwa, imeorodheshwa katika kalenda ya matukio ya kila mwaka ya Chase na imekuwa maarufu sana.
Kuna mambo mengi ambayo mke mwenye mapenzi na msaada hufanya kwa mume wake, na hii ni fursa kwa waume kutazama nyuma na kukumbuka mambo makubwa na madogo ambayo huongeza thamani kwenye maisha yao.
Jinsi ya kuadhimisha siku ya kumuenzi mkeo wako
Mbali ya kumununulia zawadi ya pete mwanaume anaweza kumuagizia mkeo shada la maua analolipenda, kumfanyia sapraizi ya kuandaa mahali mtakapopata chakula cha jioni pamoja au kumpeleka kwenye mapumziko mafupi ya kimapenzi. Pia unaweza kumnunulia manukato au kitu cha kipekee ambacho kitabaki kama kumbukumbu kwa siku nyingi zijazo.
Hii haimlazimishi anayeifanya kutumia fedha nyingi, anaweza kuiandaa kulingana na mazingira na kipato chake ilimradi muhusika ambaye ni mke afurahi na kuona namna anavyothaminiwa na mumewe.
|
Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha demokrasia katika kipindi ambacho, wanazuoni na ri
|
Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha demokrasia katika kipindi ambacho, wanazuoni na ripoti mbalimbali zinaonyesha dosari katika misingi ya demokrasia ya nchi.
Kwa mitazamo ya wanazuoni hao, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, ndiyo uliokuwa ukomo wa safari njema ya demokrasia nchini, baada ya kushuhudiwa misingi kadhaa ikivunjwa.
Uchaguzi huo, ulimweka madarakani Hayati John Magufuli aliyemshinda mpinzani wake kutoka chama cha upinzani cha Chadema, Edward Lowassa.
Uongozi wa Hayati Magufuli, unatajwa kukiuka misingi lukuki ya kidemokrasia, ikiwemo kuzuia mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzani, lakini kukomesha uhuru wa vyombo vya habari.
Hali iliyoshuhudiwa mwaka huo, iliendelea na demokrasia haikuwahi kutengemaa hadi sasa, kwa mujibu wa wanazuoni hao waliozungumza na gazeti hili.
Historia ya Tanzania katika safari ya demokrasia, ilianza baada ya uhuru mwaka 1961, wakati huo nchi ikiendeshwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha TANU na baadaye CCM baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Mfumo huo wa chama kimoja uliendelea hadi mwaka 1992, wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa rasmi.
Hii ilifungua milango kwa vyama vya siasa kushiriki katika uchaguzi na kutoa fursa kwa raia kushiriki katika maamuzi ya kisiasa.
Iliharibika tangu 2016
Akizungumza na Mwananchi Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Dk Conrad Masabo anasema demokrasia ya Tanzania ilishaharibiwa tangu mwaka 2016.
Kuharibika kwake, Dk Masabo anasema kulitokana na uamuzi uliofanywa na Watanzania kuamini mtu na sio utaratibu na hilo lilifanyika tena mwaka 2021 alipoaminiwa mtu na sio mifumo.
“Tunachokipitia ni matokeo ya hayo maamuzi yetu. Demokrasia kama haki nyingine hudaiwa na sio kuombwa, pia inapaswa kulindwa ili walioitoa wasiipokonye tena,” anasema.
Katika vipindi hivyo, Dk Masabo anasema Watanzania wote waliamini Hayati John Magufuli ni mkombozi na 2021 waliamini Rais Samia Suluhu Hassan atakomboa, hadi kupigiwa chapuo na vyama vya upinzani.
Kwa mtazamo wa mwanazuoni huyo, kwa hali ilivyo hadhani kama maboresho yanawezekana.
Lakini, anaeleza uwezekano upo katika mambo mawili ambayo ni kuja kwa kiongozi mwenye hisani aijenge, ingawa hilo ni gumu kwa mfumo wa demokrasia ya vyama uliopo.
Jambo la pili, anasema au wananchi wajiunge kuidai kitu ambacho ni kigumu kwa vile raia wameamua kuwaachia wanasiasa jukumu hilo.
“Kuna uwezekano mkubwa wa kulipa thamani kubwa ili kurejea tulipokuwa 2015, swali ni nani wa kulipa gharama hii?,” anahoji.
Dk Masabo anasema kinachoitesa Tanzania ni kwa sababu demokrasia yake ni ya vyama na sio ya raia, hivyo raia au wananchi wanaamini hawana wajibu wa kudai na kuilinda.
“Mafanikio ya Reject Financial Bill (kuondolewa kwa muswada wa fedha) ya Kenya ni kwa vile ilikuwa inaongozwa na kusimamiwa na raia na ndio maana baada ya vyama kuingia, malengo na mafanikio yamepotea,” anafafanua.
Mtazamo kama huo unatolewa pia na Mwanazuoni mwingine, Profesa Mohamed Bakary anayesema kuna anguko kubwa la demokrasia linaloendelea kushuhudiwa nchini, ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo.
Anasema Tanzania ilianza kuingia katika mfumo wa demokrasia kwa mguu wa kulia, lakini kwa kadri siku zinavyokwenda hali inakuwa mbaya zaidi.
Msingi wa hoja yake hiyo ni kile anachofafanua, Tanzania ilianza kuiishi demokrasia baada ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi na katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, ilishuhudiwa demokrasia ya hali ya juu.
Anasema hali ilikuwa hivyo hadi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, vyama vya upinzani vilishuhudiwa vikipata nafasi ya kuongeza katika ngazi ya mitaa, vijiji, vitongoji na hata majimbo.
“Ile hali iliashiria kuimarika na kuendelea kukua kwa demokrasia tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza,” anaeleza.
Anguko, anasema lilianza kushuhudiwa mwaka 2015, ule uhuru wa uchaguzi na ambo mengine yanayoijenga misingi ya demokrasia ilianza kuyeyuka.
Badala ya kusonga mbele, Profesa Bakary anasema Tanzania ilianza kurudi nyuma kidemokrasia hadi ulifika wakati idadi ya washindi wa vyama vya upinzani katika nafasi mbalimbali ziliporomoka.
“Hata matukio ya watu kupotea yanayoripotiwa sasa ni ishara ya kuonyesha kwamba tumerudi nyuma. Tulitarajia kama tungekuwa tumepiga hatua haya matukio yangefanyiwa uchunguzi na watuhumiwa wangetangazwa hadharani na hatua zingechukuliwa,” anasema.
Lakini hali iliyopo sasa, mwanazuoni huyo anasema unakuta watu wanajichukuliwa sheria mkononi na uwajibikaji hauonekani.
“Kuna kurudi nyuma kwa kiwango cha kutisha na inaweza kuleta hatari ya demokrasia kusambaratika kabisa,” anasema.
Demokrasia kwa mtazamo wa tafiti mbalimbali
Hali mbaya ya demokrasia nchini, inapigiwa msumari na Ripoti ya Freedom House ya mwaka 2023, iliyoipa Tanzania alama 32 kati ya 100 katika kipimo cha uhuru.
Katika utafiti huo, nchi hupimwa kulingana na uhuru wa kisiasa na kiraia na kwa mujibu wa takwimu hizo Tanzania imetafsiriwa kuwa nchi isiyo huru.
Hali inaashiria changamoto katika maeneo kama uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na uwazi wa uchaguzi.
Mbali na Freedom House, Ripoti ya Democracy Index ya The Economist Intelligence Unit (EIU) mwaka 2022, iliiorodhesha Tanzania kuwa nchi yenye utawala wa mabavu, ikiwa na alama 3.44 kati ya 10.
Hii ni ishara kuwa bado kuna vikwazo vinavyoathiri demokrasia ya nchi, hasa katika ushirikishwaji wa kisiasa na utawala wa sheria.
Sambamba na ripoti hizo, mifano ya hivi kaibuni nayo in aonyesha changamoto katika demokrasia, mathalan Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Katika uchaguzi huo, kuliibuka madai ya ukiukwaji wa haki za upinzani, udanganyifu katika kuhesabu kura na kuzuiliwa kwa wagombea wa upinzani kufanya kampeni zao kwa uhuru.
Kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) wakati huo, aliyeshinda uchaguzi huo ni Hayati Magufuli akipata asilimia 84 ya kura zote.
Hata hivyo, vyama vya upinzani kama CHADEMA na ACT-Wazalendo vilipinga matokeo hayo, vikidai uchaguzi haukuwa huru na wa haki.
Kuna fursa ya kuboresha
Licha ya changamoto hizo, kuna fursa ya kuboresha hali ya demokrasia nchini. Mabadiliko yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani mwaka 2021 yanaonyesha matumaini.
Rais Samia ameonyesha utayari wa kufanya mageuzi katika maeneo kama uhuru wa vyombo vya habari na haki za kisiasa.
Serikali yake imeruhusu upya mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani, hatua iliyopongezwa na viongozi wa kisiasa na wanaharakati wa haki za binadamu.
Pia, kumekuwa na jitihada za marekebisho ya katiba. Wanaharakati wa haki za binadamu na vyama vya siasa wameendelea kusisitiza haja ya katiba mpya, itakayoweka misingi imara ya haki za kiraia, usawa wa kisiasa, na uhuru wa vyombo vya habari. Rais Samia ameonyesha utayari wa kufufua mjadala wa katiba mpya, na hii ni ishara ya matumaini kwa maendeleo ya demokrasia nchini.
|
Baadhi ya wanazuoni na wadau wa haki jinai, wamesema hatua ya kuibua tuhuma zinazolichafua Jeshi la
|
Baadhi ya wanazuoni na wadau wa haki jinai, wamesema hatua ya kuibua tuhuma zinazolichafua Jeshi la Polisi, inawatengenezea sumu wananchi na hivyo wanajenga dharau kwa chombo hicho cha ulinzi na usalama.
Dharau hizo kwa mujibu wa wadau hao, matokeo yake ni vitendo vya uvamizi wa vituo vya polisi na hatimaye kulifanya jeshi hilo lishindwe kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Wamekwenda mbali zaidi na kusisitiza, makosa ya askari wachache wasio waadilifu ndani ya jeshi hilo, yasitumike kulichafua jeshi zima, lililojitoa kulinda usalama wa raia na mali zao.
Ingawa wadau hao wameibuka na mtazamo huo, wanazuoni wengine wamepingana na hoja hizo, wakisema kinachoshuhudiwa ni wananchi kupoteza imani na vyombo vya ulinzi na usalama na sio kuvidharau.
Hata hivyo, wanazuoni hao wanasema kupotea kwa imani hizo ni matokeo ya utendaji wa jeshi la polisi na vyombo vingine, ikiwemo matumizi ya nguvu yaliyoondoa maana ya huduma kwa wananchi badala yake imekuwa kuwaonea.
Hatua mbaya
Akizungumza na Mwananchi Jaji mstaafu, Francis Mihayo, amesema miongoni mwa hatua mbaya kuwahi kutokea ni wananchi kulidharau jeshi la polisi kiwango cha kuvamia kituo.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo wa sheria aliyehudumu katika mahakama kwa miongo kadhaa, polisi ndiyo mamlaka yenye jukumu la kulinda watu na mali zao, inapotokea wanadharauliwa ni mwelekeo mbaya.
“Sisi tukiwa vijana isingewezekana mtu akimbilie kituo cha polisi alafu atokee mtu akalazimishe kumtoa, ni jambo gumu na lisingewezekana, najiuliza kwanini haya yanatokea sasa,” amesema.
Alikwenda mbali zaidi na kueleza tabia hiyo itasababisha taifa lifikie hatua hatari zaidi hasa ya wananchi kuona vituo vya polisi ni maeneo ya kawaida.
Lakini yote hayo kwa mujibu wa Jaji Mihayo, yanachochewa na kauli za baadhi ya viongozi kushusha lawama na tuhuma kwa jeshi hilo, zikiwemo za utekaji na mauaji ya watu.
“Naanza kuona kama vile baadhi ya viongozi wanawafanya wananchi wasiliamini jeshi kwa kulitupia lawama kila wakati,” amesema.
Kwa sababu polisi, amesema ni chombo chenye mamlaka ya ulinzi wa amani, si vema kulilaumu na kulituhumu hadharani kwa matendo ya wabaya wachache.
“Jeshi ni chombo kizuri isipokuwa wapo wabaya ndani yake, sasa wabaya hao wasitumike kuwachafua wengine au kulichafua jeshi la polisi kwa ujumla wake,” amesema.
Amesisitiza umuhimu wa viongozi kuepuka kauli zinazolilaumu jeshi hilo, kwa kuwa kufanya hivyo kunapandikiza sumu kwa wananchi na hatimaye wanaanza kuwadharau polisi.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi, Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi amesema kati ya mambo mabaya yanayofanywa nchini, ni kulifarakanisha jeshi la polisi na wananchi.
Amesema hilo linafanywa ilhali katika baadhi ya maeneo wananchi wanajenga vituo vya polisi kwa nguvu zao na wanaomba wapelekewe polisi.
“Tunazunguka mikoani, mnaona wananchi wanavyojenga vituo vya polisi wenyewe na wanaomba wapelekwe askari. Ina maana kwa wananchi wa kawaida polisi wanafanya kazi yao vizuri.
“Sasa haiwezekani kukitokea polisi wawili watatu wenye matatizo ninyi mnataka wananchi wawakasirikie polisi nchi nzima hili halikubaliki ni jambo la ovyo kuliko yote ninayoyafahamu,” amesema.
Wasichokijua baadhi ya watu, amesema polisi ni miongoni mwa watumishi wanaotoa maisha yao kwa ajili ya wananchi kuliko inavyodhaniwa.
Ameijenga hoja yake hiyo kwa kurejea takwimu za miaka mitano kuanzia 2017/2023, akisema jumla ya polisi 42 waliuawa katika mapambano na majambazi, huku 141 wakijeruhiwa.
“Tafakari kwa dakika moja tu, hivi polisi wote wakisema wamechukua likizo kwa saa 24 itkuwaje katika nchi hii,” amesema.
Tumefikaje, madhara na tunatokaje
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk Revocatus Kabobe amesema utamaduni wa baadhi ya wananchi wa kujichukulia sheria mkononi si sahihi ukirejea hasa kwenye kuvamia vituo vya polisi.
Amesema ni hatari zaidi wananchi kukosa imani na jeshi la polisi ambalo kimsingi lipo kuwalinda raia na mali zao.
“Turudi kwenye misingi ya utawala wa sheria ambapo ni mahakama tu yenye mamlaka ya kusema nani mwenye kosa na nani hana.
“Tukianza kuchukua sheria mkononi tutabomoa taifa letu wenyewe kitu ambacho sio sawa. Haya ndo madhara ya kulidharau jeshi la polisi,” amesema.
Amesema yawezekana wananchi wana hoja ya msingi juu ya hatua wanayochukua, lakini kuchukua sheria mkononi na kuvamia vituo vya polisi haiwezi kuwa njia bora ya kutatua tatizo.
“Polisi wana silaha na wanapozitumia kujihami dhidi ya raia walowavamia madhara ni makubwa zaidi,” amesema.
Hata hivyo, amesema vitendo hivyo ni ishara kwamba kuna mahali taifa limeteleza kwa kudharau utawala wa sheria na kutotimiza wajibu kama raia na upande wa polisi pia.
Pia, amesema kuna matukio mengi ambayo jeshi la polisi linatuhumiwa kutotenda haki, jambo linalowafanya wananchi wawe na hasira hadi kujichukulia sheria mkononi.
“Matukio mbalimbali yanayoashiria polisi kujihusisha na siasa kitu ambacho ni kinyume na sheria zetu. Haya yote yanawafanya wananchi wapate taswira tofauti ya jeshi la polisi,” amesema..
Ili kujiepusha hilo, amependekeza kurudi kwenye misingi ya ujenzi wa taifa na kuiishi, ikiwemo utawala wa sheria.
Amependekeza polisi wawajibike kwa mujibu wa sheria na kanuni zao zilizojengwa kuwahudumia wananchi kwa kuwalinda na mali zao.
Kwa upande wa wananchi, amesema wanapaswa kutii sheria bila shuruti, wawajibike kushirikiana na polisi katika kutimiza majukumu yao.
“Jeshi la polisi liendelee kutoa elimu kwa wananchi juu ya haki na wajibu wao katika kulinda usalama wa nchi na watu wake. Bila polisi hakuna usalama,” amesema.
Sio dharau, hawana imani
Kwa mtazamo wa Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Sabatho Nyamsenda, kilichopo sio wananchi kulidharau jeshi hilo, bali wamekosa imani nalo.
Kukosa kwao imani na jeshi hilo, amesema ndiko kunakowafanya waamue kujichukulia sheria mkononi.
Hatua ya wananchi kukosa imani na jeshi hilo, imetokana na kile alichoeleza, badala ya kutoa huduma, polisi wameonekana wakitumia nguvu zaidi kulinda usalama wa raia.
“Kwa ujumla mara nyingi linatumia nguvu na linaonekana lipo kwa ajili ya kuwanyanyasa na sio kuwatumikia. Wananchi wanaona halitoi huduma bali linawanyanyasa,” ameeleza.
Kwa mujibu wa Dk Nyamsenda, mazingira hayo yameondoa uhusiano mzuri kati ya jeshi la polisi na wananchi tangu muda mrefu.
“Kilichotokea Geita ni kwamba wananchi waliona jeshi la polisi halitoi majibu sahihi juu ya kupotea kwa watoto na hata walipoandamana jeshi ilitumia nguvu kiasi cha kupoteza uhai wa raia mmoja.
“Kuna uwezekano mkubwa kwamba chombo hicho pengine kinafumbia macho au baadhi ya maofisa wake wasio waaminifu pengine ni wahusika wakuu, huu ndiyo mtazamo wa wananchi,” amesema.
Katika mazingira hayo, amesema kuna haja ya kuliangalia upya jeshi hilo, kama linaonekana kwenda kinyume na misingi ya kuanzishwa kwake, lifumuliwe.
“Kwa bahati mbaya polisi wanapotuhumiwa, majibu yao ni kuonyesha vitisho zaidi. Kama nchi ni vema kuchukua hatua kubwa ikiwemo kulifumua jeshi moja kwa moja.
“Nadhani huu sio muda wa kutoa vitisho na kuwalazimisha watu wawe na utii na chombo ambacho wanaona kinawaonea, badala yake tufikiri namna mpya ya kukifanyia Mageuzi,” amesisitiza.
Amesema kwa sababu jeshi hilo limeundwa na Watanzania, halitakuwa jambo gumu kulibadili kuwa namna ambavyo jamii ingetamani liwe.
|
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere (MNF), Joseph Butiku amewataka viongozi wa vyombo vy
|
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere (MNF), Joseph Butiku amewataka viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wasiseme hawawajui wahusika wa uhalifu, kufanya hivyo kunaondoa sababu za wao kuwa na nafasi walizonazo.
Ameisisitiza hoja yake hiyo kwa kuweka wazi kuwa, wahalifu wa utekaji, mauaji na ulawiti wanajulikana kwa kuwa wanaishi miongoni mwa wananchi, makanisani, misikitini na kwenye vyombo vya dola.
Sambamba na hilo, Butiku ametaka uwajibikaji wa viongozi inapotokea maeneo waliyopewa kuyaongoza yameingia doa kwa namna yoyote.
Kauli hiyo ya Butiku, inakuja katika kipindi ambacho kumekuwa na mfululizo wa taarifa za matukio ya utekaji na mauaji ya raia na Ripoti ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ilioroshesha watu 83 waliokumbwa na kadhia hizo.
Hata hivyo, kauli ya kiongozi huyo wa zamani serikalini tangu awamu ya kwanza, inakoleza mwendo wa matamko ya wadau hasa baada ya tukio la kuuawa kwa kada wa Chadema, Ali Kibao, aliyekamatwa Septemba 6, mwaka huu na wasiojulikana wakiwa katika usafiri wa umma.
Butiku ametoa kauli hiyo leo, Septemba 10, 2024 alipozungumza na waandishi wa habari, katika Ofisi za taasisi hiyo, Posta jijini Dar es Salaam.
“Wasitwambie hawajui, IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) asitwambie hajui, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa asitwambie hajui, lazima wajue laa sivyo hawana sababu ya kuwa pale,” amesema.
Butiku amesema lazima Serikali iwajue kwa sababu wanaishi miongoni mwa wananchi, katika kaya, wapo ndani ya vyombo vya dola, wapo makanisani na katika misikiti.
“Viongozi wa vyombo hivi wasitwambie kwamba hawajui kinachotokea wanajua, wasitwambie kwamba wanamwogopa Rais wasimsingizie,” amesema.
Kwa mtazamo wa Butiku kutokana na mwenendo wa matukio hayo, viongozi wa vyombo vya usalama wanapaswa kuwajibika, huku akiwasihi wananchi waendelee kuviamini vyombo hivyo.
"Huwezi kuwa Waziri, halafu watu wanatekwa na kuuwawa kisha unasema Rais ameagiza, Rais kazi yake ni kupewa taarifa ili aagize, wajibu wa kwanza kwenye matukio haya ni wako wewe kiongozi wa ulinzi na usalama.
“Ukipewa kundi uliongoze, mambo ya aibu yakitokea katika kundi lile, nani unamuuliza. Tunachosema kuhusu vyombo vya ulinzi na usalama sio wote, hatutaki kuwalaumu wote.
“Ndani mule kuna watu wa ovyo wamefundishwa vizuri lakini hawakuiva kiusalama tunatarajia viongozi wao wawe wanajua,” amesema.
Katika mkutano wake huo, Butiku amesema Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa Tanzania sio taifa la wauaji wala wahuni ni la watu wanaoishi kwa kuzingatia Katiba na sheria.
“Hakuna nafasi wala ruhusa kwa raia yeyote wa nchi kuishi nje ya utaratibu huo na huo ndiyo msingi wa amani, umoja na maendeleo yanayoshirikisha wananchi wote kwa faida yao. Kwa maana hii sisi Watanzania ni wastaarabu,” amesema.
Amewataka wananchi kumsaidia Rais kuwapata wabaya ili wachukuliwe hatua kwa kuwa mkuu huyo wa nchi ana vyombo vya dola vyenye utaalamu.
“Tanzania ina Rais mmoja aliyekabidhiwa katiba aitumie kuiongoza nchi na kulinda taifa na mali zake, anapaswa kuungwa mkono bila kusita na katika hilo bila maswali,” amesema.
Kuhusu kuundwa kwa tume huru kwa ajili ya kuchunguza, Butiku amesema hilo linapaswa kufanyika iwapo itabainika kuna ombwe la ujuzi kwa vyombo vya uchunguzi vilivyopo,
Hata hivyo, ameeleza kwa miaka 60 tangu uhuru wa Tanganyika haamini kama vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo vimekosa utaalamu huo.
Kuhusu suala la utekaji kutojadiliwa bungeni, amesema muhimili huo una utaratibu hasa katika mambo magumu yanapotokea.
Amesema kuna kamati na mambo yanapokuwa magumu, mnakwenda kwenye kamati hizo na Waziri Mkuu ndiye mwenyekiti huko kila mtu anayehusika atanyooshewa kidole.
“Mnayaamua alafu mnarudi bungeni bila kuwaletea wananchi mambo ya ovyo ovyo,” ameeleza.
|
Mataifa mbalimbali duniani yameeleza kusikitishwa na taarifa za vitendo vya ukatili, kupotea na vifo
|
Mataifa mbalimbali duniani yameeleza kusikitishwa na taarifa za vitendo vya ukatili, kupotea na vifo dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu na kisiasa nchini, huku yakisisitiza uchunguzi wa haraka kubaini wanaohusika.
Masikitizo ya mataifa hayo 15 yanayounda Umoja wa Ulaya (EU) yalitolewa na balozi zao zilizopo nchini, yakiisihi Serikali kuhakikisha ulinzi wa upinzani, ili kuendana na falsafa ya R4 kama alivyoahidiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Falsafa hiyo yenye tafsiri ya Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga upya, ilitambulishwa na Rais Samia mapema baada ya kuapishwa kuwa Rais Machi mwaka 2021, kama msingi wa utendaji wake.
Mataifa hayo 15 ni Ubelgiji, Uingereza, Canada, Denmark, Ufaransa, Finland, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Poland, Hispania, Sweeden na Uswisi.
Hata hivyo, tamko la mataifa hayo linakuja muda mchache tangu alipozikwa kada wa Chadema, Ali Kibao aliyekutwa ameuawa Ununio jijini Dar es Salaam, siku moja baada ya kukamatwa na wasiojulikana akiwa kwenye usafiri wa umma.
Kuuawa kwake kulimuibua Rais Samia kupitia mitandao ya kijamii, akiandika kusikitishwa na tukio hilo, huku akiviagiza vyombo vya uchunguzi kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha taarifa kwake.
Katika taarifa yake hiyo, mkuu huyo wa nchi, alisisitiza Serikali chini yake haitavumilia vitendo vya namna hiyo.
Katika tamko la pamoja na mataifa hayo, lililotolewa leo, Septemba 10, 2024, nchi hizo zimeisihi Tanzania kulinda haki za msingi wa wananchi ukiwemo uhuru wa kujieleza.
“Jumuiya ya Umoja wa Ulaya unasikitishwa na taarifa za hivi karibuni za vitendo vya ukatili, kupotea kwa watu na vifo vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu,” limeeleza tamko hilo.
Umoja wa nchi hizo, umetaka uchunguzi wa kina wa matukio hayo, huku ukiwapa pole wanafamilia wote walioathiriwa na vitendo hivyo.
“Tunakaribisha wito wa Rais wa kuanzisha uchunguzi wa haraka ili kubaini wahalifu waliohusika na kuhakikisha kuna uwajibikaji,” imeelezwa katika tamko hilo.
Tamko hilo limetoa wito wa ulinzi wa upinzani, ili kuakisi falsafa ya R4 ya Rais Samia.
“Tunatambua kwa wasiwasi mkubwa kwamba matukio haya ya hivi karibuni yanatishia misingi ya kidemokrasia na haki za wananchi wa Tanzania.
“Katika nchi inayoheshimika kimataifa kwa amani na utulivu, na tunaungana na wito wa kulinda amani na utulivu wa nchi,” limeeleza tamko hilo.
|
Licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuelekeza mamlaka za uchunguzi zichunguze matukio ya mauaji, wadau
|
Licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuelekeza mamlaka za uchunguzi zichunguze matukio ya mauaji, wadau wamependekeza njia mbadala ya uchunguzi huo, wakitaka vyombo vya dola visihusike kutekeleza jukumu hilo.
Kwa mujibu wa wadau hao, kamisheni maalumu inapaswa kuundwa na mkuu huyo wa nchi itakayohusisha vyombo mbalimbali vya kijamii na kwamba pamoja na matukio hayo ilichunguze pia na Jeshi la Polisi.
Rais Samia alielekeza kufanywa kwa uchunguzi huo, juzi kupitia mitandao yake ya kijamii alipoandika kusikitishwa na tukio la kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema, Ally Kibao.
“Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi.
"Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii,” aliandika Rais Samia katika mitandao yake hiyo.
Mzizi wa maelekezo hayo ya mkuu huyo wa nchi ni tukio la kukamatwa kwa Kibao na baadaye kukutwa ameuawa Ununio jijini Dar es Salaam.
Taarifa za uchunguzi kutoka Hospitali ya Mwananyamala zilibaini kifo chake kimetokana na kipigo na kumwagiwa tindikani usoni.
Mbali na tukio la Kibao, uchunguzi unaozungumzwa na Rais Samia unatarajiwa kuhusisha matukio lukuki, likiwemo la kupotea, kutoweka na kutekwa kwa waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati nchini.
Mwaka 2017, kada wa Chadema, Ben Saanane alitoweka katika mazingira ya kutatanisha na hadi sasa hajawahi kupatikana.
Tukio kama hilo, lilitokea kwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda aliyetoweka baada ya kufuatwa na watu nyumbani kwake mwaka 2017 hadi sasa hajulikani alipo.
Mwaka huo huo, aliyekuwa Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu ambaye sasa ni Makamu Mwenyekiti bara wa chama hicho, alishambuliwa kwa risasi na hadi sasa wahusika wa shambulio hilo hawajapatikana wala uchunguzi kufanyika.
Lakini, Agosti mwaka huu, wanasiasa kadhaa akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Deusdedith Soka na wenzake wawili walitoweka baada ya kuitwa na watu wanaodaiwa kuwa na askari wa jeshi la polisi, hadi sasa haijulikani walipo.
Kada wa Chadema, Kombo Mbwana pia alitoweka nyumbani kwake katika mazingira ya kutatanisha, lakini baadaye jeshi la polisi lilikiri kumsikilia, licha ya siku za nyuma kukataa kuwa naye.
Hiyo ni mifano michache kati ya matukio mengi yanayohusisha utekaji, kutoweka na kuuawa kwa watu katika mazingira ya kutatanisha.
Hata hivyo, Agosti mwaka huu, Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) ilitoa orodha ya watu 83 waliotekwa, kutoweka na hata kuuawa, jambo lililoiibua Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kufanyia uchunguzi (THBUB).
Uchunguzi utakaofanywa na chombo huru ndiyo wito ulioonekana kutolewa na wadau wengi kama njia ya kupata jawabu la matukio hayo na Ubalozi wa Marekani ni miongoni mwa wadau hao.
Uchunguzi uwe hivi
Akizungumzia na Mwananchi jana, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi alisema uchunguzi huo haupaswi kufanya na jeshi la polisi kwa kuwa lenyewe ndilo linalotuhumiwa.
Badala yake, alitaka viongozi wa juu wa jeshi hilo wawekwe chini ya uchunguzi, utakaofanywa na Kamisheni maalumu itakayoundwa na Rais Samia.
“Tunasema polisi wasichunguze kwa sababu wenyewe ndiyo watuhumiwa namba moja. Mara zote waathirika wametoa ushuhuda wakilitaja jeshi hilo au mazingira yanayolihusisha na matukio hayo,” alisema.
Kwa mtazamo wa Mwabukusi, kamisheni hiyo itakayoundwa na mkuu wa nchi, inapaswa kuwa na mwakilishi kutoka TLS, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Wawakilishi wengine kwa mujibu wa Mwabukusi ni Wanasheria kutoka sekta ya umma, Usalama wa Taifa na Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo anapaswa kuwa Jaji mstaafu wa Mahakama.
“Kamisheni hiyo ipewe kazi ya kulichunguza jeshi la polisi na vikosi kazi vyote. Hao watu watakaoteuliwa wasiteuliwe kwa majina, bali kila taasisi ielekezwe kupeleka jina la mwakilishi wake,” alieleza.
Katika pendekezo lake hilo, Mwabukusi alitaka kamisheni hiyo ipewe siku 60 kutekeleza jukumu hilo la uchunguzi kisha ikabidhi ripoti yake.
Wakati uchunguzi unaendelea, Rais huyo wa wanasheria Tanganyika alisema Serikali itoe tamko la dharura la kutoruhusiwa askari yeyote au kikundi chochote kwenda kukamata mtu bila hati ya mahakama au kiongozi wa Serikali za Mitaa.
“Kama mtu yupo kwenye chombo cha usafiri, abiria na dereva waruhusiwe kumpeleka mtu huyo kwa pamoja hadi katika Kituo cha Polisi kilichopo karibu naye,” alisema.
Hayo, alitaka yaende sambamba na hatua ya Rais Samia kutoka hadharani alaani, kukemea na aelekeze kuachiwa mara moja kwa wananchi wote waliotekwa au kukamatwa kwa uonevu, akiwemo Deusdedith Soka na Haji Kombo.
“Kwa sababu hawa ndiyo waathirika watakaoleza ukweli wa nini kipo nyuma ya pazia,” alisema.
Mtazamo wa Mwabukusi, haukutofautiana na Mwanazuoni wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Emeritus Fimbo aliyetaka kuundwa kwa tume ya kijaji itakayofanya uchunguzi wa jumla.
“Inawezekana wakati polisi wanafanya uchunguzi kuhusu tukio la Kibao, kukawa na chombo kingine cha uchunguzi kwa sababu kuna wanaohisi kwamba watendaji wa mambo haya ni polisi,” alisema Profesa Fimbo.
Hata hivyo, alisema mwenye mamlaka ya uundaji wa tume hiyo ni mkuu wa nchi na kwa utashi wake ndiyo anateuwa wajumbe na viongozi wa tume husika.
Alisema pamoja na kuundwa kwa tume hiyo, anachotilia shaka ni kuwekwa hadharani kwa ripoti itakayobainika kwa kuwa historia inaonyesha ripoti nyingi zilifichwa.
Kuhusu tukio la Kibao, alitaka uchunguzi utakaofanywa na Polisi uhusishe kuangalia kuangalia ilikuwaje, hizo gari zilizotumika ni za aina gani.
“Wale walioingia kwenye basi wachunguzwe wote waliokuwepo waliona nini. Alikaa siti gani na nani na waliokuwepo walisikia nini kutoka kwa aliyekuja na pingu,” alisema.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda naye alipendekeza kuundwa kwa tume hiyo ya kijaji kwa ajili ya kuchunguza matukio ya utekaji na mauaji.
“Mheshimiwa Rais taifa linahitaji tume ya kjaji kuchunguza matukio yote ya utekaji na mauaji,” aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.
Jaji Werema awapa jukumu wanahabari
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Jaji mstaafu Frederick Werema alisema kabla ya uchunguzi mwingine, vyombo vya habari vinapaswa kuhakikisha vinafanya habari za uchunguzi kubaini mzizi wa tatizo.
“Wanahabari wanapaswa kufanya habari za uchunguzi kubaini sababu za tatizo, kama huyu niliyesikia kwamba amechukuliwa akiwa kwenye basi, uchunguzi wa wanahabari uje na jawabu la kwanini basi lilimwachia abiria wake kwa watu wasiojitambulisha,” alieleza.
Jaji Werema ambaye amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisema zaidi ya hivyo ni vema wananchi wasubiri uchunguzi ufanyike kama ilivyoelekezwa na Rais Samia kisha itajulikana kinachofuata.
Wito wa kuundwa kwa tume ya kijaji, ulitolewa pia na Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo bara, Issihaka Mchinjita alisema ni muhimu Rais Samia aunde tume ya kijaji kuchunguza matukio hayo.
Akiwa katika mazishi ya Kibao mkoani Tanga, Mchinjita alisema sababu ya kuundwa kwa tume hiyo ni kukosekana imani kwa vyombo vya ulinzi na usalama kama vinaweza kuwa sahihi kuchunguza matukio hayo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye aliungana na wadau wengine kutaka tume ya kijaji ichunguze matukio hayo na vyombo vya dola kwa ujumla.
“Wote tumesikia kauli ya Rais jana, lakini kauli ya Rais ambayo inaelekeza vyombo vile vile ambavyo ni watuhumiwa namba moja wakajichunguze wenyewe tunaona hiyo haiwezekani hii nchi haitarekebika.
“Rai ya waombolezaji katika msiba huu, kamwambie Rais yeye pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuunda tume ya kijaji ya kimahakama ambayo inaweza ikachunguza matukio yote haya na mengine mengi yaliyojificha,” alisema.
Alieleza ni imani yake kuwa, hiyo ndiyo njia pekee itakayowezesha kukomesha vitendo hivyo.
“Sisi ambao tuna ushahidi tutakuwa tayari kueleza mbele ya tume hii,” alisema.
Ubalozi wa Marekani
Katika hatua nyingine, Ubalozi wa Marekani umesisitiza uchunguzi huru na wa uwazi dhidi ya tukio hilo na mengine ya utekaji.
“Mauaji na kupotea kwa watu, kukamatwa, kupigwa na juhudi nyingine za kuwaengua raia katika uchaguzi zilizotokea mwezi ulipita, havipaswi kuwa na nafasi katika demokrasia,” imeelezwa katika tamko hilo.
Kwa mujibu wa tamko hilo, vitendo hivyo vinadhoofisha haki, za kikatiba.
TEF
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), liliongeza nguvu katika wito wa kuundwa kwa Tume ya Majaji kuchunguza wimbi la utekaji na mauaji.
“Tunaomba uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani katika ngazi zote, ujitafakari iwapo unastahili kuendelea kuwapo wakati tuhuma hizi nzito za watu kutekwa zikiendelea kusikika sehemu mbalimbali nchini.
“Tunao mfano hai wa alichofanya Mzee Ali Hassan Mwinyi mwaka 1976 kwa nia ya kuleta uwajibikaji wafungwa walipouawa kwa kuteswa wakiwa gerezani mkoani Shinyanga,” imeeleza taarifa hiyo.
|
Gari mbili zilizokuwa na namba za usajili nyeupe zilizoandikwa kwenye vibao vyeusi, ndizo zilizotajw
|
Gari mbili zilizokuwa na namba za usajili nyeupe zilizoandikwa kwenye vibao vyeusi, ndizo zilizotajwa na mashuhuda kuhusika katika tukio la ukamatwaji wa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema, Ally Kibao Septemba 6, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, tukio hilo lilitokea saa 1 jioni, muda ambao tayari giza lilishaanza kuingia na hakukuwa na aliyekuwa na wasiwasi kwa kuwa walidhani wakamataji ni askari wa Jeshi la Polisi.
Kibao alikamatwa Septemba 6 Tegeta mbele ya Jengo la Kibo Complex na siku moja baadaye mwili wake uliripotiwa kupatikana Ununio jijini Dar es Salaam, akiwa amefariki, huku uso wake umeharibika kiasi cha kutotambulika.
Hata hivyo, taarifa ya uchunguzi wa kitaalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, imebaini kifo chake kimetokana na kipigo na kwamba alimwagiwa tindikali usoni.
Alivyokamatwa
Mwananchi imefika Tegeta alikokamatwa Kibao, ni umbali wa takriban mita 20 kutoka Jengo la Kibo Complex ni eneo ambalo aghalabu mabasi yanayoelekea Tanga, Moshi na Arusha husimama kupakia abiria.
Kama ulivyo utaratibu wa kawaida, basi hilo la TASHRIF alilokuwa amepanda Kibao lilisimama kupakia abiria kwa mujibu wa mashuhuda, gari mbili moja Land Cruiser na lingine ni V8 zenye namba za usajili nyeupe zilifika.
Shuhuda huyo amesema Land Cruiser iliegeshwa mbele ya basi hilo na V8 iliegeshwa nyuma ya basi hilo na kisha watu wanne walishuka kwenye gari hizo.
“Wanne wote walikuwa na risasi (akimaanisha bunduki) alienda kwenye mlango wa basi na wawili wakaingia ndani, wawili walibaki mlangoni,” amesema.
Alichokisikia shuhuda huyo ni kauli kutoka kwa mmoja wa watu hao kuwa, ‘tumemfuata mtu wetu’ na kwa namna walivyokuwa kila mmoja alidhani ni polisi.
Amesema walioingia ndani ya basi walitoka na Kibao wakiwa wamemfunga pingu na hata aliyekamatwa naye hakuwa na wasiwasi, hali iliyofanya mashuhuda waondoe wasiwasi zaidi.
“Walivyotoka naye wakamuongoza hadi kwenye Land Cruiser wakamwingiza humo na wengine wakaenda kupanda V8 wakaondoka naye,” ameeleza.
Uelekeo wa safari hiyo, shuhuda mwingine amesema ni Bagamoyo, lakini gari hizo awali zilifika hapo zikitokea uelekeo wa Mwenge.
“Kila mmoja akawa anasema jamaa amekamatwa na polisi atakua mhalifu, hakuna aliyekuwa na mashaka. Mimi niliangalia namba za usajili wa gari wakati zinaondoka lakini sikuzizingatia, nilichoona ni rangi nyeupe na zimeandikwa kwenye kibao cheusi, sio za kawaida,” ameeleza.
Alichoshuhudia mwandishi
Eneo kilipo kituo hicho ni mita 20 kutoka Jengo la Kibo Compex lenye Kamera za CCTV.
Kwa namna ilivyo, isingekuwa rahisi kwa Kamera za Kibo Compex kuona kinachofanyika katika kituo hicho.
Mbali na mazingira hayo, woga na hofu zimekita mizizi katika mioyo ya mashuhuda wa tukio hilo, wengi walioulizwa walidai hawafahamu kilichotokea.
Wachache waliosimulia, waliomba hifadhi ya majina yao kwa kile walichodai wana familia zinazowategemea na mazingira yaliyomtokea Kibao yasije kuwatokea wao pia.
“Kama mtu amekuja kumchukua mtu hapa mbele yetu na baadaye akamuua, anashindwa vipi kunifuata mimi hohehahe akanimaliza,” ameeleza shuhuda mmoja.
Mwingine amesema ameshafuatwa na watu zaidi ya watatu kuulizwa kuhusu alichoshuhudia wakati wa tukio hilo, lakini hakutoa ushirikiano kwa hofu ya kuhusishwa katika kesi hiyo.
|
Saa chache baada ya kuripotiwa kwa mauaji ya Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema Ally Kibao, Jeshi la
|
Saa chache baada ya kuripotiwa kwa mauaji ya Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema Ally Kibao, Jeshi la Polisi limesema limeanza uchunguzi mkali kubaini wahusika wa mauaji hayo ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Taarifa za kuuawa kwa Kibao zilisambaa leo, Septemba 8, 2024 katika mitandao ya kijamii, baada ya mwili wake kukutwa Ununio jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku mbili baada ya kukamatwa.
Kibao alikamatwa na watu waliodhaniwa ni askari wakiwa na silaha za moto, Septemba 6, mwaka huu akiwa ndani ya basi la Kampuni ya TASHRIF lenye namba za usajili T 343 EES, alipokuwa safarini kwenda nyumbani kwao, mkoani Tanga.
Hata hivyo, tayari mwili wake ulishafanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Mwananyamala na kubainika aliuawa baada ya kipigo kikali kisha kumwagiwa tindikali usoni.
Taarifa kuhusu uchunguzi wa polisi, imetolewa na Msemaji wa jeshi hilo, David Misime baada ya kuulizwa na Mwananchi Digital kuhusu kinachoendelea kutokana na tukio hilo.
Katika majibu yake, Misime amesema sambamba na uchunguzi huo, timu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (Ramadhan Kingai) imetumwa kuongeza nguvu ili kuhakikisha waliofanya mauaji hayo wanapatikana na kifikishwa mahakamani.
“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi mkali na timu kutokà Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai imetumwa kuongeza nguvu ili kuhakikisha waliofanya mauaji hayo wanapatikana na kifikishwa mahakamani,” alisema.
|
‘Ni utata mtupu’ ndiyo maneno yanayoakisi tukio la kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema, All
|
‘Ni utata mtupu’ ndiyo maneno yanayoakisi tukio la kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema, Ally Kibao lililotokea siku moja baada ya kukamatwa akiwa katika usafiri wa umma kwenda nyumbani kwao mkoni Tanga.
Kinachojenga msingi wa utata ni mazingira ya kukamatwa kwake kulikofanyika Tegeta, mbele ya Jengo la Kibo Complex, jijini Dar es Salaam na watu waliokuwa na gari mbili zilizozuia safari ya usafiri huo wa umma aliokuwa amepanda Kibao.
Hatua hiyo ilisababisha usafiri huo ambao ni basi la kampuni ya TASHRIF lenye namba T 343 EES kusimama na watu waliobeba silaha za moto waliingia ndani hadi alikokaa Kibao na kumfunga pingu kisha kuondoka naye.
Baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo, utata zaidi uliibuka siku moja baadaye, ziliposambaa taarifa katika mitandao ya kijamii, zikieleza kada huyo amekutwa Ununio jijini Dar es Salaam, akiwa tayari ameshafariki na usoni alijeruhiwa kiasi cha kutoonekana vema.
Mwili wake ulipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini hapa, kwa taratibu za uchunguzi, uliobaini kifo chake kilisababishwa na kipigo kikali, kadhalika alimwagiwa tindikali usoni, kama ilivyoelezwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alipotoa taarifa za uchunguzi wa hospitali hiyo.
Bado mazingira tata yanaendelea kugubika mauaji hayo, kwa kile kinachohojiwa na wadau, ni nani anayeweza kumkamata mtu akiwa na mtutu wa bunduki na pingu, silaha ambazo aghalabu hutumiwa na Jeshi la Polisi, hivyo wapo wanaohusisha tukio la Kibao na askari wa jeshi hilo.
Maswali zaidi yanaibuka hasa kutokana na ukweli kwamba, yaliyomtokea Kibao yanaongeza idadi kati ya raia wengine zaidi ya 80 waliotekwa, kutoweka na baadhi yao kuuawa na wasiojulikana, kama ilivyoripotiwa Agosti mwaka huu na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Wito wa uchunguzi ili kuwabaini wahusika na kuundwa tume ya kijaji itakayochunguza matukio yote kwa ujumla, ndiyo sauti inayoonekana kuwa moja kutoka kwa wadau wa haki za binadamu, wanasiasa na wanaharakati nchini.
Hata hivyo, wadau wanatoa wito huo wakati tayari Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), ilishaanza uchunguzi wa matukio ya namna hiyo yanayohusisha zaidi ya watu 80.
Kutokana na tukio hilo la Kibao, kuhusishwa na askari wa jeshi la Polisi, Mwananchi ilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alitaka atumiwe ujumbe na alipotumiwa hakujibu.
Jibu kama hilo lilitolewa pia na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ambaye pia alipotumiwa ujumbe hakujibu.
Hata simu ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni nayo iliita bila majibu na alipotumiwa ujumbe mfupi hakuujibu.
Heka heka za uchunguzi ‘Postmortem’
Awali, uliibuka mzozo katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala ulikopelekwa mwili huo, baada ya uchunguzi wa kitaalamu kubaini sababu ya kifo cha kada huyo kuonekana kuchelewa.
Ndugu wa marehemu, wafuasi na makada wa Chadema waliofurika katika hospitali hiyo, walitaka mchakato wa haraka kujua kiini cha kifo cha Kibao na shinikizo lao ilikuwa uchunguzi huo ufanywe mbele ya Wakili wa chama hicho, Hekima Mwisapu.
Ilionekana hali ya kutoelewana kati ya walinzi wa chumba cha kuhifadhia maiti ulikokuwa unafanyikia uchunguzi huo na makada na wafuasi wa Chadema, kwa kuwa wakili huyo alizuiwa kuingia chumbani humo.
Hoja ya walinzi hao kuhusu sababu ya kumzuia Mwisapu ilijengwa na kile walichoeleza, itifaki zinaruhusu ndugu pekee kushuhudia uchunguzi huo na si mwingine yeyote.
Lakini wafuasi wa Chadema, walishinikiza Mwisapu awepo ndani, kwa kile walichodai, itawezesha kusikia uhalisia wa sababu za mauaji hao na baadaye aliruhusiwa kuingia.
Subira ilionekana kuwashinda wafuasi wengi wa Chadema waliokuwepo nje ya hospitali hiyo, kwa kuwa ilichukua muda mrefu kabla ya majibu ya uchunguzi huo kutolewa.
Kutoka saa 12:07 uchunguzi ulipoanza hadi 2:50, ndipo Mbowe na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika walipoitwa ndani kusikia majibu ya uchunguzi huo.
Akitoa taarifa ya awali ya uchunguzi huo mbele ya vyombo vya habari, Mbowe amesema sambamba na kipigo kikali, uso wa Kibao ulimwagiwa tindikali.
“Ni dhahiri ameuawa baada ya kupigwa sana na hata kumwagiwa tindikali katika uso wake," amesema.
Mbowe amesema wameshauriana na familia ya marehemu na kukubaliana kuwa, washeria wa Chadema washiriki katika kikao cha uchunguzi, kujua Kibao ameuawa kwa namna gani.
Amesema mwili unaandaliwa ili taratibu nyingine za kifamilia zifanyike, huku mashauriano yakiendelea kuona hatua za kisheria zinazoweza kuchukuliwa.
Ameeleza hawataruhusu hali hiyo iendelee, huku akivituhumu vyombo vya dola kama mtuhumiwa namba moja kutokana na mazingira ya tukio.
Kwa kuwa imeshindikana suala la utekaji kuzungumzwa bungeni, amependekeza Rais Samia Suluhu Hassan aunde tume ya kijaji ya kimahakama kuchunguza matukio yote.
"Polisi hawana weledi wa kuchunguza jambo hili hata kidogo kwa sababu wao wenyewe ni sehemu ya watuhumiwa," amesema.
Ndugu wa marehemu
Mdogo wa marehemu huyo, Sharif Ally amesema wameshtushwa na taarifa za kifo cha ndugu yao na kwamba tayari mwili huo umepelekwa nyumbani Morocco jijini Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu za kuusafirisha kwenda Tanga kwa ajili ya maziko.
Maziko amesema yatafanyika kesho, saa 7 mchana maeneo ya Sahale nyumbani kwa marehemu, njia ya kuelekea Pangani.
Wadau walaani
Tukio hilo, lilikiibua Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kilichoisihi Serikali ifnye uchunguzi wa kina na haraka kubaini wahusika na wachukuliwe hatua.
Kituo hicho kimesisitiza uchunguzi huo unapaswa kuwa wa wazi ili kuondoa sintofahamu na kurudisha imani ya wananchi kwa vyombo vya ulinzi na usalama.
Kadhalika, kimezitaka mamlaka husika zielekeze juhudi kudhibiti matukio ya namna hiyo ili kupunguza taharuki kwa jamii.
“Jeshi la Polisi lithamini na lidhibiti mianya ya uhalifu ndani ya vyombo vya dola, kuhakikisha watu wasiokuwa dhamana hawapati nafasi ya kujipenyeza na kufanya uhalifu wakijifanya sehemu ya vyombo vya ulinzi,” kimeeleza katika taarifa yake kwa umma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Anna Henga imemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Hamad Masauni), ajitathmini na kuwajibika kwa madhila yanayowakumba wananchi.
Kituo hicho, kilitoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan atoe tamko la kukemea matukio hayo ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini.
Chama cha ACT-Wazalendo nacho, kimelaani tukio hilo, kikisema kunaongeza hofu juu ya usalama na amani na kuchafua imani iliyopo kwa wananchi.
“Maswali tunayojiuliza hivi ni nani anayeweza kufanya matukio haya siku zote hizo bila kukamatwa? Je, vyombo vyetu vinazidiwa uwezo na watekaji? Majibu ya wananchi ni kuwa vyombo vyetu ndiyo vinahusika ndio maana haviwezi kujiwajibisha vyenyewe.
“Tunajiuliza utekaji unafanyika kwa maslahi ya nani? Na kwa lengo lipi?” kilihoji.
Sambamba na hoja zake hizo, kilimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camiliu Wambura awaeleze wananchi wanaohusika na vitendo hivyo, huku bunge likitakiwa kuunda kamati maalumu kuchunguza mauaji yote ya raia yanayohusisha vyombo hivyo.
CCM yataka uchunguzi
Katika hatua nyingine, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amelitaka jeshi la polisi kutimiza wajibu wake katika uchunguzi wa tukio hilo.
"Nimekuwa nikifuatilia toka asubuhi, sisi ni vyama vya siasa linapokuja suala la ubinadamu, siasa unaweka pembeni. Niliombe jeshi la polisi likatimize wajibu wake wa kuendelea na uchunguzi ili tupate taarifa baada ya uchunguzi,” amesema Makalla.
|
Wimbi la vitendo vya mauaji katika siku za hivi karibuni, limehusishwa na kukithiri kwa matatizo ya
|
Wimbi la vitendo vya mauaji katika siku za hivi karibuni, limehusishwa na kukithiri kwa matatizo ya afya ya akili, kumomonyoka kwa maadili, uelewa duni wa namna ya kuishi, huku umasikini uliopitiliza nao ukitajwa kama moja ya sababu.
Kwa mtazamo wa kisaikolojia, wanazuoni wanasema vitendo hivyo ni dalili ya jamii kupunguza uwezo wa kufikiri vema na kufanya maamuzi sahihi, kunakosababishwa na shida katika afya ya akili.
Lakini, viongozi wa dini wamekwenda mbali zaidi na kuhusisha vitendo hivyo na dalili za mwisho wa ulimwengu kama ilivyotabiriwa katika vitabu vitakatifu, huku mmomonyoko wa maadili ikiwa ni sababu nyingine iliyotajwa nao.
Msingi wa hoja za wanazuoni na viongozi hao wa dini ni mwenendo wa matukio ya mauaji ya watu, yaliyotokea katika miezi miwili kuanzia Julai hadi Agosti mwaka huu.
Matukio ya mauaji
Miongoni mwa matukio hayo ni lile la Julai 8, mwaka huu, uhai wa mwanafunzi wa kidao cha pili katika Shule ya Sekondari Kalunde mkoani Tabora, Salma Mussa (15) ulipokatishwa alipokuwa akielekea shuleni.
Siku hiyo hiyo katika Mkoa wa Dodoma, Stephen Mabula (44), aliingia mikononi mwa polisi baada ya kumnyonga mwanawe wa kambo hadi kufa, baada ya ugomvi uliohusisha wivu na mapenzi na mwenza wake.
Kama hiyo haitoshi, Mkazi wa Mgongola ‘A’ mkoani Tanga, alipoteza maisha baada ya kukatwa kichwa na watu wasiojulikana akiwa anachuma mboga shambani, Julai 27, mwaka huu.
Tukio hilo lilifuatiwa na lililotokea usiku wa kuamkia Julai 31, mwaka huu, wivu wa mapenzi ulikatisha uhai wa Mary Mushi, mkazi wa Moshi, mkoani Kilimanjaro, aliyeuawa kwa kukatwa mapanga. Baada ya kuuawa, mwili wake ulitupwa shambani kwao.
Agosti 9, mwaka huu katika Mkoa wa Dodoma, maisha ya Angela Joseph yalikatishwa baada ya kuuawa na mpenzi wake kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.
Angela aliuawa kikatili na mwili wake kufungwa kwenye mfuko wa nailoni kisha kuingizwa kwenye kiroba na baadaye kutupwa porini.
Kesho yake, Agosti 10, mwaka huu, Mganga wa Kienyeji, Nkamba Kasubi alikamatwa na Jeshi l Polisi kwa kuua na kuwafukia watu 10 katika Mikoa ya Dodoma na Singida. Baadhi yao walizikwa wakiwa hai.
Katika Mkoa wa Tabora, Agosti 14, mwaka huu, Juliana Mbogo (40) alinyongwa hadi kufa na mwenza wake na mwili wake kufichwa uvunguni mwa kitanda. Wivu wa mapenzi ulitajwa kama moja ya sababu.
Mwili wa mfanyabishara ndogondogo maarufu Machinga, John Gerald (30) umekutwa umetupwa baada ya kuuawa kwa kuchomwa visu kadhaa tumboni mkoani Dodoma Agosti mwaka huu.
Agosti 28, mwaka huu mkoani Dodoma, Michael Richard alipoteza uhai baada ya kuuawa kisha nyumba yake kuchomwa moto, hali iliyowajeruhi mkewe na mwanawe. Sababu inadaiwa ni kisasi.
Maadili ni tatizo
Akizungumza na Mwananchi jana, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kulitheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa alihusisha mwenendo huo na kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili uliosababishwa na binadamu kuacha kumwamini Mungu.
Hali hiyo kwa mtazamo wa Askofu Malasusa, imesababisha binadamu kuamini katika ushirikina, jambo linalowafanya wengi kujikuta katika matendo ya mauaji.
Alieleza matukio hayo si hatari kwa binadamu pekee, bali ni chukuzi kwa Mungu na maombi ya kuzitakasa roho ziondokane na fikra za mauaji ndiyo silaha njema itakayokabili changamoto zilizopo.
“Kwanza matukio haya ni chukizo mbele za Mungu. Watu wote tunahimizwa kuomba ili roho ya mauaji itoweke ili watu wasiishi kwa hofu,” alisema.
Umuhimu wa elimu hasa za kidini ndilo jambo alilopendekeza, ili kuwafanya binadamu watambue baadhi ya matendo hayampendezi Mungu.
“Tutambue kuwa ushirikina ni chukizo kwa Mungu. Ushirikina ni kazi ya shetani. Watu wamrudie Mungu na kuachana na imani potofu,” alisisitiza.
Sauti ya pamoja kukemea vitendo hivyo, alisema ndiyo njia muhimu inayopaswa kutumika kupunguza au kumaliza kabisa mwenendo huo.
“Upendo wa Mungu ukitawala hatutakuwa na roho ya mauaji,” alisema Askofu Malasusa.
Dalili za mwisho wa ulimwengu
Kwa mtazamo wa kiroho matendo hayo ni dalili za mwisho wa ulimwengu, kama inavyofafanuliwa na Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji John Kamoyo.
“Labda siyo rahisi kupata jibu la moja kwa moja. Nikiwa mchungaji na mtumishi wa mambo ya kiroho mimi nitakupeleka katika mambo ya kiroho zaidi, hii ni dalili ya mwisho wa maisha,” alisema.
Aliujenga mtazamo wake huo kwa kurejea kitabu cha Biblia Timotheo 3:1-5, akisema kuna aya zinazoakisi namna binadamu tunavyoishi siku za mwisho ambazo huwa ni za hatari.
“Ukisoma aya hiyo utaona inaeleza watu wenye kujipenda wenyewe na wasiowapenda wa kwao,” alieleza.
Kujenga hofu ya Mungu mioyoni mwa watu, Mchungaji huyo aliitaja kama suluhu pekee ya matendo hayo, huku akisisitiza umuhimu wa kuwafundisha watu kuziepuka jamii zenye tabia mbaya.
“Tuwafundishe watu kuwa na hofu ya Mungu, japokuwa unabii huu utaendelea sana mpaja Yesu atakaporudi. Kuwafundisha watu wajiepushe na watu wa namna hiyo wakimwamini Yesu kweli kweli,” alieleza.
Uelewa duni na umasikini
Mwanazuoni wa masuala ya ustawi wa jamii, Dk Zena Mabeyo alisema uelewa duni wa namna sahihi ya kuishi na kutimiza malengo ndiyo sababu kuu ya vitendo hivyo.
Katika ufafanuzi wake, alisema baadhi ya watu wanakwenda kwa waganga na kushauriwa wauwe ili kupata utajiri, wanajikuta wakitekeleza kwa sababu hawana uelewa wa njia sahihi za kutajirika.
Hata wale wanaouwa kwa sababu ya wivu wa mapenzi, alisema ni kwa sababu hawana uelewa wa mbinu za kukabili hisia zao au kudhibiti matendo yatakayowasababishia wivu huo.
“Kwetu (Tanzania) kuna shida ya elimu na uelewa sahihi wa nini binadamu anatakiwa afanye ili kufikia malengo yake,” alisema.
Umasikini uliopitiliza nao ni sababu nyingine iliyotajwa na Dk Zena kama chanzo cha watu kujihusisha na vitendo vinavyokatisha maisha ya wengine.
“Umasikini wa mali unasababisha umasikini wa fikra hatimaye kila unachoshauriwa unajikuta unafanya, ndiyo hawa tunaowaona wameua kisa watajirike na vinginevyo,” alisisitiza.
Lakini yote hayo, Dk Zena alisema msingi wake ni uelewa duni wa namna ya kuishi, akifafanua iwapo watu wangeelewa kwamba kiungo cha mtu hakiwezi kukusababishia mafanikio wasingevitafuta.
Mwanazuoni huyo ambaye pia ni Mhadhiri katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii, alisema kunahitajika nguvu ya pamoja kukabili vitendo hivyo, isiachiwe Serikali pekee.
“Tunapaswa kujengeana uwezo wa kiuchumi kwa sababu wengine wanaingia huko kwa sababu za kukosa njia ya kujiinua kiuchumi,” alisema.
Lakini kuchukuliwa kwa hatua kali dhidi ya watakaobainika kufanya vitendo hivyo ni suluhu nyingine kwa kuwa inajenga woga kwa wenye matarajio ya kufanya hivyo.
Dk Zena, alisema ni vema kuwa na mbinu za kudhibiti mapema, wale wote wanaoibuka kutaka usajili wa kutoa huduma mbalimbali mathalan za tiba asili au za kiroho.
“Tunapaswa kudhibiti watu kuanzisha asasi mbalimbali za kiroho na kidini, wanaotaka usajili wachunguzwe wanakotoka na mwenendo wa maisha yao,” alisema.
Afya ya akili
Akizungumzia mwenendo huo, Rais wa Chama cha Wanasaikolojia Tanzania, Dk Magolanga Shagembe alisema ni dalili ya kukithiri kwa matatizo ya afya ya akili miongoni mwa wananchi wengi.
Tatizo la afya ya akili kwa mujibu wa Dk Shagembe, linaathiri uwezo wa binadamu kufanya maamuzi sahihi na hisia zake kwa ujumla, hivyo mara nyingi anajikuta akiangukia kuamua vibaya.
Katika ufafanuzi wake huo, alieleza hata anayefanya mauaji kwa sababu za kishirikina, aghalabu hujikuta katika kitendo hicho baada ya kujiuliza maswali mengi na uwezo wake wa kufanya maamuzi umepungua kiasi cha kumshinikiza aue.
“Mtu mwenye akili timamu lazima atajiuliza kuna faida gani ya kupata ninachokitaka kwa mganga kama nitapoteza uhai wa mtu wangu wa karibu, kwanini nifanye hivi kutimiza mahitaji yangu.
“Akijiuliza hayo kama akili yake ipo sawa kabla hajafikia kutoa uhai wa mtu mwingine anakuwa ameshapata majibu yanayomuondoa kwenye nia ya kufanya mauaji,” alisema.
Dk Shagembe alisema kwa mtu mwenye matatizo ya akili anapojiuliza maswali kama hayo, mara nyingi hapati majibu chanya na ndipo anajikuta akifanya mauaji kama alivyoelezwa na mganga.
Mazingira hayo hayo, alisema ndiyo yanayowakabili wale wanaokatisha uhai wao, akifafanua hufanya hivyo baada ya kujiuliza maswali mengi na kushindwa kupata majibu sahihi.
Lakini, mwenendo huo, Dk Shagembe alisema unaashiria uwepo wa ombwe la upatikanaji wa huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia katika jamii.
“Tunahitaji kufikiria namna ya kuzitoa huduma hizi nje ya hospitali na katika ustawi wa jamii ili kuruhusu hata watoa huduma binafsi waanzishe vituo vyao kwenye vijiji na mitaa ili mtu akipata changamoto ajue eneo la kukimbilia kabla hajafanya maamuzi hatari,” alieleza.
Malezi ni sababu nyingine iliyotajwa na Dk Shagembe, akifafanua baadhi ya watu wamelelewa kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha na hivyo inakuwa rahisi kuamua vibaya pale anapokabiliwa nazo.
Ili kukabiliana na hayo, alisema ni muhimu kutoa elimu kwa jamii iwe na utambuzi wa masuala ya kisaikolojia na kuwawezesha wananchi kutatua changamoto zinazowakabili.
Alieleza elimu hiyo ni vema ijikite kuwajuza wananchi kuwa haiwezekani kunufaika au kutatua changamoto zako kwa kukatisha uhai wa mwingine.
Alipendekeza uwekezaji ufanyike kwenye utafiti wa kubaini sababu za kina za matendo hayo na mbinu za kitaalamu za kuyakabili.
Kadhalika, alitaka Serikali ije na sheria inayowatambua, kuwasajili na kuwasimamia watoa huduma za afya ya akili, saikolojia ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa kuzingatia maadili.
“Kumekuwa na wimbi la watu wanaozitoa hizi huduma badala ya kusaidia watu, wanawaumiza zaidi hali inayosababisha wanakata tamaa na kujikuta wakifanya maamuzi yasiyofaa,” alisema.
Alieleza kuna umuhimu wa shuleni kutolewa elimu ya stadi za maisha zitakazomwezesha mtu kukabili changamoto na ajue wapi anakopaswa kukimbilia pindi atakapotatizwa.
|
Ushindani wa kupeperusha bendera mtini, ndiyo unaotajwa kuchochea ugomvi uliomsababishia kipigo na h
|
Ushindani wa kupeperusha bendera mtini, ndiyo unaotajwa kuchochea ugomvi uliomsababishia kipigo na hatimaye majeraha kiongozi wa Chadema Wilaya ya Tanga, Hussein Ally kutoka kwa vijana wanaodaiwa kuwa wa CCM.
Hatua hiyo, ilifikiwa baada ya vijana wa CCM kushusha bendera ya Chadema iliyokuwepo kwa takriban miaka mitatu katika mti uliopo kwenye Kituo cha Bodaboda cha Mgandini mkoani humo na baadaye ziliibuka vurugu za kila upande kutaka bendera yake ipepee.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema uchunguzi unafanyika kubaini muhusika wa vurugu hizo ili hatua zichukuliwe.
Mzizi wa tatizo
Mzizi wa tatizo ni ugomvi uliozuka baada ya madereva bodaboda wa Kituo cha Soko la Mgandini ambao pia ni wafuasi wa Chadema kutaka bendera ya chama hicho ipandishwe katika mti uliokuwepo kwenye eneo hilo, kama inavyosimuliwa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe.
Kwa mujibu wa Jumbe, bendera hiyo ya Chadema ilikuwepo katika mti huo kwa takriban miaka mitatu sasa, lakini juzi vijana wa CCM walifika na kuishusha.
Hatua ya kushushwa kwa bendera hiyo, ilitokana na kile kilichoelezwa na Jumbe kuwa, vijana hao wa CCM waliipandisha ya kwao wakidai kunafanyika shughuli za chama hicho tawala na hivyo ya Chadema ishushwe wakimaliza itapandishwa.
Aliitaja shughuli iliyokuwa inafanywa na CCM ni uzinduzi wa shina lililojengwa karibu na eneo hilo, ambalo pia lilikuwa na vijana wa bodaboda waliogawanyika kutoka wale wale wa Mgandini na wakawa wafuasi wa CCM.
Uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali, Jumbe alisema ulifanyika huku bendera iliyokuwa inapepea ni ya chama hicho tawala na ya Chadema ilishashushwa na hakukuwa na ugomvi.
Katika uzinduzi huo, alisema kiongozi mmoja wa CCM alitoa Sh2 milioni kwa vijana wa bodaboda waliokuwa kwenye kijiwe hicho cha chama tawala na wengine wa waliahidi kutoa jumatatu jumla ikawa Sh4 milioni.
“Lakini zilizotolewa ni Sh2 milioni na Sh2 milioni zilikuwa ahadi na waliahidiwa wangepewa jumatatu (Septemba 9, mwaka huu) na pale vijana wa bodaboda walikuwa 50 hao wa CCM, ukiachana na hawa waliokuwepo kwenye kijiwe cha Chadema,” alisema.
Alisema shida iliibukia kwenye mgawo wa fedha hizo (Sh2 milioni), kwani wengine walipunjwa na baadhi walipewa zaidi, mazingira ambayo yalisababisha mgogoro wa wao kwa wao.
Hatua hiyo, alisema ilisababisha baadhi ya vijana hao hasa waliopunjwa kurudi katika kituo cha bodaboda walipo wafuasi wa Chadema wakisema wanarudi kwenye chama chao na wakataka bendera ipandishwe.
“Waliposema lazima ipande yule kiongozi ndiyo akaona amepata washirika na wakaanza kupandisha. Wale vijana wa CCM walipiga simu akaja Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa (Ramadhani Omari) na kundi lake wakampiga sana kiongozi wetu wakampakia mshikaki na wakaondoka naye,” alisema.
Baada ya kupokea taarifa hizo, alisema alikwenda katika vituo mbalimbali vya polisi bila kumpata Ally, hadi saa 10 alasiri alipopigiwa simu kutoka Hospitali ya Mombo kuambiwa kuna nduguye anahitaji kupatiwa huduma.
“Nilikwenda nikamkuta ameumizwa sana, hakuwa anajiweza tukalipa akaanza kupatiwa huduma,” alisema.
UVCCM yajibu
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Mwenyekiti wa UVCCM Tanga, Ramadhani Omari alisema licha ya uwepo wa tukio hilo, lakini uhalisia wake ni tofauti na linavyoelezwa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, tukio hilo linakuzwa ilhali halikuwa kubwa na yaliyotendeka si makubwa kama inavyosimuliwa.
Alipoulizwa uhalisia ukoje, alijibu asingeweza kuelezea zaidi kwa sasa, lakini itakapolazimu atalitolea tamko.
“Kwa sasa siwezi nikalielezea lakini itakapolazimu tutatoa tamko. Kikubwa uhalisia hauko hivyo,” alijibu.
Polisi
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Mkoa huo.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, tukio hilo linahusisha kushambuliwa kwa mtu anayedaiwa kuwa ni kiongozi wa Chadema na tayari uchunguzi umeanza ili kubaini wahusika.
“Suala hilo lipo katika hatua za kiuchunguzi, limetokea jana (Septemba 5, 2024), uchunguzi unaendelea kubaini undani wake,” alisema kamanda huyo.
Kuhusu muhusika wa shambulio hilo, kamanda huyo alisema atajulikana pale uchunguzi utakapokamilika na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Katika ufafanuzi wake, alieleza tukio hilo lilitokea jana kwenye Kata ya Msabweni mkoani humo.
|
Kamati Kuu ya CCM, imewateuwa makada wake 10 kugombea ubunge wa Afrika Mashariki (EALA), kurithi naf
|
Kamati Kuu ya CCM, imewateuwa makada wake 10 kugombea ubunge wa Afrika Mashariki (EALA), kurithi nafasi iliyoachwa wazi na Dk Shongo Sedoyeka aliyefariki Juni 13, mwaka huu.
Hata hivyo, uamuzi huo wa kamati kuu umewakata makada wengine 37 waliotia nia kuomba ridhaa ya chama hicho kuwateuwa kugombea ubunge wa EALA.
Taarifa ya uteuzi wa wagombea hao, imetolewa leo Jumapili, Septemba 1, 2024 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla baada ya kikao cha sekretarieti ya chama hicho na kamati kuu maalumu iliyoketi leo.
Amewataja walioteuliwa ni Gladness Salema, Maria Sebastian, Queenelizabeth Makune, Ester Chaula, Profesa Neema Kumburu, Lucia Pande, Fatuma Kange, Hawa Mkwela, Fatma Msofe na Theresia Dominic.
Hatua ya kupigiwa kura kwa wagombea hao, Makalla amesema itafanyika kesho Septemba 2, 2024 na kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM, saa 8 mchana, jijini Dodoma.
Hilo litafuatiwa na uchaguzi wa mbunge huyo utakaofanyika Septemba 5, 2024, utakaohusisha wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Katibu Mkuu wake, Dk Emmanuel Nchimbi hakukimbia mdahalo kama ili
|
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Katibu Mkuu wake, Dk Emmanuel Nchimbi hakukimbia mdahalo kama ilivyoelezwa na Mtangazaji, badala yake hakukuwa na mawasiliano rasmi ya kumwalika.
Kwa mujibu wa taarifa ya CCM, hadi matangazo ya kufanyika mdahalo huo yanasambazwa mitandaoni, Dk Nchimbi hakuwa amethibitisha kushiriki wala kuahidi kutuma mwakilishi na tayari alishamshauri mwandaaji njia sahihi ya kumwalika.
Kauli hiyo ya CCM inajibu madai ya Mtangazaji wa Kipindi cha Medani za Siasa, Edwin Odemba kinachorushwa na Kituo cha Luninga cha Star TV kuwa, kutofanyika kwa mdahalo huo, kumesababishwa na Dk Nchimbi kutotokea.
Mzizi wa yote hayo ni mdahalo uliopangwa kufanywa na Star TV ukihusisha Makatibu Wakuu wa vyama vitano vya siasa nchini ambavyo ni CCM, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na ACT-Wazalendo.
Lakini, siku ya mdahalo huo uliopangwa kufanyika katika Ukumbi wa Maktaba Kuu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) ilifika na watendaji wakuu wa vyama vingine walikuwepo, isipokuwa Dk Nchimbi na Ahmed Masoud wa CUF.
Baada ya mazingira hayo, Odemba alifungua kipindi hicho na kutangaza mdahalo wa viongozi hao hautafanyika kwa kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema hatashiriki kama Dk Nchimbi hayupo.
Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu naye alidai hatoshiriki kwa sababu Mnyika amekataa kushiriki, kwa mujibu wa Odemba aliyezungumza mbele ya luninga huku akibubujikwa machozi.
Katika mazingira hayo, Odemba alitangaza kutofanyika kwa mdahalo huo, badala yake mada zilizopangwa zilijadiliwa na wahudhuriaji wengine na kwa sehemu kubwa walimtupia lawama Dk Nchimbi kwa kutoshiriki.
Kutokana na lawama hizo, CCM katika taarifa yake ya leo Jumapili, Septemba 1, 2024 iliyotiwa saini na Katibu wa Dk Nchimbi, Dennis Msacky ilieleza kusikitishwa na kauli ya Odemba katika kipindi hicho.
“CCM inautaarifu umma kuwa Katibu Mkuu hakukimbia wala hakudharau mdahalo huo. Balozi Nchimbi alifanya kila jitihada za mawasiliano na muandaaji na tunasikitishwa na jinsi alivyoupotosha umma,” imesema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Agosti 10, 2024 Odemba alimtafuta Dk Nchimbi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) akimuomba ashiriki mdahalo huo wa viongozi wa vyama vya siasa.
“Katibu Mkuu alimjulisha kuwa masuala ya vyombo vya habari yanaratibiwa na Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla hivyo awasiliane naye na akampa namba ya simu ya mkononi ya Makalla,” imesema.
Amesema kwa sababu ambazo Odemba anaweza kuzieleza mwenyewe, katika kipindi cha takriban wiki tatu, hakufanya mawasiliano au kumtafuta Makalla kama alivyoelekezwa na kushauriwa na Dk Nchimbi.
“Baada ya kuhisi kwamba nafasi ya Katibu Mkuu inaweza kuwa ngumu kupatikana kutokana na majukumu yake ya kazi za chama, Odemba alimtafuta tena Balozi Nchimbi akiomba amuandae mwakilishi huku matangazo ya mdahalo huo yakiendelea kumtaja Katibu Mkuu wa CCM kuwa ndiye atakayeshiriki,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Amesema badala yake Katibu Mkuu alimwelekeza Odemba kutofanya lolote kabla ya kupata mawasiliano na Sekretarieti ya CCM.
“Kimsingi Odemba alitaka wananchi wadanganywe kuwa CCM kupitia kwa Katibu Mkuu ilikuwa imethibitisha kushiriki katika mdahalo huo jambo ambalo si sahihi.
“Katika mazingira ya kustaajabisha tumeshangazwa na machozi ya Odemba aliyotoa jana akielekeza lawama kwa CCM na kwa Katibu Mkuu wakati alijua bayana kwamba alikuwa hajapata uthibitisho wowote wa CCM kushiriki
“Ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba yeye mwenyewe alishajua kwamba alikuwa akiendelea kutangaza kuhusu mdahalo huo kama "promo" pasipo kupata ridhaa ya CCM,” imesema.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa CCM ndiye Mwenyekiti wa Sekretarieti na siku nzima ya jana ambayo ndiyo siku Odemba alipanga kufanyika kwa mdahalo huo, kulikuwa na vikao vya maandalizi ya Kamati Kuu Maalum ambayo inafanyika leo.
“Jambo ambalo kwa namna yoyote Katibu Mkuu asingeweza kuwapo katika mdahalo huo hata kama angekuwa amethibitisha awali. Kushiriki kwenye mdahalo kunahitaji mashauriano na maafikiano kati ya waandaji na waalikwa,” imeeleza.
Imesema Katibu Mkuu hakuwa ametoa uthibitisho wa kuhudhuria mdahalo huo na hakukuwa na makubaliano yoyote rasmi ya yeye au mwakilishi wake kuhudhuria katika shughuli hiyo.
“Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Nchimbi yupo tayari kwa midahalo, majadiliano na makongamano yanayolenga kujenga umoja wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa kadiri ya taratibu zilizopo na ratiba yake ya kazi inavyoruhusu,” imesema
|
Haitakuwa lazima tena kwa kila muhitimu wa shahada ya sheria kupita Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria
|
Haitakuwa lazima tena kwa kila muhitimu wa shahada ya sheria kupita Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST), iwapo hana mpango wa kufanya kazi za uanasheria katika utumishi wa umma.
Matarajio ya kutokea hilo yatafikiwa baada ya marekebisho ya Sheria ya kuanzishwa kwa LST, ambayo kwa sasa inalazimu yeyote anayetaka kufanya kazi za uanasheria katika utumishi wa umma afaulu masomo ya uanasheria kwa vitendo.
Tayari wabunge wamepitisha muswada wa marekebisho ya sheria hiyo yaliyopendekezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala, Katiba na Sheria.
Sambamba na hilo, marekebisho mengine yaliyopitishwa ndani ya muswada huo ni kuongeza wigo kwa LST kutoa mafunzo ya kozi nyingine maalumu za mafunzo ya sheria.
Hata hivyo, hatua hiyo inatajwa na wanasheria kuwa, itapunguza wimbi la wanaofanya kazi ya uwakili kwa sababu wamepitia misingi ya utendaji wa taaluma hiyo LST kwa sharti la kisheria lililopo.
Muswada huo ulipitishwa bungeni jijini Dodoma jana baada ya kuwasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.
Katika wasilisho lake, Profesa Kabudi alisema shabaha ya marebisho hayo ni kutatua changamoto zilizobainika katika utekelezaji wa masharti ya sheria.
Marekebisho hayo kwa mujibu wa Profesa Kabudi, yatahusisha kifungu cha 5 ili kuongeza wigo kwa LST kutoa mafunzo ya kozi nyingine maalumu za mafunzo ya sheria.
Kadhalika, amesema Ibara ya 7 ili kuondoa sharti la kila muhitimu wa shahada ya sheria kulazimika kupitia na kufaulu masomo ya sheria kwa vitendo katika hata kama hakusudii kufanya kazi za uanasheria katika utumishi wa umma.
Nini maana yake
Akizungumzia hilo, Wakili wa Kujitegemea, Ipilinga Panya alisema sharti la kila anayehitimu shahada ya sheria kulazimika kusomea uwakili, ndiyo lililosababisha uwepo wa watu wanaojifanya mawakili ilhali hawastahili.
“Kwa sababu mtu anahitimu shahada anakwenda LST kwa namna yoyote ile anapata kujua undani wa utendaji wa wakili naye anajinasibu kuwa wakili hata kama haikuwa nia yake. Hapa ndipo wanapotokea watu wasio waadilifu,” alisema.
Kuondolewa kwa sharti hilo, Panya ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alieleza kutasaidia kupunguza mawakili wasiostahili.
Hata hivyo, aliweka wazi kuwa TLS itapitia muswada huo wote na kama itaonekana inafaa Rais wake, Boniface Mwabukusi atauzungumzia.
Akifafanua muswada wa marekebisho hayo, Makamu Mkuu wa Taasisi, Mipango, Fedha na Utawala wa LST, Profesa Ambrose Kessy alisema kinachomaanishwa ni kuondoa ulazima wa mtu anayesoma shahada ya sheria kupitia LST kama hataki kufanya kazi za sheria.
“Lakini wote wanaotaka kufanya kazi za sheria kama wanasheria serikalini au kwenye vitengo vya sheria serikalini, mawakili binafsi, mahakimu, lazima waende LST. Kimsingi ni wote wanaotaka kuitwa wanasheria,” alifafanua.
|
Ukiihesabu miaka minne kwa umri wa binadamu, basi ni mtoto anayemudu kutembea, anakimbia na sasa ana
|
Ukiihesabu miaka minne kwa umri wa binadamu, basi ni mtoto anayemudu kutembea, anakimbia na sasa anatamka karibu kila neno, hicho ndicho kipindi ambacho Bakari Machumu amehudumu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji katika Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).
Machumu amekuwa na nafasi hiyo tangu Aprili 29, mwaka 2021 alipotangazwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Nation Media Group (NMG), Stephen Gitagama na sasa wadhifa wake huo unakoma Agosti 31, mwaka huu baada ya kutangaza kuondoka.
Hata hivyo, miaka minne katika nafasi ya ukurugenzi, inafanya jumla ya muda aliohudumu katika kampuni ya MCL kwa nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mhariri Mtendaji wa Gazeti la The Citizen, ufikie miongo miwili.
Ingawa ameng’atuka mapema katika cheo cha ukurugenzi, Machumu anajivunia mafanikio yanayoifanya kampuni hiyo itazamwe na jamii kwa jicho la matumaini, ikiakisi kauli mbiu yake ya ‘Kuliwezesha Taifa’.
Katika mahojiano maalumu aliyofanya na gazeti hili ofisini kwake, Machumu anaeleza ingawa anaondoka, inapaswa kueleweka kuwa, ukuaji wa MCL katika miaka ijayo utategemea kuendelezwa kwa misingi iliyonayo ambayo ni ubunifu na kuzingatiwa kwa maboresho.
“Kwa hiyo ninaondoka MCL nikiwa ninaiangalia kwa ukubwa huo na nikijivunia kuwa sehemu ya safari hiyo na naiona ikiendelea kufanya hivyo kama itabaki katika misingi ile ile na tena ina fursa ya kukua,” anaeleza.
Anasema anaondoka MCL, ikiwa moja ya kampuni kubwa, yenye nguvu na inayofuatiliwa na makundi mbalimbali kutokana na uwezo wake wa kuleta matokeo kwenye jamii.
Kwa kadri jamii inavyoifuatilia MCL, anasema ndivyo watendaji wake wanavyopaswa kuwajibika kuhakikisha hawawaangushi wanaoifuatilia.
“Tunatakiwa tuheshimu kwamba watu wanaiangalia MCL kwa sura tofauti. Naposema watu nazungumzia jamii zote yaani Serikali, sekta binafsi na wananchi wote wanaingalia Mwananchi kwa jicho la matumaini tusiwaangushe.
“Nguvu iliyonayo MCL haipaswi kutupanda vichwani tukaitumia vibaya. Ni nguvu inayotakiwa kutumika vizuri kuchochea maendeleo ya nchi hii na mtu mmoja moja,” anaeleza.
Kwa mujibu wa Machumu, msingi wa chochote kinachofanywa katika kampuni hiyo ni kuliwezesha taifa, ama kwa kuibua udhaifu ili urekebishwe na kuokoa maisha ya watu au kuonyesha fursa jamii ichangamkie.
“Hiyo ndiyo nguvu tuliyonayo na sio nguvu ya kwenda mbele unasema mimi ni MCL nitakushughulikia hapana, hiyo utashughulikiwa wewe,” anaeleza.
Aliwahi kukaribia kujiuzulu
Ingawa mitihani ni sehemu ya maisha katika uongozi, Machumu anasema uamuzi uliohusisha kuwasimamisha wahariri wanne katika chumba cha habari, ndiyo uliokuwa mtihani mgumu zaidi kwake.
Ugumu wa mtihani huo ulitokana na kile anachoeleza, alitakiwa kufanya uamuzi huo katika wakati ambao hakuwa na ushahidi uliojitosheleza wa tuhuma dhidi ya wahariri hao.
“Pale nilijitafuta nikasema hawa ni watu wanaoripoti kwangu, wametuhumiwa walivyotuhumiwa, sijapewa ushahidi wa kutosha, lakini natakiwa nitekeleze, nikitekeleza maana yake nini.
“Je, mimi nimesimama na watu ninaowaongoza au nimewatosa ninaowaongoza, nitalala usingizi kwa mtindo huo. Moyo wangu ukawa unakataa,” anaeleza.
Hata hivyo, anaeleza umahiri wa uongozi wa NMG unaotoa nafasi kwa viongozi kujadiliana kuhusu masuala yanayolinda uhai wa kampuni na wafanyakazi wake, ndiyo uliomwezesha kuuvuka mtihani huo.
Anaeleza mazungumzo yalifanyika na walikubaliana kuwasimamisha na sio kuwafukuza kazi, kisha kujiridhisha kwa kufanya uchunguzi wa kina na baadaye walibaini wahariri hao hawakuwa na hatia.
“Tuliwarudisha kwa gharama kubwa zaidi kwa sababu nafasi zao tulishaweka watu wengine, sasa bodi ililazimika kutengeneza nafasi nyingine nne kwenye bajeti yake ili kuwapa nafasi ya kuendelea kuwepo.
“Kwa sababu kulikuwa na ngao hiyo ndiyo sababu niliahirisha kujiuzulu, lakini isingekuwepo kile kilikuwa kipindi cha mimi kubwaga manyanga na nikasema ngoja nikalime,” anasema.
Kutofautiana na Serikali
Nafasi yake ya ukurugenzi wa MCL, anasema mara kadhaa imewahi kumtofautisha kimtazamo na viongozi mbalimbali ndani ya Serikali, hasa kutokana na baadhi ya maudhui zinazochapishwa na magazeti ya kampuni hiyo.
“Hiyo haiepukiki, lakini tumetokaje hapo? Mimi nimekuwa nikitumia sana kueleza kwamba hakuna chochote tutakachofaidika nacho kwa kuishutumu Serikali au kiongozi yeyote.
“Hata Aga Khan aliwahi kusema hakuanzisha vyombo vya habari, viwe sauti ya wapinzani, chama kilichopo madarakani au mtu yeyote asiyeenda sawa na jamii, bali ameanzisha ili visaidie kuleta matokeo chanya kwenye jamii tunayoishi,” anaeleza.
Ikitokea kutofautiana kwa mitazamo, Machumu anasema aghalabu hujikita kueleza kwanini dhima ya MCL, sera ya chumba cha habari na kama kuna makosa ya kibinadamu.
“Lakini haijawahi kuwa sera ya MCL kwamba kusimama kumshughulikia mtu fulani. Bodi hairuhusu, sera zetu haziruhusu na ndiyo sababu bodi ile ile inayokulinda kufanya uandishi wa habari kwa uhuru, ni hiyo hiyo inayokushughulikia ukiikanyaga sera yake,” anaeleza.
Mahojiano na Wakuu wa nchi
Machumu anasema hadi mkuu wa nchi anakubali kufanya mahojiano na mwandishi, inatokana na kushawishika na jambo fulani, ikiwemo nia njema ya mwandishi.
“Kwa hiyo anakuona kabisa hauwi tishio kwake au haulengi kwenda kumuaibisha unayemfanyia mahojiano. Nadhani tatizo tunalolifanya ni kwamba unakuja kutaka taarifa kutoka kwangu alafu unanichafua au kunivuruga ukitarajia nitakupa taarifa, sitakupa,” anaeleza.
Siri pekee ya kufanikiwa kupata mahojiano na watu wenye hadhi hiyo, anasema ni kuwafanya waamini unahitaji taarifa kutoka kwao, kuwa mnyenyekevu, muadilifu na mwenye heshima.
“Ikijenga tabia kwamba wewe ndivyo ulivyo na ukifanikiwa kufanya mahojiano na mmoja mwingine akiona, atakuwa sawa kufanya mahojiano na wewe,” anaeleza.
Hata hivyo, anaeleza katika mahojiano hayo mara nyingi amekuwa akifanya mwenyewe kuonyesha kuwa, licha ya ukurugenzi wake lakini bado ni mwanahabari.
“Tulifanya mahojiano na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi alipokuwa mgombea wa nafasi hiyo, Hayati Maalum Seif Sharif Hamad, Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson, Job Ndugai akiwa Spika wa Bunge, Rais Samia Suluhu Hassan mara mbili,” anaeleza.
Miaka 20 ya The Citizen
Miaka 20 ya utumishi wa Machumu ndani ya MCL inakwenda sambamba na maadhimisho ya miongo miwili ya kuanzishwa kwa Gazeti la The Citizen.
Kwa mujibu wa Machumu, safari ya kuanzishwa kwa gazeti hilo ilikuwa na milima na mabonde kwani mwanzo halikuwa na wasomaji wengi na lilitafsiriwa kuwa ni tafsiri ya gazeti la Mwananchi.
Anaeleza gazeti hilo lilianzishwa na mwonekano tofauti, likiwa dogo tofauti na ilivyozoeleka kwa magazeti mengi ya kiingereza nchini.
Kwa kadri siku zilivyokwenda, anasema yalifanyika mabadiliko mbalimbali ya maudhui kuhakikisha gazeti hilo linapata wasomaji wengi.
Mabadiliko hayo kwa mujibu wa Machumu, yalilifikisha hatua gazeti hilo likawa chanzo cha maudhui zilizopata mwitikio zaidi nchini na hatimaye kutumika kama rejea na vyombo vingine vya habari.
Anaeleza wakati huo, The Citizen ndilo lililokuwa kinara wa uandishi wa habari za uchunguzi likijitofautisha na mengine.
Kwa mujibu wa Machumu, alipoajiriwa ndani ya MCL, aliligeuza gazeti hilo kujikita zaidi katika habari za biashara kama sehemu ya utambulisho wake na kujitofautisha na Mwananchi.
Anasema hatua hiyo iliwezesha kulitofautisha na likapitia mageuzi mbalimbali na sasa limejikita katika maudhui ya kibiashara na kimataifa.
“Sehemu ya biashara kwa kweli The Citizen imepambana kwa kiasi kikubwa na nafurahi kwamba sasa hivi imejikita katika kuitangaza Tanzania kimataifa,” anaeleza.
Rising Woman
Alipoulizwa kuhusu msingi wa kuanzishwa kwa Jukwaa la Rising Woman, Machumu anasema ilitokana na sehemu ya malengo ya MCL kutafuta mbinu za kuzalisha katika nyakati ambazo magazeti si biashara kubwa kama ilivyokuwa zamani.
“Mitandao ya kijamii iliharibu soko kwa hiyo kukawa na msukosuko. Kwenye msukosuko huo tukawa tunajitafuta tunafanya nini ili tuvuke. Ujio wa Rising Woman ulilenga kufanya uandishi wa habari wa matukio eneo ambalo halikuwa linatazamwa zaidi,” anasema.
Katikati ya mazingira hayo, anaeleza viongozi wenzake walimshauri juu ya kuanzishwa kwa jukwaa hilo, huku wakiwa na wasiwasi wa kupingwa, kwa kuwa MCL yenyewe haijafikia usawa wa asilimia 50 kwa 50 katika uongozi.
Anaeleza jukwaa hilo liliwavutia wengi hadi kufikia hatua ya kupata ushiriki wa Rais Samia.
Machumu anasema mwaka huu MCL ilifikia uwiano wa 40 kwa 60 katika uongozi, ingawa kwa sasa baadhi yao wamepata fursa katika maeneo mengine na wamekwenda huko, hivyo kwa kiasi fulani uwiano huo umerudi nyuma.
Kurudi nyuma huko, anasema kunatokana na uchache wa wanawake wenye sifa zinazohitajika, hivyo kampuni nyingi zinawagombea.
Alivyoingia MCL
Kwa mujibu wa Machumu, safari yake ya kuingia MCL ilianza kwa kushawishiwa kuomba nafasi na wafanyakazi wenzake aliokuwa anafanya kazi nao awali.
Hata hivyo, anasema alipofuatilia nafasi hiyo ya maombi, alikuta muda umeshapia, lakini baadaye ilitangazwa tena na akajaribu kuomba.
“Wakati nimepata ile nafasi, mama yangu aliniuliza Bakari wewe unaondoka ulipo ukiwa Mhariri wa Habari, unakokwenda unaenda kuwa Mhariri wa Biashara mbona unarudi nyuma. Nilimwambia mama ile ni kampuni yenye hadhi ya kimataifa, nitajifunza zaidi na nitapata uzoefu zaidi na mshahara mnono,” anasema.
Anaeleza aliingia MCL akiwa na mtazamo wa ukubwa wake kutokana na historia ya ukubwa wa NMG.
Mitihani ya gazeti nyakati za uchaguzi
Machumu anasema Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ulimkuta akiwa Mhariri Mtendaji wa The Citizen na ndiyo wakati alipobaini ugumu wa kusimamia gazeti nyakati hizo.
“Watu wanatafuta kushinda kwa hiyo namna gani mnasimama katikati, namna gani mnasimamia mwongozo wa uchaguzi, kwa hiyo kile mlichopanga kufanya kukifanya kwa uhakika wake, anasema.
Pamoja na mitihani hiyo, anasema mambo yalikwenda vema na hata walipolaumiwa ilikuwa ni kwa sababu pengine umeandikwa ukweli na sio kumwonea mtu.
“Nakumbuka kuna habari moja wakati wa uchaguzi tulisema kila mtu atakayefanya mkutano apewe picha ya ukurasa wa kwanza. Kuna mgombea alifanya mkutano Buguruni alikuwa peke yake na watoto pale, ikapigwa picha ikawekwa mbele.
“Watu walichukulia kama kichekesho lakini mjadala hapa ndani ulikuwa, hivi huyu hapa anafanya kampeni au vipi, lakini tukawaeleza tuliahidi kuwapa nafasi wote,” anasema.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, anasema alikuwa na nafasi ya Mhariri Mtendaji Mkuu anayesimamia magazeti yote ya MCL.
Huyu ndiye Bakari Machumu
Machumu alijiunga na MCL mwaka 2004 akiwa Mhariri wa Biashara wa The Citizen, baadaye aliteuliwa kuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo na akahudumu kwa miaka saba.
Aliendelea kupanda katika nafasi za uongozi hadi kuwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL mwenye mamlaka ya usimamizi wa magazeti yote, ambayo ni Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.
Kabla ya kujiunga na MCL, Machumu alifanya kazi katika kampuni ya Business Times Litd iliyokuwa inachapisha magazeti ya Majira, Business Times, Daily Times na Dar Leo kwa nafasi za uandishi na baadaye mhariri.
Kitakachokushangaza, Machumu hakuingia kuitumikia taaluma ya habari akiwa mwanataaluma hiyo, ana shahada ya Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) alikohitimu mwaka 1998.
Miaka 20 baadaye alipata shahada ya uzamili katika usimamizi wa biashara (MBA) kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Uongozi ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI).
Pia, amehitimu shahada ya uzamili ya uongozi katika vyombo vya habari kutoka Chuo Kikuu cha Aga Khan nchini Kenya.
|
Umajumui wa Afrika, uzalendo na uzoefu ndizo sababu zilizotajwa na baadhi ya mataifa ya Afrika Masha
|
Umajumui wa Afrika, uzalendo na uzoefu ndizo sababu zilizotajwa na baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki kama turufu kwa Raila Odinga katika nafasi ya Uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).
Viongozi hao katika hotuba zao, wamemwelezea Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Kenya, kuwa ndiye anayestahili kuwa kiongozi wa jumuiya hiyo inayobeba sauti ya pamoja ya Afrika.
Odinga anagombea nafasi hiyo, kumrithi Moussa Faki Mohamed, Waziri Mkuu wa zamani wa Chad anayetarajia kumaliza muhula wake wa pili wa uenyekiti wa AU mapema mwakani.
Hii ni mara ya pili Kenya inatupa karata yake katika kuwania nafasi hiyo, ilifanya hivyo mwaka 2017 alipogombea Amina Mohammed lakini hakufanikiwa.
Katika uchaguzi wa nafasi hiyo, wakuu wa nchi za Afrika, hupiga kura kwa siri na inahitaji kupata angalau theluthi mbili ya 36 ili utangazwe kuwa mshindi.
Marais waliomwaga sifa hizo kwa Odinga ni Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Yoweri Museven wa Uganda, Salva Kiir wa Sudani Kusini na William Ruto wa Kenya.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni za nafasi hiyo ya Odinga, Rais Museven amesema jumuiya ya AU ndilo jukwaa linaloiwezesha Afrika kuwa na sauti ya pamoja katika majadiliano na ulimwengu.
Kwa sababu hiyo, amesema Odinga ni mgombea sahihi kwa nafasi hiyo kwa kuwa mara nyingi amekuwa akisisitiza umajumui wa Afrika.
“Kwa sasa tunataka mtu atakayetuongoza kutupeleka kwenye ustawi na sio yule ambaye anatafuta kazi tu. Kwa hiyo Odinga ni mgombea sahihi kwenye nafasi hii,” amesema.
Ameijenga hoja yake hiyo kwa kurejea uhalisia wa hali ya nchi za Afrika, akisema ugonjwa mkubwa unaozikabili ni umasikini na kukosa ustawi.
Lakini ustawi wa mataifa hayo, amesema utafikiwa iwapo nchi hizo zitakoma kutegemea misaada na badala yake kila raia, wakiwamo wazee wajishughulishe na shughuli za uzalishaji.
“Kama utazalisha bidhaa na huduma na ukawa na hesabu nzuri utapata fedha na kuuepuka umasikini. Kwa hiyo hiki ndicho kipimo chetu,” amesema.
Museven amesema kitakachozalishwa kitauzwa katika mataifa ya ndani ya Afrika aliyodai yanaendekeza ukabila na udini, bila kuzalisha.
“Kuna ambaye hana kile unachozalisha na huyo ndiye utakayemuuzia ndani ya Afrika, kwa hiyo sisi wenyewe tunaweza kuzalisha na kuuza ndani,” ameeleza.
Kwa mujibu wa Museven, siri nyingine ya mafanikio ya mataifa ya Afrika ipo katika uzalendo, akifafanua kwa namna yoyote nchi zinahitajiana.
“Unaponunua bidhaa zetu unatupa nafasi ya kwenda juu, lakini ukitufungia, najua kuna watu wamefungia kununua sukari tafadhali fungua sukari hiyo,” ameeleza huku akiangua kicheko.
Amesema inapotokea mataifa ya Afrika yanafungiana kuuziana bidhaa, yanaukaribisha umasikini.
Amesisitiza namna pekee ya kuuondoa umasikini kwa nchi za bara hilo ni kudumisha uzalendo ndani ya nchi, kadhalika umajumui wa Afrika kwa ujumla.
“Kwa hiyo uongozi unapaswa uwe moja ya jawabu la uchumi katika jamii zetu. Uongozi uchambue jamii zinakosa nini na uhakikishe unazipatia,” ameeleza.
Katika mazingira hayo, amesema Odinga ndiye mtu sahihi katika nafasi ya uenyekiti wa kamisheni ya AU, kwa kuwa historia yake inaashiria uwezo wa utendaji wenye manufaa kwa waafrika.
Katika hotuba yake, Rais Samia Suluhu Hassan amesema licha ya hatua zilizopigwa ni muhimu kwa nchi za Afrika kuhakikisha AU inaendelea kuwa imara ili kukabili changamoto za ulimwengu.
Katika kulitekeleza hilo, amesema kunahitajika mambo mengi ikiwamo mageuzi ya kitaasisi ili kuimarisha uwajibikaji na kudumisha amani ili kukomesha vita katika mataifa ya bara hilo.
Sambamba na hayo, ameeleza ili AU ifikie ajenda ya maendeleo inahitaji kuangalia mipango ya miundombinu yake na kuhakikisha sauti ya Afrika inasikika katika mijadala ya kidunia.
Katika kuzingatia umuhimu wa yote hayo, amesema Tanzania imeamua kumuunga mkono Raila Odinga katika nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).
“Tanzania inamjua Odinga kama mwanamajumui wa Afrika. Amelinda uhusiano wa viongozi wengi wa Afrika na hata wadau wengine nje ya bara hili,” ameeleza.
Amesema ni vema kwa uzoefu wake kutumikia nafasi hiyo itakayowezesha kuleta maendeleo ya miundombinu na kutatua changamoto nyingine.
Amesema ni imani yake kuwa, Ondinga ndiye msingi wa mageuzi ya Afrika na watu wake.
Kwa upande wa Rais wa Sudan Kusini na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Mashariki (EAU), Salva Kiir amesema ushiriki wake katika uzinduzi wa kampeni hizo unatoa ishara ya taifa lake kumuunga mkono Odinga.
Rais Ruto wa Kenya, amesema hatua yake ya kumshabikia Odinga katika nafasi mbalimbali haikuanza sasa, amekuwa akifanya hivyo tangu zamani na imempitisha katika madhira mbalimbali.
“Nimewahi kushitakiwa katika mahakama mbalimbali za kimataifa kwa sababu ya kumshabikia Odinga kwa hiyo nimekuwa mshabiki wake wa muda mrefu,” amesema.
|
Licha ya Sera ya Afya ya mwaka 2007 kutoa haki ya huduma bure za matibabu kwa makundi kadhaa ya watu
|
Licha ya Sera ya Afya ya mwaka 2007 kutoa haki ya huduma bure za matibabu kwa makundi kadhaa ya watu wakiwamo watoto, imebainika sehemu kubwa ya kundi hilo hugharimika kupata matibabu kinyume na matakwa ya sera hiyo.
Kwa mujibu wa sera ya afya, huduma hizo kwa wazee, wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano zinapaswa kutolewa bure, lakini uhalisia ni tofauti.
"Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi inayotoa huduma bila faida, na mashirika ya kimataifa, itaendelea kutoa huduma bila malipo kwa; wanawake wajawazito, watumiaji wa huduma za uzazi wa mpango na watoto wenye umri chini ya miaka mitano" inaeleza sera hiyo.
Mwema Ngenda anayeishi Kitonga jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa waathirika wa hilo, anayesimulia kutozwa zaidi ya Sh1 milioni kwa ajili ya matibabu ya mjukuu wake aliyekuwa na umri wa siku mbili.
Kinacholalamikiwa na Ngenda kinaakisi malalamiko ya wengi wanaodai kutozwa fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, huku sababu ikitajwa ni wengine kutofahamu mchakato unaowezesha kupata huduma hizo bure.
Wanavyosema waliotozwa
Katika simulizi yake Mwema anasema mjukuu wake alizaliwa kabla ya wakati (Njiti) akiwa njiani kuelekea kituo cha afya cha Mvuti.
Baada ya mtoto huyo kuzaliwa Agosti 2, 2024 anasema walifika katika Kituo cha Afya cha Mvuti na mzazi pekee ndiye aliyehudumiwa na walipewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Amana kisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya huduma za mtoto.
“Tulipofika Amana walisema tunaweza kwenda nyumbani kwa sababu wanampeleka Muhimbili ambapo hata tukiwepo hatutaweza kuruhusiwa kuingia hivyo asubuhi tuwahi huko tukakubaliana nao,” anasema Mwema.
Kesho yake, anasema walikwenda Muhimbili na walipofika walikabidhiwa karatasi ya malipo (Mwananchi inayo), wakitakiwa kulipa Sh1.124 milioni kwa ajili ya huduma za mtoto.
Kwa mujibu wa Mwema, muda huo walikuwa na Sh400,000 pekee na walilazimika kwenda kulipa baada ya kupewa namba ya malipo na walipofanikisha, hali ikawa tofauti.
“Tulipopewa karatasi tumekwenda kulipa siku inayofuata tukaambiwa hiyo karatasi tuliopewa ni malipo ya mtoto pekee hawajaweka na mama hivyo katika pesa tuliotoa wamepunguza deni la mtoto Sh250,000 na mzazi wamekata Sh150,000,” anasema.
Alichodhani baada ya kupewa karatasi ya malipo ni kwamba kiasi cha fedha kilichoandikwa kinahusisha huduma za mtoto na malazi ya mama kwa siku zote zilizokadiriwa, kumbe ilikuwa tofauti.
Anasema katika Sh1.124 milioni aliambiwa inahusu huduma za mtoto pekee na kwamba kuhusu malazi ya mzazi gharama zake zinajitegemea.
Agosti 16, anasema walilipa Sh200,000 wakidhani wamepunguza deni lile la Sh1.124 milioni, lakini ndipo walipopokea taarifa za malipo ya mzazi pia.
Katika mazingira hayo, anasema walijichangisha na kuuza shamba lao, wakapata Sh600,000 na walichukua Sh400,000 kwenda kulipa, wakaambiwa deni lao limebaki Sh700,000.
Hatua ya kuishiwa fedha na kukosa namna mbadala, anasema iliwalazimu kukimbilia kwenye msahama wa matibabu, lakini hawakufanikiwa, walijibiwa wanapaswa kulipa.
Mazingira hayo, anasema yamewafanya kuendelea kusalia hospitali hapo kwa takribani siku 16 hadi sasa, licha ya kuruhusiwa tangu Agosti 10, mwaka huu.
“Tumejichanga tena na tumekopa kwa watu mbalimbali tumefanikiwa kulipa Sh550,000, kwa sasa tunadaiwa Sh124,000 na tumeomba tuilipe Septemba 31, mwaka huu na tumeacha kitambulisho chetu cha Taifa,” anasema.
Anasema hayo yanatokea ilhali mara kadhaa wanaambiwa matibabu ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano ni bure.
Anasisitiza baada ya kutoka hospitali watakabiliwa na mzigo wa kulipa madeni na hivyo wana mashaka kuhusu lishe ya mzazi akiwa nyumbani.
Muhimbili yajibu
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema huduma katika hospitali hiyo hutolewa katika makundi manne ambayo ni msamaha, fedha taslimu, bima na kuchangia.
“Hivyo tunawasihi ndugu wenye uwezo wa kuchangia huduma kufanya hivyo na kama hawana uwezo tunatoa msamaha,” amesema Aligaesha.
Amesema hospitali ya Muhimbili Upanga peke yake imetoa huduma kwa njia ya msamaha katika miaka mitatu ya fedha 2023/24 Sh13 bilioni, 2022/23 Sh18 bilioni na 2021/22 Sh19 bilioni.
“Hivyo unaweza kuona ni kwa namna gani Muhimbili inatekeleza miongozo na sera mbalimbali za Serikali kwa vitendo,” amesema.
Alipoulizwa kuhusu tukio la Mwema, Eligaesha aliomba muda wa kufuatilia na siku nne baadaye alipoulizwa alijibu kwa ufupi “wameruhusiwa.”
Pamoja na Eligaesha kujibu hivyo, Mwananchi ilimtafuta tena Mwema kujua iwapo wameruhusiwa, alijibu bado wapo hospitali kwa kuwa wameambiwa wasubiri hadi Agosti 25 (leo).
Mtazamo wa mdau
Mtaalamu wa Afya ya Jamii, Dk Ali Mzige anasema sera zilizopo zinasemwa lakini utekelezaji wake unahitaji miongozo na bajeti maalumu kwa ajili ya matibabu bila malipo kwa watoto.
“Kama yapo matibabu bure tukumbuke asilimia 20 ni ya umri wa watoto chini ya miaka mitano na asilimia 20 ni wajawazito endapo utatoa matibabu bila malipo lazima kujua kuna asilimia 40 za watu watapata matibabu bure kwani maendeleo yanakwenda na idadi ya watu,” anasema Dk mzige.
Kutokana na hali hiyo, anasema Serikali inapaswa kuongeza bajeti itakayokuwa maalumu kwa makundi yanayohudumiwa bila malipo.
Hata hivyo, anasema Umoja wa Mataifa unazitaka nchi za Afrika kutumia asilimia 15 ya bajeti zake kwa ajili ya sekta ya afya, lengo ambalo bado Tanzania haijalifikia.
Mwisho.
Licha ya kushindwa katika uchaguzi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na baadaye kukata rufaa dhidi ya matokeo ya uchaguzi huo, Wakili Sweetbert Nkuba hatimaye ameiondoa rufaa hiyo.
Uamuzi wake wa kuiondoa rufaa hiyo kwa mujibu wa Nkuba, umekuja baada ya mazungumzo yake na mshindi wa kiti cha urais wa TLS, Boniface Mwabukusi na wagombea wengine, wakilenga kuwaunganisha mawakili.
Nkuba alitangaza kukata rufaa Agosti 3, mwaka huu baada ya Kamati ya Uchaguzi ya TLS kumtangaza Mwabukusi kuwa rais wa chama hicho kwa kupata kura 1,274 dhidi ya kura 807 alizopata Nkuba.
Alitangaza rufaa hiyo kwa kile alichodai kulikuwa na kasoro katika uchaguzi huo, ikiwemo kuishiwa karatasi za kupigia kura na watu kuruhusiwa kupiga kura hata baada ya muda wa ukomo uliotangazwa kuisha.
Nkuba ameieleza hatua yake hiyo jana, alipokuwa akifanyiwa mahojiano maalumu katika kipindi cha Medani za Siasa kinachorushwa na Kituo cha Luninga cha Star TV.
Amesema baada ya ushindi wa Mwabukusi baadaye walizungumza juu ya kasoro alizozilalamikia kwa lengo la kuhakikisha hazijitokezi tena katika uchaguzi ujao.
Baada ya mazungumzo hayo na kwa kuwa msingi wa wagombea wote ulikuwa ni kuwaunganisha mawakili, ameamua kuiondoa rufaa yake hiyo na kwamba anakubaliana na ushindi wa Mwabukusi.
“Nilikata rufaa na baadaye tukazungumza juu ya umuhimu wa kutengeneza umoja wa mawakili na kwa sababu hiyo tulikubaliana kuhusu mapungufu na kuona namna gani tutakavyoyatatua wakati mwingine,” amesema.
Hata hivyo, amesema kushindwa kwake katika uchaguzi huo, hakuondoa ukaribu wake na Mwabukusi, akisisitiza ni kama kaka yake waliojuana muda mrefu.
“Boniface ni kaka yangu, ni rafiki yangu na bahati nzuri wakati anahama kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya kufanya kazi zake huko mimi ni mmoja wa watu alioniomba ushauri.
“Boniface alikuwa meneja wa kampeni wangu katika uchaguzi wa TLS uliopita. Kwa hiyo ni kaka yangu kabisa na tunaongea vizuri,” ameeleza.
Hata hivyo, ameeleza kinachopaswa kupewa kipaumbele katika utendaji wa urais wa TLS ni kusimamia kifungu cha nne cha sheria ya kuanzishwa kwa chama hicho, kama inavyofanywa na Mwabukusi.
Amesema kifungu hicho kinaeleza wajibu wa chama hicho kwa Serikali, wananchi, bunge, kutoa elimu ya kisheria, kutetea haki za wananchi na mambo mengine.
Apendekeza mgombea huru
Katika mahojiano hayo, Nkuba amesema anaamini katika siasa zitakazoruhusu mgombea binafsi na ndiyo sababu iliyomfanya awe na mapenzi na mwanasiasa wa upinzani Hayati Christopher Mtikila.
Mtikila ndiye mwanasiasa aliyepeleka kesi mahakamani akipinga mabadiliko ya katiba mwaka 1993 yaliyokuwa yanazuia mgombea binafsi na mwaka 1994 alishinda.
Lakini alipeleka tena kesi hiyo mahakamani na kushinda, ingawa hadi sasa hilo halijawahi kutekelezwa.
Kwa mujibu wa Nkuba, mgombea huru ingetoa nafasi ya kupata wasiopenda kujihusisha na vyama vya siasa, lakini ni viongozi wazuri.
“Sijui uoga uko wapi lakini natamani siku moja ndani ya taifa letu waruhusu mgombea binafsi au mgombea huru,” amesema.
Amesisitiza umefika wakati kama ilivyo mambo mengine kuangalia uwezekano wa kuwa na mgombea huru, hata kama sio kwa ngazi ya urais angalau ngazi nyingine.
Chombo kuchunguza polisi
Wakati wanaharakati wakishinikiza kuundwa kwa chombo huru kitakachochunguza mwenendo wa jeshi la polisi, Nkuba naye ana msimamo kama huo, akifafanua kisiishie kwa polisi kichunguze vyombo vyote vya ulinzi na usalama.
Uwepo wa chombo hicho kwa mujibu wa Nkuba, utaongeza hali ya usimamizi wa vyombo vya dola.
“Hii inasababisha hata kama bila kuingilia majukumu, angalau na wao wanaweza kuwa na uoga kwamba sisi tusipofanya kwa kadri sheria inavyotaka kuna chombo kitatuchunguza na ikaanika maovu tutakayoyafanya,” amesema.
Ameeleza kwa maendeleo yaliyofikiwa sasa, ni muhimu kuwa na aina kama hiyo ya chombo.
Msingi wa majibu yake hayo ni swali aliloulizwa kuhusu hatua ya jeshi la polisi kujichunguza lenyewe linapokosea.
Aliambatanisha majibu yake hayo na msisitizo kuwa hafurahishwi na kuongezeka kwa matukio ya utekaji kama inavyoripotiwa, kadhalika anachukizwa na aina nyingine zote za uhalifu unaofanyika nchini.
Ili kudhibiti vitendo hivyo, ametaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwa makini zaidi hasa kuhakikisha vinawekeza kwenye kuzuia, badala ya kusubiri matukio yatokee ili kuyakabili.
Katika hilo, amesema wananchi wana wajibu wa kulisaidia jeshi la polisi kwa kutoa taarifa mapema pale wanapoona kuna tukio linakaribia.
Kwa upande wa jamii, amesema ni wadau wa kwanza kuhakikisha usalama wa watu na mali zao kwa sababu idadi ya askari haikidhi mahitaji ya ulinzi wa watu wote.
Kuhusu Ngorongoro
Alipoulizwa msimamo wake kuhusu yanayoendelea Ngorongoro, wakili huyo amesema kwa kuwa mgogoro kati ya wananchi na mamlaka hiyo ya hifadhi umedumu tangu miaka ya 1990, kuna haja ya pande mbili kufanya mazungumzo.
“Natamani kuona pande mbili zinakaa kujadili kuona kwa nini jambo hili halifiki mwisho na angalau kuwepo na maelewano,” amesema.
Amesema baraza la uongozi la TLS limetoa tamko na kwamba anaunga mkono kuwa yafanyike mazungumzo angalau wananchi wapate taarifa na kupatikana maelewano ya pande zote.
Maadhimisho ya Bavicha kuzuiwa
Alipoulizwa kuhusu kuzuiwa kwa maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yaliyoandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Nkuba amesema kama waliomba kibali na kuruhusiwa, walipaswa waachwe wafanye maadhimisho hayo.
Nkuba ambaye ni kada wa CCM aliyewahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho mwaka 2015 hadi 2020, amesema kama kuna sababu zinazoitwa za kiintelejensia, jeshi hilo linapaswa kuzitaja.
"Chombo kama Polisi kuzuia, inapaswa sababu zisiwe za jumla kunapaswa kuelezwe wazi sababu ya kina. Watu wanapoandaa mkutano wanakuwa wametumia gharama kubwa.
“Nadhani msingi wa kisheria ni hawa kukaa pamoja na kuzungumza kwamba katika hiki mnachotaka kukifanya kuna tishio moja au mbili, sasa tushirikiane namna ya kuzuia,” amesema.
Ameeleza haki hiyo ipo kikatiba na sheria zinatungwa kwa ajili ya kuhakikisha inalindwa.
Sheria za uchaguzi
Hata hivyo, Nkuba haoni sababu ya wakurugenzi wa halmashauri kutiliwa shaka juu ya kuusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa, ingawa vyama vya upinzani vina haki ya kulalamika.
Hoja yake hiyo inatokana na kile alichofafanua, mkurugenzi anapokwenda kusimamia uchaguzi anaapa na kiapo hicho kinaondoa unasaba wake na Serikali na nafasi yake ya uteuzi.
Hata hivyo, ameelezea mabadiliko ya jina la tume na kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), akisema yataongeza ufanisi katika utendaji ndani ya watumishi wake.
“Mabadiliko ya jina la tume yatamfanya hata anayefanya kazi ndani ya tume kuhakikisha anasimamia jambo bila kuingiliwa,” amesema.
Sambamba na hayo, Nkuba aliulizwa iwapo ana nia ya kuwania ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani kama ilivyokuwa mwaka 2015, amesema ni mapema kutangaza nia.
Amesema kwa kuwa utaratibu wa chama chake CCM unataka mbunge aliyepo kwenye nafasi aachwe afanye kazi kwa chake chote, naye analifuata hilo.
“Bunge litakapovunjwa, ukiniuliza Nkuba unakwenda kugombea na wapi hapo nitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kueleza. Lakini sio sasa,” amesema.
|
Wakati wadau wakilalamikia wimbi la utekaji nchini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kim
|
Wakati wadau wakilalamikia wimbi la utekaji nchini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepigia msumari kuundwa kwa tume ya majaji itakayofanya uchunguzi wa kina utakaowezesha kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Rais Samia Suluhu Hassan ndiye mwenye mamlaka ya kuunda tume hiyo chini ya Sheria ya Uchunguzi Mahususi.
Chadema si wa kwanza kupendekeza kuundwa kwa tume ya namna hiyo, Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Agosti 9, mwaka huu kilitoa pendekezo kama hilo kikishinikiza uchunguzi ufanyike.
Chama hicho kimeibuka na hoja hiyo kikirejea ripoti ya TLS iliyotaja orodha ya watu 83 waliotekwa na hadi sasa hawajulikani walipo.
Katika orodha hiyo, Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi aliwataja watu aliosema wametekwa na hadi sasa hawajulikani walipo, huku akisisitiza kuundwa kwa tume ya kijaji kwa ajili ya uchunguzi.
Wakati kukiwa na mashinikizo hayo, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imetangaza kufanya uchunguzi maalumu wa matukio hayo katika mikoa 15 yaliyotokea kati ya mwaka 2020 hadi 2024, ili kubaini chanzo na wahusika wake.
Mbowe aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chadema, Mikocheni.
Katika uchunguzi huo, alisema tume hiyo itapaswa kuzisikiliza familia za waathirika wa matukio hayo na kwamba anaamini tume hiyo itafanya kazi kwa haki, ukweli na uhuru.
Ili kushinikiza utekelezwaji wa hayo, Mbowe alimtaka Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kuwasilisha waraka mahususi kwa Rais Samia.
“Kama wasaidizi wake hawatampatia waraka wetu kuhusu mambo haya ya utekaji, basi tutamfikishia barua hiyo moja kwa moja,” alisema.
Katika ufafanuzi wake kuhusu matukio hayo, Mbowe alieleza kushangazwa na kuendelea kwa vitendo hivyo bila vyombo vya dola kuingilia kati au kuvitolea kauli.
Badala yake, alisema mamlaka mbalimbali zinaishia kuwabeza waathirika wa vitendo hivyo, jambo alilosema limesababisha chama hicho kiibuke kuzungumza.
“Inapotokea taarifa ya watu 80 kwenye mazingira yasiyoeleweka alafu vyombo vya dola vikakaa kimya na wengine wakaendelea kubeza, tumelazimika kuungana na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kupaza sauti,” alisema.
Kwa mujibu wa Mbowe, anatambua athari za kukemea vitendo hivyo hadharani, lakini ameamua kuzungumza ili hatua za kuvikomesha zichukuliwe.
Katika kile alichokiita uchunguzi uliofanywa ndani ya chama hicho, Mbowe alisema wamebaini asilimia 60 ya matukio ya kutekwa na kuuawa kwa watu yametokea katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Mbowe alieleza uchunguzi wao huo umebaini kuundwa kwa kikosi kazi ndani ya Jeshi la Polisi kilichohusisha jeshi hilo, Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Usalama wa Taifa kwa ajili ya kudhibiti uhalifu.
Lakini baadaye, alisema JWTZ liliondoka ndani ya kikosi hicho lilibaki jeshi la polisi na usalama wa taifa na majukumu yalibadilika kutoka kudhibiti uhalifu hadi kuteka wananchi.
Kwa mujibu wa Mbowe, kikosi kazi hicho kipo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Katika mazingira hayo, Mwenyekiti huyo alimtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa utaratibu wa uanzishaji wa vikosi kazi ndani ya vyombo vya dola.
Alieleza uwepo wa vikosi kazi hivyo unasababisha utekelezwaji wa majukumu kinyume na matakwa ya sheria, badala yake vinafanya kazi kwa kufuata utashi wa mtu.
Sambamba na hilo, alitaka kufanyika mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 2023, kuondoa kifungu kinachowapa maofisa usalama mamlaka ya kumkamata mtu pale zinapomuona anaweza kuhatarisha amani ya nchi.
Mamlaka hiyo waliopewa maofisa hao kwa mujibu wa Mbowe, ndiyo inayovunja utaratibu wa ukamataji watu kwa sababu usalama wa taifa hawa mfumo rasmi wa ukamataji na mahali pa kumpeleka aliyekamatwa.
Katika mazingira hayo, aliwataka Watanzania wasiendelee kupiga magoti wakati wanamalizwa na kwamba yeyote anayekwenda kuwakamata bila kujitambulisha wakatae.
“Raia tufike mahali tukatae kukamatwa kama kuku. Kama wanataka kukamata mtu wamfuate wajitambulishe kama PGO inavyotaka,” alisema.
Familia za waathirika
Mke wa Laifah Mbise ni mke wa Laifah Mbise mmoja wa vijana wanaodaiwa kutekwa, alisema kilio chake ni mumewe apatikane kwani zimeshapita siku kadhaa hajamwona.
Kinachomuumiza zaidi, alieleza ni kutoweka kwa mumewe ilhali wana mtoto mdogo waliokuwa wanamlea na sasa amebaki mwenyewe bila msaada.
“Alinitumia ujumbe kwamba anaitwa wakachukue pikipiki polisi, tangu hapo sijaonana na mume wangu hadi leo,” alisema.
Jackline Massawe ni Dada wa Jacob Mlay alisema tangu kaka yake ametoweka hakuonana naye hadi sasa akiwataka watanzania wasimame kushinikiza kukoma kwa vitendo vya utekaji.
Tume yachunguza
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu alisema tume hiyo inaendelea na uchunguzi wake wa matukio hayo ya tangu mwaka 2020 hadi 2024.
Jaji Mwaimu aliitaja miko itakayofanyiwa uchunguzi ni Dar es Salaam, Singida, Mara, Shinyanga, Mwanza, Kagera, Geita, Kugoma, Tanga, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Arusha, Ruvuma na Rukwa.
Matukio watakayoyafanyia kazi, alisema ni ya watu waliopotea na kuripotiwa kwenye vyombo vya habari pamoja na taasisi nyingine.
Alisema tayari tume hiyo imeshachukua hatua kadhaa kwa ajili ya uchunguzi wa matukio hayo ikiwemo utambuzi wa matukio hayo kulingana na vyanzo mbalimbali vya taarifa, uchambuzi kwa maana ya sehemu yalikotokea na watu wanaodaiwa kuhusika.
"Idadi ya matukio ya watu kupotea inatofautiana kutokana na Mikoa Kuna Mikoa ina idadi kubwa ya matukio na mingine ina idadi ndogo kwa hiyo tutakwenda kwenye maeneo 30 kwa ajili ya kuchunguza matukio hayo kwa muda wa wiki mbili hadi tatu na tutakuja na taarifa ya tulichokibaini huko," alisema.
Kuhusu matukio ya Shinyanga na Simiyu yaliyosababisha wananchi kuandamana baada ya kupotea kwa watoto, alisema uchunguzi utafanyika na watapendekeza hatua mahususi kwa taasisi husika.
"Kwa hiyo wananchi waliona ya kwamba hakuna hatua zozote zinazochukuliwa, lakini tume inaamini kwa kushirikiana na vyombo vingine vinavyohusika ni mambo yanayoweza kushughulikia na kupata ufumbuzi," alisema.
Kwa namna wanavyofuatilia Shinyanga, alisema vivyo hivyo wanafuatilia katika mkoa wa Simiyu na taarifa yake itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amelitaka Shirika la Nd
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amelitaka Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kuangalia zaidi safari za ndege zake zitakazopitia Zanzibar ili kukuza uchumi.
Kwa mujibu wa Dk Mwinyi, hatua hiyo itawezesha kuwavutia watlii wanaotembelea vivutio vilivyopo visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Rais Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 20, 2024 alipohutubia wananchi katika hafla ya mapokezi ya ndege aina ya Boeing 878-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Sheikh Abeid Amani Karume.
Katika hotuba yake hiyo, amesema ni muhimu shirika hilo likaangalia zaidi safari za ndege hizo zinazopitia Zanzibar ili kuvutia watalii wanaotembelea vivutio vilivyopo.
“Serikali itaendelea kusimamia sera na sheria za usimamizi wa anga ili kuona mashirika mengi ya anga yanafanya safari hapa nchini kwa manufaa ya uchumi wa nchi,” amesema.
Kuendelea kukua kwa kasi kwa sekta ya utalii nchini na kuongezeka kwa faida inayotokana na uchumi wa buluu, amesema kunategemea ufanisi wa ATCL.
Amesema kuwepo kwa usafiri wa anga wa uhakika unaoendana na mikakati ya kukuza uchumi ni muhimu.
“Hapa nataka nisisitize umuhimu wa kufanya safari za ndege kati ya Pemba na sehemu nyingine za nchi yetu kutokana na umuhimu wa fursa za utalii zilizopo huko ambazo bado hazijatumika,” amesema.
Kwa mujibu wa Dk Mwinyi, uwekezaji unaofanywa ndani ya ATCL una mchango mkubwa katika kukuza nchi na kuiunganisha kikanda na kimataifa.
Licha ya kukua kwa uchumi, Dk Mwinyi amesema bado kuna changamoto zinazowakabili wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi na kwamba, zinapaswa kutatuliwa.
Aliitaka Wizara ya Uchukuzi kuisimamia bodi ya ATCL ili kuhakikisha ndege zilizonunuliwa zinakuwa na tija iliyotarajiwa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara amesema hiyo ni ndege ya nane kupokewa katika Utawala wa awamu ya sita.
Amesema ndege hiyo ina uwezo wa kutembea saa 14 hadi 24 bila kutua, imegharamiwa na Serikali kwa zaidi ya Sh300 bilioni.
Amesema baada ya ndege hiyo, ATCL linakuwa la kwanza katika ushoroba wa kati hivyo inachochea matumizi makubwa ya Bandari na reli na kuongeza uchumi wa taifa.
Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa, ATCL limekua kutoka wastani wa Dola za Marekani 17 milioni hadi Dola za Marekani 70 milioni kwa mwaka.
"Shirika linaendelea kuchochea uchumi limechangia Dola za Marekani 182 katika Pato la taifa, wapo wanaweza kusema kuna hasara lakini kiuchumi kuna faida kubwa," amesema
Amesema kuongezeka kwa ndege za aina hiyo na kufikia tatu kunapunguza changamoto ya kukosa safari pindi ndege moja inapoharibika.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema ndege hiyo zimefanya kufika ndege 16 ikiwemo ndege moja ya Bombadia iliyokuwapo
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Zanzibar, Dk Khalid Mohamed Salum amesema Serikali inaendelea kufanya maboresho ya miundombinu ikiwemo upanuzi na ujenzi wa viwanja vya ndege Unguja na Pemba.
Amesema kwasasa unafanyiwa marekebisho Uwanja wa Terminal 2 ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 1.4 milioni na baada ya kukamilika Zanzibar itakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 300 kwa mwaka.
Pia amesema Uwanja wa ndege wa Pemba upo Kwenye mchakato wa kuanza ujenzi wake ambapo utaongezwa urefu kutoka mita 1500 hadi 2500 na utakuwa na uwezo wa kutua ndege kubwa za Kimataifa aina ya Dreamliner kama hiyo iliyopokewa.
"Kadhalika linajengwa jengo jipya la abiria, baada ya kukamilika miradi yote hii uchumi wa Nchi utafunguka kwa Kiasi kikubwa," amesema
Amesema uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume umepata tuzo nne kwa kipindi kifupi ikiwemo ya kiwanja Bora barani Afrika ambapo inatarajiwa kupokewa Septemba mwaka huu Atlanta Marekani.
Tuzo zingine ni kiwanja Bora kusafirisha abiria chini ya milioni mbili, kiwanja Bora vyakula na vinywaji, na tuzo ya Uwanja Bora wa kusafirisha mizigo na abiria kwa usalama zaidi.
Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 262 ambapo viti 22 ni vya daraja la Biashara na viti 240 daraja la kawaida.
Pia ndege hiyo ina uwezo wa kubeba mizigo kati ya tani 15 hadi 20 kulingana na ujazo wa abiria na mizigo.
Hii ni Ndege ya 15 kununuliwa na Serikali tangu mwaka 2016 Serikali ilipochukua hatua za kuifufua kampuni ya ATCL.
Awali ndege hiyo ilipaswa kupokewa Agosti 19, 2024 katika Uwanja huohuo lakini ilishindikana kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana hali mbaya ya hewa ilipotengenezwa nchini Marekani hivyo ikashindwa kupaa.
|
Miongo sita iliyopita siku kama ya leo, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lilizaliwa baada ya kukami
|
Miongo sita iliyopita siku kama ya leo, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lilizaliwa baada ya kukamilika mchakato wa kuunganishwa kati ya lile la Zanzibar na Tanganyika.
Jeshi la Zanzibar wakati huo liliitwa la Ukombozi, huku Tanganyika likiitwa Military Force na muungano huo uliunda jina la Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania, tangu Septemba 1, 1964.
Kama utahusianisha miaka ya jeshi hilo na umri wa binadamu, kwa miongo sita ni mzee aliyefikia umri wa kustaafu kwa lazima katika utumishi wa umma.
Lakini, umri huo kwa JWTZ ni tafsiri halisi inayoakisi kuzaliwa, kukua, kukomaa na sio kuzeeka kama ilivyo kwa binadamu.
Katika kusherehekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ, maofisa wa jeshi hilo, viongozi na wananchi wamefurika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kushuhudia shamra shamra hizo.
Hali ya wingu zito na manyunyu ya mvua, hayakuwa kikwazo kwa wananchi kuhudhuria sherehe hizo.
Mbali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Wakuu wa Wilaya zote za Dar es Salaam, Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson alihudhuria sherehe hizo.
Dk Tulia alifuatiwa na Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, kisha Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.
Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ndiye aliyefuatia, kisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Suleiman Abdullah.
Abdullah alifuatuwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyefika katika uwanja huo saa 3:19 asubuhi.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob Mkunda ndiye aliyefuatia, kisha Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango aliingia.
Alivyoingia Rais Samia
Rais Samia Suluhu Hassan amewasili katika viunga hivyo saa 3:57 asubuhi na kuzunguka uwanja wote akiwa kwenye gari maalumu kusalimia waliohudhuria.
Baada ya kuzunguka Mkuu huyo wa nchi aliyekuwa amevalia gwanda la JWTZ, mizinga 21 isiyo na madhara ilipigwa ikisindikizwa na wimbo wa taifa na beti mbili za wimbo wa Afrika Mashariki.
Kisha, Rais Samia alikwenda kukagua gwaride katika vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama na wimbo wa taifa uliimbwa tena.
Wimbo huo ulifuatiwa na gwaride la vikosi mbalimbali vya JWTZ na lililoonekana kuwavutia wengi zaidi ni lile la wanamaji kutokana na mavazi yake meupe.
Kama ungekuwa nje ya uwanja huo, ungedhani ni kelele za wanaoshangilia mchezo wa mpira wa miguu, lakini shangwe hizo, ziliakisi furaha ya wahudhuriaji juu ya mwendo na matendo sambamba yaliyofanywa na wanagwaride.
Mistari ya vikosi vya ulinzi na usalama hivyo, ilipangwa mithiri ya iliyonyooshwa kwa rula na haikuwa hivyo, kwa JWTZ pekee, hata Mgambo walikuwa vema.
Nakosa mnyama rahisi wa kumfananisha ukubwa sawia na mbwa walioshuhudiwa na kikosi cha mbwa cha JWTZ, ni wakubwa mithiri ya simba jike aliyezaa mara kadhaa.
|
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camilius Wambura amemuondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mal
|
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camilius Wambura amemuondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya na nafasi yake kurithiwa na George Katabazi, huku jeshi hilo likitangaza kuwafikisha mahakamani leo wanaotuhumiwa kumbaka na kumlawiti binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya.
Kamanda Mallya anaondolewa katika nafasi hiyo, siku moja baada ya kutoa kauli juu ya mwenendo wa upelelezi wa tukio la kulawitiwa na kubakwa kwa binti huyo, lililoanza kusambaa katika mitandao ya kijamii tangu Agosti 2, mwaka huu.
Katika kauli yake hiyo alipozungumza na Mwananchi jana, kamanda huyo alisema: “Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza ‘kahaba’.”
“Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo,” alisema Kamanda Mallya.
Sambamba na kuondolewa katika nafasi hiyo na kurudishwa Makao Makuu, jeshi hilo limeyakana maneno ya kamanda huyo likisema si msimamo wa chombo hicho cha dola.
Taarifa ya Polisi kumhamisha kamanda Mallya na kukana maneno yake, imetolewa leo Jumatatu, Agosti 19, 2024 na kutiwa saini na Msemaji wa jeshi hilo, David Misime.
“Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa kauli hiyo kama inavyoonekana kwenye hicho kichwa cha habari siyo msimamo wa Jeshi la Polisi na kwamba kauli sahihi ya Jeshi la Polisi ni kama zilivyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kwa umma Agosti 4, 6 na 9, 2024,” imeeleza taarifa hiyo.
Kichwa cha habari kilichotajwa na jeshi hilo kimenukuliwa katika vyombo vya habari kikisema "RPC: ANAYEDAIWA KUBAKWA NA KULAWITIWA ALIKUWA KAMA ANAJIUZA".
Taarifa hiyo imesema kichwa hicho cha habari kimetokana na mazungumzo kwa njia ya simu na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi.
Katika mawasiliano ya wawili hao, taarifa hiyo inafafanua mwandishi alimuuliza kamanda huyo Je, upelelezi wa kesi umekamilika? na swali lingine alilomuuliza inadaiwa alikuwa anajiuza? Majibu ya kamanda aliyomjibu mwandishi huyo ni kwamba hata kama ni hivyo hangestahili kutendewa hivyo.
“Vile vile, tungependa kujulisha kuwa watuhumiwa wa kesi hiyo watafikishwa mahakamani leo Agosti 19, 2024,” imeeleza.
Hata hivyo, jeshi hilo limeomba radhi kwa kila mmoja aliyeguswa na kuchukizwa na kauli hiyo inayosambaa kwenye vyombo vya habari wakati ufuatiliaji ukifanyika kupata usahihi wake.
|
Maswali tata yamegubika mwenendo wa uchunguzi wa tukio la kubakwa na kulawitiwa kwa binti anayedaiwa
|
Maswali tata yamegubika mwenendo wa uchunguzi wa tukio la kubakwa na kulawitiwa kwa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theropista Mallya kufafanua kuhusu hatua za uchunguzi huo.
Maelezo ya kamanda huyo yaliyoibua maswali ni kuhusu vijana hao kutotumwa na afande, lakini aliwataja walikuwa kama walevi na wavuta bangi, huku binti akidaiwa kujiuza ‘kahaba.’
Ufafanuzi huo wa Kamanda Mallya alioutoa katika mazungumzo yake na Mwananchi jana, umehojiwa na wadau wakiuliza, ukahaba wa binti huyo unahalalisha kubakwa au kulawitiwa?
Maswali hayo yameibuliwa leo Jumatatu, Agosti 19, 2024 na Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka alipozungumza na Mwananchi Digital baada ya majibu ya polisi.
Licha ya madai ya polisi kuwa, binti huyo alikuwa anafanya biashara ya ngono ‘Ukahaba’ Madeleka amehoji Je, hilo linahalalisha kubakwa au kulawitiwa?
Swali lingine lililoibuliwa na wakili huyo ni ukahaba alionao binti huyo unamnyima haki ya uraia, kulindwa na kuhakikishwa usalama wake na vyombo vya dola?
Kadhalika, amehoji kilichoelezwa na Kamanda Mallya kuwa waliohusika ni walevu na wavuta bangi Je, sifa hizo zinawapa uhalali wa kutenda tukio hilo na hawaruhusiwi kukamatwa?
Kwa mtazamo wa jumla, wakili huyo amesema kilichozungumzwa na jeshi hilo hakina mashiko ya kisheria na ni uthibitisho kuwa aliyezungumza hastahili kuendelea kuwa kiongozi ndani ya jeshi la polisi.
“Ni kauli ya kibaguzi kwamba anayefanya biashara ya ngono anastahili kubakwa na kulawitiwa,” amesema Madeleka.
Maoni ya mtandaoni
Watu maarufu nao hawakuwa nyuma kutoa maoni kuhusu kauli hiyo, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani twitter), Msanii wa Muziki wa HipHop, Frida Amani ameandika: “Yaani tuone mtu akibakwa halafu tuambiwe aliyebakwa alikuwa anajiuza.
“Kwa nini tutafute njia ya kuonesha alichofanyiwa ni sawa jamani hii leo imeniuma sana,” ameandika Frida.
Maoni yanayofanana na hayo yaliandikwa pia na Carol Ndosi aliyeandika tukio lililofanywa kwa binti huyo la kinyama.
“Wanaojaribu kulirahisisha na kuwatengenezea njia wale vijana na waliomtuma wasiwajibishwe ni wanyama zaidi. Tujuane kama taifa,” ameandika.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Msichana Initiative, Rebeca Gyumi ameandika Polisi haina mamlaka ya kuchambua ushahidi na kuhitimisha bila kupeleka mahakamani.
“Polisi imegeuka mahakama inaamua kesi yenyewe, polisi haina mamlaka ya kuchambua ushahidi na kuhitimisha bila kupeleka mahakamani. Polisi is gaslighting us makusudi kabisa, mnatuchochea,” ameandika.
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Tito Magoti ameandika kulinda wahalifu sababu ya ushirika wao na Serikali ni kuutomasa utawala wa sheria.
“Jeshi la polisi kwa mara nyingine mmetukosea sana. ni ‘kahaba,’ so what? Nyie ni mahakama? priority ni victimisation ya victim? mna maslahi gani na ule uhalifu? Hamfai na mnalithibitisha hilo,” ameandika.
Maoni mengine yalimlenga moja kwa moja Kamanda Mallya, kama ilivyoandikwa na miriamah187 kupitia mtandao wa Instagram.
Ameandika:” Bahati nzuri wewe ni mama umezaa katika uzao wako una binti kama huna wano wa ndugu zako, tusema Amina Mwenyezi Mungu kama anasikia na kuona video inajieleza yenye omba msamaha kwa afande.”
Ameongeza video hiyo inajieleza lakini haki inapindishwa bila huruma, jambo alilodai linatiwa woga.
“Kuna siku watu wataamka ipo siku. Siku zote maumivu yakikomaa unaingiza ujasiri ipo siku,” ameandika.
Alichoandika Dk Gwajima
Katika mtandao huo huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima amesema tayari alishawasilisha maoni ya wananchi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni.
Amewataka wananchi wampe muda Masauni afanyie kazi maoni hayo kisha atatoa taarifa.
Majibu yake hayo, amesema yametokana na kupokea maoni mengi ya wananchi wakionyesha hisia zao juu ya mwenendo wa upelelezi wa tukio hilo.
“Ndugu Wananchi, ni dhahiri kuwa, alichofanyiwa 'Binti wa Yombo' ni kitu kibaya kisicho cha utu hivyo, anastahili haki yake kwa mapana yote,” ameandika.
Hata hivyo, amewataka wananchi waendelee kujipa muda kwani haki itatendeka kwa mujibu wa sheria na itaonekana bayana na si vinginevyo.
Historia ya tukio
Tukio hilo lilianza kwa kusambaa kwa picha jongefu katika mitandao ya kijamii zilionyesha Agosti 2, mwaka huu likionyesha vijana watano wakimbaka na kumlawiti binti huyo aliyejitambulisha kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Dar es Salaam.
Katika kipande hicho cha video, binti huyo alishurutishwa kumwomba radhi mtu aliyetajwa kuwa Afande na alisikika akifanya hivyo.
BaadayeAgosti 9, mwaka huu, Jeshi la Polis kupitia Msemaji wake, David Misime lilitangaza kuwakamata vijana wanne waliohusika na ubakaji huo na wengine wanne kwa kosa la kusambaza video hiyo.
Lakini, jana kamanda Mallya amesema upepelezi wa tukio hilo umekamilika na wakati wowote jalada litafika kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
|
Baada ya kupotea kwa siku nne ikidaiwa ametekwa na vijana watatu hatimaye, Ally Pweku (22) Mkazi wa
|
Baada ya kupotea kwa siku nne ikidaiwa ametekwa na vijana watatu hatimaye, Ally Pweku (22) Mkazi wa Mbwate, mkoani Pwani, amekutwa amefariki vichakani.
Inadaiwa kijana huyo alitekwa usiku wa Agosti 14, 2024 kwenye moja ya baa zilizopo mtaani hapo, alikokuwepo akipata kinywaji cha pombe.
Kwa mujibu wa wakazi wa mtaa huo, wamegundua mwili wa Ally baada ya kuhisi harufu kali iliyotokea eneo ulikokuwepo mwili huo, ambalo si mbali sana na makazi ya watu.
Mmoja wa majirani hao aliyeomba hifadhi ya jina lake, amesema wakati anarudi nyumbani kutoka kwenye shughuli zake, alihisi harufu kali na ndipo alipoamua kuifuatilia.
"Nikafuatilia na nilipokaribia nikaona mwili wa mtu amefariki nikashituka," amesema.
Baada ya kubaini hilo, amesema alimfuata Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kumpa taarifa na walipokwenda pamoja walikuta mwili umeharibika.
Akizungumzia hilo, Menyekiti huyo, Abdalah Mtandi amesema tayari walishafanya mawasiliano na jeshi la polisi kwa ajili ya kuuchukua mwili huo kwa kuwa ulishaharibika.
Waliposikia taarifa za kutekwa kwa Ally, amesema walimtafuta katika maeneo mbalimbali bila mafanikio na hadi unapatikana mwili wake, walikuwa katika harakati za kumtafuta.
"Alipopotea tulimtafuta kwa juhudi kubwa lakini hatukumpata na hatimaye leo amepatikana akiwa amefariki na tumeshawapa taarifa polisi wamesema wanakuja" amesema.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa siku ya tukio la kutekwa kwake, wanasema alifika katika baa hiyo kwa ajili ya kunywa pombe ilipofika saa nne usiku walitokea vijana watatu walimbeba kwa nguvu na kutokomea naye kusikojulikana.
Mama mzazi wa kijana huyo, Tatu Putu amesema siku ya tukio mwanawe alirudi mapema kutoka kazini na limuaga kuwa anakwenda baa na angerejea baadaye.
Amesema hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kuzungumza na kuonana na mwanawe huyo kwani hakurejea kama alivyoahidi, jambo lililompa wasiwasi kupitiliza.
Kutokana na mazingira hayo, amesema alikwenda kwa Mwenyekiti huyo kutoa taarifa za kutoweka kwa kijana wake na juhudi za kumtfuta ziliendelea bila mafanikio.
Balozi wa mtaa huo, Linda Salimu amesema baada ya taarifa ya kutekwa kwake aliambatana na viongozi wengine kwenda hadi eneo la tukio, lakini hawakumkuta Ally wala waliodaiwa kumteka.
Juhudi za kumtafuta ziliendelea bila mafanikio na hatimaye wamepokea taarifa kuwa, amefariki.
Mhudumu wa baa
Mhudumu wa zamu katika baa alikokwenda kunywa pombe kijana huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Neema amesema Ally alifika hapo saa mbili usiku akaagiza kinywaji na baadaye waliingia watu wengine.
Ameeleza baada ya kuingia watu hao watatu walikuwa katika mazungumzo na Ally na baadaye ikaonekana wanamchukua kwa nguvu na kutokomea naye.
"Hakukuwa na watu wengi lakini alipofika aliagiza pombe nikamhudumia nikaenda jikoni wakati niko huko nilisikia hali ya mvutano kama wanagombana na niliporudi niliwasikia kwa mbali wanasema ndio huyu ndio huyu na wakatokomea naye," amesema.
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema wamepata taarifa juu ya tukio hilo na kwamba watalitolea ufafanuzi kesho.
|
Joto la uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) linaanza ku
|
Joto la uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) linaanza kufukuta, huku likiibuka swali la nani kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu atakayepitishwa kuipeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi hiyo.
Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, ameshaonyesha kusudio la kuwania wadhifa huo na tayari ameshamwandikia barua Katibu Mkuu, John Mnyika kuonyesha nia yake.
Sio siri tena, nia yake hiyo ameiweka wazi hata katika mahojiano mbalimbali aliyoyafanya katika vyombo vya habari, akisema amemwandikia Mnyika barua ya nia ya kugombea urais 2025 na nia ya kuwania nafasi aliyonayo sasa ndani ya chama hicho.
Wakati mambo yakiwa hadharani kwa upande wa Lissu, Mbowe ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chadema taifa, ameamua kukaa kimya, lakini duru zinaeleza naye ni miongoni mwa wakata tiketi ya kuomba ridhaa ya Chadema kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani.
Halitakuwa jambo jipya kwa yeyote kati yao kuwania urais, kwa nyakati tofauti walishawahi kushiriki kinyang’anyiro hicho, Mbowe katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na Lissu aligombea mwaka 2015.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Mbowe alipata kura 668,756 akishika nafasi ya tatu dhidi ya kura 9,123,952 za mshindi wa kiti hicho aliyekuwa mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete. Nafasi ya pili ilishikwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 1,327,125.
Wakati wa Lissu nao mambo yalikuwa hivyo hivyo, aliukosa urais kwa kupata kura 1,933,271 akishika nafasi ya pili dhidi ya mgombea wa CCM, John Magufuli aliyeshinda wadhifa huo kwa kura 12,516,252 sawa na asilimia 84.
Hata hivyo, wagombea wote hawana historia ya kushiriki au kufanya siasa nje ya Chadema, wote walisikika wakiwa upinzani na umaarufu wao wa kisiasa umetokana na chama hicho.
Katika historia ya Chadema, haikuwahi kurudia kumsimamisha mgombea aliyeshiriki kinyang’anyiro hicho, jambo linaloibua swali Je, mwakani kitamrejesha aliyewahi kushindwa nafasi hiyo?
Kauli ya Lissu
Akihojiwa katika kipindi cha Medani za Siasa kinachorushwa na Kituo cha Luninga cha Star TV juzi, Lissu alisema alishamwandikia Katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika barua ya nia yake ya kuwania urais mwaka 2025 na kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti bara katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho.
“Mwanachama anayetaka kugombea kwa mujibu wa kanuni kwa kutegemea nafasi anayotaka, anatakiwa kumwandikia Katibu wake wa ngazi husika barua ya kusudio la kutaka kugombea,” alisema.
Hata hivyo, aliweka wazi kuwa iwapo chama chake hakitampitisha yeye, atamuunga mkono mgombea yeyote atakayependekezwa na chama hicho kuwania nafasi hiyo.
“Sikuzaliwa nije kuwa mgombea urais wa Chadema nilijiunga na Chadema hata miaka 20 haifiki na nimefanya hivyo nikidhani ndicho chama chenye msingi ya ukweli wa mabadiliko ya kijamii na kila kitu. Nimekuwa tayari na niko tayari kutumikia nafasi yoyote ile,” alieleza.
Lakini, alisema atakaposhinda urais moja ya vitu atakavyofanya ni kujiuzulu wadhifa wake ndani ya Chadema ili kutenganisha dola na chama, tofauti na ilivyo sasa kwa CCM.
Chadema yathibitisha
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alikiri kupokea barua za Lissu akitia nia katika nafasi hizo.
Kinachofuata baada ya hatua hiyo, alisema ni kupeleka kusudio hilo la Lissu mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho kwa ajili ya uamuzi wa kupitishwa au vinginevyo.
“Muongozo wa utiaji nia katika kanuni za chama chetu (Chadema), mamlaka ya Katibu Mkuu yanaishia kwenye kupokea barua lakini si kutangaza majina. Hivyo nitapeleka Kamati Kuu kwakuwa ndiyo yenye mamlaka ya kuamua,” alieleza.
Alipoulizwa iwapo kuna barua za watiania wengine mbali na Lissu, Mnyika alifafanua ni kinyume na kanuni za chama hicho kuliweka hadharani hilo.
“Nimekujibu kuhusu Lissu kwa sababu umeniambia mwenyewe ameweka wazi, sasa siwezi kuweka wazi kama nimepokea nia ya mwingine yeyote au laa na siwezo hata kutaja ni kinyime na matakwa ya kanuni,” alisisitiza.
Nani anafuatiliwa zaidi
Takwimu za Google Trends katika kipindi cha miezi mitatu yaani siku 90 zilizopita, zinaonyesha Lissu amefutiliwa zaidi ukilinganisha na Mbowe katika mikoa mitano ya Tanzania bara.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, katika Mkoa wa Morogoro Lissu alifuatiliwa kwa asilimia 66, dhidi ya asilimia 34 alizofuatiliwa Mbowe, vivyo hivyo katika Mkoa wa Arusha.
Katika Mkoa wa Pwani Lissu aliongoza kufuatiliwa kwa asilimia 60 dhidi ya asilimia 40 za Mbowe, huku mkoani Dodoma Lissu akiongoza kwa asilimia 70 dhidi ya 30 za Mbowe.
Ni Mkoa wa Kilimanjaro pekee ndiko ambako Mbowe ameongoza kufuatiliwa kwa asilimia 54, akimzidi Lissu aliyefuatiliwa kwa asilimia 46.
Mitazamo ya wanazuoni
Ingawa Mbowe ana haiba ya kiuongozi, lakini Lissu anawavutia wapiga kura zaidi, kama inavyoelezwa na Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Out), Dk Revocatus Kabobe.
Kwa mujibu wa Dk Kabobe, wawili hao wanatofautiana haiba ya kiuongozi na mvuto kwa wapiga kura, kila mmoja ana turufu yake kwa wanachama na wafuasi wa Chadema.
“Hawa watu wawili wana siasa za tofauti mbele ya wapiga kura. Kariba ya Lissu ni ya kimageuzi wakati Mbowe anawaza zaidi maridhiano. Mikikimikiki ya Lissu inaonekana kushawishi wapiga kura wengi zaidi ya Mbowe,” alieleza.
Kwa mtazamo wa mwanazuoni huyo, Lissu pia anabebwa na uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja na kuifafanua kwa umma, ikaeleweka, tofauti na Mbowe.
Katika mazingira ya sasa, Dk Kabobe alisema Chadema inahitaji mgombea mwenye uwezo wa kujenga hoja na kuonyesha mbinu za kutatua changamoto za watu.
Kadhalika, alisema chama hicho kinahitaji mgombea mwenye uwezo wa kufafanua hoja zilizoibuliwa na zitaibuliwa na wapinzani wao kwenye majukwaa ya kisiasa, akisisitiza “Maoni yangu binafsi naona mtu sahihi zaidi kwenye haya ni Lissu."
“Kama Chadema wangeamua kuchagua mgombea leo nadhani turufu yao ingeenda kwa Lissu na kumwacha Mbowe abaki kama baba na mlezi wa viongozi wa sasa na wa baadaye ndani ya chama. Pengine tunaweza ona tofauti kadiri mda unavosogea,” alieleza mwanazuoni huyo.
Mzani upo sawa
Wakati Dk Kabobe akiwa na mtazamo huo, Mhadhiri mwingine wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Mohamed Bakari alisema kuna mizania sawa ya nguvu za kisiasa kwa Lissu na Mbowe.
Kwa uwezo, historia, harakati na ushawishi wawili hao, alisema ni kama wanalingana, kunahitajika utafiti kubaini nani zaidi na sio kwa jicho la kawaida.
“Kwa hali ilivyo wote wana nguvu ya siasa. Ni vigumu kuonyesha nani zaidi bila utafiti, lakini nyakati zinabadilika tusubiri siku zijazo pengine ataonekana yupi zaidi,” alisema mwanazuoni huyo.
|
Uamuzi wa mamlaka ya uteuzi kuwang’oa viongozi hasa katika Baraza la Mawaziri, umetajwa kuchochewa n
|
Uamuzi wa mamlaka ya uteuzi kuwang’oa viongozi hasa katika Baraza la Mawaziri, umetajwa kuchochewa na kasoro za ufanisi katika utendaji wao.
Kwa mujibu wa wanazuoni, mabadiliko yoyote hasa yanayohusisha kumuondoa kabisa kiongozi, yanalenga kuleta ufanisi ambao usingepatikana kama angebaki aliyekuwepo.
Wanazuoni hao wanakuja na mtazamo huo, baada ya mabadiliko yaliyofanywa katika baraza la mawaziri, ambayo pamoja na wengine kuhamishwa, Ummy Mwalimu ameondolewa kabisa.
Ummy aliyekuwa katika baraza hilo kwa zaidi ya miaka saba akihudumu wizara mbalimbali ikiwemo ya Afya na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ameondolewa jana Agosti 14, mwaka huu.
Kwanini wameondolewa
Akizungumzia baadhi ya viongozi waliong’olewa, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Out), Dk Revocatus Kabobe alisema kilichochochea mabadiliko ya baadhi ya mawaziri ni utendaji.
Alimtolea mfano Ummy, pamoja na kusifiwa na Rais Samia katika siku za karibuni, kwa namna yoyote kuna kasoro za kiutendaji alizozionyesha na kusababisha kuondolewa.
“Hizi ni kasoro za kiutendaji hata kama alisifiwa pengine amekosea hivi karibuni na ameondolewa. Kwa sababu kama Rais anasema mabadiliko yamelenga kuongeza ufanisi maana yake aliyemtoa hakuwa na huo ufanisi,” alisema.
Hata hivyo, alifafanua hilo haliwahusu wale waliohamishwa kutoka eneo moja kwenda lingine, akimtolea mfano Jaji Eliezer Feleshi ambaye ametoka kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufani.
“Feleshi yeye kapanda kwa sababu nafasi aliyonayo sasa ina ulinzi zaidi ya aliyokuwa nayo. Hawezi kutumbuliwa haguswi ni nafasi atakayotumikia hadi atakapostaafu kwa hiyo amepanda,” alisema.
Mwanazuoni wa Sayansi ya Siasa, Profesa Ambrose, Profesa Kessy alisema mabadiliko hayo msingi wake ni kuongeza ufanisi wa kazi katika ofisi za umma.
Alisema waliohamishiwa maeneo mengine, ni utaratibu wa kawaida ambao aghalabu Serikali inaufanya baada ya kuona uwezo wa mtumishi husika unafaa zaidi eneo lingine.
“Ikitokea mamlaka ya uteuzi inaona mtu ana uwezo mzuri lakini haustahili kwenye nafasi aliyonayo sasa na anapwaya inamhamisha kumpeleka anakostahili, yote lengo ni kuongeza ufanisi,” alisema.
Kwa upande wa walioachwa, alisema bado lengo la kuongeza ufanisi ndilo sababu za uamuzi huo.
Kuhusu viapo
Akizungumzia msisitizo wa Rais Samia kuhusu wateule kuzingatia viapo vyao, Profesa Kessy alisema kiapo ndilo agano kati ya mtumishi, wananchi na mamlaka ya uteuzi.
Mteule anapoapa, alieleza anafunga agano au kukubali kuwajibika na kutumikia kwa niaba ya wananchi na Serikali iliyompa nafasi hiyo.
“Kiapo maana yake ni lile agano ulilopewa kati ya Serikali na wananchi kwa maana utaboresha huduma na kutumikia kama unavyopaswa,” alisema.
Rais Samia anapowasisitiza wazingatie viapo vyao, alisema analenga kuwasihi wasiende kinyume na makubaliano ya dhamira ya kuteuliwa kwao.
Kwa maneno mengine, alisema anawasisitiza wakawahudumie wananchi na kuitumikia Serikali ambao ndiyo msingi wa kiapo.
Na hata waliorudishwa akiwemo Profesa Palamagamba Kabudi na William Lukuvi alisema mamlaka ya uteuzi imeona nafasi walizopewa zinawafaa wao.
Alichokisema Rais Samia
Akizungumza wakati akiwaapisha wateule hao, Rais Samia Suluhu Hassan aliwataka kwenda kufanya kazi kwa kutumia umahiri wa taaluma walizosomea na panapotakiwa kujiongeza wafanye hivyo.
Mkuu huyo wa nchi, aliyetumia chini ya dakika tatu kutoa neno kwa wateule aliowaapisha, ameahidi kuwaita viongozi hao kila sekta kwa ajili ya kuzungumza nao.
“Ninachotaka kusema ni kile alichokisema Makamu wa Rais kuwa kwenye kufanya kazi zenu kuna umahiri wa ulichosomea na kujiongeza kutumia common sense. Pale unapoona common sense inaweza kutumika vizuri tumieni, jiongeze fanyeni kazi tuwatumikie wananchi,” alisema Samia.
Kutokana na safari aliyokuwa nayo leo ya kuhudhuria vikao vya Jumuiya ya Maendeleo za Kusini mwa Afrika (SADC), alisema atazungumza na wateule hao kwa sekta zao kwa kadri itakavyopangwa.
Hata hivyo, alieleza mabadiliko aliyoyafanya ni ya kawaida yanayolenga kuongeza ufanisi katika utendaji.
“Tunachotarajia kwenu ni kuongeza ufanisi katika maeneo yenu. Mmeapa hapa kiapo cha maadili na kiapo kwa dini zenu mnazoamini, mkaishi na viapo hivyo lakini pia mkafuate maadili ya kikazi yanayotakiwa,” alisema Rais Samia.
Tatizo sio sheria
Akizungumza katika hafla hiyo, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma alisema mapungufu ya sheria, bajeti au taasisi si changamoto zinazozikabili nchi zinazoendelea, bali tatizo ni wanaopewa nafasi za kutekeleza sheria na wale wanaolengwa nazo.
Kwa mujibu wa Profesa Juma, matatizo kwa wanaopewa nafasi hizo yanatokana na wengi wao kuwa na tabia na tamaduni binafsi ambazo aghalabu hupoteza malengo yanayolengwa na sheria.
“Kwa hiyo tunapokwenda sehemu zetu za kazi, pamoja na kuangalia sheria lakini lazima tuangalie nafsi zetu wenyewe, tuna fikra hasi zozote, tuna tabia ambazo zinafanya sheria zisifanye kazi,” alisema.
Sambamba na hilo, Jaji Mkuu huyo alisema ni muhimu jamii isiweke msisitizo zaidi katika kudai haki, bila kutimiza wajibu wanaopaswa.
“Watu wengi wameshajitokeza kwamba sasa hivi tunataliwa zaidi na haki lakini tunasahau kwamba demokrasia inajengwa zaidi na kuwajibika wewe mwenyewe mwananchi unayelengwa na sheria una wajibu kwa nchi yako tunatimiza hilo sharti kwa namna gani,” alisema.
Aliwataka wateule wote kulinda imani waliyopewa na Rais Samia, akisema kinyume na kufanya hivyo wataipoteza imani hiyo.
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango aliwataka wateule wote kuviishi viapo walivyokula na kutimiza matumaini ya Rais Samia ya kuona Watanzania wanapata huduma bora.
“Kila mmoja akafanye kazi kwa bidii mkashirikiane na viongozi wengine mtakaowakuta kwenye nafasi zao ili twende sawa kama taifa,” alisema.
|
Unyeti wa Wizara ya Maliasili na Utalii na rundo la wajibu unaotegemea utashi wa wizara nyingine, nd
|
Unyeti wa Wizara ya Maliasili na Utalii na rundo la wajibu unaotegemea utashi wa wizara nyingine, ndiyo sababu iliyotajwa na wadau kuifanya wizara hiyo iwe mapito ya muda mfupi kwa kila anayeteuliwa.
Kauli hiyo ya wadau inakuja, wakati ambao Wizara ya Maliasi na Utalii imeonekana kukumbwa na kila wimbi la mabadiliko yanayofanywa na mamlaka ya uteuzi.
Waziri wa sasa katika wizara hiyo ni Dk Pindi Chana aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan jana Agosti 14, 2024 akichukua nafasi ya Angellah Kairuki aliyehudumu kwa miezi 11 pekee.
Si ajabu katika historia ya wizara hiyo, kukuta waziri amehudumu muda mfupi kama aliohudumu Kairuki na wengine wametumikia chini ya muda huo.
Kwa kipindi cha miaka 19, tangu 2005 alipoingia madarakani Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete hadi sasa Agosti mwaka 2024, Wizara ya Maliasili na Utalii imetumikiwa na mawaziri 14.
Hiyo ni sawa na kila waziri amehudumu wastani wa mwaka mmoja na miezi mitatu ndani ya wizara hiyo kwa kipindi hicho cha miaka 19.
Lakini, tangu uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Wizara ya Maliasili na Utalii, imetumikiwa na mawaziri 27 hadi sasa. Sawa na kila waziri amehudumu kwa wastani wa miaka miwili na miezi mitatu.
Zakhia Megji ndiye mwanasiasa mwenye rekodi ya pekee ya kudumu zaidi ndani ya wizara hiyo, akihudumu tangu mwaka 1997 alipoteuliwa na Rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa hadi mwaka 2005.
Mawaziri tangu uhuru
Baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Tewa Tewa ndiye aliyefungua pazia la utumishi katika wizara hiyo akiteuliwa na Baba wa Taifa, Julius Nyerere mwaka 1962 hadi 1965.
Aliyemfuata ni Dereck Bryceson aliyehudumu kuanzia mwaka 1965 hadi 1970, kisha Hosnu Makame aliyekuwa waziri kuanzia mwaka 1970 hadi 1975.
Upepo wa kuhudumu kwa miaka mitano mitano, uliishia kwa Solomon Saibul aliyeongoza kuanzia mwaka 1975 hadi 1980 na waliofuatia ilikuwa ni mwaka mmoja, miwili au mitatu isipokuwa Megji pekee.
Saibul alifutiwa na Isaack Sepetu kuanzia 1980 hadi 1982, kisha Ali Hassan Mwinyi aliyehudumu kuanzia 1982 hadi 1983 na alifuatiwa na Geogre Kahama mwaka 1983 hadi 1984.
Wengine ni Paul Bomani (1984-1985), Getruda Mongela (1985-1987), Arcardo Ntagazwa (1987-1989), Marcel Komanya (1989-1990), Abubakar Mgumia (1990-1993), Juma Omar (1993-1995) na Juma Ngasongwa (1995-1996).
Baadaye walifuata, Zakhia Megji (1997-2005), Anthony Diallo (2005-2006), Jumanne Maghembe (2007-2008), Shamsa Mwangunga (2008-2010), Ezekiel Maige (2010-2012) na Khamis Kagasheki (2012-2013).
Mbali na hao, Lazaro Nyalando alihudumu (2014-2015), Jumanne Magembe (2015-2017), Dk Hamisi Kigwangallah (2017-2020), Dk Damas Ndumbaro (2020-2022), Dk Pindi Chana (2022-2023), Mohammed Mchengerwa (Februari 2023- Agosti 30, 2023), kisha Angellah Kairuki (2023-2024) na sasa amerudi tena Dk Chana.
Kwanini mabadiliko?
Unyeti wa wizara hiyo na uzito wa majukumu ndani yake ni moja ya sababu za mabadiliko ya mara kwa mara, kama inavyoelezwa na Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli za Kitalii Tanzania (HAP), Kennedy Mollel.
Kinachoipa unyeti wizara hiyo ni kile alichoeleza, imebeba sekta inayoingiza fedha za kigeni zaidi ya eneo lingine lolote na yenyewe imejikita katika huduma na sio bidhaa.
Sambamba na unyeti, amesema wizara ya utalii inagusa sekta nyingine zote na utendaji wake unahitaji mazungumzo na mawaziri wa wizara nyingine ili kutatua changamoto zitakazoibuliwa na wadau.
“Mwekezaji wa utalii anaweza kusema gharama za kuendesha biashara ni kubwa, lakini hili halitokani na wizara ya maliasili na utalii ni wizara nyingine kama ya fedha, kazi, ofisi ya makamu wa rais mazingira.
“Leo hii ukiwa Waziri wa Maliasili na Utalii wadau wako wakija wanakwambia changamoto yetu iko wizara ile pale kwa hiyo ukaongee na waziri yule pale,” amesema.
Katika mazingira hayo, amesema waziri wa wizara husika anajikuta na jukumu la kuwaomba mawaziri wenzake vitu vingi kwa ajili ya wizara yake.
“Kwenye kuomba sasa napo kuna gharama zake. Unamuomba mtu afanye mabadiliko yatakayoinufaisha wizara yako na wakati mwingine yanaathiri wizara yake, huwa hali inakuwa ngumu,” amesema.
Kwa msingi huo, amesema kila waziri anayeingia atajikuta anajikita katika maeneo yale yale yaliyozoeleka kufanywa, lakini si kuondoa vikwazo na kukuza zaidi idadi ya watalii.
Amesema kuna haja ya nchi kukaa pamoja na kuona namna ya kuiendesha biashara ya sekta hiyo, ili waziri atakayewekwa awe na misingi ya kufuata wakati wa utendaji wake.
Mollel amependekeza kutengenezwe malengo ya muda mrefu ya kutangaza vivutio na fursa mbalimbali za utalii, ndani yake kila waziri atapaswa kutekeleza hayo.
“Kila anayekuja atatekeleza malengo hayo na akitoka anayefuata ataanzia alipoishia kwenzake ataendeleza na sio kuja na mipango mipya. Hivi ndivyo watadumu, badala ya kila mtu kuja na vipaumbele vyake kila siku watabadilishwa,” amesema.
Kuna tatizo la mfumo
Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Out), Dk Revocatus Kabobe amehisi uwepo wa tatizo la kimfumo wa utendaji ndani ya wizara ndiyo unaofanya kila waziri aonekane hatoshi.
“Wizara hii imekuwa ikifanyiwa mabadiliko mengi tangu uhuru mpaka sasa. Pamoja na kwamba sababu za utenguzi wa mawaziri wa wizara mbalimbali anazo mteuzi, kwa maoni yangu nadhani kuna tatizo la kimfumo kwenye utendaji kazi ndani ya wizara hii ambao bado haujapatiwa tiba sahihi tangu uhuru,” amesema.
Ingawa utenguzi wa mawaziri unaweza kuambatana na sababu mbalimbali ukiwemo utendaji usiokidhi malengo ya mteuzi, amehoji kwanini hali hiyo iwe zaidi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Hata hivyo, amesema utaliii ni miongozi mwa sekta muhimu na inayochangia mapato mengi serikalini, ukiondoa madini.
Kwa kigezo hicho, amesema mikikimikiki ya wizara hiyo haiwezi kuwa rahisi kama sekta nyingine ambazo uchangiaji wa mapato kwa mfuko mkuu wa Serikali ni wastani.
Wingi wa vishawishi vya rushwa ni jambo lingine lililotajwa na Dk Kabobe kuwa sababu ya mawaziri kuhudumu kwa muda mfupi zaidi ndani ya wizara hiyo.
Lakini, amehusisha wingi wa changamoto ikiwemo vita ya ujangili, migogoro ya hifadhi za wanyama na binadamu, ugawaji vitalu, migongano baina ya watendaji na ukiukwaji wa haki za binadamu yote yanachochea kumuondoa waziri madarakani iwapo hatasimamia vema.
“Haya yote sio mambo rahisi yanahitaji msuli wa kuyakabili na msuli wenyewe haupaswi kuwa msuli wa mtu bali msuli wa kimfumo na kimkakati.
“Kwa maoni yangu, siamini kama kweli wale wote wanaoteuliwa wana uwezo mdogo wa kuongoza wizara hii la hasha. Nadhani kuna tatizo la kimfumo katika utendaji ndani ya wizara hii,” amesema.
Amesisitiza umuhimu wa mamlaka kutazama upya mfumo wa utendaji ndani ya wizara hiyo aliyoitaja kama miongoni mwa zile muhimu katika taifa.
Kitakachomkabili Pindi
Kibarua kitakachomkabili Waziri anayeingia sasa, Mollel amesema ni kuendana na uchumi wa kidigitali ambao ndiyo mwenendo wa ulimwengi wa sasa.
Jukumu lingine, amesema ni kuhakikisha anatangaza utalii sio tu kwa kuishia Serengeti, Kilimanjaro na Zanzibar, matangazo yahusishe vivutio vingine ikiwemo Mkomazi na maeneo mengi.
“Atakuwa na kazi ya kuhakikisha kwa muda wa miezi minne iliyosalia anatimiza malengo yaliyowekwa na Serikali ya kufikisha watalii milioni tano kufikia mwaka 2025. Hili atatimiza iwapo atakuja na mkakati utakaomshawishi mtalii aliyekuwa na lengo la kukaa wiki moja avutiwe kukaa wiki tatu nchini,” amesema.
|
Licha ya sifa zinazonadiwa na Serikali juu ya mwenendo sahihi wa utawala wa awamu ya sita, robo ya W
|
Licha ya sifa zinazonadiwa na Serikali juu ya mwenendo sahihi wa utawala wa awamu ya sita, robo ya Watanzania wameonyesha taifa lilikuwa katika mwelekeo mbaya kwa mwaka 2022.
Wakati wananchi wakiwa na mitazamo hiyo, asilimia 67 ya Watanzania waliohojiwa hawaelewi kuhusu hali zao za maisha, huku asilimia 20 wakisema ni mbaya na asilimia 13 wakiona nzuri zaidi.
Katika mazingira hayo, idadi ya walioonyesha mwelekeo mbaya wa Tanzania imeizidi ile ya mwaka 2021 ambao ni asilimia 16 ndiyo walioona nchi ipo katika mwelekeo huo, huku asilimia 18, wakiona inaelekea pazuri.
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa Taasisi ya Twaweza uliohusisha miaka 10 yaani 2013/23, katika asilimia 25 wanaoonyesha nchi ipo katika mwelekeo mbaya, asilimia 26 ni wanawake na wanaume ni asilimia 24.
Wakati wengine wakiwa na mtazamo huo, ripoti hiyo iliyozinduliwa leo, Agosti 13, 2024 unaweka wazi, kundi lingine ambalo ni asilimia 44 linaloonyesha halijui chochote kuhusu mwelekeo wa nchi kwa mwaka 2022.
Kundi lisilojua chochote kuhusu mwelekeo wa taifa, lilijitokeza pia mwaka 2021, ambalo ni asilimia 66.
Lakini utafiti huo unakwenda mbali zaidi na kuonyesha hali ilikuwa mbaya katika awamu ya tatu ya Serikali (chini ya Hayati Benjamin Mkapa) mwaka 2012/14, ambapo asilimia 73 ya wananchi waliona taifa lina mwelekeo mbaya.
“Kati ya mwaka 2017 na mapema 2021 watanzania wengi waliona nchi inaelekea pazuri na tangu mwaka 2021, wananchi walionyesha kupunguza imani zao na wengi hawakujua kama ilielekea pazuri au pabaya. Hili limetokea katika nyakati za mabadiliko ya utawala kutoka Hayati John Magufuli hadi Rais Samia Suluhu Hassan,” imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.
Wakati hali ikiwa hivyo kwa Tanzania, Kenya na Uganda nako hali si shwari, ripoti hiyo inaonyesha asilimia 52 waliona mwelekeo mbaya wa taifa la Kenya, huku 48 waliona hivyo kwa Uganda mwaka 2022.
Sambamba na mitazamo hiyo ya wananchi juu ya mwelekeo wa mataifa hayo, ripoti hiyo imeweka bayana mambo yanayowaathiri wananchi kiuchumi, kijamii na kiuongozi.
Kwa upande wa uchumi, Watanzania wanaathiriwa zaidi na gharama za maisha, umasikini, ukosefu wa ajira, njaa, ardhi na kilimo kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Katika huduma za kijamii, watanzania wanaathiriwa zaidi na changamoto katika huduma za afya, usafirishaji, miundombinu, elimu bora na upatikanaji wa maji safi.
Wakati athari za kiuchumi na huduma za jamii zikigusa maeneo hayo, ripoti hiyo inataja rushwa, uongozi na hofu kuwa sehemu za athari za kiutawala.
Shughuli za kilimo zimetajwa na ripoti hiyo kuwa ndiyo chanzo kikuu cha mapato cha kaya za Tanzania, zikitegema kwa asilimia 39, ikifuatiwa na kujiajiri asilimia 38, kisha ajira rasmi asilimia 10, kazi za kawaida asilimia saba na mafao ya ustaafu ni asilimia nne.
Hali hiyo ni tofauti na Uganda ambayo kwa sehemu kubwa kaya zinategemea kazi za kawaida kama chanzo kikuu cha mapato kwa asilimia 37, huku kilimo kikitegemewa kwa asilimia 25 pekee na Uganda kaya zinategemea zaidi kilimo kwa asilimia 69.
Hali ya uchumi
Kwa upande wa hali ya kiuchumi, asilimia 50 wameeleza hawaelewi kuhusu uhalisia wao wa kiuchumi, asilimia 14 wamesema ni mbaya na 16 wakisema nzuri zaidi.
Katika mwaka huo huo 2020, asilimia 36 wamesema wanaridhishwa na mwelekeo wa Serikali katika kutengeneza kipato na fursa za ajira, huku asilimia 28 wakisema hawaridhiki na asilimia 37 hawajui.
Kuhusu kupunguza gharama za maisha, asilimia 49 wanaridhishwa na asilimia 17 hawaridhishwi huku asilimia 35 wakiwa hawaelewi.
Asilimia 41 ya Watanzania waliohojiwa, wamesema wanamiliki biashara kwa sasa, huku asilimia 47 hawakuwahi kumiliki na 12 walimiliki lakini hazikudumu.
Hata hivyo, ripoti hiyo imeweka wazi asilimia 42 ya Watanzania walisema vipato vyao vinakidhi mahitaji yao ya siku kwa Oktoba mwaka 2020.
Katika mwaka huo huo, ripoti inonyesha Watanzania kwa asilimia 40 walikuwa na hofu ya kuishiwa na chakula, huku asilimia 20 walikuwa na njaa lakini walishindwa kula na zaidi ya asilimia 10 walishinda na njaa kutwa.
Unachopaswa kujua ni kwamba Watanzania wanamiliki zaidi ardhi kwa asilimia 77, kuliko vyombo vya usafiri ambavyo pikipiki ni asilimia 12, gari asilimia mbili, baiskeli asilimia 46 na mifugo asilimia 34.
Lakini Watanzania hao hao, wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ya kunywa, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
“Kwa wastani watanzania wanatumia dakika 49 kutafuta maji ya kunywa kwa maeneo ya mijini,” inaeleza sehemu ya ripoti.
Hata hivyo, njia mbalimbali ndizo zilizotajwa kutumika zaidi kuyatibu maji hayo ya kunywa kwa asilimia 62 Tanzania, huku asilimia 50 wakichemsha na asilimia tisa wakiyachuja kwa nguo.
Ripoti hiyo inaeleza, asilimia tano wanayatibu kwa kemikali asilimia moja wanayaacha yatuliue ndiyo yatumike, asilimia moja wanayachuja kwa chujio la maji na asilimia 0.1 hutumia njia nyinginezo.
Kwa asilimia 28 Watanzania wanaishi mbali na vituo yanapopatikana maji, asilimia 23 wanakabiliwa na uhaba wa vituo hivyo, asilimia 20 maji machafu na asilimia 21 ni usambazaji mbaya wa huduma hiyo.
Ripoti hiyo pia inaeleza asilimia 10 ya Watanzania wameripoti kukumbwa na gharama kubwa za maji, asilimia nane wanajua vilipo vituo vya maji lakini havifanyi kazi na asilimia 23 hawana tatizo la maji.
Maoni ya wataalamu
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mchambuzi wa Masuala ya Kijamii aliyezungumza akiwa nchini Kenya, Charles Obbo amesema kilimo ndiyo shughuli kuu nchini Kenya, lakini inashangaza chanzo kikuu cha mapato ya wananchi ni shughuli za kawaida.
“Kenya inafahamika kilimo ndiyo uti wa mgongo na nilitegemea tungekuwa tegemezi kwenye eneo hilo lakini wananchi wanategemea shughuli za kawaida kupata kipato, hii ni kutokana na yanayoendelea kwenye jamii ambayo yanawaondoa watu kulima na kutegemea vitu vingine,” amesema.
Mtafiti wa Masuala ya Kijamii kutoka Kenya, Christine Mwangi kutoka nchini Kenya amesema jambo lililomshangaza kupitia takwimu hizo ni kuona imani ya wananchi ikipungua kwenye matumizi ya vituo vya huduma za afya vinavyomilikiwa na Serikali.
“Pia nimebaini namna ambavyo usalama wa chakula nchini Kenya upo chini na watu hawana imani na huduma za kijamii kutokana na kupoteza imani dhidi ya Serikali na watawala, watu wanajiuliza kama huduma hawawezi kuzifikia wala kuzipata kwanini viongozi waliopo waendelee kuwepo,” amesema.
Amesema ni muhimu Serikali ione namna gani inazitumia takwimu hizo kutatua matatizo yaliyopo.
“Nchini Kenya asilimia 75 ya wananchi hawana kipato cha kupata mlo wao wa kila siku,” amesema.
Mwanahabari kutoka Tanzania, Sammy Awami amesema ukosefu wa ajira ndiyo changamoto kubwa nchini ndiyo maana kila unapokwenda utakutana na watu wakiuza bidhaa mbalimbali barabarani.
“Ukienda maeneo mbalimbali barabarani utakutana na watu wakiuza vitu na hii ni kutokana na kukosekana kwa ajira rasmi hivyo watu kuamua kuingia kwenye ujasiriamali,” amesema
Akizungumza na Mwananchi, Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Out), Dk Timoth Lyanga anasema kila ongezeko linaloshuhudiwa kwa Tanzania linatokana na maboresho ya kisera yanayofanywa na Serikali.
Amesema kazi imefanyika kuhakikisha maisha ya watu wanaimarika kiuchumi na kijamii, ingawa zipo changamoto zinazowakabili.
Katika maelekezo yake, mwanazuoni huyo amesema mwelekeo mbaya wa taifa unategemea na eneo linalohusishwa, lakini kiuhalisia kuna matumaini.
“Tukiangalia hatuwezi kusema ni mwelekeo mbaya kwa sababu hakuna vitu vilivyotajwa kuhusu mwelekeo huo,” amesema.
|
Shirika la Kimataifa la Kupigania Haki za Binadamu la Amnesty International limeungana na wadau wa n
|
Shirika la Kimataifa la Kupigania Haki za Binadamu la Amnesty International limeungana na wadau wa ndani kulaani vitendo vya kukamatwa kwa viongozi na wafuasi wa Chadema.
Matamko ya kulaani vitendo hivyo yameendelea kutolewa na wadau mbalimbali wa haki za binadamu, wakipinga uamuzi wa Jeshi la Polisi nchini kuwashikilia viongozi wa Chadema.
Makundi ya wanaoshikiliwa na jeshi hilo, yanahusisha viongozi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti, Freeman Mbowe, wanahabari na wadau wengine.
Kushikiliwa kwao kunatokana na uamuzi wao wa kuelekea jijini Mbeya kushiriki maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yaliyopangwa kufanywa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).
Hata hivyo, Jeshi la Polisi lilishaingilia kati shughuli hiyo na kupiga marufuku isifanyike kwa kile lilichodai kuwa vuguvugu la kuvunjwa kwa amani na vurugu ndani yake.
Sambamba na tamko la Amnesty International, Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) wameshalaani vitendo hivyo.
Katika taarifa yake ya leo, Agosti 12, 2024, shirika hilo la kimataifa limezitaka mamlaka nchini kuheshimu, kulinda na kutekeleza haki za binadamu wote kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.
“Mamlaka zinapaswa kukomesha ukamataji haramu wa wanasiasa wa upinzani na kuweka vizuizi juu ya haki ya wananchi kujumuika,” imeeleza taarifa ya shirika hilo.
Limekwenda mbali zaidi na kutaka wote walioshikiliwa waachiwe huru na kama kuna mwenye hatia mamlaka zinapaswa kuheshima haki zao za kuwaeleza sababu za kuwakamata.
Katika hatua nyingine, TLS kimeungana na wadau wengine kulaani kukamatwa kwa viongozi na wafuasi wa Chadema na wanahabari kulikofanywa na Jeshi la Polisi.
“Jeshi la Polisi pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imekuwa na Uzito mkubwa katika kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika hasa pale zinapotolewa kauli zenye viashiria vya uhalifu kutoka kwa upande wa viongozi wa Chama Tawala,” imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeitaja Ibara ya 18 na 20(1) ya Katiba ya nchi inayotoa haki na uhuru wa watu kujieleza, kukusanyika na kujumuika.
Kadhalika, imeeleza haki hizo zinalindwa kwenye Mikataba mbalimbali ya Kimataifa na Kikanda ambayo Tanzania imeiridhia na hivyo ina wajibu wa kuziheshimu na kuzitekeleza ipasavyo.
“TLS inasikitishwa na ukiukwaji huu wa Katiba na ukamatwaji huu unaoendelea ambao unafifisha uhalisia wa 4Rs za Rais Samia Suluhu Hassan ambazo ni maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko na kujenga upya,” imesema.
Chama hicho kimetoa wito na kulisihi Jeshi la Polisi nchini, kuheshimu utawala wa sheria na mara zote lijielekeze katika kulinda raia na mali zao na kuacha kuingilia shughuli za vyama vya siasa ambazo kimsingi zinaongozwa na sheria ya vyama vya Siasa.
“Hivyo basi, tunalisihi Jeshi la Polisi kuacha mara moja matendo yenye kuashiria uminyaji wa haki ya kujumuika na kujieleza jambo ambalo ni uvunjwaji wa Katiba na sheria za nchi.
“Tunavitaka vyombo vya usalama hususan Jeshi la Polisi viimarishe uwezo wao wa kulinda makundi haya wakati yanapotaka kutumia haki zao za Kikatiba katika shughuli zao kwa mujibu wa taratibu na sheria zetu na watambue kwamba wajibu wao ni kutoa Ulinzi na kama kuna viashiria vya uhalifu wavidhibiti na siyo kuzuia vyama au makundi ya kiraia kujumuika kwasababu za kiujumla zisizo na maelezo yanayojitosheleza,” kimeeleza chama hicho.
Imeeleza chama hicho kupitia Kamati maalumu ya mawakili kimeelekeza kufanyika tathmini na kuchukuliwa kwa hatua stahiki za kisheria kwa kila Ofisa aliyehusika kusababisha kadhia hiyo kwa jina lake na kuhakikisha utii na uzingatiwaji wa matumizi bora ya madaraka katika Ofisi za Umma.
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) nalo limelaani tukio la kukamatwa kwa waandishi wa habari, huku likivitaka vyombo vya dola kuwaachia mara moja.
Waandishi wanaodaiwa kukamatwa kwa mujibu wa taarifa ya TEF ni Ramadhan Hamis na Fadhili Kirundwa wa Jambo TV na Francis Simba Mpiga Picha wa Chanzo TV.
Imesema uwepo wa waandishi hao katika tukio hilo, ulilenga kufanya kazi na si sehemu ya siasa au chochote kilichokuwa kinaendelea.
“Tunalaani matukio ya kukamata waandishi wa habari. Matukio haya yanaharibu heshima kubwa ya Tanzania katika kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari aliyoijenga Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 kwa kurejesha uhusiano mzuri na vyombo vya habari,” amesema.
Katika taarifa hiyo, TEF imesema inazo taarifa kuwa waandishi hao kwa sasa wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Mbalizi.
“Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inatoa haki ya watu kukusanya, kuchakata na kusambaza taarifa bila kujali mipaka ya nchi. Sambamba na Katiba, Kifungu cha 7(1)(a)(b) na (c) cha Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2023, kinatoa haki kwa waandishi wa habari kufanya kazi ya uandishi wa habari.
“Ni jukumu la waandishi wa habari kuhabarisha umma juu ya kila jambo linaloendelea, hivyo mwandishi hapaswi kukamatwa au kuadhibiwa kwa kufanya kazi hii,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
|
Hofu ya viongozi juu ya kilichotokea nchini Kenya na Bangladesh ni moja ya jambo lililotajwa kama sa
|
Hofu ya viongozi juu ya kilichotokea nchini Kenya na Bangladesh ni moja ya jambo lililotajwa kama sababu ya Serikali kuliwekea vikwazo Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), kufanya shughuli ya Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani.
Kwa mujibu wa wanazuoni wa sayansi ya siasa, utawala katika mataifa kadhaa ulimwenguni umekumbwa na mtikisiko uliosababishwa na vuguvugu la vijana, hivyo kujenga hofu kwa wengine kutoa mwanya kama huo.
Bavicha ilitangaza kufanya maadhimisho hayo Agosti 12, mwaka huu katika viwanja vya Ruandazove jijini Mbeya, huku Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Lakini shughuli hiyo ilikumbwa na vikwazo kutoka mamlaka mbalimbali za Serikali akiwemo Msajili wa Vyama vya Siasa, aliyeiandikia barua Chadema ya kuisihi isitishe shughuli hiyo kwa kuwa inakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa.
Sambamba na Msajili, Jeshi la Polisi nalo lilipiga marufuku Bavicha kufanyika kwa maadhimisho hayo, kwa kile lilichoeleza kuna viashiria vya uvunjifu wa amani ndani yake.
Ingawa Chadema ilipingana na marufuku hizo, lakini shughuli hiyo haikufanyika, badala yake makundi ya wafuasi na viongozi wake waliishia kutiwa mikononi mwa polisi.
Ktika taarifa ya Chadema iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Benson Kigaila viongozi na wafuasi 443 wanashikiliwa na jeshi hilo katika vituo mbalimbali ambavyo hadi sasa hawajajua walipo.
Aliwataja viongozi wanaoshikiliwa ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu John Mnyika, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi na viongozi wengine wa Bavicha.
Hata hivyo, Kigaila alitoa wito kwa jeshi hilo kuwaachilia viongozi na wanachama wa Chadema kabla ya usiku wa Agosti 12, kupita, huku akiwataka viongozi wa ngazi mbalimbali kusubiri maelekezo kutoka ngazi ya taifa.
Alipoulizwa watafanya nini iwapo hawataachiliwa, Kigaila alijibu kwa kifupi akisema: “Tutauvuka mto tutakapoufikia,” akimaanisha watajua iwapo muda utafika.
Kwanini Serikali izuie?
Hatua ya Jeshi la Polisi kuingilia kati shughuli hiyo ya Bavicha, imesababishwa na wasiwasi wa watawala unaotokana na mabadiliko ya mwenendo wa siasa za ulimwengu, kama inavyoelezwa na Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Dk Conrad Masabo.
Kwa mujibu wa mwanazuoni huyo, imeshuhudiwa katika mataifa mengi ikiwemo Kenya na Bangladesh vijana wamewatikisha watawala na hata kuwaondoa madarakani.
“Hii hatua ya kuzuiwa inatokana na wasiwasi walionao viongozi juu ya uwezekano wa maandamano hayo kutengeneza nafasi ya kisiasa ya kufanya wanayotaka kuyafanya.
“Kama ilivyokuwa Kenya ilianza kama oparesheni ya muswada wa fedha na baadaye ilibadilika na kuja katika sura halisi ya siasa za taifa hilo, kwa mtazamo wangu hii ndiyo hofu ya viongozi,” alisema.
Katika mazingira hayo, alisema viongozi nchini hawana uhakika kwamba wakitoa mwanya wa maadhimisho hayo, utaishia kwenye kuadhimisha siku hiyo pekee.
Kwa mtazamo wa mhadhiri huyo, siasa hubadilika kutokana na matukio ya wakati husika na kuzuiwa kwa shughuli hiyo ya Bavicha kunaakisi hilo.
“Wakati Chadema wanaruhusiwa kufanya maandamano nchi nzima Dunia ilikuwa imetulia hata siasa hazikuwa na mambo mengi. Lakini sasa kuna matukio mengi yameshuhudiwa yakisababisha mabadiliko na mitikisiko kwa watawala ndiyo maana kuna hofu,” alieleza.
Hoja inayofanana na Dk Masabo, ilitolewa pia na Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Mohamed Bakari aliyesema kuna hofu ya watawala kuepuka yaliyotokea katika mataifa kadhaa duniani.
Alisema matukio katika mataifa kama Kenya na Nigeria yanatumiwa kama rejea na funzo kwa viongozi wa mataifa mengine ikiwemo Tanzania, juu ya umuhimu wa kudhibiti matukio kama hayo mapema.
“Katika nyakati hizi ambapo kuna kumbukumbu ya matukio hatari ya kisiasa yaliyosababishwa na vijana, mtawala huwa na hofu ya kuruhusu uhuru wa shughuli hizo kama ilivyokuwa katika maandamano,” alieleza.
Polisi
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Juma Haji alisema wapo katika mchakato wa kutoa taarifa za kina kuhusu hilo.
Pamoja na mambo mengine, alieleza taarifa hiyo itahusisha watu wangapi wapo nao kwa kuwa walikaidi marufuku iliyotolewa na jeshi hilo.
“Muda si mrefu tutatoa taarifa tukiwa Mbeya, kueleza wangapi tupo nao kwa kuwa walikaidi marufuku,” alisema.
Wadau walaani
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) jana, ulitoa tamko la kulaani kukamatwa kwa viongozi, wanachama wa Chadema na wanahabari, ikisema ni kunavunja Katiba.
Katika tamko lake, THRDC imenukuu Ibara ya 18 na 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotoa haki na uhuru wa watu kujumuika, kufanya mikutano, maadhimisho na kueleza mawazo yao.
“Haki hizi hazipo kwenye Katiba peke yake bali zipo kwenye Mikataba mbalimbali ya Kimataifa na Kikanda ambayo Tanzania imeridhia,” imeelezwa katika sehemu ya tamko hilo.
Imeeleza ukamatwaji huo unafifisha uhalisia wa maridhiano, ustahimilivu na mabadiliko ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akihubili tangu alipoingia madarakani.
“Tunatoa wito kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kuwaachilia huru watu wote waliokamatwa bila masharti ili kuadhimisha siku ya vijana duniani kama ambavyo vyama vingine tayari vimekwisha adhimisha na hatukuona wakikamatwa,” imeeleza taarifa hiyo.
Kama ilivyokuwa kwa THRDC, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nacho kililaani ukamataji huo, kikitaja Ibara ya 20 ya Katiba ya nchi inayotoa uhuru na haki ya kukusanyika.
Taarifa hiyo pia, ilionyesha kinachoendelea kinapingana na kauli za wakati wote za Rais Samia kuwa, anatekeleza R4 katika utendaji wake.
“Hatua ya Polisi kuingilia shughuli halali ya kisiasa inakwenda kinyume na falsafa ya R4 ya Rais Samia zinazolenga kuleta ustahimilivu, kujadiliana, kuvumiliana na kujenga upya,” imeeleza taarifa hiyo.
ACT nayo yakwama
Wakati Chadema ikikabiliwa na hayo, Chama cha ACT Wazalendo nacho kimekwaa kisiki katika mpango wake wa kufanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Charambe Agosti 12 kuadhimishia siku ya Vijana duniani.
Chama hicho kimekwa kisiki baada ya Kituo cha Polisi Wilaya ya Mbagala kutoa taarifa ya kuzuia mikutano ya hadhara na ile ya ndani.
Jeshi hilo lilikuwa linajibu barua iliyowasilishwa na chama hicho, likisema: “Pamoja na barua hii napenda kukujulisha kuwa mikutano yote ya hadhara naya ndani imezuiliwa hadi hapo yatakapotolewa maelezo mengine.”
Hatua hiyo ilimuibua Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi aliyesema kinachojitokeza ni hali ya jeshi hilo kujichanganya kwani, hakuna tamko rasmi la kufuta mikutano ya hadhara na ile ya ndani.
“Kilichotokea naona kama Polisi wamejichanganya hakuna tamko rasmi lilotolewa la kuzuia mikutano ya hadhara na ya ndani kwakuwa jeshi la Polisi lina ngazi aulizwe Msemaji wake anaweza kuwa na majibu sahihi,” alisema Jaji Mutungi.
Si Jaji Mutungi pekee, hata Jeshi la Polisi Makao Makuu kupiti taarifa yake iliyotolewa na Msemaji wa jeshi hilo, David Misime ilijitenga na taarifa ya Kituo cha Polisi Wilaya ya Mbagala.
“Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa halijapiga marufuku kufanyika mikutano ya nje ya hadhara na ile ya ndani ili mradi inafuata matakwa ya sheria ya nchi,” ilieleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Misime, walichopiga marufuku ni mkusanyiko ulioitishwa na viongozi wa Chadema, huko jijini Mbeya kwa kivuli cha kuadhimisha siku ya vijana duniani.
|
Itakuhitaji ama uamue kukubali kubeba mzigo wa dhambi zisizokuhusu na ukae kimya au uwe muwazi na mw
|
Itakuhitaji ama uamue kukubali kubeba mzigo wa dhambi zisizokuhusu na ukae kimya au uwe muwazi na mwenye misimamo ambayo hatma yake ni kuvunja amani ya familia.
Hayo ni machaguo mawili yanayoakisi uhalisia wa maisha ya yeyote aliyeamua kuishi kwa ndugu, ambaye aghalabu mikasa, vituko na masimango huwa sehemu ya maisha yake.
Ingawa hayo hayabadilishi ukweli wa uwepo wa baadhi ya familia ambazo mgeni ni furaha kwao, kwa sehemu kubwa maisha kwa ndugu ni shubiri kama inavyosimuliwa na Janeth Peter aliyewahi kukumbwa na mikasa hiyo.
Janeth anayeishi Tabata, Dar es Salaam anasema harakati za utafutaji wake zilimlazimu kuishi kwa kaka yake na huko ndiko aliposhuhudia magumu ya maisha kwa ndugu.
Anasema hakuwa wa kwanza kuishi kwenye familia hiyo, alitanguliwa na dada yake ambaye wakati yeye (Janeth) anafika nyumbani hapo mwenziwe alishaondoka na kuanza kujitegemea.
Hatua ya dada yake kuishi kwa kaka yake huyo hadi kufikia kujitegemea, anasema ilimhamasisha kuona kuwa nyumbani hapo ni eneo zuri kuishi wakati unajitafuta.
Mtazamo huo ulibadilika siku hadi siku kwa kadri alivyoyaanza maisha kwa ndugu yake huyo, kwani tofauti na alivyotarajia alijikuta katika wimbi la visa na mikasa.
Mkasa mkubwa zaidi ni ule anaosema akiwa kwa Kaka yake huyo, wifi yake (mkewe kaka yake) hakuwa anatumia vema fedha zilizoachwa kwa ajili ya chakula.
Kutokana na mazingira hayo, anasema kuna wakati walilazimika kushinda njaa na Kula usiku pekee Kaka yake anaporudi kutoka kazini.
Kumbe fedha zilizokuwa zinaachwa, wifi yake alizipunguza na kuzipeleka kwenye michezo bila mumewe kujua.
Anasema mambo yalikuwa mabaya zaidi pale Kaka yake alipogundua tabia ya mkewe, ilizua ugomvi kwa wawili hao.
Kwa sababu wifi yake aliishi muda wote na tabia hizo bila kubainika, anasema hatua ya kujulikana ilimfanya ahisi mgeni ndiye aliyetoa siri.
“Wifi alichukia sana na kujua kuwa mimi ndiyo nilimwambia kaka kuhusu tabia hiyo,” anasema.
Nyakati nyingine mbaya kwake, anasema ni zile ambazo kaka yake alizungumza maneno yanayomlenga yeye lakini si kwa lugha nzuri na hakuwa anajua yanatoka wapi.
“Kuna muda mnakuwa mmekaa kama familia lakini kaka alikuwa akiongea maneno ambayo kiuhalisia yananilenga mimi na kuniumiza, kuna kipindi akijisikia atapiga familia nzima bila kujali chochote kama unahusika au laa na utabebeshwa hata visivyokuhusu hata ikiwa aliyefanya ni mwingine,” anasema.
Baada ya hapo, anasema maisha yake yote katika familia hiyo yaliishia kuhukumiwa kwa makosa ya dada yake aliyewahi kuishi hapo.
“Yule dada aliyetangulia kuishi kwa Kaka alikuwa na tabia ya kuongea maneno chonganishi na alikuwa anatunga,” anasema.
Ukiachana na mikasa iliyomkumba, anawashauri ndugu wenye nia ya kusaidia wengine wahakikishe wana uwezo wa kufanya hivyo, kinyume na hapo wataonekana wanawanyanyasa.
Familia zilizowahi kupokea ndugu nazo zinalalamikia ndugu wengine hawabebeki na wamekosa shukurani hata wasaidiwe kwa namna gani.
Mkazi wa Sinza, Flackian John ni mmoja wa viongozi wa familia, anasema wageni wengi wakishazoea hujenga misimamo yao na hapo ndipo vurugu zinapoanza.
Anaeleza unapokwenda kuishi kwenye familia ya mwingine, jitahidi kufuata taratibu na sio kuweka za kwako.
“Unakuta mtu anakuja kwako alafu anataka kubadilisha taratibu walizozikuta. Anajipa mamlaka asiyostahili,” anasema.
Kwenye familia yenye baba na mama, anasema mara nyingi mipango hupangwa wote, lakini baadhi ya ndugu wanapofika hupangwa vinginevyo.
“Wakifika wanataka taratibu zibadilike kama ni ndugu wa mume basi waanze kupanga mipango na ndugu yao na si mke wake tena, kitu hiki si rahisi mke kukubaliana nacho na hapa huleta hali ya sintofahamu katika familia hiyo,” anasema.
Kwa Marium Abdala yeye maisha kwa ndugu yake ni historia nzuri kwake, akisimulia namna mama yake alivyosaidiwa na ndugu baada ya kuhitimu dadasa la saba.
“Hawa waliomsaidia mama yangu hawakuwa wazazi wake, lakini walimtoa mama yangu kijijini akiwa na ujauzito alioupata akiwa na umri mdogo,walimlea mpaka kujifungua na baadaye walimrudisha shule,” anasema.
Ameeleza kuwa kipindi mama yake anasomeshwa yeye alilelewa na ndugu hao na kuhudumiwa kwa kila kitu na alipoanza kusoma walimsomesha pia.
“Mama yangu alisomeshwa mpaka alipomaliza na kupata kazi. Muda huohuo waliendelea kunisomesha mimi mpaka nilipomaliza elimu yangu na kupata kazi,” anasema.
Mtazamo wa kisaikolojia
Mtaalamu wa Saikolojia, Saldin Kimangale anasema yanayowasibu wanaoishi kwa ndugu zao yanaathiri ustawi wao.
Katika mazingira hayo, anasema mtu huwa na hisia za kutengwa, kukataliwa, kunyanyapaliwa, jambo linaloacha kovu katika hisia za mtu na kuibua tabia za kujipendekeza.
“Mara nyingi watu hukataliwa kwa imani kuwa amevunja uaminifu na hakuna namna bora ya kuishi sehemu itakayoweza kumridhisha kila mtu,” anasema.
Anasema ili kuepuka hayo kila mtu anapaswa azingatie kilichompeleka kwa nduguye na mengine ayaache.
Pia, anasema anapaswa kuishi kwa malengo na kuzilea familia katika hali ya upendo ili kuaminiana, kuweka mipaka na kuondoa mwanya wa kudhaniana vibaya.
Mkufunzi wa Maisha na Ushauri, Fiona Nkya anasema swala la ndugu kuja katika familia yako na kuanza kusababisha migongano ni matokeo ya wanaowapokea.
“Kuwa na mipaka ni kitu kizuri lakini pia tengeneza sheria za nyumbani kwako na anapokuja mgeni mkalishe chini na umwambie hizi ndo sheria za nyumbani kwangu,” anasema.
Anasema kila ndugu anayefika kwako hakikisha anakuja kwa malengo na si kukaa tu, kama amefuata masomo akimaliza aondoke.
“Wengi wanaokuja bila malengo wengi wao ndio huwa chanzo cha ugomvi katika hizi, ndugu huamua kuja kukaa tu baada ya wewe kuwa muwazi kupitiliza na kukosa mipaka na hata kuelezea mengi kuhusu familia yako kitu ambacho hakina ulazima,” anasema.
“Kutoa misaada ni sawa lakini kama hakuna sababu za msingi za ndugu kuja kwenye familia yako basi ni vyema umsaidie akiwa kwao ili kuepuka purukushani na sintofahamu hizi,” anasema.
|
Vikwazo vimeiandama shughuli ya Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani iliyopangwa kufanywa na Baraza
|
Vikwazo vimeiandama shughuli ya Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani iliyopangwa kufanywa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), baada ya mamlaka za Serikali kudai kuna ishara ya hamasa ya uvunjifu wa amani na vurugu ndani yake.
Kilichoiponza Bavicha hadi kukumbwa na vigingi vya Serikali kuelekea shughuli hiyo, ni kauli yake iliyohusisha mfano wa kilichofanywa na vijana wa Kenya, ikiwasifu wamejitambua, jambo lililotajwa kama dalili ya vurugu.
Bavicha ilipanga kufanya shughuli hiyo, Jumatatu Agosti 12, 2024 katika viwanja vya Ruandazove jijini Mbeya na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ndiye aliyetajwa kuwa mgeni rasmi.
Ilianzia kwa Msajili
Mapema baada ya tangazo la kufanyika kwa shughuli hiyo lililotolewa na Katibu Mwenezi wa Bavicha Taifa, Twaha Mwaipaya Msajili wa Vyama vya Siasa aliandika barua ya kuisihi Chadema isitishe maadhimisho hayo.
Barua hiyo iliyosainiwa na Naibu Msajili, Sisty Nyahoza ilisema kilichoelezwa na Mwaipaya katika tangazo la kuelekea shughuli hiyo kinakiuka matakwa ya kifungu cha 6A na 9(2) vya Sheria ya Vyama vya Siasa.
Katika barua hiyo, yalinukuliwa maneno ya Mwaipaya yanayovunja sheria hiyo: ”Siku ya Agosti 12, waje washuhudie vijana wote nchi nzima tunakutana Mbeya, siku hiyo ni siku ya kwenda kuweka hatama ya Tanzania...tupo serious sana na jambo hili.
“Vijana wa CHADEMA kama ambavyo vijana wa Kenya wamejitambua, tunakwenda kuacha uteja wa Serikali na kuweka maazimio makubwa ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2025,” imeeleza sehemu ya barua hiyo ikimnukuu Mwaipaya.
Ikafuatiwa na Polisi
Barua ya Msajili ilifuatiwa na marufuku ya Jeshi la Polisi lililoitaka Chadema iache mara moja kufanya shughuli hiyo, lakini lenyewe lilijikita katika hoja ya kulinda amani na vurugu zinazoashiriwa kutokana na tangazo la kuendelea maadhimisho hayo.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Mbeya, Kamishna wa leo Jumapili, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, Awadhi Juma Haji amepiga marufuku maandalizi ya shughuli hiyo.
Amesema tayari wamejipanga kikamilifu kukabilia na watu watakaothubutu kukiuka agizo hilo, huku likiwa limetoa maelekezo kwa makamanda wa Polisi nchi nzima kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto na kubaini watu waliojipanga kusafiri au kuanza safari kwenda Mbeya.
"Jeshi la Polisi nchini linatoa onyo kali na katazo kwa mtu au kikundi cha watu kinachojipanga kufanya mikusanyiko kuacha mara moja kwani limejipanga vizuri kuhakikisha ulinzi, usalama, amani na utulivu vinatawala nchini," amesema.
Haji amesema wale waliosafiri kutoka mikoa mingine kwenda Mbeya kushiriki maadhimisho kama walivyohamasishwa wameshauriwa kusitisha safari hizo, kwani tayari wametoa maelekezo kwa makamanda wa Polisi nchi nzima.
"Nimetoa maelekezo kwa makamanda wa Polisi nchi nzima kufuatilia katika maeneo yao na wakibaini viashiria vya ambao wanafanya safari kuja Mbeya, kwenye kongamano lililopangwa kwa ajili ya uvunjifu wa amani kuwakamata na kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria," amesema.
Haji amesema wamejipanga kukabiliana na viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani na kwamba halitasita kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria kwa mtu yoyote atakayekiuka katazo hilo.
Amesema kutokana na kauli zinazotamkwa na viongozi wa chama hicho ikiwamo, "kuamua hatma ya Taifa la Tanzania na kwamba wapo "Serious) sana kama vijana wa Kenya walijitambua na kuacha uteja na Serikali," amenukuu.
Amesema mbali na nukuu hizo zipo taarifa nyingine ni viashiria tosha kuwa malengo yao sio kwenda kuadhimisha siku ya vijana duniani bali ni kuanzisha vurugu ili kusababisha uvunjifu wa amani.
Amefafanua kufuatia matamko mbalimbali ya viongozi Jeshi la Polisi limeamua kupiga marufuku maadhimisho na mikusanyiko ya aina yoyote ndani na nje, inayotumika kama mwamvuli katika siku hiyo duniani mkoani Mbeya na maeneo mengine.
Kauli zilizochukuliwa kuashiria uvunjifu wa amani kwa mujibu wa Haji ni "Kama kijana yeyote unaipenda nchi yako ya Tanzania, umeshalia miaka yako yote, siku hiyo ya Agosti 12, 2024 tunakwenda kuweka hatma ya Taifa letu la Tanzania mkoani Mbeya, kwa hiyo kijana yeyote uliyepo popote Tanzania njoo uwanja wa Ruanda Nzomve Mbeya."
Kauli nyingine ni, "Tupo serious sana na jambo hili, kwa hiyo vijana wote wa CHADEMA kama ambavyo vijana wa Kenya wamejitambua, siku ya tarehe 12/08/2024 tunakwenda kuacha uteja kwa Serikali vijana wa Kitanzania na kuweka maazimio makubwa ya uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2025."
Hatimaye kamata kamata
Baada ya taarifa hiyo ya Polisi, Makamu Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Moza Ally alitangaza kuzuiwa kwa misafara ya magari 20 aina ya Coaster yaliyobeba vijana wa baraza hilo wakielekeza mkoani Mbeya kushiriki maadhimisho hayo.
Kutokana na hilo, Moza amewataka vijana wote ambao misafara yao inazuiwa na Polisi njiani, kuzima magari na kufunga barabara ili kuzuia shughuli yoyote isifanyike.
Amewataka wafanye hivyo hadi pale, jeshi hilo litakapoamua kuwaruhusu kuendelea na safari ya kwenda jijini Mbeya kuadhimisha siku yao Agosti 12, mwaka huu.
Ameambatanisha taarifa hiyo na onyo lake kwa Jeshi la Polisi kusitisha mara moja uamuzi wake wa kuzuia misafara hiyo ya vijana, akihoji kwa nini hawakuzuia shughuli ya vijana wa CCM iliyofanyika Zanzibar jana Jumamosi.
“Hapakuwa na shida yoyote, inakuwaje kama vijana wa Chadema tunataka kuadhimisha siku yetu ya vijana duniani mnaanza kutufanyia hujuma namna hii.”
“Hatuko tayari kuendelea kunyanyaswa, kuonewa katika nchi yetu, vijana ambao tayari wameshafika Mbeya ni Coaster 80, zilizozuiliwa ni 20 na zilizopo njiani ni 100,” amesema.
Kwa mujibu wa Moza, matarajio yao ni kuona Coaster 200 zilizobeba vijana zinafika Mbeya.
“Tupo tayari kwa namna yoyote ile kuadhimisha siku yetu ya vijana kama vijana wao walivyoadhimisha yao kule Zanzibar. Vijana wote mtakaozuiliwa kuendelea na safari, hakikisheni mnafunga barabara shughuli zozote zisiendelee mpaka mtakapoachiwa kuja jijini Mbeya,” amesema.
Amesisitiza maandalizi ya shughuli hiyo yanaendelea na wanatarajia kuwapokea viongozi mbalimbali akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu.
Walichoandika viongozi mtandaoni
Kabla ya tamko hilo la Bavicha, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani twitter), Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ameandika akimtaka Rais Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camilius Wambura kusitisha kile alichokiita hatua haramu zinazofanywa nao kuzuia shughuli hiyo.
“Sitisheni hatua haramu zinazofanywa na Jeshi la Polisi kuzuia shughuli halali inayofanywa na Bavicha ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Vijana.
“Zuiazuia na kamatakamata hii ni kinyume na haki na ni dharau kwa 4R mnazojinasibu nazo,” aliandika.
Lissu naye katika mtandao huohuo, alionyesha kusikitishwa na kumwomba Rais Samia kulitaka Jeshi la Polisi kutotumia nguvu kuwazuia vijana kusherekea siku hiyo: “…siku ya Vijana Duniani inasherehekewa duniani kote. Kwa nini mapolisi wako wanazuia vijana wa Chadema barabarani & kuwakamata?”
Ujumbe mwingine uliochapishwa naye ni: “Kwa vijana wote mlioko na mnaoelekea Mbeya, Na mimi (Lissu) niko njiani kuja Mbeya kuungana nanyi.
“Kama ni kuzuiliwa au kukamatwa, na mimi wanizuie au kunikamata. Huu sio wakati kukaa kimya, kuogopa au kuuma uma maneno. Ni wakati wa kusimama na kuhesabiwa. Tupaze sauti kwa nguvu zetu zote,” ameandika.
Kilichoshuhudiwa
Picha mbalimbali jongefu zilishuhudiwa zikionyesha vijana baadhi wamevalia sare za Chadema, wakiwa ndani ya gari la polisi na wengine wakieleza wanapelekwa vituoni.
Kwa mujibu wa video hizo, hata wale waliokwenda kuwasaidia wenzao baada ya kudai wamekamatwa na Polisi nao waliunganishwa na kupelekwa kituoni kufanyiwa mahojiano kwa ajili ya hatua zinazofuata za kisheria.
Sehemu kubwa ya lawama zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii na wafuasi wa Chadema, ziliishukia Serikali kwamba imeanza kuonyesha sura yake halisi.
Hali ilivyo uwanjani
Saa chache baada marufuku ya polisi, magari ya jeshi hilo yalishuhudiwa yakizunguka huku na kule katika Jiji la Mbeya kudhibiti kikamilifu shughuli hiyo.
Mwananchi Digital imeshudia magari zaidi ya sita yakiwa yanapishana barabara kuu ya Tanzam jijini Mbeya yakiwa yamewabeba askari polisi waliokuwa na silaha.
Mbali na barabarani, katika viwanja yalikotarajiwa kufanyika maadhimisho pia, kumezingirwa askari hao wakiwa na mitutu ya bunduki na hakukuwa na vijana wa Bavicha, zaidi ya watoto ambao siku zote huwa hapo wakicheza mpira.
|
Jumla ya magari 20 aina ya Coaster yaliyobeba vijana wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), zimez
|
Jumla ya magari 20 aina ya Coaster yaliyobeba vijana wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), zimezuiliwa na Jeshi la Polisi kwenda mkoani Mbeya kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani.
Hata hivyo, baraza hilo limeweka wazi kila kinachofanywa dhidi yao kuelekea siku hiyo, hakitakuwa kikwazo cha kuadhimishwa kwa siku ya vijana na kwamba maandalizi yanaendelea.
Bavicha ilitangaza kufanya maadhimisho hayo katika viwanja vya Ruandazove jijini Mbeya kesho na hata hivyo, shughuli hiyo imepingwa na Jeshi la Polisi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Upinzani wa mamlaka hizo za Serikali dhidi ya maadhimisho hayo ya Bavicha unatokana na kile kilichoelezwa, kuna viashiria vya uhamasishaji wa uvunjifu wa amani na vurugu katika shughuli hiyo, jambo linalokiuka matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa.
Jeshi la Polisi nalo, katika taarifa yake limetoa marufuku ya kufanyika kwa shughuli hiyo, likiahidi kuwa imara kuhakikisha linadhibiti na kuchukua hatua kwa yeyote atakayekiuka marufuku hiyo.
Katika kulitekeleza hilo, tayari misafara ya vijana kutoka mikoa mbalimbali kwenda jijini Mbeya imezuiwa, huku wengine hasa viongozi wa Bavicha wakiwa mikononi mwa jeshi hilo.
Wakati mamlaka zikifanmya hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Moza Ally amewataka vijana wote ambao misafara yao inazuiwa na polisi njiani, kuzima magari na kufunga barabara ili kuzuia shughuli yoyote isifanyike.
Amewataka wafanye hivyo hadi pale, jeshi hilo litakapoamua kuwaruhusu kuendelea na safari ya kwenda jijini Mbeya kuadhimisha siku yao Agosti 12, mwaka huu.
Ameambatanisha taarifa hiyo na onyo lake kwa jeshi la polisi kusitisha mara moja uamuzi wake wa kuzuia misafara hiyo ya vijana, akirejea katika shughuli ya vijana wa CCM Zanzibar jana kwanini hawakuzuiwa.
“Hapakuwa na shida yoyote, inakuwaje kama vijana wa Chadema tunataka kuadhimisha siku yetu ya vijana duniani mnaanza kutufanyia hujuma namna hii.
“Hatuko tayari kuendelea kunyanyaswa, kuonewa katika nchi yetu, vijana ambao tayari wameshafika Mbeya ni Coaster 80, zilizozuiliwa ni 20 na zilizopo njiani ni 100,” amesema.
Kwa mujibu wa Moza, matarajio yao ni kuona Coaster 200 zilizobeba vijana zinafika Mbeya na tayari 100 zimeshafika huku 20 zikizuiwa na 80 zipo njiani.
“Tupo tayari kwa namna yoyote ile kuazimisha siku yetu ya vijana kama vijana wao walivyoadhimisha yao kule Zanzibar. Vijana wote mtakaozuiliwa kuendelea na safari, hakikisheni mnafunga barabara shughuli zozote zisiendelee mpaka mtakapoachiwa kuja jijini Mbeya,” amesema.
Amesisitiza maandalizi ya shughuli hiyo yanaendelea na wanatarajia kuwapokea viongozi mbalimbali akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu.
Walichoandika viongozi mtandaoni
Kabla ya tamko hilo la Bavicha, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani twitter), Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika aliandika akimtaka Rais Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camilius Wambura kusitisha kile alichokiita hatua haramu zinazofanywa nao kuzuia shughuli hiyo.
“Sitisheni hatua haramu zinazofanywa na Jeshi la polisi kuzuia shughuli halali inayofanywa na Bavicha ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Vijana.
“Zuia zuia na kamata kamata hii ni kinyume na haki na ni dharau kwa 4R mnazojinasibu nazo,” aliandika.
Lissu naye katika mtandao huo huo, aliandika: “Rais Samia usilete mambo ya ajabu ajabu ya Magufuli. Siku ya Vijana Duniani inasherehekewa duniani kote. Kwa nini mapolisi wako wanazuia vijana wa CHADEMA barabarani & kuwakamata?
“Matumizi ya mapolisi yalimshinda Magufuli na wewe yatakushinda. Fungua barabara vijana waende Mbeya”
Ujumbe mwingine uliochapishwa naye ni: “Kwa vijana wote mlioko na mnaoelekea Mbeya: Na Mimi niko njiani kuja Mbeya kuungana nanyi.
“Kama ni kuzuiliwa au kukamatwa, na mimi wanizuie au kunikamata. Huu sio wakati kukaa kimya, kuogopa au kuuma uma maneno. Ni wakati wa kusimama na kuhesabiwa. Tupaze sauti kwa nguvu zetu zote,” ameandika.
Marufuku ya Polisi, Msajili
Kutokana na vuguvugu hilo la Bavicha, Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano na mikusanyiko ya aina yoyote ile ya ndani au nje ya Mbeya inayotaka kufanyika kwa mwamvuli wa kuadhimisha siku ya vijana duniani.
Sababu ya marufuku hiyo ni kile kilichoelezwa katika taarifa ya jeshi hilo kuwa, mikusanyiko hiyo inalenga kuleta uvunjifu wa amani Mbeya na maeneo mengine nchini.
“Jeshi la Polisi nchini linatoa onyo kali na katazo kwa mtu au kikundi cha watu kinachojipanga kufanya maandamano na mikusanyiko kuacha mara moja.
Taarifa hiyo inaongeza jeshi hilo lipo imara na limejipanga kuhakikisha ulinzi, usalama, amani na utulivu vinatawala nchini na lipo tayari kuzuia na kupambana na viashiria vyovyote vya uvunjifu wa Amani.
“Halitasita kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria kwa mtu yeyote atakayekiuka katazo hili,” imeeleza taarifa hiyo.
Kauli zilizochukuliwa kuashiria uvunjifu wa amani kwa mujibu wa taarifa hiyo ni "Kama kijana yeyote unaipenda nchi yako ya Tanzania, umeshalia miaka yako yote, siku hiyo ya Agosti 12, 2024 tunakwenda kuweka hatma ya taifa letu la Tanzania mkoani Mbeya, kwa hiyo kijana yeyote uliyepo popote Tanzania njoo uwanja wa Ruanda Nzovwe Mbeya."
Kauli nyingine ni, "Tupo serious sana na jambo hili, kwa hiyo vijana wote wa CHADEMA kama ambavyo vijana wa Kenya wamejitambua, siku ya tarehe 12/08/2024 tunakwenda kuacha uteja kwa Serikali vijana wa kitanzania na kuweka maazimio makubwa ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2025."
Kabla ya jeshi hilo, tayari Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi alishaiandikia Chadema barua ya kuiasa isitishe shughuli hiyo kwa kile alichoeleza ndani ya barua hiyo kuwa, kuna ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Msingi wa hoja ya msajili ndani ya barua hiyo ni nukuu ya maneno yaliyozungumzwa na Katibu Mwenezi wa Bavicha, Twaha Mwaipaya, kama yanavyosomeka katika nukuu zilizotajwa na jeshi la polisi.
Hata hivyo, chama hicho, kimesisitiza kuendelea na maandalizi ya kufanya shughuli hiyo.
|
Kampuni ya Orca Energy Group Inc, iliyoorodheshwa katika soko la hisa la Toronto ikitokea katika vis
|
Kampuni ya Orca Energy Group Inc, iliyoorodheshwa katika soko la hisa la Toronto ikitokea katika visiwa vya vya Virgin vya Uingereza, imewasilisha madai makubwa ya Dola za Marekani bilioni 1.2 (Sh3.2 trilioni) dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Hatua hii ya kisheria, iliyochukuliwa na kampuni ya Orca inayomiliki kampuni za PanAfrican Energy Tanzania (PAET) na Pan African Energy Corporation Mauritius (PAEM), kampuni hiyo imeeleza mvutano huo unaoibuka juu ya madai ya ukiukaji wa majukumu ya mikataba na uwekezaji.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa katika mtandao wa kampuni hiyo, inaeleza madai ya ukiukwaji wa Mkataba wa Uwekezaji wa Mauritius-Tanzania Bilateral Investment Treaty (BIT), PSA (Production Sharing Agreement), na GA (Gas Agreement).
Gazeti dada la The Citizen lilimtafuta Mwanasheria Mkuu wa Tanzania lakini hakuzungumza chochote juu ya madai hayo wala taarifa ya Orca.
Mgogoro huo unatokana na TPDC kukataa mapendekezo ya PAET ya masharti ya kibiashara ya ziada ya gesi (AG) na mkataba mpya wa mauzo ya gesi, licha ya kumalizika kwa stahili za PG.
PAET inashikilia kuwa hatua hizi zinakiuka haki na matarajio yao ya kimkataba na inatafuta fidia inayozidi dola bilioni 1.2 (Sh3.2 trilioni).
Notisi ya mzozo huo inataka mazungumzo na serikali ya Tanzania na TPDC, huku taratibu za usuluhishi zikisubiriwa ikiwa masuluhisho hayatafikiwa ndani ya muda uliopangwa.
“Chini ya Notisi ya Migogoro, PAET na PAEM wanataka mazungumzo zaidi na Serikali ya Tanzania na TPDC, endapo azimio halitafikiwa: (i) ndani ya miezi sita kuanzia tarehe ya Notisi ya Mgogoro kuhusiana na Mauritius- Tanzania BIT (Bilateral Investment Treaty); na (ii) ndani ya siku 45 baada ya Notisi ya Mgogoro kuhusu PSA (Production Sharing Agreement) na GA, PAEM na PAET, kwa mtiririko huo, zitaanza mashauri ya usuluhishi kwa mujibu wa BIT PSA na GA ya Mauritius-Tanzania,” inasomeka kauli.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mvutano uliongezeka pale PAET ilipoiomba TPDC kuomba kuongezewa muda wa leseni Aprili 2023. Licha ya PAET kuomba mara kwa mara, TPDC ilishindwa kuchukua hatua, kutokana na kuwepo kwa hoja mbovu za kisheria kuhusiana na kuendelea kwa PG. Kusitasita kwa TPDC na tuhuma zisizo na uthibitisho dhidi ya PAET kulisababisha kuvunjika kwa mazungumzo.
Aprili 15, 2024, Wizara ya Nishati ya Tanzania iliingilia kati, na kuiagiza TPDC kuendelea kuzalisha PG zaidi ya tarehe ya mwisho ya PPA, kinyume na makubaliano yaliyokuwepo.
“PAET imekata rufaa kwa maamuzi haya kwa Wizara ya Nishati. Hata hivyo, kutokana na msimamo uliotolewa na Serikali ya Tanzania hadi sasa, PAET inatarajia kuwa Wizara ya Nishati nayo itakataa isivyostahili kuuzwa kwa gesi na PAET kwa masharti ya kibiashara.”
Taarifa hiyo inaongeza kuwa: Mnamo Agosti 5, 2024, hii ilithibitishwa na barua iliyopokelewa na PAET kutoka Wizara ya Nishati, ambapo Wizara ya Nishati iliitaka PAET kupendekeza maneno yanayofaa kwa "mpangilio wa muda" wa kupanua utoaji wa PG. Barua hiyo inaeleza zaidi kwamba ikiwa PAET itashindwa kufanya hivyo, namna nyingine inatafutwa "njia mbadala" za kuendesha kitalu husika.
Agizo hili lilitafsiriwa na PAET kama tishio la kupokonya mali, na kuwafanya watoe Notisi ya Mzozo mnamo Agosti 7, 2024.
“PAET imetafsiri barua hii kuwa ni tishio la wazi kwamba iwapo PAET haitavumilia TPDC na Serikali ya Tanzania ukiukwaji wa haki zake, Serikali ya Tanzania itanyang’anya haki za PAET kuhusiana na kitalu hicho,” inasomeka taarifa hiyo.
PAET imekuwa mwekezaji katika sekta ya nishati nchini Tanzania kwa zaidi ya miongo miwili, ikianza shughuli zake Oktoba 11, 2001.
Katika kipindi hiki, kampuni hiyo inadai kuwa imewekeza zaidi ya dola milioni 311 katika uchumi wa Tanzania, na hivyo kuchangia pato la taifa kwa zaidi ya dola milioni 725 kila mwaka na kutoa zaidi ya dola milioni 900 za mtiririko wa fedha kwa serikali ya Tanzania.
Hata hivyo mambo yaliyotokea hivi karibuni yamezorotesha uhusiano kati ya PAET na mamlaka za Tanzania.
Suala kuu linahusu Leseni ya kuendeleza Songo Songo, iliyotolewa kwa TPDC mwaka 2001 kwa ajili ya kuendeleza kitalu wa Songo Songo.
Makubaliano hayo, ambayo yanajumuisha Mkataba wa Kugawana Uzalishaji (PSA) na Mkataba wa Gesi (GA), yalipangwa kuwasilisha Gesi hadi Julai 31, 2024, hasa kwa ajili ya uzalishaji wa umeme katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kesi hiyo inaangazia utata wa mikataba ya kimataifa na changamoto zinazowakabili wawekezaji katika kudumisha uzingatiaji na kulinda maslahi yao.
Makubaliano hayo, ambayo yanajumuisha Mkataba wa Kugawana Uzalishaji (PSA) na Mkataba wa Gesi (GA), yalipangwa kuwasilisha Gesi Tendwa (PG) hadi Julai 31, 2024, hasa kwa ajili ya uzalishaji wa umeme katika viwanja vya Ubungo karibu na Dar es Salaam.
Kesi zilizotatuliwa hivi karibuni
Mnamo Julai 29, Tanzania ilifikia makubaliano ya suluhu na Indiana Resources Limited, kutatua mzozo wa muda mrefu wa kunyang’anywa Mradi wa Nickel wa Ntaka Hills.
Kutokana na hali hiyo, serikali ya Tanzania ilikubali kulipa jumla ya dola milioni 90 (takriban Sh237 bilioni) kwa Indiana Resources na taasisi zinazohusika, na hivyo kuhitimisha takriban miaka saba ya usuluhishi katika Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID). kitengo cha Benki ya Dunia.
Indiana Resources ina hisa nyingi za Ntaka Nickel Holdings Ltd (NNHL), Nachingwea UK Ltd (NUKL), na Nachingwea Nickel Ltd (NNL), Tanzania inatarajia kufanya malipo hayo kwa awamu tatu.
Awamu ya kwanza ya dola milioni 35 tayari imepokelewa, na dola milioni 25 zinapaswa kulipwa kabla ya Oktoba 25, 2024; na dola milioni 30 za mwisho zitalipwa kufikia Machi 30, 2025.
Mnamo Oktoba 2023, Tanzania ilisuluhisha na kampuni ya uchimbaji madini ya Winshear Gold Corp ya Canada, kulipa dola milioni 30 (Sh75 bilioni) kufuatia mzozo wa kunyang'anywa kwa Mradi wake wa Dhahabu wa SMP ulio kusini-magharibi mwa Tanzania, ukitaka fidia ya zaidi ya Sh250 bilioni.
Makubaliano hayo, ambayo yanajumuisha Mkataba wa Kugawana Uzalishaji (PSA) na Mkataba wa Gesi (GA), yalipangwa kuwasilisha Gesi Tendwa (PG) hadi Julai 31, 2024, hasa kwa ajili ya uzalishaji wa umeme katika viwanja vya Ubungo karibu na Dar es Salaam.
Kesi za hivi majuzi zimetatuliwa
Mnamo Julai 29, Tanzania ilifikia makubaliano ya suluhu na Indiana Resources Limited, kutatua mzozo wa muda mrefu wa kunyang’anywa kwa Mradi wa Nickel wa Ntaka Hills.
Kutokana na hali hiyo, serikali ya Tanzania ilikubali kulipa jumla ya dola milioni 90 (takriban Sh237 bilioni) kwa Indiana Resources na taasisi zinazohusika, na hivyo kuhitimisha takriban miaka saba ya usuluhishi katika Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID). kitengo cha Benki ya Dunia.
Indiana Resources, ambayo ina hisa nyingi za Ntaka Nickel Holdings Ltd (NNHL), Nachingwea UK Ltd (NUKL), na Nachingwea Nickel Ltd (NNL), Tanzania inatarajia kufanya malipo hayo kwa awamu tatu.
Awamu ya kwanza ya dola milioni 35 tayari imepokelewa, na dola milioni 25 zinapaswa kulipwa mnamo au kabla ya Oktoba 25, 2024; na dola milioni 30 za mwisho zitalipwa kufikia Machi 30, 2025.
Kadhalika Oktoba 2023, Tanzania ilikubaliana na kampuni ya uchimbaji madini ya Winshear Gold Corp ya Canada, kulipa dola milioni 30 (Sh75 bilioni) kufuatia mzozo wa kunyang'anywa kwa Mradi wake wa Dhahabu wa SMP ulio kusini-magharibi mwa Tanzania, ukitaka fidia ya zaidi ya Sh250 bilioni.
Serikali yafafanua
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alisema Serikali ipo katika majadiliano na kampuni hiyo na hakuna kesi mahakamani.
Alieleza hafikirii kushindwa kuafikiana kupitia majadiliano hayo kwa kile alichodokeza, wamekuwa wakifanyakazi na kampuni hiyo kwa muda mrefu.
“Lakini ikilazimika kufikia huko (mahakamani) tutafika lakini sidhani kama tunaweza kufika huko,” alisema.
Kwa mujibu wa Kapinga, mkataba wa kampuni hiyo na Tanzania unatarajiwa kuisha mwaka 2026 na kwamba hawezi kueleza kwa kina yaliyopo ndani ya majadiliano.
“Kwa kuwa tupo kwenye majadiliano, tukiyaeleza tutakuwa tunaingilia majadiliano,” alisisitiza.
|
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amesema mafanikio ya kupanua wigo wa kod
|
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amesema mafanikio ya kupanua wigo wa kodi nchini, yatafikiwa kwa kuoanisha mifumo ya mamlaka hiyo na taasisi nyingine za Serikali.
Kupitia uoanishaji mifumo, Mwenda amesema kutawezesha kubaini mwenendo na ukubwa wa biashara za mfanyabiashara husika na hatimaye atatozwa kodi kwa kiwango anachostahili.
Pengine mkakati wa Mwenda utajibu malalamiko ya wafanyabiashara nchini, wanaolalamikia wigo mdogo wa kodi nchini, jambo linalosababisha wingi wa kodi kwa wafanyabiashara wachache.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania (TPSF), Tanzania kwa sasa ina jumla ya walipakodi milioni mbili pekee na ni robo ya idadi hiyo ndiyo waadilifu.
Mwenda ameeleza mikakakti hiyo leo, Ijumaa Agosti 9, 2024 wakati wa uzinduzi wa program tumizi ya Sikika itakayotumika na wananchi kutoa maoni, mapendekezo na malalamiko na kumfikia moja kwa moja Kamishna.
Kwa mujibu wa Mwenda, mamlaka hiyo kwa sasa inaunganisha mifumo yake ili isomane na taasisi nyingine za Serikali, jambo linalotarajiwa kupanua wigo wa kodi.
Katika uoanishani mifumo huo, amesema zitajulikana taarifa za nani anafanya nini na atakapogundulika atasajiliwa na kutozwa kodi kulingana na anachokifanya.
Kamishna huyo amekiri kuwe kwa wigo mdogo wa kodi kwa upande wa wafanyabiashara, ingawa kila mtanzania katika kila bidhaa anayonunua analipa kodi.
“Mifumo hiyo pia itawezesha kuirasimisha sekta isiyo rasmi ambayo ni kubwa na namna gani tunaitambua na kuiweka katika wigo wa kuchangia ni jambo tunaloshughulikia,” amesema.
Katika maelezo yake, Mwenda amesema mifumo hiyo itawezesha kuoanisha mifumo 300 ya taasisi mbalimbali za Serikali na hilo litakamilika Januari 1, mwakani.
“Mifumo hii itafanya kumjua mfanyabiashara kwa mfano wale wanaosafirisha mizigo kwenye mizani tutaona amepira mara ngapi na anapitisha mzigo gani kwa ukubwa gani na akiwa anastahili tutamsajili,” amesema.
Sambamba na hilo, amesema idadi ya sasa ya watumishi TRA ni kubwa baada ya kuongezwa, hivyo itawezesha kuwafikia wafanyabiashara wengi na kuwabaini wale wanaostahili kusajiliwa na kuwa sehemu ya kodi.
Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Hamis Livembe amesema ni kiu yao kuona hilo linatekelezwa.
Ametoa angalizo utekelezwaji wa hilo uzingatie kuongeza vyanzo vipya vya kodi vitakavyotokana na watu wapya badala ya vyanzo vipya kwa wale wale.
“Kuna wakati TRA wanasema wamepanua wigo wa kodi kwa kuongeza kodi au kutunga kodi mpya kwa walipakodi wale wale, hii mifumo isiguse hilo, wakatafute walipakodi wapya ndiyo kiu yetu,” amesema.
Amesema inashangaza Tanzania yenye watu zaidi ya milioni 60 ina walipakodi milioni mbili na kati yao wanaolipa kwa hiari ni 500,000 wakati Kenya yenye watu milioni 32 walipakodi ni milioni tisa.
Katika maelezo yake Mwenda amesema wanashirikiana na mamlaka za Serikali za mitaa kuwafikia wafanyabiashara waliopo katika hatua hizo, ambao kwa sehemu kubwa si walipakodi.
Kitu kingine wanachokifanya kuongeza wigo wa kodi, amesema ni kujenga hamasa ya wafanyabiashara kwa hiari kutoridhishwa na kuwa katika sekta isiyo rasmi na wafurahie kuwa rasmi.
“Tunataka kuondoa faida zinazofanya wang’ang’ane kutokuwa rasmi ili waone umuhimu wa kuwa rasmi,” ameeleza.
Pamoja na mkakati huo, amesema atakachokifanya ni kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na mabalozi kuhakikisha anasikiliza na kutatua changamoto zao ili kuongeza ulipaji kodi wa hiari.
Elimu ya kodi, mifumo bora ya kikodi, ushirikiano na tume iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kurekebisha masuala ya kikodi ni jambo lingine atakalolifanya katika uongozi wake.
Amesema atasimamia kukomesha vitendo vya ukwepaji kodi na kuhakikisha kila anayestahili analipa kodi kwa kiwango sahihi bila kumwonea wala kumpendelea.
Kuhusu soko la kariakoo
Kuhusu Kariakoo, amesema wanafikiria kulifanya soko hilo kanda maalumu ya kikodi, hatua itakayotanguliwa na kuboresha mazingira ya biashara sokoni hapo.
Katika kushughulikia changamoto za wafanyabiashara sokoni hapo, amesema umeandaliwa utaratibu wa kukutana nao mara tatu kila mwezi.
Kuhusu programu hiyo, amesema itamwezesha mfanyabiashara au mwananchi kutoa maoni, malalamiko na ushauri wa kikodi kwa TRA na moja kwa moja utamfikia kamishna.
Amesisitiza katika utoaji wa taarifa hizo kutakuwa na usiri mkubwa wa mtoa taarifa.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema ni muhimu kuimarishwa ushirikiano kati ya TRA na wanahabari ili kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kulipa kodi.
|
Jeshi Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema upelelezi wa tukio la binti aliyebakwa na kulaw
|
Jeshi Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema upelelezi wa tukio la binti aliyebakwa na kulawitiwa kisha video yake ikasambazwa katika mitandao ya kijamii upo hatua za mwisho.
Sambamba na hilo, jeshi hilo limekanusha taarifa ilizodai za uzushi kuhusu kifo cha binti alitefanyiwa ukatili huo, likidai yupo hai.
Video za binti huyo akifanyiwa ukatili huo zilisambaa Agosti 4, 2024 katika mitandao ya kijamii, akionekana na vijana watano waliomfanyia vitendo hivyo.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni alithibitisha kukamatwa kwa waliohusika na ukatili huo, huku Jeshi la Polisi ngazi ya taifa likieleza kuwa katika hatua nzuri za kiuchunguzi.
Taarifa za hatua iliyofikiwa ya kiuchunguzi imeelezwa leo, Jumatano Agosti 7, 2024 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.
Amesisitiza upelelezi kuhusu tukio hilo upo katika hatua za mwisho na hivi karibuni Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime atalitolea ufafanuzi.
“Tupo kwenye hatua ya mwisho hivi karibuni msemaji wa jeshi la polisi atalitoolea taarifa,” amesema Muliro wakati akionya taarifa za uzushi kwa kile alichoeleza zinaingilia uchunguzi wa polisi.
Katika hatua nyingine, ametangaza kumshikilia Amos Rwiza (54), Mkazi wa Tegeta kwa kosa la kusambaza taarifa hizo za uzushi juu ya kifo cha binti huyo.
"Tumemkamata mtuhumiwa kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo na ameingilia masuala ya kiuchunguzi,” amesema.
Murilo amesema jeshi hilo linafuata Katiba ya nchi na si kwamba linakataa watu kutoa maoni, isipokuwa linakerwa na upotoshaji huku likiahidi kuendelea kuchukua hatua za kisheria.
Kuhusu mtuhumiwa aliyekamatwa, amesema alileta taharuki kwenye jamii, baada ya kusambaza taarifa hizo za uongo.
Ametoa wito kwa jamii inapobaini kuna vitendo viovu vinafanyika watoe taarifa ili zifanyiwe kazi.
|
Vuguvugu la kurejea ndani ya Chadema kwa baadhi ya wabunge wa viti maalumu kati ya wale 19 waliowahi
|
Vuguvugu la kurejea ndani ya Chadema kwa baadhi ya wabunge wa viti maalumu kati ya wale 19 waliowahi kuvuliwa uanachama wa chama hicho limeanza.
Harakati hizo zinaanza katika kipindi ambacho, Tanzania inakaribia kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani.
Wabunge hao ni wale ambao Novemba 27, mwaka 2020 Kamati Kuu ya Chadema iliwavua uanachama kutokana na uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu ilhali msimamo wa chama hicho ulikuwa ni kususia nafasi hizo.
Sababu ya kususa kwa chama hicho ni kile kilichoelezwa mara kadhaa kuwa, hakikubaliani na matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020, hivyo walifanya hivyo kushinikiza mabadiliko.
Walioapishwa kuwa wabunge katika nyakati hizo ni Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Sophia Mwakagenda, Salome Makamba, Halima Mdee, Grace Tendega, Cecilia Pareso, Agnes Lambart, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa na Hawa Mwaifunga.
Wengine ni Tunza Malapo, Asia Mohammed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Kunti Majala, Stella Flao, Anatropia Theonest na Conchesta Rwamlaza.
Taarifa ambazo Mwananchi linazo si wabunge wote 19 walioianza safari ya kurudi Chadema ni wachache na hata hivyo uamuzi wa kurejea kwao unawagawa vigogo ndani ya chama hicho wengine wakibariki na baadhi wakipinga vikali.
Wakati wengine wakiianza safari hiyo, wapo ambao kwa matendo yao wamejipambanua kwenda CCM na wameanza kusaka nafasi katika majimbo mbalimbali kwa tiketi ya chama hicho tawala, akiwemo Nusrati Hanje.
Hanje anaonekana akilinyemelea moja kati ya majimbo ya Mkoa wa Singida kama ilivyo kwa Jesca Kishoa. Lakini Salome Makamba naye yu katika harakati za kuusaka ubunge katika moja ya majimbo mkoani Shinyanga kwa tiketi ya CCM.
Rasha rasha za kurejea
Rasharasha za baadhi ya wabunge hao kurejea ndani ya Chadema, zilianza na kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu alipotoa salamu za Chadema katika msiba wa mama mzazi wa Halima Mdee juzi.
Katika salamu hizo, Mwalimu alisema CCM itamuota sana Mdee juu ya kuhamia katika chama hicho.
“Baba Paroko kuna jambo limechokozwa, lakini limeshajibiwa, eti anafanana na huko? (aliuliza Mwalimu na kujibiwa hapana na waombolezaji, kisha akaendelea..) hafanani ee… basi watamuota sana,” alisema.
Mwalimu alitoa kauli hiyo akijibu kilichozungumzwa awali na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Ramadhan Mahanyu aliyemkaribisha Mdee ndani ya chama hicho tawala.
“Sasa dadaangu Halima kwa sababu huko kwingine hakueleweki, njoo huku (CCM),” alisema.
Mwalimu anatoa kauli hiyo katika kipindi ambacho chama hicho kilishawafuta uanachama kina Mdee na wenzake 18, hivyo hakina nasaba nao katika itikadi za kisiasa.
Kauli yake ya kudai wanaomtaka ahamie CCM watamuota sana inaibua swali la amejuaje kama uamuzi huo kwa Mdee utabaki kuwa ndoto?
Mwalimu akana kauli yake
Kutokana na swali hilo, Mwananchi jana ilimtafuta Mwalimu kuzungumzia kwa kina kauli yake na katika majibu kuhusu hilo, alijikana mwenyewe kwa kile alichoeleza jambo la msibani na liliishia huko.
“Tulichokifanya ni kwamba CCM walituchokoza na sisi ikabidi tuwajibu, lakini yaliyotokea msibani yaishie pale pale. Tungetaka yatoke nje tungeyazungumze nje,” alisema.
Alisisitiza alichokizungumza hakulenga kutafsiri chochote, akifafanua itafsiriwe kuwa kauli ya msibani na iishie kwenye msiba.
“Nachosema kilichosemwa pale kinaishia kwenye mazingira yale yale na kitaishia kwenye eneo lile lile. Mimi ukitaka kutafsiri lolote usinilazimishe mimi kutafsiri unavyotaka,” alisema.
Si kauli ya bahati mbaya
Gazeti hili lilikwenda mbali zaidi kufahamu iwapo kuna dalili za wabunge hao kurejea Chadema na moja ya chanzo cha uhakika kutoka ndani ya chama hicho kilieleza kauli ya Mwalimu haikuwa ya bahati mbaya.
Chanzo hicho ambacho ni sehemu ya uongozi wa juu wa Chadema, kilisema alichokisema Mwalimu kinalenga kuwaanda mapema wanachama juu ya kurejea kwa kina Mdee na baadhi ya wenzake.
Hata hivyo, alieleza kuna jitihada kubwa zinafanyika za kuhakikisha kina Mdee na wenzake akiwamo Bulaya wanarejea kundini kama ilivyokuwa miaka iliyopita.
“Kuna jitihada kubwa zinafanyika kina Mdee kusamehewa ili kurejeshwa katika chama, sio wote watakaorejea kwa sababu wengine wameshaonyesha nia ya kwenda CCM. Lakini mkakati mkubwa ni Mdee, Bulaya , Sophia Mwakagenda, wakati Nusrat ameshaenda chama tawala kabisa na Salome ameonyesha nia kwenda CCM pia,” alisema.
Watarejea hivi…
Kiongozi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa sababu za kiitifaki, alisema kuna uwezekano wa wanasiasa hao kuandika barua ya kuomba msamaha, kisha kamati kuu itawasamehe.
“Wanaweza kuandika barua za kuomba msamaha, kisha kamati kuu inawasamehe na wanakuwa wanachama wa kawaida, maisha yanaendelea, lakini ukweli kuna jitihada kubwa zinafanyika ili kina Mdee kurejea,” alieleza.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, hatua ya Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa Chadema), Mdee na Bulaya kukutana katika harambee ya kuchangia kanisa mwaka 2023, ilisababisha mgogoro ndani ya chama hicho.
Mgogoro huo ulitokana na kile alichoeleza, baadhi ya makada wa chama hicho walihoji Mbowe anapata wapi ujasiri wa kuwaalika kina Mdee.
Harambee hiyo ilifanyika Desemba 31, mwaka jana ikilenga kufanikisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa kanisa la Betheli usharika wa Nshara Machame na Mbowe alishiriki kwa mwaliko wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Dk Fredrick Shoo.
Lakini, Mbowe naye aliwaalika John Mnyika (Katibu Mkuu Chadema), Mdee na Bulaya na kuwaomba wachangie harambee hiyo na wote walishiriki kwa kwenda kanisani na kuchangia.
Katika mazingira hayo, chanzo hicho kinaeleza Askofu Shoo aliwaita wabunge hao na baadhi ya viongozi wa Chadema kutafuta suluhu nyumbani kwake, lakini kigogo mmoja wa chama hicho aliamua kuondoka kikaoni kwa kususa.
Kuondoka kwake, alisema kulitokana na msimamo wake mkali dhidi ya wabunge hao 19.
“Katika chama wenye misimamo mikali kuhusu suala la kina Mdee wapo wawili, ambao hawataki kusikia biashara ya suala la wabunge 19, lakini ukweli kuna hiyo movie inafanywa ili hawa watu warudi katika chama kauli ya Salum siyo bahati mbaya bali ni kimkakati ya kuwaandaa watu,” alisema.
Aliongeza kuwa katika kikao cha kamati kuu cha siku mbili kitakachoanza leo, pamoja na mambo mengine watajadili suala la uteuzi wa makatibu wa kanda za Nyasa, Victoria, Magharibi na Serengeti zilizomaliza uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya.
“Suala la kina Mdee linaweza kuchomoza ndani ya kamati kuu, kama mengine mengineyo lakini siyo ajenda,” alisema.
Ni suala la kawaida katika siasa
Kutokana na vuguvugu hilo, Mwanazuoni wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Dk Conrad Masabo alisema ni vigumu kupima athari na faida za kurejea kwa baadhi ya wanasiasa hao ndani ya Chadema.
Isipokuwa, alisema kama watarejea litakuwa suala la kawaida akirejea kama Chadema ilimpokea Hayati Edward Lowassa kutokea CCM, inashindwaje kuwapokea wanasiasa iliyowalea yenyewe.
“Moja ni chama cha siasa mtaji wake ni wanachama na wakati wowote unapoona chama kinafukuza wanachama sio kwamba kinapenda ila ni katika kuangalia wale wanaosababisha udhaifu kwenye chama.
“Inaweza kuwa ni dhana ya kawaida katika siasa na ukizingatia siasa si uadui ni ushawishi katika muda fulani na kwa sababu fulani,” alieleza.
Iwapo watarejea, alisema hakuna kati ya Chadema wala wabunge hao atakayepaswa kuonekana mkosaji.
“Lakini kipindi kile ilikuwa lazima uongozi uchukue hatua ili kuleta utulivu ndani ya chama,” alisema.
Hata hivyo, alisema Mdee na Bulaya ni miongoni mwa wanachama muhimu na Mbowe amewahi kukiri hilo na licha ya kukiuka utaratibu hadi kufukuzwa, wakiwa nje ya Chadema baadhi yao hawakuwahi kufanya kitu kibaya.
|
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hatari ya kutokuwepo kwa chakula na kupanda zaidi kwa bei ya sukari
|
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hatari ya kutokuwepo kwa chakula na kupanda zaidi kwa bei ya sukari nchini, kutawaingiza barabarani vijana wa kizazi cha Z maarufu GenZ.
Kauli hiyo ya Rais Samia inaakisi kilichotokea katika mataifa kadhaa ya Afrika, yakitanguliwa na Kenya ambapo vijana waliozaliwa mwaka 2000, waliingia barabarani kuandamana kupinga muswada wa sheria ya fedha waliodai unaongeza ugumu wa maisha.
Katika ufafanuzi wake kuhusu kauli hiyo, mkuu huyo wa nchi amesema ni jumuku la Serikali kusimamia maslahi ya makundi yote na inapoonekana kuegemea upande wa wananchi, ni kwa sababu ya jukumu hilo.
Hata hivyo, kauli ya Rais Samia ni kama inafafanua dhamira ya uamuzi wa Serikali kuondoa jukumu la uagizaji sukari kutoka wa wazalishaji wa bidhaa hiyo hadi kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).
Awali, sheria ya sukari iliwapa wazalishaji jukumu la uagizaji wa bidhaa hiyo unapotokea uhaba, lakini baadaye wakaonekana kudorora jambo lililotafsiriwa ni nia ovu ya kutaka kupandisha bei.
Katika mazingira hayo, wazalishaji nao walitoka hadharani na kuishutumu Serikali hasa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), kuchelewesha kutoa vibali vya uagizaji huo.
Kutokana na hayo ndipo Serikali ilikuja na mabadiliko ya sheria ya sukari na kuipa NFRA jukumu la uingizaji wa sukari unapotokea uhaba, ikisema inafanya hivyo kwa maslahi ya wananchi na wazalishaji walilalamika kwa Serikali kutowajali.
Rais Samia aliyasema hayo mkoani Morogoro wakati akizindua Bwawa la Umwagiliaji la Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika Mkoa huo.
Alisisitiza inapoonekana Serikali imeegemea upande wa kundi linaloonekana kukosa nguvu haimaanishi ina maslahi huko, bali ni katika msingi wa kutekeleza jukumu la kutetea maslahi ya wote.
“Wanasema chakula ni siasa, kukiwa hakuna chakula ile Generation Z haitatulia itaingia barabarani, au ukiwapandishia sukari kilo kwa Sh7,000 hawatatulia,” alisema.
Alieleza Serikali inaposimamia kundi la wananchi wanaotaka sukari kwa bei ya uhakika na himilivu, msingi wake ni huo.
Sambamba na hayo, Rais Samia aliwasihi wawekezaji waendeleee kuwekeza kwenye teknolojia na mbinu za kisasa katika uzalishaji ili kupunguza gharama na kuongeza tija zaidi.
Aliahidi kufanyia kazi ombi la ujenzi wa Barabara ya Wami-Dawawa-Madizini lililotolewa na kiwanda cha Mtibwa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema Serikali inatoa Sh220 bilioni ikiwa ni misamaha ya Kodi katika seta ya sukari.
Misamaha hiyo, alisema inalenga kuhakikisha sekta ya sukari nchini inaimarika, huku uzalishaji ukiongezeka.
Kwa mujibu wa Bashe, Serikali kwa sasa inaandaa Sera ya Taifa ya fedha katika sekta ya kilimo ili kuhamasisha uwekezaji wa muda mrefu.
Alisema mahitaji ya sukari nchini kwa sasa ni tani 650,000, lakini matarajio ya uzalishaji mwaka huu ni tani 550,000.
Lakini, kufikia mwaka 2026, alisema uzalishaji unatarajiwa kufikia tani 750,000, huku mwaka 2030 ukifika tani milioni moja.
Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Mtibwa, Seif Ally Seif alipendekeza kuboreshewa barabara kutoka Wami Dakawa hadi katika eneo la Kiwanda.
Kadhalika, alipendekeza kuwepo mazingira wezeshi yanayohamasisha uwekezaji na taasisi za fedha ziongeze ukopeshaji.
Lakini yote hayo, alisema yataoaswa kubebwa na uwepo wa sera zinazotabirika za uwekezaji.
Alieleza katika mradi wa upanuzi wa mradi huo, mitambo mitambo 47 imeshafungwa na mradi utakapokamilika itafikia 112.
Alisema uwekezaji umefanyika kwa kuweka mitambo mipya kiwandani na wanachakata miwa tani 180,000 kwa saa na wanatarajia kufikia 230,000 mwaka 2027.
…Akiwa Mvomero
Akizindua programu ya Tutunzane inayolenga kuwaweka pamoja wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Mvomero, Rais Samia alitaka wenyeviti wa vijiji wadhibiti migogoro hiyo badala ya kutanguliza kunyoosha mikono kupokea fedha.
Alisema malalamiko yaliyopo ni uongozi wa vijiji kuwa wepesi wa kunyoosha mikopo kupokea fedha badala ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
“Mamlaka za Mikoa na Wilaya hakikisheni yeyote atakayeingilia uhuru wa mwenzake kwa kuingiza mifugo kwenye shamba lake, mnamchukulia hatua,” alisema.
Katika hotuba yake hiyo, alisema programu ya Tutunzane itaepusha migogoro na kutunza amani kwa wakulima na wafugaji wa maeneo mbalimbali.
Pia, alieleza itaongeza wigo kwa wakulima na wafugaji wa kukopesheka kupitia hati watakazozipata.
Alisema wakulima na wafugaji ni kama watoto waliozaliwa kwenye familia moja, kwa kuwa wanategemeana.
Alisema nchi huwa na nguvu zaidi iwapo kutakuwa na umoja, kwani migogoro husababisha machafuko.
Katika maelezo yake, alirejea Katiba ya Tanzania inayomtaka kila mmoja afanye mambo yake bila kuingilia haki ya mwingine.
Aliitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha inatafuta wadau hasa wa sekta binafsi kuwekeza kwenye programu hiyo ya kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji
Hata hivyo, alisema ni vigumu kuyaepuka mabadiliko ya namna ya kulima na kufuga kwa sababu ardhi haiongezeki huku binadamu wanaongezeka.
“Lazima tuwe wabunifu wa kuja na mbinu zitakzofanya ardhi tuliyonayo izalishe zaidi. Kama ni mkulima azalishe zaidi kwa kipande cha ardhi alichonacho vivyo hivyo kwa mfugaji,” alisema.
Alitaja uwepo wa changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, akisema teknolojia za kisasa ni muhimu kuhakikisha wanalima, kufuga na kupata vya kutosha.
Awali, akizungumzia programu hiyo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema wakulima 1,066 wamesajiliwa.
Hata hivyo, alisema Sh70 milioni imeombwa na Halmashauri ya Mvomero kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
“Tayari nimeshamwelekeza Katibu Mkuu (Gerald Mweli) kuangalia fedha hiyo na kuifikisha kwa halmashauri hiyo kwa ajili ya kutekeleza programu,” alisema.
Akizungumza katika tukio hilo, Mbunge wa Mvomero, Jonas Zeelan aliomba kujengwa kwa kilomita 25 za barabara ya Magole kwenda Mvomero.
Alisema barabara hiyo inauunganisha Mkoa wa Morogoro na Tanga hivyo anaomba ijengwe kwa kiwango cha lami.
Pamoja na barabara hiyo, Zeelan ameomba Mvomero iwe moja ya maeneo yatakayonufaika na mradi wa maji unaotarajiwa kuhudumia Morogoro Mjini.
Kadhalika, Mbunge huyo alieleza uwepo wa changamoto ya tembo katika Tarafa ya Mlari, akisema inawalazimu wananchi waishie kulima ufuta pekee.
“Naomba wale tembo warudishwe hifadhini na kujengwe ukuta utakaozuia wasitoke hifadhini na kuja katika mashamba ya wakulima,” alisema.
Ombi lake kuhusu kunufaika na mradi wa maji, lilijibiwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akisema mradi ho hautafika Morogoro Mjini kabla haujawanufaisha wakazi wa Mvomero.
Kuhusu barabara, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema ujenzi umeshaanza kwa upande wa Tanga na kwamba itafika hatua kioande hicho kitajengwa.
|
Licha ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni kuthibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa wa ub
|
Licha ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni kuthibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa wa ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa mkazi wa Yombo Dovya, bado kuna utata wa taarifa juu ya mwenendo wa hatua dhidi ya tukio hilo.
Utata huo unatokana na taarifa ya Jeshi la Polisi ya jana jioni, iliyoeleza kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea vema, wakati tayari Waziri Masauni alishathibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa.
Hata hivyo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax naye amejibu madai ya askari wa jeshi la ulinzi kuhusika katika tukio hilo, akitaka watafutwe polisi kwa kuwa ndiyo wenye mamlaka ya kuchunguza na hatimaye kugundua muhusika.
Video za tukio hilo zilisambaa Agosti 4, mwaka huu katika mitandao ya kijamii zikionyesha vijana watano wakimbaka na kumwingilia msichana huyo kinyume na maumbile.
Sambamba na ukatili huo, katika video nyingine vijana hao wanasikika wakimhoji binti huyo na kushurutisha amwombe radhi mtu aliyetajwa kwa jina la Afande, naye alifanya hivyo.
Baada ya tukio hilo, wanamitandao mbalimbali walilaani kupitia mitandao ya kijamii na kutaka Serikali ichukue hatua za haraka dhidi ya wahusika.
Mbali na wanamitandao, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kililaani tukio hilo, huku kikimtaka Rais Samia atoke hadharani kukemea ukatili huo na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Camilius Wambura achukue hatua za haraka hadi kuhakikisha watuhumiwa wanafikishwa mahakamani.
Mfululizo wa wanaokemea uliendelea hadi kwa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), kupitia taarifa iliyotolewa na Rais wake, Boniface Mwabukusi kililaani pia tukio hilo.
Ilieleza inaendelea kufuatilia kwa karibu kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha htua stahiki kwa waliohusika zinachukuliwa.
Wakili Peter Mdeleka kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani twitter), aliahidi kuingilia tukio hilo na kuchukua hatua za kisheria iwapo mamlaka hazitafanya hivyo ndani ya saa 24 tangu lilipotokea.
Majibu ya Masauni, Tax
Alipoulizwa na Mwananchi jana iwapo watuhumiwa hao wameshakamatwa, Masauni alijibu kwa kuandika “tayari” kupitia ujumbe huo huo wa njia ya WhatsApp.
Hata hivyo, alisema bado yu kwenye mkutano kwa wakati huo.
Mbali na kilichojibiwa na Masauni, swali lingine lilimlenga Dk Tax kuhusu madai ya askari wake kuhusika, alijibu Jeshi la Polisi ndilo lenye mamlaka ya kufanya uchunguzi na kutoa jawabu la nani wa namna gani aliyehusika.
Kwa sababu jeshi hilo limeshaeleza linaendelea kufanya kazi yake, alisema maswali yote kuhusu nani anahusika yaelekezwe huko.
“Unaponiuliza mimi ni kama unamuuliza mtuhumiwa, anayehusika na uchunguzi wa kubaini mhalifu ni jeshi la polisi, uliza jeshi la polisi kujua hayo.
“Ukimtaja huyo askari wangu nitasema umetaja mtu, lakini sijathibitisha kwa sababu anayefanya uchunguzi ni mtu mwingine (Polisi),” alisema.
Hata hivyo, alisema Serikali haitavumilia uvunjwaji wa aina yoyote wa sheria na yeyote atakayebainika kufanya hivyo, atachukuliwa hatua stahiki.
Majibu ya Polisi
Wakati mawaziri wakijibu hivyo, taarifa iliyotolewa na Polisi jana, kupitia msemaji wake, David Misime ilieleza uchunguzi unaendelea vizuri na wananchi waendelee kuwa na subira.
Katika taarifa hiyo, Misime alisema; “Taarifa itatolewa baada ya kukamilisha yale ambayo sheria za nchi zinavyoelekeza.”
“Jeshi la Polisi linatoa wito sote kwa pamoja tuendelee kutafakari namna tunavyoendelea kujadili jambo hili na tunavyotoa maoni kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari je hatuendelei kumtonesha huyu binti majeraha aliyonayo moyoni? Je kwa kuendeleza hayo familia yake hatuendelei kuijeruhi kisaikolojia?,” alihoji.
Alisisitiza mwenye taarifa ya ziada aziwasilishe kwa njia sahihi kwa kutumia mifumo iliyopo bila kuendelea kumuumiza muathirika.
‘Aliyewatuma akamatwe’
Pamoja na kufurahishwa na hatua ya kukamatwa kwa watuhumiwa, Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga alisisitiza aliyewatuma pia anapaswa akamatwe.
Kwa mujibu wa Henga, kilichofanyika ni kosa la jina na katika jinai, aliyewaza na aliyetenda wote wanakuwa na kosa linalofanana.
“Kiu yetu ni kuona aliyewatuma huyo aliyemuita Afande naye anakamatwa kwa sababu amefanya kosa lile lile kama walilofanya hao vijana walioonekana kwenye video,” alieleza.
Hata hivyo, alisema kwa sababu jamii inaonyesha kukerwa zaidi na tukio hilo, isiwe shinikizo la watuhumiwa hao kufanyiwa ukatili wakati wa mahojiano.
“Wanapaswa kuhojiwa kawaida kama inavyofanyika kwa watuhumiwa wengine na isitokee tena na wao wakafanyiwa ukatili kama ambavyo wao wamefanya ukatili.
“Kuna watu wanasema wanyimwe dhamana hiyo ni haki yao kwa sababu kosa lao linadhaminika, isipokuwa wafanyiwe hivyo kama itaonekana kuna hatari ya usalama wao,” alisema.
Lakini, alisisitiza jambo muhimu ni kuhakikisha hatua za kisheria zinafanyika na wahukumiwe kama inavyopaswa kwa mujibu wa sheria.
Juhudi za kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania zimeshindikana baada ya simu yake kuita mara kadhaa bila kupokelewa.
|
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax amesema Serikali haitavumilia uvunjwaj
|
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax amesema Serikali haitavumilia uvunjwaji wa aina yoyote wa sheria na yeyote atakayebainika kufanya hivyo, atachukuliwa hatua stahiki.
Kauli ya Dk Tax inajibu tukio la kubakwa na kulawitiwa kwa binti mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam, lililofanywa na vijana watano wanaodaiwa kuwa ni askari wa jeshi la ulinzi.
Video za tukio hilo zilisambazwa juzi Agosti 4, 2024 katika mitandao ya kijamii zikionyesha vijana hao wakimbaka na kumlawiti binti huyo kwa kile walichodai ametembea na mume wa mtu.
Katika video hizo, vijana hao wamesikika wakimtaka binti huyo amwombe radhi mtu waliomwita Afande.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ameshathibitisha kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo, ingawa hajaweka wazi hatua zinazofuata.
Agosti 4, 2024, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime alitoa taarifa kwa umma kuzungumzia tukio hilo, akiahidi kulifanyia kazi huku akilaani.
“Jeshi limetoa wito kwa wananchi wote waache kuendelea kusambaza video hiyo, kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria, lakini ni kitendo cha kuendelea kudhalilisha utu wa binadamu mwenzetu.
“Tunatoa wito kwa mwenye taarifa ya kuhakikisha mkono wa sheria unawafikia kwa haraka waliofanya ukatili huu asisite kutusaidia kwa kutupa taarifa au kumpatia kiongozi yeyote yule wanayemwamini kwamba taarifa ikimfikia watu hao watapatikana haraka iwezekanavyo,” alisema Misime.
Dk Tax ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 6, 2024 alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kuhusu tukio hilo.
Alipoulizwa iwapo waliohusika ni askari wa jeshi la ulinzi, amejibu Jeshi la Polisi ndilo lenye mamlaka ya kufanya uchunguzi na kutoa jawabu la nani wa namna gani aliyehusika.
Kwa sababu jeshi hilo limeshaeleza linaendelea kufanya kazi yake, amesema maswali yote kuhusu nani anahusika yaelekezwe huko.
“Unaponiuliza mimi ni kama unamuuliza mtuhumiwa, anayehusika na uchunguzi wa kubaini mhalifu ni jeshi la polisi, uliza jeshi la polisi kujua hayo.
“Ukimtaja huyo askari wangu nitasema umetaja mtu, lakini sijathibitisha kwa sababu anayefanya uchunguzi ni mtu mwingine (Polisi),” amesema.
Katika msisitizo wa hilo, amesema Serikali haitavumilia uvunjwaji wa aina yoyote wa sheria na yeyote atakayebainika kufanya hivyo, atachukuliwa hatua stahiki.
Hata hivyo, wadau mbalimbali kikiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wamelaani tukio hilo wakiitaka Serikali ichukue hatua.
|
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuridhia pendekezo la Wizara ya Kilimo la kuongeza bei ya kilo m
|
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuridhia pendekezo la Wizara ya Kilimo la kuongeza bei ya kilo moja ya mpunga kutoka Sh500 hadi Sh900.
Sambamba na hilo, ametaka Serikali inunue zao hilo kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kuepuka madalali ambao mara nyingi wanawakandamiza wakulima.
Uamuzi huo wa Serikali umeibua furaha kutoka kwa wakulima, wakisema utaondoa changamoto ya masoko kwa upande mmoja, lakini utawafaidisha kutokana na shughuli zao.
Hadi Rais Samia anafikia uamuzio huo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alishawasilisha pendekezo la kuongezwa kwa bei hiyo, akilenga kuondoa madalali.
Rais Samia alitangaza uamuzi huo jana, alipowahutubia wananchi wa Wilaya ya Ifakara mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.
Alisema pamoja na nyongeza ya bei hiyo pia Serikali inapaswa kununua mpunga huo kwa wakulima kupitia NFRA.
Walichosema wakulima
Kutokana na uamuzi huo, Meneja wa Ushirika wa Wakulima Wadogo wa Umwagiliaji wa Mpunga (Uwawakuda), Wilbard Olomi alisema ongezeko la bei hiyo litawafanya wakulima wanufaike na shughuli zao.
Kwa mujibu wa Olomi, nyongeza ya Sh400 kutoka katika bei ya awali ni karibu nusu yake na kwamba itawaepusha na madalali.
Lakini kwa upande mwingine, alieleza uamuzi wa Serikali kununua mpunga huo, utawapa wakulima hasa wadogo uhakika wa soko la mazao yao ya kilimo.
“Tumekuwa tukilima na hatimaye kunakosekana soko la uhakika ndiyo maana tunajikuta tunaishia kuwauzia madalali. Wenzetu wanakwenda kwenye masoko wanayaongezea thamani mazao na wanafaidika,” alisema.
Meneja wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (Tari) Kituo cha Dakawa kinachojihusisha na utafiti wa zao la mpunga, Dk Jerome Mghase alisema ongezeko la bei ni fursa kwa wakulima.
Kutokana na ongezeko hilo, alieleza gunia lililokuwa linauzwa kwa Sh70,000 kwa sasa litauzwa kwa Sh90,000 ikiwa ndiyo bei inayoeleweka.
Katika mazingira hayo, alieleza mkulima atanufaika na kilimo, lakini hata wafanyabiashara hawatapata hasara.
Lakini, alieleza punguzo hilo litawanufaisha zaidi wale wakulima ambao si wafanyabiashara, kwa maana wanaolima na kuuza shambani.
“Kuna wale ambao huwa wanauziana wenyewe kwa wenyewe na ili auze anasubiri bei ichanganye, pengine hawa hawataguswa maana atasubiri kipindi cha uhaba ndiyo auze,” alieleza.
Wakati anayaeleza hayo, Rais Samia aliwataka viongozi wasiwe sehemu ya wanaowakandamiza wakulima katika ununuzi wa mpunga huo, akisema vitendo hivyo vinavunja haki.
“Tumeweka viongozi ngazi mbalimbali tuwasaidia wananchi, mnapoijiingiza kwenye biashara hii na kwenda kunyonya nguvu ya mkulima hufanyi haki, uwe diwani uwe nani kama unafanya biashara hii ya kuongeza kipimo kwenye debe la mkulima hufanyi haki,” alisema.
Sababu ya kauli yake hiyo ni kile alichoeleza, ana taarifa za uwepo wa viongozi ambao nao wanajihusisha na shughuli za biashara hiyo.
Awali, akizungumza katika mkutano huo, Bashe alipendekeza kuongezwa kwa bei ya mpunga kutoka Sh500 kwa kilo hadi Sh900.
Siasa na uvamizi maeneo ya hifadhi
Wakati huo huo, Rais Samia alikemea tabia ya uanzishwaji wa vijiji vipya unaofanywa kwa maslahi ya kisiasa, akisema ndiyo inayochochea uvamizi wa maeneo ya hifadhi.
Tabia za uanzishwaji vijiji vipya, alisema aghalabu hufanyika katika nyakati zinapokaribia chaguzi, wagombea wakilenga kunufaika kisiasa.
“Inapokaribia chaguzi hizi hasa madiwani, mtu akiona yuko vibaya upande mwingine wa eneo lake, anakwenda kusogeza watu kuanzisha kijiji.
“Sasa haya ya kuanzisha vijiji bila kujali tunavianzisha maeneo gani, vijiji vingi vilivyoanzishwa ndani ya maeneo ya hifadhi ni kwa ajili ya wanasiasa wameanzisha, iwe ni madiwani iwe wabunge,” alisema.
Pamoja na kwamba wanasiasa hao ndiyo wanaowapeleka wananchi katika maeneo hayo, alisema hao hao baadaye wanageuka kuwa watetezi wao, akidai wanapoondolewa kwenye hifadhi wanaonewa.
“Alafu ni hao hao wanaokuja kusimama kuwatetea watu walioingia ndani ya hifadhi, maana yake hawa wananchi wetu, wanateseka wanapata shida, lakini ulipowapeleka ulikuwa unajua ni eneo la hifadhi,” alisema.
Msisitizo wa Rais Samia ni kukoma kwa tabia hiyo, kwa kuwa inavunja sheria na kuathiri uhifadhi wa ardhi kwa matumizi ya baadaye.
Katika hatua nyingine, alimtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Angelar Kairuki kulinda maeneo ya hifadhi, badala ya kuacha wananchi wavamie hadi kuweka makazi ya kudumu.
“Mpaka wananchi wanahamia wanajenga, wanajenga shule, kituo cha afya bado mnawaangalia baadaye huko wameshatulia ndiyo aah vijiji wamevamia watoke, hii nayo sio haki,” alisema.
Wanaodai fidia
Katika hotuba yake hiyo, Rais Samia aliwataka wananchi wanaoidai Serikali fidia baada ya kupitiwa na miradi, wasubiri miradi hiyo ikamilike kwanza, kisha utaratibu utafanyika kuhakikisha wanalipwa.
Kinachosababisha uamuzi huo, alisema ni umuhimu wa miradi hiyo kwa wananchi, hivyo Serikali inaona ianze kuitekeleza kwanza kwa manufaa ya wengi ndipo ichakate utaratibu wa fidia.
Mkuu huyo wa nchi aliibuka na hoja hiyo baada ya malalamiko ya wananchi wa Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Morogoro kudai malipo ya fidia baada ya kupitiwa na mradi wa umeme wa Kihansi yaliyoibuliwa na mbunge wa Mvomero, Aboubakar Assenga.
“Kwa hiyo kwa wale wanaotudai fidia zao kwa maendeleo yao wenyewe tunaomba muwe na subira. Tuacheni tumalize miradi ya maendeleo wananchi wengi wafaidike alafu tutaangalia masuala ya fidia,” alisema Rais Samia.
Katika maelezo yake aligusia uwepo wa baadhi ya watu wanaoweka vikwazo vya utekelezwaji wa miradi husika kwa sababu hawajalipwa fidia.
“Tuacheni tufanye miradi, mambo ya fidia mimi nawahakikishieni hatonyimwa mtu haki yake. Tukiwa tayari tutalipa fidia, kwa hiyo niwaombe sana wananchi achieni miradi ijengwe kwa manufaa yenu fidia itakuja kulipwa,” alisema.
Mchengerwa atoa wiki mbili
Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa alitaka uchunguzi wa malalamiko ya wananchi kuchangishwa fedha ufanyike.
Uchunguzi huo, unalenga kile alichoeleza, kuna malalamiko ya wananchi wa Kijiji cha Namawala wilayani Kilombero, kuchangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mganga wa Halmashauri na Mwalimu.
Lakini, Mchengerwa alisema anazo taarifa kuwa fedha hizo zilizochangwa zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mwenyekiti wa Kitongoji.
Kutokana na mazingira hayo, alimwagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Dunstan Kyobya afanye uchunguzi na ndani ya wiki mbili awasilishe ripoti kwake.
Kuhusu changamoto za masuala ya ushuru, alisema jana angekutana na uongozi wa Mkoa huo kwa ajili ya kujadili namna ya kuelewana.
|
Rais Samia Suluhu Hassan amekemea tabia ya uanzishwaji wa vijiji vipya unaofanywa kwa maslahi ya kis
|
Rais Samia Suluhu Hassan amekemea tabia ya uanzishwaji wa vijiji vipya unaofanywa kwa maslahi ya kisiasa, akisema ndiyo inayochochea uvamizi wa maeneo ya hifadhi.
Sambamba na hilo, ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii isisubiri wananchi wavamie na kuyaendeleza maeneo ya hifadhi ndiyo ishtuke, badala yake inapaswa kuyalinda mapema.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo leo, Jumatatu Agosti 5, 2024 alipowahutubia wananchi wa Wilaya ya Ifakara mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.
Tabia za uanzishwaji vijiji vipya, amesema aghalabu hufanyika katika nyakati zinapokaribia chaguzi, wagombea wakilenga kunufaika kisiasa.
“Inapokaribia chaguzi hizi hasa madiwani, mtu akiona yuko vibaya upande mwingine wa eneo lake, anakwenda kusogeza watu kuanzisha kijiji.
“Sasa haya ya kuanzisha vijiji bila kujali tunavianzisha maeneo gani, vijiji vingi vilivyoanzishwa ndani ya maeneo ya hifadhi ni kwa ajili ya wanasiasa wameanzisha, iwe ni madiwani iwe wabunge,” amesema.
Pamoja na kwamba wanasiasa hao ndiyo wanaowapeleka wananchi katika maeneo hayo, amesema hao hao baadaye wanageuka kuwa watetezi wao, akidai wanapoondolewa kwenye hifadhi wanaonewa.
“Alafu ni hao hao wanaokuja kusimama kuwatetea watu walioingia ndani ya hifadhi, maana yake hawa wananchi wetu, wanateseka wanapata shida, lakini ulipowapeleka ulikuwa unajua ni eneo la hifadhi,” amesema.
Msisitizo wa Rais Samia ni kukoma kwa tabia hiyo, kwa kuwa inavunja sheria na kuathiri uhifadhi wa ardhi kwa matumizi ya baadaye.
Katika hatua nyingine, amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Angelar Kairuki kulinda maeneo ya hifadhi, badala ya kuacha wananchi wavamie hadi kuweka makazi ya kudumu.
“Mpaka wananchi wanahamia wanajenga, wanajenga shule, kituo cha afya bado mnawaangalia baadaye huko wameshatulia ndiyo aah vijiji wamevamia watoke, hii nayo sio haki,” amesema.
Wanaodai fidia
Katika hotuba yake hiyo, Rais Samia amewataka wananchi wanaoidai Serikali fidia baada ya kupitiwa na miradi, wasubiri miradi hiyo ikamilike kwanza, kisha utaratibu utafanyika kuhakikisha wanalipwa.
Kinachosababisha uamuzi huo, amesema ni umuhimu wa miradi hiyo kwa wananchi, hivyo Serikali inaona ianze kuitekeleza kwanza kwa manufaa ya wengi ndipo ichakate utaratibu wa fidia.
Mkuu huyo wa nchi ameibuka na hoja hiyo baada ya malalamiko ya wananchi wa Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Morogoro kudai malipo ya fidia baada ya kupitiwa na mradi wa umeme wa Kihansi yaliyoibuliwa na mbunge wa Mvomero, Aboubakar Assenga.
“Kwa hiyo kwa wale wanaotudai fidia zao kwa maendeleo yao wenyewe tunaomba muwe na subira. Tuacheni tumalize miradi ya maendeleo wananchi wengi wafaidike alafu tutaangalia masuala ya fidia,” amesema Rais Samia.
Katika maelezo yake amegusia uwepo wa baadhi ya watu wanaoweka vikwazo vya utekelezwaji wa miradi husika kwa sababu hawajalipwa fidia.
“Tuacheni tufanye miradi, mambo ya fidia mimi nawahakikishieni hatonyimwa mtu haki yake. Tukiwa tayari tutalipa fidia, kwa hiyo niwaombe sana wananchi achieni miradi ijengwe kwa manufaa yenu fidia itakuja kulipwa,” amesema.
Serikali kununua mpunga
Rais Samia amemwagiza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuuelekeza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwenda kununua mpunga mkoani humo.
Hata hivyo, amesema kuanzia sasa badala ya Sh500 iliyokuwa bei ya kilo moja ya mpunga mkoani humo, kwa sasa imeongezeka hadi Sh900.
Hadi anafikia uamuzi wa kupandisha bei hiyo, mkuu huyo wa nchi alishaombwa rifaa ya kulitekeleza hilo na Bashe kwa kile kilichoelezwa bei ya awali iliwakandamiza wakulima.
Wakati anayaeleza hayo, Rais Samia amewataka viongozi wasiwe sehemu ya wanaowakandamiza wakulima katika ununuzi wa mpunga huo, akisema vitendo hivyo vinavunja haki.
“Tumeweka viongozi ngazi mbalimbali tuwasaidia wananchi, mnapoijiingiza kwenye biashara hii na kwenda kunyonya nguvu ya mkulima hufanyi haki, uwe diwani uwe nani kama unafanya biashara hii ya kuongeza kipimo kwenye debe la mkulima hufanyi haki,” amesema.
Sababu ya kauli yake hiyo ni kile alichoeleza, ana taarifa za uwepo wa viongozi ambao nao wanajihusisha na shughuli za biashara hiyo.
Awali, akizungumza katika mkutano huo, Bashe amependekeza kuongezwa kwa bei ya mpunga kutoka Sh500 kwa kilo hadi Sh900.
Hata hivyo, amesema Serikali inafanya mikakati ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji, hasa kwa kuliendelea bonde la Kilombero.
|
Hatari ya bidhaa bandia nchini
Juma Issihaka, Mwananchi
jissihaka@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam.
|
Hatari ya bidhaa bandia nchini
Juma Issihaka, Mwananchi
jissihaka@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Licha ya changamoto za kikodi zinazowakabili wafanyabiashara na zinatafutiwa jawabu, uzalishwaji na uingizwaji wa bidhaa bandia ni tatizo lingine kwa sekta ya biashara nchini.
Duniani asilimia 2.5 hadi 3.5 ya biashara zinazofanyika zinahusisha bidhaa bandia, kama ilivyowahi kuelezwa na Tume ya Taifa ya Ushindani (FCC).
Tanzania ni sehemu ya takwimu hizo na kwa mujibu wa wafanyabiashara kuna ongezeko la ama uingizwaji au uzalishwaji wa bidhaa bandia kwa sasa.
Madai ya wingi wa bidhaa hizo yaliibuliwa na Mjumbe wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Ali Suleiman Amour aliyesema pamoja na athari nyingine, wingi wa bidhaa bandia unaathiri biashara.
Amour aliyezungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa TPSF katika mkutano wa baraza la taifa la biashara, Julai 29, mwaka huu, alisema kuna idadi kubwa ya uingizwaji wa bidhaa bandia nchini.
“Changamoto nyingine ni ongezeko la uingiaji wa bidhaa feki na bandia nchini, jambo ambalo linaathiri biashara zetu,” alisema Amour katika mkutano huo ulioongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika kulifafanua hilo, Mkurugenzi wa TPSF, Raphael Maganga anasema wingi ulioelezwa katika mkutano huo umepimwa kwa ongezeko la malalamiko kutoka kwa wazalishaji wa ndani.
Ingawa ukusanyaji takwimu haujakamilika, anaeleza idadi ya kampuni zinazolalamikia uwepo wa bidhaa bandia nchini ni kubwa, ndiyo sababu jambo hilo lilielezwa.
“Wazalishaji wa ndani wamekuwa wakilalamika na kwa sasa malalamiko yameongezeka. Kabla ya mwezi huu (Agosti) kuisha tunatarajia kutoa takwimu za eneo hilo, tumesema kwa sababu malalamiko ni mengi,” anasema.
Hata hivyo, madai ya wingi wa bidhaa bandia, yaliwahi kuibuliwa pia Julai 31, mwaka huu na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Heineken, Obabiyi Fagade.
"Tupo wafanyabiashara ambao tunafuata taratibu zote za nchi katika uingizaji na usambazaji wa bidhaa, na tunalipa kodi stahiki kwa Serikali, bahati mbaya wapo watu wa ndani na nje ya nchi ambao wanafanya biashara haramu ya kuingiza bidhaa feki ya vinywaji tunavyoingiza sisi, hii inasababisha taifa kupoteza mapato lakini na sisi kuathiri biashara zetu," alisema.
Malalamiko kama hayo, yaliibuliwa pia na Mkurugenzi wa kampuni ya ndani ya Mabibo Wine, Jerome Rugemalira aliyesema waagizaji wa bidhaa feki vikiwemo vinywaji wanarudisha jitihada za Serikali za kukusanya kodi.
"Ni kweli zipo bidhaa feki za vinywaji, tunaamini Serikali ina mkono mrefu na inajua nani ni muagizaji rasmi wa bidhaa gani, wafanyabiashara wasio waaminifu wanapaswa kubanwa kutoingiza bidhaa feki," anasema.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Hussein Sufian anasema malalamiko yamekuwepo na waliwahi kufanya utafiti katika eneo hilo.
Kilichosababisha utafiti huo ni ukubwa wa tatizo na athari zake kwa wazalishaji wa ndani.
“Sisi hatukuishia kulalamikia tuliwahi kufanya utafiti na tukaonyesha ukubwa wa tatizo. Hii ililenga kuonyesha hali ilivyokuwa na athari wanazopata wazalishaji,” anaeleza.
Kauli ya mdhibiti
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Ushindani (FCC), William Erio anasema ingawa wamekuwa wakiziteketeza kila zinapobainika bidhaa hizo, kiuhalisia zinazoingia si nyingi kama ilivyoelezwa.
Kwa mujibu wa Erio, pengine wingi unaoripotiwa unasababishwa na uelewa duni wa wadau juu ya tafsiri ya kisheria ya bidhaa bandia na hivyo wanachanganya na bidhaa hafifu.
Anaitafsiri bidhaa bandia kisheria, akisema ni ile ambayo ama mtu au kampuni imeamua kuiga nembo ya bidhaa ya kampuni nyingine na kuiingiza sokoni ili kuvuta soko la bidhaa husika.
“Leo hii ikitokea kampuni fulani inazalisha bidhaa zake zenye soko kubwa, kisha ikatokea nyingine ili kupata soko hilo, inaamua kutengeneza bidhaa inayofanana na ile ile na inaiga na nembo ya kampuni ya awali,” anasema.
Hata hivyo, anasema anayeweza kuibua madai ya uwepo wa bidhaa bandia ni yule mzalishaji halisi wa bidhaa na atakapokwenda kulalamika FCC atatakiwa kuthibitisha ubandia anaoueleza.
“Hata sisi FCC ni vigumu kusema kuwa bidhaa hii ni bandia, anayeweza kueleza hilo au kugundua ni yule ambaye alikuwa na bidhaa yake na amebaini kuna mzalishaji mwingine anayetumia nembo yake kuizalisha bidhaa ile ile,” anasisitiza.
Erio anaeleza wapo wengi wanaoitafsiri bidhaa hafifu kama bandia, akifafanua ni ile ambayo ama imeingia nchini ilhali haijakidhi vigezo au imeingizwa bila nembo wala utambulisho wa inapotokea.
“Watu wanachanganya kwenye eneo hili, kuna bidhaa zisizo na utambulisho ambazo kimsingi ni hafifu na FCC sio wahusika wa hizo, mamlaka nyingine ndiyo inayoshughulika nazo,” anasema.
Alipoulizwa wanavyodhibiti bidhaa bandia, Mkurugenzi huyo anasema kila zinapobainika FCC imekuwa ikichukua hatua na hasa ni kuziteketeza.
Hata hivyo, Erio anaweka wazi mara nyingi bidhaa bandia huzalishwa kutoka katika zile zenye soko kubwa nchini.
Athari za kiuchumi
Kukithiri kwa bidhaa bandia kunamwathiri zaidi mzalishaji wa bidhaa halali, kama inavyoelezwa na Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Jehovaness Aikaeli.
Mwanazuoni huyo anasema bidhaa bandia huja na bei rahisi isiyolingana na halali na hiyo itapata wateja zaidi.
Mzalishaji wa bidhaa halali, anasema hawezi kuuza kwa bei rahisi kwa sababu ana gharama kubwa za uzalishaji unaozingatia viwango.
“Uzalishaji wa bidhaa bandia unawatoa sokoni wale wanaozalisha bidhaa halisi na katika mazingira hayo, watapata hasara, Serikali itakosa kodi na pengine biashara zitakufa kabisa,” anaeleza.
Athari nyingine kwa mujibu wa Profesa Aikaeli, ni upande wa mlaji ambaye atakachokipata hakitakuwa na ubora kulingana na mahitaji yake.
“Kama ni dawa atakunywa atapona leo lakini kesho ugonjwa utarudi. Kweli pengine amenunua kwa bei rahisi lakini ndani ya mwezi atalazimika kununua mara nyingi zaidi na wakati mwingine hata zaidi ya bei ambayo angenunua ile halisi,” anasema.
Ili kudhibiti, anasema hakuna uchawi zaidi ya mamlaka zilizopewa jukumu hilo kisheria kuhakikisha zinalitekeleza inavyopaswa.
Mwanazuoni huyo anafafanua pasi na kuwajibika wazalishaji wa bidhaa bandia watatumia mwanya huo kujitengenezea faida, huku Serikali ikiendelea kupata hasara.
|
Vitendo vya matumizi mabaya ya fedha za umma vimeendelea kuwa kitendawili kisichoteguka nchini, baad
|
Vitendo vya matumizi mabaya ya fedha za umma vimeendelea kuwa kitendawili kisichoteguka nchini, baada ya Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kubaini kasoro katika matumizi ya mabilioni kwenye mikoa mitano.
Mikoa iliyoguswa na ripoti hiyo ya utendaji kazi wa Takukuru kwa kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu ni Geita, Shinyanga, Katavi, Singida na Mtwara, ambayo katika miradi tofauti imebainika kuuingia mtego huo.
Hali hiyo inaendelea licha ya viongozi mbalimbali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan kukemea hadharani huku wakielekeza usimamizi thabiti wa fedha za umma.
“Fedha nyingi tunazileta fedha zinaliwa, zinaharibiwa mnaangalia tu, hakuna uchunguzi hakuna kinachoendelea hadi viongozi waje waseme hapa kafanye uchunguzi, hapa msimamishe, hapa fanya hivi hatuendi hivyo ndugu zangu.
“Niwaombe kwamba miradi inayoletwa huku ni ya kwenu, mimi na mawaziri wangu tunatoka maeneo tofauti na sisi tunapiga kelele huko kwetu kama mambo hayaendi kwa hiyo inayokuja huku ni ya kwenu simamieni,” alisema Rais Samia Februari 6, 2022 wakati wa kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mkoani Mara.
Hata hivyo, ilichokibaini Takukuru kwenye mikoa hiyo ni sawia na kile ambacho mara kadhaa, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti zake.
Katika ripoti ya CAG ya mwaka 2022/23, ilibainika makusanyo ya Sh6.18 bilioni yaliyokusanywa kupitia mashine za POS hayakuwasilishwa katika akaunti za benki za mamlaka 96 za Serikali za Mitaa.
Pia, kwa mujibu wa CAG, sehemu za huduma za afya na vifaatiba vilivyonunuliwa vyenye thamani ya Sh4.94 bilioni havitumiki jambo linaloisababishia Serikali hasara.
Ripoti ya Takukuru
Katika Mkoa wa Shinyanga, Takukuru ilimfikisha mahakamani Meneja wa Chama cha Ushirika Kahama (Kacu), Abduly Mauga kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Kadhalika, imewaburuza mahakamani vongozi nane wa vyama vya msingi Kangeme na Mshindi mkoani humo kwa tuhuma za rushwa.
Kati ya kesi tano zilizofunguliwa mahakamani nne zinaendelea na moja Jamhuri imeshinda huku wahusika wakiamriwa kurejesha Sh24 milioni waliyoipata kwa rushwa.
Hayo yalibainika baada ya uchunguzi uliofanywa na Takukuru katika chama hicho, kinachojishughulisha na kilimo cha Tumbaku, Pamba na mazao mchanganyiko.
Ilibainika vyama vya msingi 13 vinavyosimamiwa na Kacu vinadaiwa madeni na wanachama wake, huku Mauga akitajwa kuhusika.
“Tulibaini kuna viongozi wanakopa fedha benki na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi, kugushi ankara za malipo (Invoce), kutoa fedha kwenye akaunti za chama na kuzigawana, na kufanyika kwa malipo yasiyo halali kwa madai ya kulipa wafanyabiashara walioleta ya pembejeo kwenye AMCOS,” alisema Kessy.
Kwa mujibu wa Kessy, hadi Julai 31, mwaka huu wahusika katika kesi ambayo Jamhuri ilishinda walisharejesha Sh12 milioni.
Vifaa vya Sh1.7 bilioni
Mkoani Geita nako, Takukuru mkoani humo imeanza uchunguzi wa upotevu wa vifaa vyenye thamani ya Sh1.7 bilioni katika mradi wa awamu ya pili wa ujenzi wa Hospitali ya Katoro.
Kwa mujibu wa Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita Alex Mpemba, walibaini vifaa hivyo vilinunuliwa lakini havijawahi kutumika na havipo kwenye eneo la mradi.
Wakati huo, taasisi hiyo inachunguza ujenzi wa nyumba ya watumishi katika Shule ya Msingi Nyamiboga inayojengwa kwa Sh27 milioni ambayo haijawekewa mashimo ya choo na mfumo wake.
Hayo yamefanyika, wakati vifaa vipo eneo la mradi na hadi sasa shughuli zimekwama kutokana na upotevu wa Sh7 milioni.
Kuhusu ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, Mpemba amesema kati ya miradi 25 yenye thamani ya Sh10.2 bilioni iliyokaguliwa, miradi mitano ilikutwa na mapungufu.
Mtwara
Takukuru mkoani Mtwara imebaini upungufu katika ujenzi wa msingi wa vyumba vinne vya madarasa vya Shule ya Msingi Litehu wilayani Tandahimba. Ujenzi wa madarasa hayo unagharimu Sh80 milioni.
Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mtwara, Elisante Mashauri amesema ilibainika matofali yaliyotumiwa yalikuwa chini ya kiwango na hivyo kupindisha msingi.
Mbali na msingi huo, Mashauri amesema taasisi hiyo imefuatilia utekelezaji wa miradi 18 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh4 bilioni katika sekta ya elimu miradi tisa, Afya (5), Ujenzi (2), Maliasili (1) na Kilimo (1).
“Miradi 14 sawa na asilimia 94.44 yenye thamani ya Sh2 bilioni imebainika kuwa na mapungufu madogo madogo,” amesema.
Katika hatua nyingine, Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi, Stewart Mwakakyondo amesema Sh150 kati ya Sh300 milioni zilizokusudiwa kulipwa kwa mzabuni wa utengenezaji samani za Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlelwa kinyume na mikataba zimeokolewa.
Kwa mujibu wa Mwakakyondo, halmashauri hiyo ilitaka kumlipa mzabuni asilimia 50 kinyume na utaratibu jambo ambalo lingesababisha upotevu wa fedha hiyo.
Aidha, Mwakakyondo amesema Takukuru baada ya kushinda kesi ya uhujumu uchumi 4002/2024, dhidi ya mzabuni wa ukusanyaji wa ushuru kwa kutumia mashine za POS wilayani Mpimbwe mkoani Katavi, Mahakama ilimuamuru kurejesha Sh20.3 milioni zilizotaka kupigwa na mkusanya mapato huyo.
Wakati huo, Takukuru mkoani humo imewalazimisha wasimamizi wa mradi wa matengenezo ya viti na meza 30 katika Sekondari Kamalampaka wilayani Mlele mkoani humo, kurejesha Sh1.9 milioni baada ya kutengeneza samani hizo chini ya kiwango.
Singida
Mkuu wa Takukuru mkoani Singida, Sipha Mwanjala ameeleza kufikishwa mahakamani kwa baadhi ya watumishi mkoani humo kutokana na matumizi mabaya ya madaraka na kughushi nyaraka.
Kati ya watumishi hao kwa mujibu wa Takukuru, yumo Ofisa Elimu Mkoa na Ofisa Michezo na Utamaduni Mkoa, kadhalika maofisa wengine wa kada ya elimu wa Manispaa ya Singida.
Mwanjala amesema katika kipindi cha miezi mitatu wameokoa zaidi ya Sh136 milioni fedha zilizotokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Katika fedha hizo, amesema zaidi ya Sh18.8 milioni zimeokolewa katika Halmashauri ya Mkalama na zaidi ya Sh1.9 milioni zikiokolewa katika Halmashauri ya Itigi huku Sh1.1 milioni katika Halmashauri ya Iramba.
Amemesema Takukuru imepokea malalamiko 55 huku 20 yakihusu vitendo vya rushwa na uchunguzi unaendelea.
"Kesi tatu zilifunguliwa mahakamani, kesi tano ziliamuliwa kati ya hizo kesi nne jamhuri ilishinda ikiwemo kesi iliotokana na maagizo ya waziri mkuu aliyoyatoa alipofanya ziara katika wilaya ya Manyoni na kesi moja ilishindwa" amesema.
Mtazamo wa wananchi
Kutokana na taarifa hizo, Mkazi wa Katoro mkoani Geita, Bakari Masanja amependekeza uchunguzi uendelee ili mengi zaidi yabainike.
“Wananchi waliaminishwa sana kwenye ujenzi wa hospitali hii (Ya Katoro), lakini kutokamilika kunawafanya wakose imani na viongozi wao. Uchunguzi huu uende mbele uje na majibu ya lini miradi itakamilika,” amesema Masanja.
Mwanazuoni wa Uchumi, Profesa Samuel Wangwe anasema vitendo hivyo vinasababishwa na kukosekana uwajibikaji kwa viongozi wengi wa ngazi za halmashauri.
Kukosa uwajibikaji huko, amesema kunawafanya wengi washindwe kusimamia bajeti kama ilivyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.
“Kunapaswa kuwe na usimamizi mzuri wa bajeti na kuwe na utaratibu wa kuhuisha matarajio ya matumizi hii itawezesha kuepuka upigaji,” amesema.
Kadhalika, amependekeza kwenye vigezo vya upimaji ufanisi matumizi ya fedha hizo za umma kiwe kimojawapo na kisimamiwe haswa.
|
Licha ya Serikali kulifungia kanisa la Christian Life Church (C.L.C), lililoongozwa na Dominique Dib
|
Licha ya Serikali kulifungia kanisa la Christian Life Church (C.L.C), lililoongozwa na Dominique Dibwe maarufu ‘Kiboko ya Wachawi’ imebainika kiongozi huyo wa dini anaendelea kutoa huduma hiyo kama kawaida, huku akiomba mamilioni ya fedha kwa waumini wake.
Tofauti na awali, Dibwe ambaye ni raia wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kwa sasa anatoa huduma ya maombezi na kile anachokiita uponyaji kwa njia ya simu, akiomba kulipwa mamilioni hayo kwa waumini wenye matatizo.
Kwa sababu hiyo hiyo ya kutoza fedha kuanzia Sh500,000 kwa waumini wake ili awape huduma ya uponyaji wa kiroho, ndiyo iliyoifanya Serikali ilifutie usajili wa kanisa lake, Julai 25, mwaka huu.
Katika barua ya kufutwa usajili wa kanisa hilo iliyotolewa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa ilieleza vitendo hivyo vinakiuka matakwa ya kifungu cha 17 cha Sheria ya Jumuiya, Sura ya 337 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali Namba 3 ya Mwaka 2019.
Mbali na kutoza fedha, sababu nyingine za kufutwa usajili wa kanisa hilo zilizotajwa katika barua hiyo ni kutoa mafundisho yenye kuleta taharuki katika jamii na mahubiri ambayo ni kinyume cha maadili, mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania.
Nyingine ni kutoa mahubiri yanayodhalilisha watu madhabahuni, kutoa mahubiri chonganishi na kuhamasisha waumini wa kanisa lake kuua watu kwa dhana au tuhuma za uchawi au ushirikina.
Hayupo nchini
Hata hivyo, gazeti hili limethibitisha kuwa Dibwe ameshaondoka nchini kurudi kwao Jamhuri ya Demokrasi ya Congo tangu Julai 29, mwaka huu baada ya kanisa lake kufutiwa usajili.
Akizungumza na Mwananchi kwa simu kuhusu alipo kiboko ya wachawi, Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania, Paul Mselle amesema uwepo wa kiongozi huyo nchini umekoma baada ya kufutwa usajili wa kanisa lake.
“Kibali alichokuwa nacho kilikuwa kinaisha Septemba mwaka huu (bila kutaja tarehe) kilikuwa kwa ajili ya uendeshaji wa kanisa, sasa Serikali ilipofuta kibali cha kanisa lake alitakiwa kuondoka nchini kwani shughuli iliyomfanya awepo nchini ilikuwa imeondolewa,” amesema Mselle.
Kufuatia kufungiwa kwa kiongozi huyo wa dini, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda amewataka viongozi wengine wa dini kufuata utaratibu kuondoa migongano isiyo ya lazima.
“Watu wafuate utaratibu kudoa migongano na mivutano isiyo ya lazima, kanisa hilo si la kwanza kufungiwa na mamlaka husika na yalipofungiwa hali ilikuwa shwari, mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote yaliyoletwa kwangu,”amesema Mapunda.
Anavyoendelea kuomba mamilioni
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kiongozi huyo wa kiroho huko huko alipo anaendelea kutoa huduma za uponyaji, akiomba kulipwa hadi Sh10 milioni.
Mwandishi wa habari hii amepiga simu kwa kiongozi huyo akijifanya mgonjwa wa kupindukia na kuomba msaada wa matibabu ya kiroho, lakini aliishia kuombwa Sh10 milioni ili ugonjwa wake upone.
Kinachoshangaza zaidi, Dibwe ameomba kiasi hicho cha fedha kipatikane ndani ya saa 24, akimtishia mwandishi (aliyejifanya mgonjwa) asipoipata ndani ya muda huo angepoteza uhai.
“Nakuona ukienda kufa ndani ya saa 24 maana kuna vitu vinakutembea kutoka kwenye moyo hadi tumboni na namuona mwanamke mmoja ameenda kwa mganga kutoa uhai wako na usipopata huduma hiyo haraka utakufa,una Sh10 milioni hapo ili upone,” alisema Dibwe kwa njia ya simu.
Dakika chache baadaye mwandishi huyo alimpigia simu tena Kiboko ya Wachawi kumweleza amepata Sh300,000 badala ya Sh10 milioni, lakini kiongozi huyo aligoma akisema kazi ya kuutibu ugonjwa huo ni ngumu na kiasi hicho cha fedha hakitoshi.
Ukiachana na huduma za kiroho, Mwananchi linazo taarifa za uhakika za kuendelea kwa ibada katika kanisa hilo, ingawa zinafanywa kwa siri na zinahusisha waumini wanaojulikana.
Sambamba na ibada, waumini hao wanakutana hapo kuelezana kinachoendelea juu ya mchakato wa kurejesha huduma kama ilivyokuwa awali.
“Huduma zipo, wachungaji wanaendelea kuhudumia lakini tatizo hujui ni nani unayemuhudumia, unaweza kuona unamsaidia kumbe unamuingiza matatizoni,” amesema Mmoja wa viongozi alipokuwa akizungumza na Mwananchi.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, tayari wameshakata rufaa kwa ajili ya kurejesha huduma za kanisa lao lakini majibu yanatarajiwa kupatikana ndani ya miezi mitatu yaani Oktoba mwaka huu.
Hali ilivyo kanisani
Ingawa Serikali imefuta usajili wa kanisa hilo, bado kuna matumaini ya kuendelea kuwepo kutoka kwa miongoni mwa waumini wake, ambao hadi sasa wamekwama Buza kwa Lulenge lilipo kanisa hilo.
Hata hivyo, matumaini hayo hayabebwi na imani walizonazo waumini, bali wengine wamelazimika kusalia hapo kwa kukosa nauli za kurejea kwao.
Mkazi wa Chamwino jijini Dodoma, Rose Stephen ni miongoni mwa waumini hao, anasema anashinda ibadani kusubiri Kiboko ya Wachawi arejee.
“Tunaamini kanisa litafunguliwa, hii ni changamoto ya muda tu, tumeshaambiwa ibada itakuwepo, kanisa lilifungwa wakati tupo ndani na hapa sasa mimi nalala chumba cha kukodi wapo wanaolipa Sh2,000 na wengine Sh3,000,” amesema.
Rose amesema wanalala mchana kanisani hapo kusubiri hatma yao huku waumini wengine kutoka mataifa mengine ambao wao hulala mazabauni nyakati za usiku na mchana hushinda kanisani wakiomba.
Muumini mmoja kutoka Congo ambaye hushinda kanisani bila kutaja jina lake amesema hawezi kuondoka kwa sababu tayari amelipa fedha kuonana na nabii na anasubiri hatma yake na hana nauli ya kurudi kwao.
“Siwezi kuondoka nitasubiri kwa sababu hela niliikopa kuja kumaliza tatizo langu,” amesema.
Hata hivyo baadhi ya mashuhuda waliliambia Mwananchi kuwa, wafuasi wa mchungaji huyo hufanya ibada kila asubuhi kuomba kanisa lifunguliwe huku wakiwalaani wote wanaowaita wapinzani waliofanikisha huduma hiyo kufungwa.
Wapo waumini wanaohusisha kufungwa kwa kanisa hilo na kile wanachokiita fitina za kidini, kama anavyoeleza Mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro, Samwel Mmbando.
Mmbando ni mmoja wa waumini wanaolipa Sh2,000 kulala karibu na lilipo kanisa hilo, bado anaamini ataonana na Kiboko ya Wachawi licha ya kukosa Sh500,000.
Alihamasishwa na matangazo kuwa, mahubiri na maombezi katika kanisa hilo hufanyika bure lakini alipofika kanisani alitakiwa kulipa fedha ndiyo aonane na nabii huyo.
Mmoja wa Mamalishe kanisani hapo, Doris James (si jina halisi) anasema wapo watenda kazi wa nabii huyo wanaendelea na ibada lakini kwa siri na mke wa Kiboko ya Wachawi ndiye anayeratibu yote.
“Mke wa kiboko alikuja kuzungumza na watenda kazi akaondoka, tangu asubuhi hadi saa 10 jioni watenda hao walikuwa kwenye ibada lakini hawaruhusu watu wengine kuingia kwa sababu hawaamini, kama wanakufahamu watakuuzia vitendea kazi ikiwepo mafuta, maji, fulana na vitu vingine ambavyo wanasema nabii alikwisha kuombea,” anasema.
Uchungaji wa Dibwe
Majirani zake akiwemo Mwalongo wanaeleza walimfahamu Dibwe akiwa anaishi Buza kabla ya kuhamia Kitonga na wakati huo hakuwa mchungaji, bali alikuwa muumini wa kawaida.
Wakati huo kwa mujibu wa Mwalongo, Dibwe alikuwa anajishughulisha na shughuli mbalimbali na hakuwa na nyumba yake.
“Mchungaji huyo alikuwa mtumishi wa kawaida kwenye kanisa hilo ambalo pia lilikuwa chini ya mchungaji mgeni kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, baada ya muda walimpa cheo wakati huo mchungaji wa awali aliondoka kanisani hapo,” anasema.
Baada ya cheo hicho kanisani, anasema baadaye Dibwe alitafuta kiwanja Kitonga na kujenga nyumba yake ndogo ya vyumba viwili vya kulala na sebule na alihamia.
Baadaye, anasema Dibwe alisafiri na aliporudi walishangaa kuona kanisa linajaza hadi barabarani na ndipo alipoomba eneo zaidi kwa ajili ya upanuzi wa kanisa.
Steven John (Si jina halisi) ni jirani yake wa Kitonga, anasema hakumfahamu kama mchungaji bali jirani na walimwita kwa jina la Baba Ephrahim.
Kwa mujibu wa John, Dibwe hakuwa anajichanganya na watu, ni mkewe ndiye aliyekuwa anafanya hivyo na alikuwa sehemu ya vikundi vya wanawake.
Agosti mwaka 2023, anasema Kiboko ya Wachawi alihitaji Sh1 milioni kwa ajili ya kusajili kanisa lake na aliomba akopeshwe na kuahidi angeilipa hata kwa riba kubwa kiasi gani.
Ilikuwa ngumu kupata kiasi hicho, kwa kile anachoeleza John kuwa, uhalisia wa maisha yao ya wakati huo uliwapa ugumu wengi kuamini kama angeweza kurejesha.
Lakini mwanzoni mwa mwaka huu, anasema hali ilibadilika kwani Dibwe alimwagiza mkewe akanunue kiwanja kwa ajili ya ujenzi na walikinunua kwa Sh7 milioni.
Hakuna aliyejua Dibwe anafanya kazi gani, lakini anasema walishangaa kuona nyumba inakamilika ndani ya miezi miwili na baadaye magari ya kifahari yalianza kununuliwa naye.
“Huku asilimia kubwa tunafahamiana pia na kazi tunazofanya tuliona wenzetu wamebadilika ghafla na hatukujua ni kazi gani wanafanya maana tunamuona mkewe nyumbani lakini wamekuwa na mafanikio ya haraka mno,” anasema.
Baada ya kugundua watu hawafahamu, mmoja wa watu anashudia kuwa aliwahi kumsimamishwa na nabii huyo barabarani na kumueleza kuwa na matatizo na chanzo cha hayo ni kaka zake watatu na ndiyo wanaomfanya akose hata gari.
Kilichoshangaza zaidi, ni kijana mmoja aliyesema aliwahi kusimamishwa na Dibwe akitabiriwa kurogwa na kaka zake ndiyo maana ana maisha magumu.
Katika utabiri huo, anasema aliambiwa asingepaswa kutembea kwa mguu, alitakiwa kuwa na gari.
“Hakujua kama nina gari nimeliacha nyumbani hivyo aliponisimamisha aliniambia mimi si wa kutembea kwa miguu na kupanda daladala kinachotokea ni kaka zangu hawapendi maendeleo yangu hivyo wananiroga,” anasema.
John anasema kilichomtafakarisha kijana huyo aliyetabiriwa na Dibwe ni kwamba hakuwa na kaka bali ni dada pekee, hivyo alishangaa maelezo ya Kiboko ya Wachawi yametoka wapi.
Amesema maelezo hayo yalimtafakarisha kwa kuwa hana kaka katika familia yake zaidi ya dada zake, hivyo alimtaka afike kwenye kanisa lake lililopo Buza kwa ajili ya kufanyiwa maombi na kufanikiwa ili awe tajiri kama wengine.
Kuanzisha kanisa
Hata hivyo, kuna mkanganyiko wa kanisa lililofutiwa usajili na lile alilokuwa akihudumu Dibwe, ikielezwa kiongozi huyo hakuwa katika kanisa la CLC.
Hilo lilielezwa na Muasisi na Askofu wa kanisa hilo lenye makao makuu yake Kawe jijini Dar es Salaam, Peter Lukindo kupitia mtandao wa Istagramu, akifafanua Dibwe alishaondoka CLC tangu Januari 31, mwaka huu.
Anaeleza Dibwe alikuwa mtumishi wa kawaida alipokuwa CLC lakini baadaye aliomba kuondoka akaanzishe kanisa lake la Kitume la Catholic Apostolical Church (C.A.C).
“Tulishauriwa na ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Temeke turudishe kibali chake cha makazi nasi tulifanya hivyo kwa barua rasmi iliyopokelewa na uhamiaji makao makuu na kugongewa muhuri wa kupokelewa Aprili 3, 2024,” anasema.
Anasema Kibali cha Dimbwe kilikuwa kinaisha muda wake Julai 8, 2024 aliambatanisha na barua ambayo Kiboko ya wachawi aliituma Januari 24, 2024 ya kujitoa kwenye kanisa hilo na kuanzisha kanisa lake.
Barua hiyo ilisema hivi “Ninatoa shukurani kwako kwa kunipokea na kufanyakazi kazi ya Mungu nikiwa chini ya uongozi wako kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.Kwa muda wote huu tumefanya kazi ya Mungu kwa ushirikiano mkubwa na sasa ninaomba niwe huru ili niweze kuanzisha kanisa langu litakaloitwa Kanisa la Kitume.
Anaongeza “Ombi hili ninalileta kwako kwa kuwa nimekuwa na maono haya ya kwa muda mrefu na ninatumaini kuwa tutaendelea kushirikiana katika huduma kwa kuwa wote tuna imani moja.”
Kwa taarifa iliyopata Mwananchi baada ya kurudishwa kwa kibali chake Kiboko ya Wachawi aliomba kibali upya na kupewa kwa miezi mitatu ambapo alilipia dola 6,000 za Marekani (zaidi ya Sh15 milioni).
Baada ya kufungiwa
Mmoja wa majirani zake aliyeomba hifadhi ya jina lake, anasema barua ya kufutwa usajili wa kanisa lake aliipata siku alipokuwa katika sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa mwanawe Ephrahim.
Kinachofanya jirani huyo ahisi hivyo ni kile alichoeleza, tangu ilipomalizika sherehe hiyo hakuwahi kumwona tena Dibwe nyumbani hapo.
Kilichoonekana siku moja baada ya kufutiwa usajili, alikuwa akiingia na kutoka nyumbani hapo na magari ya kifahari huku akisindikizwa na walinzi wake, akiwemo Mwarabu Fighter.
Viti na vifaa vingine, anasema vimeshuhudiwa vikishushwa nyumbani hapo na kwamba mkewe amekuwa akitangaza kuviuza maeneo mbalimbali.
Dalali wa kiwanja
Mke wa dalali aliyemuuzia kiwanja alikojenga nyumba ya ghorofa, (jina lake limehifadhiwa) anasema walidhani Kiboko ya Wachawi ni Mtanzania na aliuziwa kama mtanzania.
“Wakati tunamuuzia alisema yeye ni raia wa hapa na hata uuzaji wake ulisimamiwa na Serikali ya Mtaa wa huku pamoja na mwenye kiwanja ambaye tulimuuzia awali kwani alikuwa anahitaji mteja,” anasema.
|
Itakugharimu wastani wa Sh3.81 milioni kwa mwaka, kumiliki jenereta linalotumia mafuta kwa ajili ya
|
Itakugharimu wastani wa Sh3.81 milioni kwa mwaka, kumiliki jenereta linalotumia mafuta kwa ajili ya umwagiliaji katika shughuli za kilimo na litadumu kwa miaka mitatu pekee.
Wakati huo huo, mkulima atagharimika Sh10 milioni kumiliki mitambo ya nishati ya umeme jua kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, ambao kiuhalisia unadumu kwa miaka 20.
Hiyo ni kwa mujibu wa tathmini ya Chama cha Nishati Jadidifu Tanzania (Tarea), kinachofafanua licha ya gharama kubwa za mwanzo katika usimikaji wa mtambo wa nishati ya umeme jua katika kilimo cha umwagiliaji, kuna unafuu mkubwa baadaye.
Unafuu huo kwa mujibu wa Tarea, unatokana na muda mrefu ambao mtambo wa nishati ya umeme jua unadumu, kadhalika hauhusishi gharama yoyote ya uendeshaji, wakati jenereta linahitaji mafuta kila siku.
Chama hicho kimekwenda mbali zaidi na kueleza, jenereta linalotumia mafuta katika shughuli za kilimo cha umwagiliaji linazalisha kilo 487 za hewa ya ukaa, ambayo ni hatari kwa mazingira.
Ushuhuda wa wakulima
Mbali na tathmini ya Tarea, mkulima anayetumia nishati ya umeme jua mkoani Dodoma, Anthony Machai anasisitiza unafuu wa nishati hiyo katika kilimo, ukilinganisha na mtambo unaotumia mafuta.
Kwa mujibu wa Machai, katika shamba la ekari tatu kwa jenereta utalazimika kununua mafuta ya Sh50,000 kila siku kuwezesha kuvuta maji kutoka kisimani hadi kwenye mazao kwa ajili ya umwagiliaji.
Gharama hizo, anasema kwa mwezi ni sawa na kutumia Sh1.5 milioni, kiasi ambacho ni maumivu kwa mkulima.
Lakini unapotumia mitambo ya umeme jua, anasema gharama ni kuifunga tu, baada ya hapo mkulima hatagharimika na chochote.
“Pamoja na mazingira hayo, ni wakulima wachache ndiyo tunaotumia nishati ya umeme jua kwenye kilimo, wengi wanaona afadhali watumie majenereta na mafuta,” anaeleza.
Kwanini wengi watumie majenereta?
Kinachochochea wakulima wengi wachague majenereta licha ya faida ndogo wanayopata ni kile kilichoelezwa na Machai kuwa, hawana uwezo wa kufunga mitambo ya umeme jua.
Machai anasema mtambo wa umeme jua unaomudu huduma za shamba la ekari nne hadi tano, unagharimu Sh9 hadi 15 milioni.
Anasema ni wakulima wachache wenye uwezo wa kuwa na viwango hicho cha fedha kwa mara moja, ndiyo maana wanachagua kuingia gharama kidogokidogo kwenye mafuta.
“Ni kweli ukifunga mtambo kwa gharama hizo hautahitajika kutoa gharama nyingine yoyote, lakini ni wakulima wachache wenye uwezo wa kupata kiasi hicho cha fedha kwa mkupuo wafunge nishati hiyo,” anasema.
Kinachopaswa kufanywa, anasema ni Serikali iangalie utaratibu wa kuwawezesha wakulima kukopeshwa mitambo hiyo ili wawe wanalipa kidogo kidogo hadi watakapomaliza
Kwa sababu anasema gharama za mitambo huo, zinarudishwa kwa awamu moja ya kilimo.
“Mimi mwaka huu nimelima ekari moja ya nyanya kwa kutumia solar nimeingiza Sh12 milioni, kwa hiyo ni msimu mmoja unakuwezesha kurudisha gharama za mtambo lakini si kila mkulima ana uwezo wa kupata fedha ya kununua mtambo kwa mara moja, wakopeshwe,” anaeleza.
Gharama kubwa za mtambo anasema zinasababishwa na kodi zilizopo katika uingizaji wa bidhaa hizo nchini.
Anapendekeza kuwepo msamaha wa kikodi katika uingizaji wa bidhaa za sola nchini ili kuwarahisishia wakulima na kuendana na mpango wa Serikali wa matumizi ya nishati safi.
Wasambazaji sola
Akizungumza kuhusu gharama za uingizaji wa sola nchini, Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya uingizaji wa mitambo ya nishati ya umeme jua ya Davis and Shirtliff, Octavian Ndago anasema imepungua maradufu.
Kupunguza huko kutatokana na kile alichoeleza, Serikali imeondoa kodi kwenye vifaa vya nishati ya umeme jua tangu miaka miwili iliyopita.
Kwa mujibu wa Octavian, kwa sasa vifaa vya nishati hiyo vimewekewa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
Hali hiyo, anasema imesababisha bei ya WAT moja ya nishati hiyo ipungue kutoka zaidi ya Sh2,000 ya mwaka juzi hadi Sh500 hadi Sh800 ya sasa.
“Serikali inafanya juhudi za kutoa msamaha ya kikodi. Hakuna VAT kwenye solar isipokuwa gharama za ufungaji mitambo hasa ya kilimo zinahusisha mambo mengi,” anasema.
Ingawa kuna msamaha huo, Octavia anasema bado ufungaji wa mitambo ya nishati hiyo kwa mkulima itakuwa na gharama kubwa.
Ukubwa wa gharama hizo, anaeleza hausababishwi na bei ya sola, bali vifaa vingine vinavyohitajika kwa ajili ya kukamilisha mtambo husika.
“Kwa mfano mteja anapotaka umfungie mtambo kwa ajili ya umwagiliaji shambani pale hautumii vifaa vya sola peke yake.
“Kuna mitambo mingine ambayo gharama zake ni kubwa na hicho ndicho kinachoongeza gharama za mitambo hiyo ya kilimo,” anasema.
Anapendekeza Serikali isiishie kupunguza kodi kwenye bidhaa za sola pekee, bali na mitambo yote inayohusika kwenye ufungaji wa nishati ya umeme jua kwa mkulima.
Wanazuoni
Ushauri kama wa Octavian unatolewa pia na Mwanzuoni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Dk Darius Mukiza anayesema gharama za mwanzo za kusimika mitambo ya umeme jua shambani zinapaswa kupungua.
Ili zipungue, anapendekeza kuwekwe msamaha wa kodi katika bidhaa za sola, kadhalika vifaa vingine vinavyoambatana katika usimikaji wa mitambo hiyo.
Mwanzuoni huyo anaweka wazi juu ya uwepo wa baadhi ya wakulima katika mikoa ya Dodoma na Morogoro wanaotumia nishati ya umeme jua, lakini si wengi kwa sababu wengine hawamudu.
“Serikali ikilipa kipaumbele hili suala la nishati ya umeme jua katika kilimo itasaidia mambo mengi. Kwa sababu ni nafuu kwa mkulima pia ina uhakika wa uzalishaji mwaka mzima,” anaeleza.
Kitengo cha kuzalisha mwaka mzima, Dk Mukiza anasema kitawezesha nchi kuwa na usalama na ustahimilivu wa chakula.
Kwa mtazamo wa Mhadhiri wa Nishati Jadidifu na Uhandisi Kilimo wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Dk Yusto Yustas kuna haja ya kuongeza uwezo kwa wataalamu ili watengeneze teknolojia za nishati hiyo ili kupunguza gharama za upatikanaji wake.
Anasema ni muhimu pia kuimarisha uwekezaji wa sekta binafsi katika kuwezesha kwenye upatikanaji wa teknolojia za nishati za jua kwa gharama nafuu.
“Bahati nzuri haya yote yanawezekana kwa sababu sera zinazohusu Kilimo, Nishati, Uchumi na Elimu zina mlengo huo. Kubwa kabisa, serikali yetu inaendelea kuboresha mikakati mbalimbali kurahishisha utekelezaji wa sera hizi,” anasema.
Katika sekta ya kilimo, anasema nishati ya umeme jua inaweza kutumika mnyororo wote wa thamani wa kilimo kuanzia mazao yakiwa shambani na hata kuyaandaa kwa ajili ya kula.
“Nishati hiyo inaweza kutumika katika maandilizi ya shamba kwa maana ya kuendeshea vifaa kuvuta maji kutoka kwenye vyanzo kwa jili ya kuandaa shamba ama umwagiliaji,” anasema.
Kadhalika, anasema nishati hiyo inaweza kutumika kwenye uchakataji wa mazao kwa maana ya kuyakausha au kuzalisha ubaridi kwa yale yanayohitaji kwa ajili ya kuyapeleka sokoni.
Nishati hiyo pia kwa mujibu wa Dk Yustas, inaweza kutumika katika mitambo ya kuhifadhi mazao yakiwa sokoni.
Hata hivyo, mwanazuoni huyo anasema nishati ya umeme jua ni muhimu katika ulinzi wa usalama wa chakula kwa kuwa inawezesha uzalishaji zaidi.
Anasema ni muhimu kuimarisha matumizi ya nishati hiyo na itumike kwa usahihi ili kuongeza thamani na ufanisi kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya chakula.
Anasisitiza umuhimu wa kuimarisha uelewa wa wananchi juu ya tija ya nishati ya umeme jua katika kukuza kilimo, upatikanaji teknolojia sahihi, nafuu na fanisi.
|
Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), kimemtangaza Boniface Mwabukusi kuwa rais wa chama hicho, huku
|
Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), kimemtangaza Boniface Mwabukusi kuwa rais wa chama hicho, huku misimamo na ujasiri wake, zikitajwa kuwa miongoni mwa turufu zilizompa ushindi.
Mwabukusi ametangazwa mshindi wa kiti hicho, kwa kupata kura …. ambazo ni sawa na asilimia dhidi ya washindani wake Sweetbert Nkuba, Revocutus Kuuli, Ibrahim Bendera, Paul Kaunda na Emmanuel Muga katika uchaguzi huo ambao kwa mara ya kwanza umefanyika nje ya Jiji la Arusha.
Kinyang’anyiro cha uchaguzi huo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma, kililenga kumpata mrithi wa Harold Sungusia anayemaliza muda wake.
Hata hivyo, matokeo ya rais mpya wa TLS yalichelewa kutangazwa tofauti na ilivyotarajiwa awali, huku msiba wa mmoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, Maria Pengo ukitajwa kuwa sababu.
Matokeo ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa saa 11 jioni, lakini yalitangazwa saa….
Maria alikutwa na umauti usiku wa kuamkia juzi jijini humo alikokwenda kushiriki mkutano mkuu wa TLS.
Mwili wake ulipitishwa katika ukumbi wa mkutano huo kwa ajili ya mawakili kutoa heshima za mwisho, huku kinyang’anyiro cha upigaji kura kikiendelea.
Kilichombeba
Safari ya Mwabukusi katika kinyng’anyiro hicho ilikumbwa na misukosuko, siku moja kabla ya kuanza kwa kampeni za urais, kamati ya maadili ya TLS ilimuengua kuwania nafasi hiyo.
Kilichotajwa kama sababu ya kuenguliwa kwake ni doa la kimaadili kinyume na kanuni za uchaguzi huo Julai 5, mwaka huu.
Baadaye Mwabukusi hakukubaliana na uamuzi huo wa kamati ya maadili ya TLS na hivyo aliamua kwenda kukataa rufaa katika Mahakama Kuu akitetewa na mawakili zaidi ya 20.
Julai 26 mwaka huu, Mahakama Kuu ilikubaliana na hoja zilizowasilishwa na Mwabukusi na kutengua uamuzi wa kamati ya maadili ya TLS na kumrejesha mgombea huyo.
Hatua ya Mwabukusi kurejeshwa katika uchaguzi huo ilizidi kulipandisha joto la mchakato huo.
Mwabukusi ambaye amejipambanua kuwa moja wa mawakili wenye msimamo na kupigania haki na masilahi ya wananchi kupitia majukwaa mbalimbali aliyowahi kushiriki ikiwemo mikutano ya hadhara.
Wakili huyo alijizolea sifa katika sakata la kupinga mkataba wa uwekezaji na uendelezaji bandari kwa kampuni ya Dubai World (DP-World), akidai hauna maslahi kwa umma, lakini Serikali ilisema mchakato huo una faida kubwa kwa Taifa.
Mbali na hilo, katika utekelezaji wa majukumu yake, Mwabukusi amekuwa akikumbana na misukosuko na changamoto mbalimbali ikiwemo kuitwa katika kamati ya maadili ya mawakili kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Akiomba kura jana
Juzi, katika mdahalo wa kuomba kura, Mwabukusi alisema ukimuondoa mgombea mwenzake Kuuli washindani wengine waliobaki ni lazima wangekuwapo katika kinyanya’nyiro hicho, ndiyo maana walijikita katika kusifu ilani na ajenda zao.
“Ilani nyingi tumeziona zenye sura za kupendeza na kuvutia, lakini kwa miaka 70 hazijawahi kutupa majibu ya changamoto zinazotukabili, tunailaumu Serikali kwa sababu moja tu, tumeacha kazi ya msingi ambayo kifungu cha nne, badala yake tunadili na mambo yasiyo ya muhimu sana.
Kifungu cha nne kinachozungumzwa na Mwabukusi ni cha sheria ya kuanzishwa kwa TLS kinachokipa jukumu chama hicho la kuishauri Serikali.
“Kwahiyo Serikali ikitutafuta hatuonekani, kwa sababu imetupa sheria inayowezesha kuonekana na ukiwa na masuala yapi, yenye uzito upi na kwa utaratibu gani? lakini sisi tunapiga sarakasi tukiwa na taulo kiuno,” alisema Mwabukusi huku akishangiliwa.
Mwabukusi alisema TLS inahitaji kiongozi atakayeirudisha wanachama wa taasisi hiyo katika misingi yao na si mwingine bali ni yeye, akiwaomba wajumbe wa chama hicho kumpigia kura kwa wingi.
“Kukosekana uhalisia na uwajibikaji, ndiyo maana tunaona huku tuna vyama vingi vya uanasheria, tunahitaji chama kimoja chenye nguvu na jumuishi. Kutokana na hili ndiyo maana Serikali inaingilia taaluma yetu kwa sababu tumekuwa kama ng’ombe aliyekatwa kichwa amechoka na kuingia sokoni,” alisema Mwabukusi.
Mwabukusi aliwaomba wajumbe wa TLS kumchagua yeye awe na rais wa taasisi hiyo ili atekeleze majukumu yake kwa misingi ya kifungu cha nne.
Kwa upande wake Nkuba, alisema yeye ni muumini wa umoja na mshikamano, akisema miongoni mwa mambo atakayoyasimamia ni pamoja na kifungu cha nne, masilahi ya kiuchumi ya mawakili ikiwemo ulipaji wa ada kwa awamu, bima ya afya, pamoja na kuwasaidia mawakili vijana katika malezi kwa kuwatengenezea kituo cha malezi.
“Kuimarisha uhusiano na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, ambayo tutaishinikiza na kujadiliana ihakikishe katika mikataba yote ya uwekezaji inakuwa na kipengele cha lazima cha huduma za kisheria kwa local content ili kulinda kazi za mawakili.
“Nitahakikisha mawakili wanaheshimiwa katika utekelezaji wa majukumu yao, katika uongozi wangu hakutakuwa na vitisho vya aina yoyote kwa mawakili dhidi polisi au chombo chochote. Pia heshima yetu itatawala katika viunga vya mahakama zetu, tutajenga uhusiano bora,” alisema Nkuba.
|
Matumaini ya kutangazwa mapema kwa mshindi wa kiti cha urais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS)
|
Matumaini ya kutangazwa mapema kwa mshindi wa kiti cha urais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) jana, huenda yameyeyushwa na pigo lililokipata chama hicho la kumpoteza mmoja wa wanachama wake.
Katikati ya matarajio ya kupatikana kwa kiongozi huyo wa mawakili mapema jana, TLS ilipata msiba wa Maria Pengo, ambaye ni mmoja wa wanachama aliyekuwa sehemu ya wajumbe waliosafiri kwenda Dodoma kupiga kura za kumpata rais wa chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mawakili hao, Maria aliiaga dunia usiku wa kuamkia jana akiwa jijini Dodoma tayari kwa ajili ya kushiriki mkutano mkuu wa TLS ambao pamoja na mambo mengine ulilenga kufanya uchaguzi.
Hata hivyo, uchaguzi huo umefanyika kama kawaida wa kumpata mrithi wa Harold Sungusia ukiwahusisha wagombea sita waliopo, ambao ni Boniface Mwabukusi, Revocatus Kuuli, Ibrahim Bendera, Sweetbert Nkuba, Paul Kaunda na Emmanuel Muga.
Ingawa gazeti hili lilikuwa na taarifa za kutangazwa kwa matokeo hayo, lakini haikufanyika hivyo mapema, yalichelewa na hata gazeti hili lilipokwenda mtamboni saa… hayakuwa yametangazwa.
Kutokana na uanachama wake katika chama hicho, mwili wa Maria kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu za mazishi, ulipitishwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC), ulipofanyikia mkutano mkuu wa TLS kwa ajili ya mawakili kutoa heshima zao za mwisho.
Katika heshima hizo za mwisho, Rais wa TLS, Harold Sungusia alieleza kusikitishwa na msiba huo, lakini aliweka wazi kuwa hakuna mwongozo wa kuwaongoza linapotokea tukio kama hilo.
“Katika mikutano yetu hatujawahi kupata tukio kama hili la mwanachama wetu aliyekuja kuhudhuria mikutano kufariki. Hatuna kanuni kwa hiyo tunatumia busara tu,” alisema.
Alisema kuwa wameamua kuaga mwili huo ukumbini kwa sababu wote wasingeweza kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kutoa heshima hizo.
Mjomba wa marehemu, Julius Msengezi alisema walipata taarifa jana asubuhi kuwa wakili huyo alipata shida ya kiafya saa 3.00 usiku lakini akapelekwa hospitali saa 7.00 usiku.
“Sisi tulipata taarifa hii mapema asubuhi kabisa, kwamba Maria alipata changamoto ya kiafya usiku wa kuamkia jana saa 3.00 usiku na kupelekwa hospitali ambapo taratibu za kujaribu kuokoa maisha yake ziliendelea,” alisema.
Alieleza baada ya mwili huo kufika Dar es Salaam wataanza taratibu za kumrejesha nyumbani kwao Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ajili ya mazishi.
Serikali yatoa salamu
Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Feleshi alisema chama chao cha TLS kimempoteza mwanachama huyo katika kipindi ambacho ni cha kuheshimu sana utumishi wake na wajibu wake.
“Kwa sababu alikuja kwa jambo ambalo lilikuwa ni kutimiza wajibu wake, haki zake, sasa kwa Mungu ameamua kumpumzisha mwenzetu tunakila sababu ya kuyapokea lakini huku tukipata wito tunao wajibu wa kumuenzi zaidi kwa vitendo kwa sababu kama unavyojua kazi yetu ni kumsaidia Mungu kutenda haki,” alisema.
|
Rais Samia Suluhu Hassan ni kama ametupa jiwe gizani, akimpigia chapuo Mbunge wa Kilosa (CCM), Profe
|
Rais Samia Suluhu Hassan ni kama ametupa jiwe gizani, akimpigia chapuo Mbunge wa Kilosa (CCM), Profesa Palagamba Kabudi, achaguliwe tena na wananchi wa jimbo hilo aendelee kuwawakilisha.
Katika kauli yake mbele ya wananchi wa Kilosa, mkuu huyo wa nchi aliwaambia; “Endeleeni kuniletea Kabudi (Profesa).”
Kauli inayofanana na hiyo aliitoa pia alipokuwa Dumila mkoani Morogoro, alipowataka wananchi wa eneo hilo wamchagulie viongozi wazuri wanaotokana na CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.
Rais Samia alimnadi Profesa Kabudi jana, alipozindua daraja la Berege wilayani Kilosa, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Morogoro.
Kabla ya kuwataka wananchi hao waendelee kumchagua mbunge huyo, alianza kwa kumsifu kwa utendaji wake jambo alilosema amekuwa akimtumia hata serikalini.
“Ndugu zangu, tunapozungumza wabunge Kilosa mmepata Mbunge. Mbunge huyu si kwenu tu hata mimi namtumia kwenye mambo mengi.
“Nikikwamakwama huko nauliza jamani Kabudi yupo, nikiambiwa yupo nasema hebu muingizeni Kamati hiyo anichapie kazi. Kwa hiyo nawashukuru sana wana-Kilosa endeleeni kuniletea Kabudi asanteni sana,” alisema.
Akiwa Dumila katika mkoa huo pia, mkuu huyo wa nchi aliwataka wananchi wa eneo hilo katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu, wamechagulie viongozi wazuri akisema wale wanaotokana na CCM.
Agizo kwa halmashauri
Katika ziara yake hiyo, Rais Samia aliziagiza Halmashauri nchini kuhakikisha zinawapanga vema watumishi walioajiriwa hivi karibuni ili wasaidie kutoa huduma katika maeneo yote yenye uhitaji.
Amesema Serikali kwa sasa haina uwezo wa kufikia asilimia 100 ya mahitaji, lakini angalau wachache waliopo wagawanywe ili wawanufaishe wananchi wote.
Mkuu huyo wa nchi ametoa maelekezo hayo wakati akijibu ombi la Profesa Kabudi aliyeomba kupatikana kwa watumishi wa afya katika zahanati na vituo vya afya wilayani humo.
“Karibuni Serikali iliajiri watumishi wengi, mgao utakapokuja hapa, halmashauri ifanye mgao mzuri ndani ya halmashauri hii ili vituo vya afya vyote na hospitali zilizoko ndani ya Wilaya hii zipate madaktari na wauguzi,” alisema.
Kuhusu Daraja la Berege alisema litasaidia kuwaunganisha wananchi na kuvusha mazao kwa magari makubwa badala ya pikipiki walizokuwa wanatumia awali.
“Kujengewa daraja ni jambo moja kulitunza ni jambo lingine. Kama mlivyosikia daraja hili limetumia fedha nyingi, niwaombe sana tunzeni daraja litumike miaka mingi vizazi na vizazi,” alisema.
Hata hivyo, ameridhia ombi la Profesa Kabudi kubadili majengo yaliyokuwa ya World Vision na kuwa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi.
Katika hatua nyingine, alipokuwa Dumila ikiwa ni mwendelezo wa safari yake ya kuelekea Morogoro Mjini, Rais Samia alitoa Sh20 milioni kwa ajili ya uboreshwaji wa Soko la Mbogamboga la Dumila.
Sababu ziara ya siku sita
Akiwa wilayani Gairo katika Mkoa huo, Rais Samia alitaja sababu ya kutenga siku sita za ziara mkoaniu humo, akisema ni kutatua kero zinazowakabili wananchi na kuwasalimu kwa kuwa hakuwahi kufanya hivyo katika eneo hilo, tangu alipoapishwa kuwa Rais.
“Nimekuja kuwaona ndugu zangu toka mwaka 2021, nilipokabidhiwa dhamana sikuja kuonana nanyi, nimeamua kuja tuonane wengi mnahamu ya kuniona. Nimekuja kusikiliza shida zenu tuzichukue na kuzifanyia kazi,” alisema.
Dhamira nyingine ya ziara hiyo, alisema ni kuona matokeo ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kuondoa changamoto za wananchi kupitia miradi mbalimbali kama zinatumika vema.
“Bahati nzuri asubuhi nimeanza na kutembelea Hospitali ya Gairo, nimeridhika na matumizi ya fedha na kazi iliyofanyika pale. Ni hospitali nzuri yenye vifaa vya kisasa, naomba tuutunze ili iendelee kutupa huduma bora,” alieleza.
Kupitia ziara hiyo, alisema ataweka mawe ya msingi sambamba na kuzindua miradi mbalimbali iliyogharimiwa na Serikali ili kuboresha huduma kwa wananchi.
“Jingine nimekuja kujionea maendeleo ya kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na mvua kubwa za Elinino,” alisema.
Mvua kubwa zilizonyesha mapema mwaka huu zilisababisha uharibifu wa miundombinu hasa ya barabara za kilomita 3,115 kati ya kilomita 6256.9 zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura).
Pia, makalavati 211 kati ya 3,500 yanayohudumiwa na Tarura yalisombwa na maji, changao hiyo ilisababisha baadhi ya watumiaji wa barabara kusitisha kutoa huduma zao kwa wiki kadhaa.
Katika hatua nyingine, Rais Samia aliwataka wananchi wa Morogoro kuitunza amani iliyopo ili viongozi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi sambamba na kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongaji utakaofanyika mwisho mwa mwaka huu.
|
Pengine kila anayeonekana na mafanikio leo, zipo nyakati ngumu alizopitia jana ambazo kama si kukoma
|
Pengine kila anayeonekana na mafanikio leo, zipo nyakati ngumu alizopitia jana ambazo kama si kukomaa asingeupata umaarufu alionao.
Katika hili, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax ni kielelezo sahihi, anayesimulia magumu aliyowahi kupitia katika safari yake ya kuisaka elimu.
Kwa mujibu wa waziri huyo ambaye ni mwanamke wa kwanza kuiongoza wizara hiyo, magumu hayo yalitokana na kigugumizi cha nini alipaswa kuchagua kati ya kulea mtoto au kwenda nje ya nchi kujiendeleza na elimu.
Ingawa wakati huo, mwanawe huyo alikuwa na umri wa miaka minne, anasema kwa mzazi isingekuwa rahisi kukubali kumwacha kisha asafiri kwenda nje ya nchi kwa zaidi ya mwaka.
Kudharauliwa kutokana na jinsi yake, maswali yenye chembechembe za ukandamizaji wa kijinsia ni magumu mengine anayosimulia kama sehemu ya vikwazo ambavyo bila mapambano, pengine asingekuwa waziri anayeonekana sasa.
Dk Tax ameyasema hayo leo Ijumaa, Agosti 2, 2024 alipozungumza katika uzinduzi wa Redio Malkia Choice FM inayoendeshwa na kurusha matangazo yenye maudhui ya wanawake pekee.
Anasimulia changamoto hiyo ilimkabili miaka minne baada ya kuolewa na kuwa na mtoto, wakati huo huo alipata nafasi ya masomo njema Tanzania.
“Nilijiuliza nitafanyaje kuhusu mtoto maana kusoma nataka, kumlea mwanangu nataka nilikuwa katikati. Lakini baadaye nilifanya maamuzi magumu ya kumwacha na kwenda kusoma,” amesema.
Ingawa ulikuwa uamuzi mgumu, anasema ndani yake alikuwa anafikiria mbinu gani itakayomwezesha kutengeneza mazingira ya baadaye kumchukua mwanawe ili awe naye nje ya nchi.
“Miezi sita baadaye nilifanikiwa kutengeneza mazingira na nikamchukua mwanangu na kuwa naye nje ya nchi,” amesema.
Mtihani mwingine anasema ulikuwa namna ya kutenga muda wa kusoma lakini wakati huo huo azingatie huduma za mtoto na ukizingatia alikuwa katika taifa lisilo lake.
Juhudi pekee, anaeleza ndizo zilizomwezesha kufanikisha hilo na baadaye alifaulu vema na kutakiwa kuendelea na masomo ya shahada ya uzamivu katika mazingira hayo hayo.
Baada ya mafanikio hayo, anasema kwa kuwa alishazoea mazingira mumewe pia alikwenda nchini humo na akawa anamsaidia shughuli mbalimbali zikiwemo kazi za nyumbani.
“Wanaume ni watu wa ajabu sana tulivyokuwa kule (nje ya nchi) alikuwa anafanya kila kitu lakini alivyorudi akaacha kila kitu. Nilimuuliza siku moja mbona ulipokuwa kule ulikuwa unanisaidia kila kitu hadi kutosha vyombo lakini tumerudi nchini umeacha.
“Akaniambia wewe una akili kweli? dada yangu anikute naosha vyombo atanielewaje,” anasema.
Changamoto nyingine anayosema pengine ndiyo iliyosababisha hata ateuliwe katika wizara hiyo, anasema ni uamuzi wa kupendekeza nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kujitegemea kwa vikosi vya ulinzi na usalama panapo machafuko.
“Nikiwa Katibu Mkuu wa SADC, nimekuta tunajisifu kwamba jumuiya iko vema lakini kwenye ulinzi na usalama lakini tulikuwa tegemezi wanapotaka kudeploy mission tulilazimika kuwa omba omba,” anasema.
Katika mazingira hayo, anasimulia kutengenezwa bajeti ya SADC itakayowezesha kuwa na vikosi vyao, jambo alilopata upinzani mkubwa kutoka kwa timu yake.
Anaeleza wengi walimpinga kabla hata hajalifikisha kwa wakuu wa nchi kuliwasilisha, lakini aling’ang’ana hadi alipopata nafasi ya kuliwasilisha.
“Siku nilipoliwasilisha lilipitishwa na mwaka huo ndipo tulipoanza kudeploy mission ya kwanza Misutu na Msumbiji kwa fedha za ndani,” anasema Dk Tax.
Mitihani mingine iliyowahi kumkabili, anasema ni kupewa majukumu huku akiwa haaminiki kutokana na jinsi yake, lakini amekuwa akiwashangaza wanaompa kwani alitekeleza kama ilivyotakiwa.
“Nimeivuka kwa urahisi mitihani hii kwa sababu kwanza najiamini, ninapopewa jukumu natumia juhudi na bidii kulitekeleza inavyotakiwa,” anasema.
Anaeleza changamoto iliyopo kwa baadhi ya wanawake, hupenda kujidharau na wanatanguliza udhaifu kabla hata jamii haijawatazama kwa tafsiri hiyo.
“Wewe mwenyewe unasema mimi ni mwanamke hii siiwezi badala ya kuangalia wewe daktari na mimi daktari basi naweza kama mwingine,” anasema.
Mkurugenzi wa redio hiyo, Johayna Kusaga anasema wanacholenga ni kutengeneza jukwaa linalolenga masuala ya wanawake na litajadili maudhui yanayoihusu jinsi hiyo.
“Tunatarajiwa wanaume pia watasikiliza kwa sababu sisi ni mama zao, wake zao na tumehusika katika kuhakikisha wanafika walipofika,” anasema.
Anaeleza katika redio hiyo wafanyakazi wote watakuwa wanawake na wasichana, akisisitiza haitakuwa ya kusutana kama wengine wanavyotafsiri.
|
Ingawa kuimarika kwa huduma za treni ya umeme ni furaha kwa abiria, kwa upande wa wamiliki wa mabasi
|
Ingawa kuimarika kwa huduma za treni ya umeme ni furaha kwa abiria, kwa upande wa wamiliki wa mabasi ni maumivu, wakilalamika juu ya kudorora kwa biashara.
Malalamiko ya wasafirishaji hao yanakuja katika kipindi ambacho, safari za treni ya umeme zinazidi kuimarika na leo, Agosti 1, 2024, Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi safari kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Hata hivyo, kinacholalamikiwa na wasafirishaji hao, kimeelezwa na Rais Samia akisema kwa namna yoyote lazima wasafirishaji kwa njia ya mabasi waathirike, lakini wanayo fursa ya kwenda katika maeneo ambayo treni hiyo haifiki.
Msingi wa malalamiko ya wasafirishaji hao ni kile wanachoeleza, wanakosa abiria na hivyo kuathirika kibiashara, jambo linalochochewa na uwepo wa treni ya umeme.
Malalamiko hayo yameibuka leo Alhamisi, Agosti 1, 2024 na Msemaji wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Mustapha Mwalongo katika mahojiano yake na Mwananchi.
Amesema abiria kwa sasa wanachagua kupanda treni badala ya mabasi, hivyo wamiliki wa usafiri huo na wafanyakazi wao kwa ujumla wanaathirika.
Kuathirika huko kunatokana na kile alichoeleza, nauli iliyopangwa katika usafiri wa treni haijapishana na basi, ilhali huduma za vyombo hivyo vya usafiri ni tofauti.
Alisema abiria anapopanda basi anatumia saa saba kufika Dodoma, wakati akipanda treni ni saa tatu pekee na kwa sababu nauli zinafanana hakuna atakayechagua kuchelewa.
“Treni imekuja kutufukuza watu wa mabasi, kwa sababu nauli zilizopangwa ni karibu zinafanana na wao wanatumia njia moja, muda mfupi zaidi, kwa hiyo nauli ilipaswa kuwa tofauti treni ingekuwa kubwa,” amesema.
Kwa mujibu wa Mwalongo, athari ni kubwa na kulipaswa kuwepo mazungumzo kati ya Serikali na watoa huduma wa mabasi kuona namna ya kwenda.
“Athari ni kubwa na ukubwa wake ni pale ambapo treni inapoonekana imejaa hawasemi imejaa wanaongeza behewa lingine, huyo atakayekuja kupanda basi atumie saa saba nani.
“Hatukatai maendeleo na siku zote huwa na changamoto lakini Serikali ilipaswa kutuita na kutafuta maneno mazuri ya kutwambia kama haitutaki tena,” amesema.
Kuhusu fursa ya kwenda katika maeneo mengine kutoa huduma hiyo, Mwalongo amesema Tanzania yote hakuna eneo lisilo na huduma ya mabasi, hivyo uwezekano wa kuongeza mabasi maeneo mengine ni mgumu.
Sambamba na hilo, amesema uanzishwaji wa safari mpya unagharimu mamilio ya fedha, jambo ambalo wasafirishaji wanaliogopa.
Kwa malori kicheko
Lakini kwa upande wa malori, Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Wadogo wa Malori (Tamstoa), Chuki Shaaban amesema uwepo wa treni hiyo ni fursa kwao.
Fursa hiyo itatokana na kile alichoeleza, eneo linakofika lori treni haina uwezo wa kufika, hivyo wataendelea kufanya kazi wanayoendelea nayo na pengine ikaongezeka zaidi.
Kwa mujibu wa Shaaban, ujio wa treni hiyo utaongeza mizigo bandarini na hivyo malori yatakuwa na kazi nyingi za kupakia kupeleka kwa wamiliki.
“Treni itabeba mzigo hadi kwenye bandari na wakati mwingine itaishia bandari kavu, ili kuufikisha kwa mmiliki lori ndilo litakaloifanya kazi hiyo, kwa hiyo sioni athari zaidi ya fursa,” ameeleza.
Amelisisitiza hilo kwa ufafanuzi kuwa, Ulaya kuna treni nyingi zaidi zinazosafirisha mizigo, lakini bado malori ni mengi kwa ajili ya shughuli zake.
“Sisi tunapongeza kwa ujio wa treni, tunaamini kazi zitaongezeka zaidi,” amesema.
|
Yametimia, ndilo neno jepesi linaloweza kuakisi uhalisia wa safari ya utekelezaji wa mradi wa Reli y
|
Yametimia, ndilo neno jepesi linaloweza kuakisi uhalisia wa safari ya utekelezaji wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), uliopitia milima na mabonde hadi kufika sasa wananchi wanaposafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.
Hoja ya yametimia inajengwa na msingi wa uhalisia kuwa, ndoto ya ukamilishwaji wa mradi wa SGR ilinasibishwa na Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli na kufariki kwake Machi 27, 2021 kulidhaniwa kutayeyusha malengo ya kukamilika kwa mradi.
Bado inabaki kuwa yametimia, kwa sababu katikati ya dhana hizo, mrithi wa Hayati Magufuli, Rais Samia Suluhu Hassan ameendeleza mradi huo na jana amebonyeza kitufe cha uzinduzi rasmi wa safari za treni ya umeme kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.
Rais Samia amepokea kijiti cha urais, Machi 29, mwaka 2021, kipindi ambacho utekelezaji wa mradi wa SGR ulikuwa asilimia 22.
Ingawa aliahidi kuendeleza mazuri yaliyoanzishwa na mtangulizi wake, ahadi hiyo ilikuwa ngumu kuingia katika akili za Watanzania wengi, wakidhani angeshindwa.
“Serikali yangu itaendelea kuendeleza mazuri yote yaliyoachwa na Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli pamoja na kuleta mema mengine mapya,” alisema Rais Samia siku chache baada ya kuapishwa kuwa rais.
Mkuu huyo wa nchi amezindua safari za treni hiyo jana, akisafiri umbali wa zaidi ya kilomita 444 kutoka Stesheni ya Posta jijini Dar es Salaam hadi Dodoma.
Awali akizungumza akiwa ndani ya treni hiyo kuelekea Stesheni ya Pugu jijini Dar es Salaam, Rais Samia alisema kwa hatua iliyofikiwa anaona mwanga na kwamba anamshukuru Mungu.
Alisisitiza ahadi yake ya kuendeleza mazuri yaliyoachwa na mtangulizi wake, akisema kwa pamoja waliuanza mradi huo na kwamba ameona auendeleze.
“Nina faraja kusema kwamba yale ambayo niliyaanza na mwenzangu marehemu (Magufuli) nimeyakamilisha kwa hiyo ni miradi ambayo kwa Tanzania ni muhimu sana,” alisema.
Agusia athari kwa wasafirishaji
Katika mazungumzo yake hayo, mkuu huyo wa nchi alisema licha ya athari zilizoanza kujitokeza kwa wamiliki wa mabasi na zinazotarajiwa katika malori kutokana na kuanza kwa treni ya umeme, bado Tanzania ina fursa nyingi za wasafirishaji hao kunufaika.
Alieleza kupungua kwa mabasi barabarani inaweza kuwa mbaya kwa wafanyabiashara lakini nzuri kwa Serikali kwa kuwa itapunguza ajali.
“Hasara moja ambayo imeanza kuonekana ni kupungua kwa mabasi barabarani, kwa wafanyabiashara ni mbaya lakini kwa nchi ni nzuri kwa sababu inapunguza ajali pia na sasa usafiri barabarani unadhibitiwa vizuri,” alisema.
Hata hivyo, alieleza bado wasafirishaji hao hawataathirika kwa kuwa kuna njia nyingine treni hiyo haijafika na hivyo wanayo nafasi ya kupeleka mabasi huko.
“Lakini sasa wanapunguza mabadi eneo moja ambalo tayari kuna maendeleo haya, lakini Tanzania ni kubwa kuna maeneo ambayo yanahitajika kwa hiyo sasa yatakwenda kule,” alisema.
Athari pia, alisema zitashuhudiwa katika usafirishaji wa mizigo kupitia malori, hasa pale ambapo treni hiyo itaanza kubeba mizigo, lakini bado kutakuwa na maeneo ambayo hayatakuwa na mradi huo.
Taboa walia
Wakati wananchi na Serikali ikifurahia mradi huo, kwa upande wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa) ni kilio, wakisema hali imekuwa mbaya kibiashara kwa kukosa abiria.
Msemaji wa Taboa, Aboubakar Mwalongo aliliambia Mwananchi kuwa, abiria kwa sasa wanachagua kupanda treni badala ya mabasi, hivyo wamiliki wa usafiri huo na wafanyakazi wao kwa ujumla wanaathirika.
Kuathirika huko kunatokana na kile alichoeleza, nauli iliyopangwa katika usafiri wa treni haijapishana na basi, ilhali huduma za vyombo hivyo vya usafiri ni tofauti.
Alisema abiria anapopanda basi anatumia saa saba kufika Dodoma, wakati akipanda treni ni saa tatu pekee na kwa sababu nauli zinafanana hakuna atakayechagua kuchelewa.
“Treni imekuja kutufukuza watu wa mabasi, kwa sababu nauli zilizopangwa ni karibu zinafanana na wao wanatumia njia moja, muda mfupi zaidi, kwa hiyo nauli ilipaswa kuwa tofauti treni ingekuwa kubwa,” alisema.
Kwa mujibu wa Mwalongo, athari ni kubwa na kulipaswa kuwepo mazungumzo kati ya Serikali na watoa huduma wa mabasi kuona namna ya kwenda.
“Athari ni kubwa na ukubwa wake ni pale ambapo treni inapoonekana imejaa hawasemi imejaa wanaongeza behewa lingine, huyo atakayekuja kupanda basi atumie saa saba nani.
“Hatukatai maendeleo na siku zote huwa na changamoto lakini Serikali ilipaswa kutuita na kutafuta maneno mazuri ya kutwambia kama haitutaki tena,” alisema.
Kuhusu fursa ya kwenda katika maeneo mengine kutoa huduma hiyo, Mwalongo alisema Tanzania yote hakuna eneo lisilo na huduma ya mabasi, hivyo uwezekano wa kuongeza mabasi maeneo mengine ni mgumu.
Sambamba na hilo, alisema uanzishwaji wa safari mpya unagharimu mamilio ya fedha, jambo ambalo wasafirishaji wanaliogopa.
Kwa malori kicheko
Lakini kwa upande wa malori, Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Wadogo wa Malori (Tamstoa), Chuki Shaaban alisema uwepo wa treni hiyo ni fursa kwao.
Fursa hiyo itatokana na kile alichoeleza, eneo linakofika lori treni haina uwezo wa kufika, hivyo wataendelea kufanya kazi wanayoendelea nayo na pengine ikaongezeka zaidi.
Kwa mujibu wa Shaaban, ujio wa treni hiyo utaongeza mizigo bandarini na hivyo malori yatakuwa na kazi nyingi za kupakia kupeleka kwa wamiliki.
“Treni itabeba mzigo hadi kwenye bandari na wakati mwingine itaishia bandari kavu, ili kuufikisha kwa mmiliki lori ndilo litakaloifanya kazi hiyo, kwa hiyo sioni athari zaidi ya fursa,” alieleza.
Alilisisitiza hilo kwa ufafanuzi kuwa, Ulaya kuna treni nyingi zaidi zinazosafirisha mizigo, lakini bado malori ni mengi kwa ajili ya shughuli zake.
“Sisi tunapongeza kwa ujio wa treni, tunaamini kazi zitaongezeka zaidi,” alisema.
Aisifu TRC
Katika mazungumzo yake ndani ya treni hiyo, Rais Samia aliusifu uamuzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuanza safari za kwenda Dodoma Julai 25, mwaka huu akisema alivyoona alifurahia, akidokeza “(Kadogosa, Mkurugenzi Mkuu wa TRC) alikuwa anaogopa kutumbuliwa.”
Katika hatua nyingine, alisema hautazami mradi huo kwa sura ya kibiashara pekee, bali wakati mwingine anautazama kama huduma kwa kuwa una manufaa katika maeneo mengine.
Sababu ya kupambania utekelezwaji wa mradi huo ni kile alichoeleza, analenga kuiunganisha Tanzania na mataifa ya Burundi na Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ili kupata soko la bidhaa.
Alisimulia zamani aliwahi kupanda treni la awali (MGR) kutoka Dar es Salaam hadi Moshi na akiwa njia alikumbwa na changamoto lukuki likiwemo vumbi.
“Hadi kufikia hatua iliyofikiwa sasa namshukuru Mungu na kwamba namuomba Mungu njia yote imalizwe hadi kufikia Burundi,” alisema.
…akiwa Pugu
Akiwa katika Stesheni ya Pugu, Rais Samia alisema ingawa kazi kubwa imefanywa matarajio ni kuutekeleza zaidi mradi huo hadi kufikia Kigoma na hatimaye nje ya Tanzania.
Katika hatua nyingine, alisema fedha zote zinazokusanywa kupitia mradi huo na kwingineko ni za wananchi na haoni sababu ya kukaa nazo ilhali wananchi wana shida.
“Fedha zinazoingizwa kwenye sekta zao zikafanye kazi ya kuwaondoshea kero za wananchi, tutaondosha kero ya afya, umeme na kila kero,” alisema.
Alitumia jukwaa hilo kumsifu Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa akisema alianza naye katika sekta ya ardhi na kwa kazi hiyo ameona ni vema amkabidhi vyombo vya habari.
“Kazi hizi ni kubwa ndugu zangu inawezekana akakaa wiki tatua nne hajaonekana lakini mjue yupo kazini ananisaidia kuijenga Tanzania, kwa hiyo naombeni mshikeni mkono,” alisema.
…akiwa Morogoro
Akiwa mkoani Morogoro aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo, kukamilisha ujenzi wa barabara ya Bigwa-Kisaki, akisema naye ni sehemu ya wanufaika wake.
“Nina mashamba pale Msonge ambayo ninataka kuyaendeleza kwa hiyo barabara hii tutajenga. Mimi ni mwana Morogoro mwenzenu,” alisema.
Barabara aliyoizungumzia Rais Samia ni ya Bigwa-Kisaki ambayo awali, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale aliomba ujenzi wake kwa mkuu huyo wa nchi.
|
Serikali imetakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kuwabaini wanaojihusisha na vitendo vya ukatili dhi
|
Serikali imetakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kuwabaini wanaojihusisha na vitendo vya ukatili dhidhi ya watoto ukiwemo utekaji, ili kutokomeza matukio yanayoendelea nchini.
Ushauri huo unatolewa katika kipindi ambacho, kumeripotiwa matukio kadhaa ya madai ya kutekwa na kutoweka kwa watoto nchini.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alikiri kuwepo kwa matukio hayo, akifafanua wingi unaoripotiwa ni tofauti na uhalisia wa idadi yake.
Ushauri huo umetolewa leo, Jumatano Julai 31, 2024 na Mwanazuoni kutoka Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Chris Peter Maina alipokuwa akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kisheria watetezi wa haki za watoto.
Amesema kuendelea kwa matukio hayo dhidi ya watoto kunaongeza hofu kwa jamii, hivyo mikakati ya kuwabaini wanaofanya vitendo hivyo itasaidia kuondoa wasiwasi uliopo.
“Watu hawaheshimu sheria, hawalei watoto wao vizuri sasa hivi kuna wimbi la watoto kupotea wengine wanauawa na kukutwa baadhi ya viungo hawana.
“Serikali ikiweka mikakati ya kuwabaini wahusika wa vitendo hivi itasaidia kuondoa ukatili unaoendelea kufanyika nchini," amesema.
Tatizo lililopo, amesema watoto hawalindwi, hawapendwi na hawataki kuiheshimu jamii inayowazunguka wakiwemo wazazi au walezi.
Akizungumzia dhamira ya mafunzo hayo, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa amesema wanalenga kujenga uwezo katika sheria na mifumo ya ulinzi na utetezi wa haki za binadamu kikanda na kimataifa.
Olengurumwa amesema lengo ni kuboresha hasa kipindi ambacho kuna wimbi la ukatili na ukiukwaji wa haki za watoto.
"Tumeona taarifa za polisi zinasema masuala ya ulawiti ,ubakaji unaongezeka kama kupotea na utekaji, watetezi wa haki za watoto wakipata mafunzo tunaamini kazi ya utetezi itaboreka zaidi hasa kule walipo wengi wao wanatoka mashuleni.
"Leo tumewaleta watetezi wanaowatetea watoto kutoka mikoa sita ya Morogoro, Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Mtwara na Lindi," amesema Olengurumwa.
Amesema taasisi za ustawi wa jamii ndiyo walinzi wa watoto katika ngazi ya Kata, lakini wengi hawaelewi sheria na mifumo hivyo wanatakiwa wajengewe uwezo ili watimize wajibu wao.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Mashirika ya Watoto, Ombeni Kimaro amewataka wazazi kuhakikisha wanawapa elimu watoto wao ili inapotokea changamoto ya ukatili watoe taarifa kunakohusika.
|
Wakati safari za treni ya umeme zikiathiriwa kwa takriban saa mbili kutokana na hitilafu ya umeme il
|
Wakati safari za treni ya umeme zikiathiriwa kwa takriban saa mbili kutokana na hitilafu ya umeme iliyosababishwa na ndege na wanyama, Shirika la Reli Tanzania (TRC), limesema kuna matarajio ya viumbe hao kuhama.
Kuhama kwa ndege na wanyama hao, kutatokana na kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa kuwa, uendeshaji wa mradi huo utayafanya mazingira hayo kutokuwa rafiki kwao.
Msingi wa ufafanuzi wa Kadogosa ni hitilafu ya umeme iliyosababisha kukwama kwa safari ya treni hiyo kwa takriban saa mbili katika Stesheni ya Kilosa na Kidete ilipokuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Awali, baada ya hitilafu hiyo iliyotokea juzi, TRC ilitoa taarifa kwa umma ikieleza sababu za hitilafu hiyo ni Ngedere na Bundi walipogusa nyaya za umeme unaondesha treni hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hitilafu ilisababisha kukatika kwa umeme katika kituo namba saba cha kupozea umeme, kuanzia saa 4:20 usiku.
Hata hivyo, taarifa hiyo iliweka wazi kuwa, mafundi wa TRC walitatua changamoto hiyo na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma, hivyo iliwasili saa 7:57 usiku.
Kadogosa alitoa ufafanuzi huo jana alipozungumza na Mwananchi kuhusu namna TRC inavyojipanga kuhakikisha changamoto kama hiyo haijitokezi wakati mwingine.
Katika majibu yake, mkurugenzi huyo alieleza kuna matarajio makubwa wanyama na ndege hao watahama kutoka katika maeneo hayo kwa kadri mradi utakavyoendelea kuendeshwa.
Hilo litatokana na kile alichofafanua, mazingira ya maeneo hayo hayatakuwa rafiki kwa ndege na wanyama hao kuendelea kukaa.
“Shirika tumejipanga kushughulikia tatizo likijitokeza, hicho ndiyo kitu cha msingi na lakini pia kadri uendeshaji unaendelea hao ndege au wanyama watahama, mazingira kwao hayatakuwa rafiki,”alisema Kadogosa.
Wadau washauri
Kutokana na kilichotokea, Mdau wa Usimamizi Dumivu wa Rasilimali za Maliasili, Clay Mwaifwani alipendekeza Serikali ifanye tathmini kipindi cha ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo ya hifadhi kama ilivyo katika maeneo mengine.
“Tuna barabara na reli ambazo zimekatiza kwenye hifadhi za wanyama na haijaathiri lakini hili ni jipya kwetu ilitakiwa kutumika hata mfumo wa maandaki au reli za juu sehemu za hifadhi ili kuepuka madhara ya wanyama na ndege,” alisema.
Alieleza kwa uhalisia wa mazingira ni rahisi wanyama kubadili maisha yao na hivyo kuondoka katika maeneo yaliyopitishwa miradi, huku akionya hilo lisifanywe katika namna ya kuathiri mazingira yao.
Kwa mujibu wa Mwaifwani, umakini unahitajika zaidi katika awamu zinazoendelea za utekelezaji wa mradi huo ili kusitokee athari kama zilizojitokeza.
Lakini, changamoto kama hiyo ilipaswa kujulikana mapema iwapo tathmini ingefanyika, kama inavyoelezwa na Ofisa Programu Chama cha Wanasheria Watetezi na Mazingira (Leaf), Franklin Masika.
“Walitakiwa kufahamu eneo husika linawanyama pori na hivyo kutafuta mbinu za upitishaji wa umeme ikiwepo kudhibiti wanyama, kuchepusha njia za umeme, kufunika au kupitisha chini ya ardhi ili kupunguza hizo changamoto,” alisema.
Alisisitiza umuhimu wa tathmini ili kudhibiti mazingira kama hayo yasijitokeze tena.
Lakini, Mtaalamu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi, Msololo Onditi alisema hilo ni tatizo la kawaida katika mazingira.
“Kimsingi hakuna njia au suluhisho la moja kwa moja la kudhibiti changamoto hiyo kwani wanyama wanatofautiana kimaumbile tabia na mazingira wanayokutana nayo jirani na miundombinu ya reli,” alisema.
Mbali na hilo, alisema utafiti ufanyike ambao wataalamu wa wanyamapori na viumbe watatoa maelekezo ya kitaalamu kutatua changamoto hiyo.
Kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi, alisema kuna uwezekano hali hiyo ikawa endelevu kwani wanyama na viumbe wanatafuta kujikimu kulingana na mabadiliko katika mazingira yao.
…Rais Samia kuzindua safari za Dom
Wakati huo huo, Rais Samia Suluhu Hassan leo, anatarajia kuzindua rasmi safari za treni hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Uzinduzi huo unafanyika zikiwa zimepita siku kadhaa tangu safari za treni hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma zianze, Julai 25, mwaka huu.
Katika uzinduzi huo, mkuu huyo wa nchi anatarajiwa kupanda treni hiyo kutokea Dar es Salaam hadi Dodoma, umbali wa zaidi ya kilomita 444.
Akizungumzia hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alisema safari za treni hiyo kwenda katika mkoa huo zitasaidia katika kukuza biashara, utalii na mapato.
“Tumejipanga Agosti Mosi 2024, kesho sisi kwetu itakuwa ni siku ya pekee ambapo mheshimiwa Rais Samia anakwenda kuzindua rasmi treni hii ya mwendo kasi, pamoja na reli ya mwendo kasi, tutakuwa zaidi ya watu 30,000 hapa kumpongeza Rais Samia kwa ujenzi wa reli hii,” alisema.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya aliagiza madereva wote kujisajili katika kituo chao ili kuepuka ugomvi unaoweza kujitokeza kwa kigezo cha watu kuvamia kituoni.
“Taratibu mtakazowekeana mzifuate, mheshimiane…la pili acheni ulevi, Serikali ilikuwa imeondoa viroba lakini kuna vipombe vingine vimekuja mnatembea navyo achaneni na hizo pombe kwanza zina madhara,” alisema.
|
Licha ya changamoto zinazotajwa katika kufikia malengo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini
|
Licha ya changamoto zinazotajwa katika kufikia malengo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, juhudi zinazofanyika zinaonyesha matumaini ya kufikiwa kunakotarajiwa.
Miongoni mwa changamoto zinazotajwa katika mkakati wa mabadiliko ya matumizi ya nishati ya kupikia ni uelewa na mitazamo hasi ya jamii.
Lakini Serikali imejiwekea lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia baada ya miaka 10 yaani mwaka 2034.
Hata hivyo, uhalisia wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa sasa ni asilimia 10.2 mwaka 2020/21 ikiongezeka kutoka asilimia 3.8 ya mwaka 2014/15, kwa mujibu wa Utafiti wa Kitaifa wa ufuatiliaji wa kaya wa 2020/21 (NPS) uliozinduliwa Januari 2023 na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Katika mazingira hayo, wanazuoni na wadau wa nishati safi, wanaonyesha matumaini ya kufikiwa kwa malengo yanayotarajiwa iwapo msisitizo utawekwa kwenye kubadilisha tabia ya jamii.
Kwa dhamira hiyo hiyo ya kubadili tabia na kuelimisha jamii ili kufikiwa lengo tarajiwa, Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inashiriki kwa kufanya mjadala kuhusu nishati safi ya kupikia kupitia ‘Jukwaa la Fikra.’
Wanachoshauri wanazuoni
Mtaalamu wa Udhibiti wa Baionuai na Mabadiliko ya Tabianchi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Dk Catherine Masao anasema mafanikio ya safari hiyo yatafikiwa iwapo elimu kwa jamii juu ya kubadili fikra itazingatiwa.
Kwa mujibu wa mwanazuoni huyo, elimu hiyo inapaswa ibadili tabia ya jamii, baada ya kueleweshwa faida za kutumia nishati safi ya kupikia na kupewa mifano halisi.
Elimu hiyo, anapendekeza iambatane na uamuzi wa Serikali kulazimisha wale wenye uwezo kuhakikisha wanahama mara moja kutoka kutumia nishati zisizostahili hadi kutumia nishati safi.
“Kwenye hili Serikali imeshaanza maana kwa taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 20 zimelazimishwa kutumia nishati safi, kwa hiyo hii ni hatua nzuri,” anasema.
Sambamba na hayo kwa mujibu wa Dk Catherine, Serikali pia inalazimika kuwekeza kwa kuanzisha utekelezaji huo ili itumike kama mfano kwa wananchi.
Serikali pia inapaswa kubuni mradi utakaowawezesha wananchi ama kutengeneza wenyewe au kuyapata majiko banifu kwa gharama nafuu kama inavyoelezwa na mwanazuoni mwingine aliyebobea katika taaluma ya mazingira, Profesa Amos Majule.
“Serikali inapaswa kubuni mradi wa namna hii, ili wananchi wenyewe wawe na uwezo wa kutengeneza majiko banifu au wayafikie kwa urahisi na gharama nafuu,” anapendekeza.
Anasisitiza hilo kwa hoja kuwa, elimu kwa jamii nalo si jambo la kupuuza.
Wawekezaji wanasemaje?
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Makampuni ya Uuzaji wa Mafuta Tanzania (Taomac), Raphael Mgaya anasema gesi asilia na nishati safi ya kupikia ndilo eneo ambalo wanachama wake wengi wanalitazama kwa sasa.
Pamoja na fursa zilizopo kwenye eneo hilo, anapendekeza maboresho ya kisheria na kikodi ili kuvutia uwekezaji zaidi na hatimaye kuwezesha kila mwananchi amudu gharama za nishati safi.
Kwa mujibu wa Mgaya, kwa sasa Serikali inatoza kodi katika vifaa vya majiko ya gesi na mitungi ambazo kimsingi zinaongeza gharama ya uuzwaji wake kwa wananchi.
“Kwa upande wa uagizaji wa vifaa vinavyotumika katika kusindika gesi kwa maana mitungi, mita, mipira inayopitisha gesi kutoka kwenye majiko, Serikali ingesaidia kama itapunguza kodi,” anasema.
Anaeleza changamoto kubwa ni wananchi kushindwa gharama za kununua mtungi uliojaa gesi kisha jiko lenyewe, lakini kama kodi itapunguzwa hata bei itashuka.
Jambo lingine linalopaswa kuboreshwa, anasema gesi yenyewe hasa ile isiyozalishwa nchini, akifafanua nayo Serikali inapaswa ifikirie kupunguza kodi ili kuleta unafuu kwa wananchi.
“Itafanya gesi hiyo iwe shindani ukilinganisha na nishati nyingine zinazotumika kama kuni, kwa sababu mwananchi anaangalia unafuu, Serikali ina nia njema lakini mwananchi anaangalia nini kitampa unafuu,” anasema.
Kwa upande wa gesi asilia inayozalishwa nchini, anasema ni vema uandaliwe utaratibu wa usambazaji katika nyumba kwa nyumba kama ilivyofanyika katika baadhi ya maeneo.
“Kuna haja Serikali kuchochea uwekezaji kwa sababu changamoto ni zile zile za kikodi na kisheria ambazo Serikali inapaswa kukaa na wadau ili kupata utatuzi wake,” anasema.
Kadhalika, Mgaya anaitaja changamoto nyingine ya kisheria inayotoa umiliki wa miundombinu yote ya usafirishaji wa gesi kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
“TPDC hana uwezo wa kusambaza mabomba nchi nzima ni ngumu lazima wawekezaji wavutiwe na lazima kuwe na vivutio kwa wawekezaji wawekeze kwenye miundombinu hiyo,” anasema.
Mkakati wa nishati safi
Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) uliozinduliwa mwaka huu, ulinukuu takwimu za Benki ya Dunia za mwaka 2023, zinaoonyesha idadi ya Watanzania wanaotumia nishati safi ya kupikia imeongezeka kutoka asilimia 1.5 mwaka 2010 hadi asilimia 6.9 mwaka 2021.
“Kiwango hiki ni chini ya kiwango cha wastani cha dunia cha asilimia 71 kwa Mwaka 2021” ilisema sehemu ya ripoti hiyo.
Mchanganuo wa takwimu hizo ni Zanzibar ni asilimia 11.6 ya wananchi ndiyo wanaotumia nishati safi ya kupikia, wakati Dar es Salaam ni asilimia 36.3.
Kwa nchi nzima, maeneo ya mjini ndiyo yanayoongoza kwa matumizi ya nishati safi ya kupikia wakifikia asilimia 28.3, huku vijijini ni asilimia 3.6.
Hata hivyo, kuzinduliwa mkakati huo ni mwendelezo wa mikakati ya nchi iliyoanza muda mrefu na Desemba 2023 kwenye mkutano mkubwa wa mabadiliko ya tabianchi (COP28) uliofanyika Dubai.
Mpango huo wa nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika (AWCCSP) unahimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kushughulikia changamoto za kiafya, kimazingira, kiuchumi na kijamii ambazo mara nyingi zinaathiri vibaya wanawake na watoto.
"Tunazindua mradi huu kwenye COP28 kuonyesha uwajibikaji wetu licha ya kuwa na utoaji mdogo wa hewa joto, suala la nishati safi ni sehemu ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na usalama wa wanawake," alisema Rais Samia Suluhu Hassan katika wasilisho wake kwenye mkutano wa COP28 mwaka jana.
|
Nani mrithi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bara, ndilo swali linalouliz
|
Nani mrithi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bara, ndilo swali linaloulizwa na wengi baada ya aliyekuwa na wadhifa huo, Abdulrahman Kinana kujiuzulu.
Taarifa ya kujiuzulu kwa Kinana ilitolewa na CCM juzi, ikinukuu sehemu ya barua ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho, akijibu ombi la mwanasiasa huyo kuwa, kwa moyo mzito amekubali.
"Nilipokuomba utusaidie kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa kwa muda mfupi kama ulivyoomba na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia.
"Lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako," imeeleza sehemu ya taarifa ya CCM ikinukuu barua ya Rais Samia kujibu ombi la Kinana kujiuzulu.
Uamuzi wa Kinana umeibua kiu ya wadau wa siasa, makada na wafuasi wa chama hicho, kujua nani atakayerithi mikoba ya mwanasiasa huyo katika wadhifa huo ndani ya CCM.
Shauku ya wadau hao inakatwa na taarifa za ndani ambazo gazeti hili linazo kuwa, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ndiye mmoja wa wanasiasa walio karibu kuirithi nafasi hiyo.
Lakini Pinda hakutajwa peke yake, Steven Wasira, Frederick Sumaye na Abdallah Bulembo ni makada wengine waandamizi wa chama hicho wanaohusishwa na urithi wa wadhifa huo.
Wakati taarifa zikieleza hivyo, mmoja wa wanasiasa hao, Wasira anasema hajaona wala hakusikia kuhusu kutajwa kwake kurithi nafasi hiyo na kwamba hana la kuzungumza katika hayo.
“Sijaona wala kusikia hizo taarifa za kutajwa kwangu. Kwa hiyo sina la kusema kwenye hilo,” alieleza kwa ufupi.
Hata hivyo, Wanazuoni wa Sayansi ya Siasa na Utawala wanataja sababu za kujiuzulu kwa Kinana, huku wakiweka wazi mzigo utakaomkabili mrithi wake.
Katiba, Kanuni ya CCM
Ili kupatikana mrithi wa Kinana, kutalazimika kuitishwa mkutano mkuu wa taifa wa dharura wa chama hicho, ambao ndiyo wenye wajibu wa kuwachagua Makamu wenyeviti wawili wa CCM yaani bara na Zanzibar.
Kwa mujibu wa Ibara ya 99(3) mkutano mkuu wa taifa wa kawaida, hufanyika mara tatu katika kipindi cha miaka mitano.
Lakini, mkutano wa dharura unaweza kufanyika wakati wowote ukiitishwa na Mwenyekiti wa CCM au ukiombwa na theluthi mbili ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho taifa.
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2017, nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM inatambuliwa katika Ibara ya 114 ya Katiba ya chama hicho.
Kwa mujibu wa Ibara hiyo, nafasi hiyo inashikwa na watu wawili, ambao mmoja anayetokea bara na atafanya shughuli zake katika eneo hilo, huku mwingine akitokea Zanzibar na atatekeleza majukumu yake huko.
Wawili hao kwa mujibu wa Ibara hiyo, ndiyo wasaidizi wakuu wa Mwenyekiti wa chama hicho na watatekeleza majukumu yote watakayopewa na mwenyekiti wao.
Lakini Kanuni za Maadili na Uongozi cha CCM, zinamtambua Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, kuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Udhibiti ya Kamati ya Usalama na Maadili Taifa.
Kamati hiyo ya udhibiti inayoundwa na wajumbe wanne, inaongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara kama Mwenyekiti, Mkurugenzi wa Maadili ngazi ya taifa kama Katibu na Wajumbe wawili wa Kamati Kuu kutoka Zanzibar na Bara kama wajumbe.
Kwa mujibu wa kanuni hiyo toleo la mwaka 2017, kamati hiyo ya udhibiti itakuwa na wajibu wa kusikiliza, kuhoji na kupendekeza adhabu kwa watuhumiwa wenye mashitaka yanayopelekwa kwa uamuzi kwenye vikao vya ngazi hizo.
Mrithi atakabiliwa na haya
Akizungumzia hilo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Out), Dk Revocatus Kabobe alisema mrithi wa Kinana ataingia akikabiliwa na majukumu matatu, ikiwemo kupanga vema timu ya sekretarieti ndani ya chama hicho.
“Utagundua kuwa Katibu Mkuu (Dk Emmanuel Nchimbi) na mwenezi (Amos Makalla) hawana muda mrefu kwenye nafasi zao. Hata viongozi wengine wa baadhi ya jumuiya za chama mathalani kwa wazazi na wanawake bado wapya.
“Anahitajika makamu mwenyekiti mwenye kulijua hilo na kuweka mikakati ya kupanga safu vizuri ndani ya sekretarieti,” alisema Dk Kabobe.
Jukumu la pili kwa mujibu wa mwanazuoni huyo ni kulikabili fukuto linalodaiwa kuwepo ndani ya chama hicho, likihusisha kujitokeza kwa mtandao wa wawania uongozi wa juu ndani ya Serikali.
Alieleza hilo limekwenda mbali zaidi hadi kuhusisha panga pangua inayoendelea kwenye baraza la mawaziri na vyombo vya dola kuwa ni mbinu za kukabiliana na mtandao huo.
Alisema Makamu Mwenyekiti anayekuja ni jukumu lake kukabiliana na hilo.
Mwanazuoni huyo alisema kiongozi huyo ajaye anakabiliwa na jukumu la uchaguzi mkuu wa mwakani na CCM mara zote inahitaji ushindi kama ilivyo nia ya kila chama cha siasa.
“Kwahyo lazima makamu mwenyekiti ajaye ajue haya mambo matatu na kuweka namna ya kuyakabili,” alisema na kusisitiza nafasi hiyo ni nyeti na nzito ndani ya chama hicho.
Uzito wa nafasi hiyo unatokana na kile kilichoelezwa na Dk Kabobe kuwa, Mwenyekiti wa chama hicho huwa na kofia ya urais hivyo muda mwingi anautumia kwenye nafasi hiyo.
Kwa sababu hiyo, alieleza Makamu Mwenyekiti ndiye anayepaswa kusimamia zaidi shughuli za chama wakati rais akivaa zaidi kofia ya urais.
“Lazima CCM ijipange kwenye hilo na sina shaka maana ni chama kikongwe chenye watu wazoefu sana ndani na nje yake. Kumpata mvaaji wa viatu vya Kinana haiwezi kuwa kazi kubwa,” alisema.
Sababu za Kinana kujiuzulu
Hata hivyo, Dk Kabobe alisema uamuzi wa Kinana kujiuzulu umechochewa na dhamira ya kupumzika kutokana na umri wake, lakini kuruhusu mabadiliko ndani ya chama hicho.
Alisema Kinana ni mwanasiasa mkongwe na mahiri, aliyekuwa kwenye siasa za ushindani tangu mwaka 1995 akiwa Meneja wa Kampeni wa Rais wa awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa.
“Anaijua siasa anaijua CCM vizuri, kuondoka kwake nakupa tafsiri mbili. Kupumzika maana katumika muda mrefu na umri umekwenda.
“Kuruhusu mabadiliko ndani ya chama ili kijipange vema zaidi kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani,” alisema.
Hoja zinazofanana na hizo, zilitolewa pia na mwanazuoni wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Mohamed Bakary aliyetaja umri na upepo wa kisiasa wa wakati husika.
Kuhusu umri, mwanazuoni huyo alifafanua katika siasa mtu binafsi anapofikia umri fulani anaamua kwa utashi wake kupumzika katika nafasi za uongozi.
“Kinana ana miaka zaidi ya 70 sasa (71), amekitumikia chama na Serikali kwa muda mrefu na unafika wakati mtu anaona hana sababu ya kuendelea. Badala ya kusubiri apumzishwe anajitathmini anaona apumzike mwenyewe,” alisema.
Kupumzika huko, Profesa Bakary alisema hakuna maana ya kukaa pembeni kabisa, bali ni kujiondoa kwenye nafasi ya uongozi, huku akiendelea kutumika na chama kama mshauri.
Sababu nyingine kwa mujibu wa mwanazuoni huyo ni hali ya siasa ya wakati husika, akisema pengine kujiuzulu kwake kumechochewa na ukaribu alionao na January Makamba na Nape Nnauye ambao Julai 21, walitenguliwa katika nyadhifa zao.
“Kinana anatajwa kuwa karibu na kina Makamba na Nape na aliwalea kiuongozi, Pengina kunakuwa na hali ya kutiliana mashaka kwa hiyo mtu kama yeye anasoma alama za nyakati anaamua kuondoka kabla ya kuondolewa ili kulinda heshima yake,” alieleza.
Kuondoka kwa Kinana katika uongozi wa CCM, alisema unakifanya chama hicho kuzikosa busara zake akiwa ndani ya nafasi, lakini vijana waliopo watakosa la kujifunza kutoka kwake.
Lakini kwa upande mwingine, alieleza kuondoka kwake ni fursa kwa vijana ambao watakuwa na nguvu zaidi au wazee walio na umri wa chini yake kuipata nafasi hiyo.
“Anavyoondoka kiongozi mmoja anaingia kiongozi mwingine na kwa asili ya CCM kuondoka sio pigo atakuja mtu ataendelea pale pale alipoishia yeye,” alisema.
Huyu ndiye Pinda
Pinda alizaliwa Agosti 12, mwaka 1948 mkoani Katavi na baadaye alipata elimu ya msingi katika Shule za Kakuni na Kaengesa mkoani Rukwa kuanzia mwaka 1957 hadi 1964.
Baadaye alijiunga na shule ya sekondari St. Francis ambayo kwa sasa inafahamika kama Pugu kwa ajili ya elimu ya sekondari mwaka 1965 hadi 1968, kisha shule ya sekondari Musoma kwa ajili ya kidato cha tano na sita.
Shahada yake ya kwanza ilikuwa katika sheria, aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) mwaka 1971 hadi 1974.
Alipohitimu shahada yake aliajiriwa kuwa Mwanasheria katika Wizara ya Sheria alikohudumu kwa miaka minne, kabla ya baadaye kuhamishiwa Ikulu akiwa Katibu Msaidizi wa Rais wa wakati huo, Julius Nyerere.
Mwanzo wake wa maisha ya siasa ulikuwa mwaka 2000 alipogombea na kushinda ubunge wa Mpanda Mashariki, wadhifa uliompa uteuzi wa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) chini ya Rais Benjamin Mkapa.
Baadaye alipanda cheo na kuwa waziri kamili katika wizara hiyo hiyo ya Tamisemi hadi wakati wa Serikali ya awamu ya nne chini ya Jakaya Kikwete na baadaye mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu akimrithi Edward Lowassa aliyejiuzulu.
Wasira
Kati ya wanaotajwa Steven Wasira pengine ndiye mwenye umri mkubwa zaidi kuwazidi wengine, alizaliwa mwaka 1945, Bunda mkoani Mara.
Elimu yake ya msingi aliipata katika shule tatu tofauti, ambazo ni Bariri, Nyambitilwa na Kisangwa kuanzia mwaka 1956 hadi 1963.
Mwaka 1964 hadi 1967 alisoma sekondari katika Chuo cha Ukufunzi Uingereza na kuhitimu kidato cha nne, na hapo hapo ukurasa wa safari yake ya kisiasa ulianza kufunguka.
Alipohitimu kidato cha nne, Wasira alianza kukitumikia chama cha TANU akiwa Katibu wa Wilaya mwaka 1967 hadi 1973 na mwaka 1975 hadi 1982 alihudumu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Baadaye mwaka 1982 aliteuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania Washington DC na akiwa huko alisema na kuhitimu Shahada ya kwanza ya Uchumi na Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Amerika hadi mwaka 1985.
Aliendelea na Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Umma kati ya mwaka 1985 hadi 1986 na aliporejea nchini kuendelea na utumishi wa uwakilishi wa wananchi, aliteuliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani mwaka 1990 hadi 1991.
Kati ya mwaka 1993 hadi 1995 alisoma tena Shahada ya Uzamili ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Amerika.
Ndani ya CCM, amekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) tangu mwaka 2007 na mwaka 2012. Pia amekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tangu mwaka 2011 na tena 2013 hadi sasa.
Akiwa na umri wa miaka 25, Wasira alianza kutumikia wadhifa wa ubunge, hii ilikuwa mwaka 1970 aliposhinda ubunge wa Mwibara na akaongoza hadi mwaka 1975 huku Rais Julius Nyerere akimteua kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
Mwaka 1985, Wasira aligombea na kushinda ubunge wa Bunda na kisha aliteuliwa Rais Mwinyi kuwa Naibu Waziri wa Serikali za Mitaa na baadaye Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo mwaka 1989 hadi 1990.
Kipenga cha vyama vingi kilipopulizwa mwaka 1995, Wasira alihitaji kuwaongoza wana Bunda lakini akaangushwa kwenye kura za maoni za ndani ya CCM na Jaji Joseph Warioba (Waziri Mkuu na Makamu wa Rais mstaafu).
Wasira hakuridhishwa na ushindi wa Warioba na aliamua kuihama CCM na kwenda NCCR Mageuzi wakati huo ikiwika na akachaguliwa kwa kura 18,815 dhidi ya 17,527 za Warioba na hivyo akawa mbunge kupitia NCCR.
Warioba alikata rufaa Mahakama Kuu nayo ikatengua ubunge wa Wasira mwaka 1996 baada ya kujiridhisha kuwa kulikuwa na rafu nyingi zilizofanyika ikiwamo matumizi ya rushwa na ikampiga marufuku kugombea kwa miaka kadhaa.
Wasira alikata rufaa mara kadhaa na kushindwa. Mahakama ya Rufaa ilikubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu.
Uchaguzi wa marudio ulipofanyika mwaka 1999 Wasira alikuwa amekwishatangaza kuihama NCCR kutokana na siasa za ugomvi na mara hii alimuunga mkono mgombea wa UDP, Victor Kubini lakini mara baada ya uchaguzi huo aliamua kurejea CCM.
Alirejea katika ulingo wa siasa mwaka 2005 na kushinda kura za maoni ndani ya CCM na akapitishwa kugombea ubunge wa Bunda alikopita bila kupingwa.
Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Maji Januari 2006 hadi Oktoba 2006, baadaye Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika hadi mwaka 2010.
Amewahi kuwa Waziri wa Tamisemi na mwaka alikuwa miongoni mwa watiania ya urais kupitia CCM mwaka 2015.
Bulembo
Katika siasa za CCM Bulembo alipata umaarufu zaidi mwaka 2012 aliposhinda uchaguzi wa ndani wa chama hicho wa nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi.
Uchaguzi huo ulifanyika kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Athuman Mhina aliyefariki dunia mwaka 2011 na kuacha wazi wadhifa huo kwa takriban mwaka mzima.
Umaarufu zaidi katika siasa uliota mizizi mwaka 2015 alipoteuliwa kuwa Meneja wa Kampeni za aliyekuwa mgombea urais wa CCM wa wakati huo, John Magufuli.
Baada ya uchaguzi, Bulembo aliteuliwa kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,nafasi aliyohudumu mwaka 2015 hadi 2020.
Ukiachana na nafasi hiyo, Juni 13, mwaka huu Bulembo aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mshauri wake katika Siasa na Uhusiano wa Jamii.
Sumaye
Alizaliwa mwaka 1950, alihudumu kwa nafasi ya ubunge tangu mwaka 1983 hadi mwaka 2005, kadhalika amekuwa sehemu ya baraza la mawaziri akiongoza wizara ya Kilimo, Mifugo na Ushirika.
Mwaka 1995 hadi 2005 Sumaye alikuwa Waziri Mkuu na ndiye anayetajwa kuhudumu wadhifa huo kwa muda mrefu zaidi ya wengine.
Sumaye naye alikuwa mmoja wa watia nia ya urais mwaka 2015 na hakufanikiwa kuchaguliwa katika mchakato wa ndani ya chama chake, baadaye alikihama CCM na kuhamia Chadema.
Alishiriki kampeni za urais ndani ya Chadema akimnadi Edward Lowassa na baadaye mwaka 2019 alitangaza kuachana na siasa za vyama. Hiyo ilikuwa baada ya kushindwa uenyekiti wa Kanda ya Pwani wa Chadema.
Haukuisha hata mwaka, Sumaye alitangaza kurejea ndani ya chama chake cha zamani, CCM hadi sasa.
|
Magumu yanayowakabili wafanyabiashara huenda yakapata mwarobaini, baada ya Serikali kutangaza mpango
|
Magumu yanayowakabili wafanyabiashara huenda yakapata mwarobaini, baada ya Serikali kutangaza mpango wa kuunda kamati ya maboresho ya mifumo ya kikodi.
Kamati hiyo itakayoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhusisha wajumbe kutoka sekta ya umma na binafsi, inatarajiwa kuja na mapendekezo yatakayofumua mifumo ya kikodi itakayohusisha sera na sheria.
Msingi wa kuundwa kwa kamati hiyo, ni kile kilichoelezwa na wafanyabiashara juu ya mifumo iliyopo, wakilalamikia kufungiwa akaunti za benki, kuchukuliwa fedha bila utaratibu sahihi, kadhalika kufungiwa kwa mashine za EFD.
Mifumo ya kikodi pia imewahi kulalamikiwa na wawekezaji kutoka nchi tisa waliowekeza nchini, ambao Juni mwaka huu waliomba kikao na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Miongoni mwa malalamiko yaliyoibuliwa nao katika barua ya ombi la kikao hicho ni makadirio ya kodi yanayozidi uhalisia hali inayosababisha baadhi yao kupata changamoto katika uendeshaji wa biashara.
Wawekezaji hao ni kutoka mataifa ya Marekani, Uingereza, Uholanzi, Ufaransa, Ubelgiji, Canada, Korea, Sweden na Ujerumani na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, January Makamba alikubali kikao hicho.
Katika hali ya kujibu changamoto hizo, Rais Samia ametangaza kuunda kamati ya maboresho ya masuala ya kikodi itakayohusisha wadau mbalimbali.
Rais Samia alitangaza kuunda kamati hiyo jijini Dar es Salaam jana, katika mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), lililofanyika Ikulu.
“Serikali imedhamiria kuondosha changamoto tutaunda kamati, itakayoshirikisha wajumbe kutoka serikalini na sekta binafsi, mpitie kwa undani alafu mtuletee mapendekezo na ushauri mtakaouona unafaa kwa nchi yetu kwenda na mfumo huo wa kodi,” alisema.
Kamati hiyo kwa mujibu wa mkuu huyo wa nchi, haitaishia kuangalia mifumo ya kikodi pekee itagusa hata sheria na sera za kikodi.
Upatikanaji wa fedha za kigeni na kuongeza uwezo wa kuuza bidhaa za Tanzania nje ya nchi ni majukumu mengine yanayotarajiwa kutekelezwa na kamati hiyo itakayoundwa.
“Wengi wamefurahia kwamba Serikali imetambua hata yale mazao yaliyokuwa yanaitwa ya chakula sasa yote ya biashara,” alisema.
Taarifa ya kuundwa kwa kamati hiyo ilichochewa na malalamiko ya wafanyabiashara yaliyowasilishwa na mwakilishi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Ali Suleiman Amour katika mkutano huo.
Katika taarifa yake hiyo alisema kuna mapungufu katika usimamizi wa sheria ya usimamizi wa kodi inayosababisha changamoto kwa wafanyabiashara.
Baada ya TPSF kukaa na wafanyabiashara, alisema walibaini walikuwepo ambao hawakuwa na madeni kabisa ya kodi na hivyo matumizi ya agency notice haikuwa sahihi kwao.
Kwa mujibu wa Amour, makosa yalibainika kwa TRA hasa katika utunzaji wa kumbukumbu.
“Mapungufu katika uthaminishaji wa mizigo bandarini na kamata kamata zilizokuwa zinaendelea Kariakoo zilishinikiza utoaji wa risiti Kariakoo. Tunatarajia utaratibu mpya usimamia vema,” alisema.
Sambamba na hayo, alisema taasisi hiyo imebaini kuongezeka kwa biashara za magendo na bandia ambazo kimsingi zinaathiri ushindani nchini.
Alieleza kufurahishwa na uanzishwaji wa ofisi ya msuluhishi wa malalamiko ya kikodi tangu mwaka 2019 na mwaka 2022 ilianza kufanya kazi.
Lakini, alipendekeza itoke chini ya TRA kwa kuwa itashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuwa linasimamiwa na yule yule anayetoza kodi.
Hoja nyingine aliyoiibua ni sekta binafsi kwa sasa inaratibiwa na wizara zaidi ya moja, akitaka kuwepo moja itakayotambulika kwa ajili yao.
Amour pia, alipendekeza umuhimu wa kuongeza wigo wa walipakodi akitaka angalau wafikie milioni 6.1, badala ya milioni mbili wa sasa.
“Katika hao milioni mbili ni robo yake ndiyo waadilifu na wanaolipa hiyo kodi,” alieleza.
Upatikanaji wa dola ni changamoto nyingine iliyoibuliwa na Amour, akisema unaathiri biashara, ununuzi wa malighafi za viwandani na hata upatikanaji wa mafuta.
Alitaka matumizi ya dola hasa kwa Serikali yanapungue kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini na sio kila mwaka kununua magari mapya kwa watumishi.
Pamoja na mapendekezo hayo, alitaka wafanyabiashara wasigeuzwe maadui, kutengenezewa mizengwe na figisu pale wanapotoa ripoti ya masuala ya rushwa na upotevu wa mapato.
Alilieleza hilo akirejea tukio alilodai lilitokea mkoani Arusha, mfanyabiashara mmoja wa TPSF, akifafanua Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amelishughulikia hilo kwa ukamilifu.
Maazimio
Akisoma maazimio ya mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNDC), Dk Godwill Wanga alisema pamoja na azimio la kuundwa kwa kamati hiyo, pia wamekubaliana kuondoa urasimu.
Alieleza kila wizara na idara ya Serikali imeazimiwa kutekeleza falsafa ya R4 kwa viongozi wa umma kuhakikisha wanakuwa wawezeshaji wa biashara na sio vikwazo.
Azimio lingine, alisema ni kukamilisha sera ya Wafanyabiashara wa Chini na Wadogo (SME) na kujengeana uwezo na kuanza kutekeleza nishati jadidifu.
Kwa mujibu wa Dk Wanga, iliazimiwa pia kila risiti inayotolewa na TRA iambatane na bahati nasibu, akieleza jambo hilo linahitaji kuangaliwa zaidi.
Kuboreshwa kwa mpango wa kurahisisha mazingira y biashara wa kila mwaka ni azimio lingine lililosomwa na Dk Wanga katika mkutano huo.
Pia, mkutano huo uliazimia kuboresha mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi na lioanishwe na suala la ‘local content.’
Kutokana na maazimio hayo, Rais Samia alieleza kila Waziri kuhakikisha anachukua linalomuhusu na kupanga muda wa kukaa na sekta binafsi kwa ajili ya kutafutia ufumbuzi.
Alisisitiza maazimio hayo yafanyiwe kazi haraka ili kitakapofika kikao cha mwakani itolewe taarifa ya utekelezaji wake.
“Kamati zitakazoundwa wakimaliza mambo yao hatua zichukuliwe ili tutakapokutana mwakani tuseme serikali imefanya hivi na sekta binafsi imefanya hivi,” alisema.
Hata hivyo, alisema ni adhma ya Serikali kujenga mahusiano mazuri na yenye manufaa na sekta binafsi ili kuongeza mapato kupitia biashara.
Sambamba na hayo, mkuu huyo wa nchi amesema anafahamu uwepo wa changamoto katika maeneo mbalimbali na kwamba ataendelea kuyafanyia kazi.
Kwa mujibu wa Rais Samia, anafahamu uwepo wa baadhi ya watendaji serikalini wasiofahamu dhamira ya kuwezesha biashara na uwekezaji.
“Nafahamu changamoto ya uratibu kati ya sekta moja na nyingine, gharama za stempu za kodi, ucheleweshaji wa vibali mbalimbali na wakati mwingine kutoshirikishwa (kwa wafanyabiashara) kwenye baadhi ya mabadiliko,” amesema.
Anaamini ufumbuzi wa changamoto mbalimbali utapatikana na kwamba dhamira itaeleweka.
|
Chama cha ACT-Wazalendo kimesisitiza msimamo wake wa kupinga uchaguzi kufanyika kwa siku mbili visiw
|
Chama cha ACT-Wazalendo kimesisitiza msimamo wake wa kupinga uchaguzi kufanyika kwa siku mbili visiwani Zanzibar, kikitaka ufanywe kwa siku moja.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho Othman Msoud Othman, hawatakubali jambo kama hilo liendelee kufanyika visiwani humo.
Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais visiwani humo, anakuja na hoja hiyo ilhali ni takwa la kisheria iliyotungwa kwa shabaha ya kutoa fursa kwa makundi mbalimbali kupata fursa ya kupiga kura.
Mara nyingi katika uchaguzi wa Zanzibar siku ya kwanza, hutumiwa na watumishi wenye kazi maalum serikalini vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kupiga kura kisha siku ya pili ndiyo wananchi wote.
Mtindo huo wa upigaji kura umekuwa ukipingwa na baadhi ya wanasiasa wakiwemo wa vyama vya upinzani, wakidai ni mbinu zinazotumiwa na chama tawala kupanga matokeo.
Othman alieleza hayo jana, katika mkutano wa hadhara wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini ikiwa mwanzo wa mikutano waliyoipa jina la bandika bandua inayofanyika kwa siku nne mfululizo Pemba.
Katika mkutano huo, amesema chama hicho kilishaelekeza kuondolewa utaratibu wa uchaguzi kufanyika kwa siku mbili, lakini hadi sasa Serikali haijajibu lolote.
“Kama watu wanajiamini wanatakiwa wazingatie katiba, waingie uwanjani masanduku ya kura ndio yaamue mwenye nguvu badala ya kutumia nguvu za kidola na mamlaka,” amesema.
Kwa mujibu wa Othman, jambo hilo linairudisha nyuma Zanzibar na kwamba iwapo Serikali hitatekeleza matakwa yao, hata uchaguzi wa siku moja pengine usifanyike.
“Ndugu zangu nawaambia kila mtu nyuso zetu zinaonyesha tumechoka, haya yanaturudisha nyuma kila siku hatuendi mbele, tunachowaambia hatuwezi kukubali haya viongozi wenu, hatutofanya uchaguzi sio tu wa siku mbili, hata wa siku moja na robo hautafanyika,” amesema.
Amesisitiza msimamo huo haujalishi mamlaka ina jeshi, polisi na hata mgambo, kinachotakiwa ni uchaguzi ufanywe kwa siku moja.
Kwa sababu chama hicho kimeamua kuondoa dhuluma, Othman amesema hawatakubali aliyesimamia uchaguzi wa mwaka 2020 ndiye asimamie wa mwaka huu.
Amesema hawatakaa tena kufanya mazungumzo, bali wataamua kupitia sanduku la kura.
Ingawa Othman hakuweka wazi mazungumzo hayo, ni Dhahiri anachokilenga ni yale yanayofanyika baada ya chaguzi yanayohusisha uundaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
“Mazungumzo yataishia kwenye sanduku la kura, ni wajibu wetu, kazi yetu kusimamia matakwa ya wananchi wa Zanzibar ili nchi yao itoke kwenye uchafu huu, itoke kwenye ujinga huu ipate kwenda mbele kwasababu uwezo wa kufanya hivyo tunao,” amesema.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Zanzibar ina uwezo kupata maendeleo zaidi ya mataifa mengi, lakini kukosekana kwa viongozi waadilifu ndiko kunakokwamisha suala hilo.
Katika hotuba yake hiyo, aliirejea bajeti ya Serikali akisema makusanyo ni Sh1.5 trilioni, kati ya hizo Sh900 bilioni zinalipa mshahara na Sh300 bilioni zinalipa madeni, hakuna fedha zinazobaki kwa ajili ya maendeleo.
Kwa sababu hiyo, amesema visiwa hivyo vitabaki kuwa masikini kama mfumo hautabadilishwa.
Ametaja jambo lingine linalokwamisha maendeleo visiwano humo ni kukosekana mamlaka ya kujiamulia mambo yake yenyewe na vitu vingi vimeingizwa katika masula ya muungano akitaja zaidi ya 41.
Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na ushuru wa forodha, gesi na mafuta, sarafu, ushuru wa bidhaa, bandari, elimu ya juu, usafiri wa anga, takwimu, leseni za viwanda na bandari.
“Mambo 41 yote yapo kwenye Muungano wewe unasema una serikali na kujikweza nipo kwenye chama tawala, unatawalaje? Wengine wanasema maneno lakini hawajui hata wanayosema, leo ukiambiwa hauna mamlaka katika mambo hayo maana yake hauna mamlaka katika kuendesha uchumi wa nchi yako,” amesema.
Wanaposema wanapambania mamlaka kamili, amesema ni kwa sababu wanajua uhalisia wa mambo na kwamba wakipata mamlaka hayo watajikwamua kutoka kwenye umasikini.
“Haiwezekeni wewe umekabidhiwa nchi unajua nchi hii inadhulumiwa lakini hauna habari, sasa kama tumekabidhi kwa watu kupoteza maisha lakini hauna habari bila kuwa na mamlaka hakuna safari tutabaki katika ufukara na umasikini wa milele, lakini sisi hatutakubali iwe hivyo,” amesema.
Awali, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Zanzibar, Ismail Jussa amesema Pemba ndiyo mwalimu wa siasa visiwani humo, hivyo wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika vuguvugu hilo la mabadiliko.
Amesema baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2020, Maalim Seif Sharif Hamad alizunguka kutafuta maoni kwa wananchi na wakakubaliana kuingia katika SUK kwa masharti ambayo yameshindwa kutekelezeka.
Amesema Maalim Seif (aliyefariki dunia Februari 17, 2021) alikuwa akisisitiza umoja, mshikamano na utekelezaji wa makubaliano lakini alifariki dunia bila hayo kufanikiwa.
Hata hivyo, amesema licha ya Maalim Seif kufariki chama hicho hakijapoteza kwani kimempata mrithi sahihi wa nafasi yake.
“Maalim kaondoka saa tumempeleka Othman ili 2025 akawafundishe namna Serikali inavyoongozwa,” amesema.
|
Suala la kupatikana kwa Katiba mpya, ulinzi wa rasilimali za taifa na matukio ya utekaji ni miongoni
|
Suala la kupatikana kwa Katiba mpya, ulinzi wa rasilimali za taifa na matukio ya utekaji ni miongoni mwa mambo yaliyojenga msingi wa hoja za wagombea wengi wa urais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).
Hoja hizo zilikuwa mithiri ya turufu kwa kila mgombea alipojibu maswali yaliyoulizwa katika mdahalo uliohusisha wagombea wote sita wa nafasi hiyo ya kuwaongoza mawakili.
Kati ya majibu ya wagombea hao kuhusu mambo hayo, wapo waliyoonyesha mikakati ya kupata ufumbuzi wake, huku mmoja akijitenganisha nayo kwa kile alichoeleza hana sababu ya kuwadanganya wapigakura kwa kuwa si jukumu la Rais wa TLS kuyasimamia hayo.
Mdahalo huo uliwahusisha mawakili sita wanaowania wadhifa huo, ambao ni Sweetbert Mkuba, Revocatus Kuuli, Boniface Mwabukusi, Paul Kaunda, Ibrahim Bendera na Emmanuel Muga.
Mengi yaliunogesha mdahalo huo, lakini unasaba wa Wakili Mkuba na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ulijenga maswali mengi dhidi yake na katika majibu yake, aliweka wazi dhamira yake ya kuwania nafasi hiyo ni kuwawakilisha mawakili na sio CCM.
Alikwenda mbali zaidi na kueleza, kila mgombea ana chama chake cha siasa ambayo ni haki ya kikatiba, kwa sababu urais wa TLS ni kwa maslahi ya mawakili hauoni uanachama wake wa CCM ukiathiri utendaji wake atakapokuwa Rais wa mawakili.
Wagombea wote sita watapima nguvu ya sera na ushawishi wao kwa mawakili wenzao Agosti 2, mwaka huu, mkoani Dodoma, ambayo ndiyo siku ya uchaguzi.
Huo ni muhtasari wa machache kati ya mengi yaliyojiri jana katika mdahalo wa wagombea urais wa TLS, uliorushwa mubashara na kituo cha Luninga cha Star Tv kupitia kipindi cha Medani za Siasa ulioanza saa 3:30 hadi 6:00 usiku.
Katiba, utekaji, rasilimali
Ahadi ya Bendera atakapopewa ridhaa ya kuwa rais wa chama hicho kuhusu Katiba, ni kuishauri Serikali ihakikishe inafanya marekebisho katika kasoro zilizopo.
Alizitaja baadhi ya kasoro hizo ni katika usimamizi wa haki za binadamu ikiwemo haki ya kuandamana na kukusanyika, kwa maoni yake haoni sababu ya kuombewa kibali kwa Polisi.
“Hakuna sababu ya kuomba kibali cha kuandamana polisi. Na nguvu ya polisi katika kumtuhumu mtu iondolewe, haya ni mambo nitakayoishauri Serikali,” alisema.
Mambo mengine, alisema ni utolewaji wa dhamana uwe chini ya mamlaka ya mahakama na sio polisi au mwingine yeyote.
Kuhusu matukio ya utekaji, pamoja na kuonyesha kukerwa nayo, pia alisisitiza atakapokuwa Rais ataishauri Serikali kuweka mazingira ya upatikanaji haraka wa taarifa za vitendo hivyo.
Katika ulinzi wa rasilimali za taifa, alisema atashirikiana na baraza la uongozi la TLS kuishauri Serikali kusimamia hilo na ikishindikana watatumia vyombo vinavyostahili ikiwemo kwenda mahakamani.
Ahadi ya Paul Kaunda haikupishana sana na Bendera kuhusu kupatikana kwa katiba mpya. Isipokuwa Kaunda yeye aliahidi kuishauri Serikali iendelee pale ilipoishia katika rasimu ya Katiba ya mwaka 2014.
Rasimu inayozungumzwa na Kaunda ni ile ambayo Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho yake alikuwa Jaji Joseph Warioba mwaka 2014.
Mchakato huo ulikwama bungeni kwa kile kilichoelezwa na wabunge wa vyama vya upinzani kuwa, CCM inaingiza maslahi yake ndani ya mabadiliko hayo.
Akijibu swali kuhusu katiba mpya Kaunda alisema: “Tayari kuna rasimu ya katiba na kwamba nitakapokuwa Rais nitaishauri Serikali kuendelea na mchakato wa ile ya Jaji Warioba.”
Kuhusu matukio ya utekaji, alisema ataishauri na kuisisitiza Serikali iunde tume ya kijaji kushughulikia masuala hayo.
Alijibu hilo akitolea mfano wa tume iliyoundwa na Baba wa Taifa, Mwaliko Julius Nyerere baada ya mauaji ya wazee na ikasababisha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi ajiuzulu.
“Nitakapokuwa Rais nitahakikisha nashinikiza na kuishauri Serikali kuunda tume ya kijaji ije ifanye uchunguzi kujua nini sababu,” alieleza.
Msimamo wa wakili Mkuba kuhusu Katiba ni kile alichoeleza kuna mapungufu katika Katiba iliyopo na kwamba atashauri kufanywa marekebisho.
Katika hoja hiyo, Mkuba alisema kwa wakati uliopo sasa kunahitajika kufanywa marekebisho ya Katiba kwa kuwa iliyopo ilifungwa kuendana na mahitaji ya zamani.
Kama ilivyo kwa Kaunda, Mkuba naye alisema ataishauri Serikali kukwamua mchakato wa katiba uliokwama mwaka 2014 ili uendelee.
Kwa upande wa matukio ya utekaji, alisema anakerwa na kuikemea vikali kutokea kwake na kwamba atakapopewa ridhaa ya kuwaongoza mawakili ataishauri Serikali kuunda sheria kali dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo.
Kuhusu ulinzi wa rasilimali za taifa, alieleza atakapokuwa Rais ataishauri Serikali kutumia vizuri mawakili waliopo katika majadiliano ya masuala ya mikataba ya kimataifa ili kuleta tija.
“Tatizo la taifa kukosa faida katika mikataba linasababishwa na kwamba mikataba hiyo inaingiwa kibiashara na Tanzania haina nguvu ya kujadiliana vema ili ipate faida,” alisema.
Wakili Muga yeye kuhusu Katiba mpya, alisema haoni kama Rais wa TLS ana mamlaka ya kufanikisha upatikanaji wake, hivyo kuahidi hilo ni kuwaongopea wapiga kura.
Vivyo hivyo, alieleza hata katika matukio ya utekaji, akisema aghalabu hufanyika gizani na Rais wa TLS hana mamlaka ya kudhibiti isipokuwa atajadiliana na wanachama kuona namna ya kutatua.
Kuhusu rasilimali za nchi, alisema kunahitajika juhudi za pamoja kuanzia kwa wananchi kisha mawakili watasimama nyumba yao kufanikisha ulinzi wake.
“Kwenye ulinzi wa rasilimali si jambo la mtu mmoja, mwananchi naye ana nafasi yake, wananchi wakisimama nasi mawakili tukawa nyuma yao tutafanikiwa,” alisema Muga.
Kuuli naye msimamo wake ni kupatikana kwa Katiba mpya, akiahidi kusimamia kifungu cha nne cha sheria ya mawakili, kitakachompa jukumu la kuishauri Serikali.
Kuhusu masuala ya utekaji, alieleza tatizo lipo kwa idara ya usalama wa taifa inayojikuta ikisubiri matukio yatokee ndiyo iyakabili badala ya kuyadhibiti kabla
Alisema atakapokuwa Rais wa TLS, ataishauri Serikali juu ya mwenendo mzuri wa kuyakabili matukio hayo.
Kama atakavyoshauri kuhusu matukio ya utekaji, alisema ataishauri pia katika ulinzi wa rasilimali za taifa.
Suala la upatikanaji wa Katiba mpya kwa Wakili Mwabukusi, alisema haitakuwa mzaha, ataliomba kwa njia zote ikiwemo kuwatumia wananchi kuisukuma utekelezwaji wake.
Kwa mujibu wa Mwabukusi, hatatumia njia moja kufanikisha mambo yenye maslahi ya taifa, yapo atakayoshauri na mengine kwenda mahakamani na hata kuwaleta wananchi.
“Kuna jambo la kushauri na kuna vingine tutawaambia Watanzania, tuingie kutafuta haki hatutatumia njia moja kupata haki,” alisema.
Vivyo hivyo, alieleza ndivyo itakavyofanyika katika kukabili matukio ya utekaji huku ulinzi wa rasilimali za taifa, akiahidi kushughulikia kama ambavyo amekuwa akifanya hivyo kabla ya kuwa rais.
Kuhusu ulinzi wa rasilimali hizo, Mwabukusi alieleza kuna sheria nzuri, lakini imekosa wasimamizi imara na atakachokifanya iwapo atapewa ridhaa ni kushinikiza utekelezwaji wake kwa mbinu mbalimbali.
Kwanini wachaguliwe wao
Swali la kwanini wao ni bora kuwa rais wa TLS liliulizwa kwa kila mgombea katika mdahalo huo na kwa upande wa Bendera alijigamba kwa uzoefu wa miaka 18 ya kutekeleza shughuli za uwakili.
Ubora wake kwa mujibu wa Bendera haujengwi na uzoefu wa kutumikia uwakili pekee, bali unajengwa pia na wasifu wake wa kuongeza kampuni mbalimbali za uwakili.
“Najiamini kwa sababu ni mkongwe kwenye taaluma uwakili na nimewahi kuziongoza kampuni za mawakili, nitatumi uzoefu wangu kuiongoza TLS,” alieleza.
Jibu la uzoefu katika uongozi lilitolewa pia na Kaunda, akijinadi kuwa Makamu wa Rais wa mawakili Afrika na kuwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Uongozi wa TLS.
Hakuishia kuwa mzoefu tu, bali alisema ameshiriki kushauri mageuzi ya kitaasisi hasa kuleta utaratibu wa kuundwa kwa kanzidata ya mawakili na upigaji kura kwa njia ya kielektroniki.
“Kama nimeyafanya hayo nikiwa mjumbe wa baraza la uongozi, nikiwa Rais nitafanya zaidi,” alisema.
Uzoefu wa uongozi pia, ulitajwa na Mkuba aliyesema amekuwa na nafasi hizo tangu akiwa shule ya msingi, sekondari na hati chuo kikuu, hivyo katika kuongeza hapaswi kutiliwa mashaka.
Ubora wake, alieleza unatokana na misimamo thabiti ambayo aghalabu huwa nayo na ndiyo inayofanya achaguliwe katika nafasi mbalimbali, hivyo anaomba akafanye hivyo na TLS.
Kuimarisha ushirikiano kati ya TLS na taasisi nyingine na kutengeneza fursa za mawakili wachanga, kadhalika kusimamia maslahi ya mawakili ni mambo mengine aliyoyataja kama sehemu ya ubora unaomtofautisha na wengine.
Taaluma mseto alizonazo Muga, ndizo alizozitaja kama turufu bora kwake tofauti na wagombea wengine na kwa sababu hiyo anastahili kuwa Rais wa TLS.
Mgombea huyo alisema mbali na taaluma ya uwakili, yeye pia ni mwanahabari aliyetumikia vyombo vya habari vya The Citizen, Daily News na BBC.
Taaluma hizo kwa mujibu wa Muga, zimemfanya kuwa na maarifa mseto, lakini amewahi kuwaongoza mawakili katika Mkoa wa Dar es Salaam, hivyo suala la uzoefu nalo hapaswi kutiliwa shaka.
Kuuli yeye alilijibu swali hilo kwa kile alichoeleza, tofauti yake na wagombea wenzake ni uzoefu wa kimataifa aliokuwa nao, akisema anataka kuleta uzoefu wa kimataifa katika taaluma ya uwakili.
Alijinadi kwa wasifu wake wa kuwa wakili wa mahakama mbalimbali za kimataifa ikiwemo ya haki za binadamu na Afrika Mashariki.
“Nitakwenda kusimamia utawala wa sheria na heshima ya chama na hadhi na heshima ya wanachama, nina uzoefu wa kutosha,” alisema.
Kwa upande wa Mwabukusi, uzoefu wa miaka 14 katika uwakili na miaka lukuki katika sekta ya sheria akaanza kuwa ofisa sheria ndani ya Serikali ni moja ya turufu zinazomtofautisha na wenzake.
Anajiona kuistahiki nafasi ya urais wa TLS kwa kile alichoeleza, amekuwa mdau wa haki za binadamu na utawala bora, kadhalika mtetezi wa wananchi katika maisha yake yote ya taaluma ya uwakili.
Alishajihisha wasifu wake huo na rejea ya harakati alizowahi kuzifanya ikiwemo kupinga baadhi ya mambo yanayofanywa na Serikali kwa kuvunja haki za wananchi na maslahi ya taifa.
“Naomba ridhaa nikayafanye haya nikiwa kiongozi wa mawakili. Nitasimamia vema na kuishauri Serikali kwa mbinu zote kuhakikisha maslahi ya taifa na wananchi yanapatikana,” alieleza.
Mengine yaliyoibuka
Katika mdahalo huo, Bendera aliulizwa iwapo kuna analojifunza kutokana na uamuzi wa Rais wa Marekani, Joe Biden kuamua kujiondoa katika harakati za kuwania urais kwa sababu ya umri wake.
Kwa mwonekano kati ya wagombea wote, Bendera ndiye aliyeonekana kuwa na umri mkubwa zaidi na alijibu bado ana umri unaostahili kuwania nafasi hiyo.
Jambo lingine ni kwa Muga aliyesema haoni kama Rais wa TLS anaweza kudhibiti vitendo vya utekaji na kuleta Katiba mpya na kwamba hayuko tayari kuwadanganya wapiga kura.
Undani kuhusu hoja tatu
Katiba mpya, utekaji na usimamizi wa rasilimali ndizo pengine zilizoonekana kuwa hoja zilizozungumzwa na wagombea wote na msingi wake ni huu.
Katiba mpy inabebwa na historia yake. Ni takwa linalokaribia muongo na nusu sasa, imewahi kuombwa na vyama vya siasa, wananchi, asasi za kiraia tangu enzi na enzi bila mafanikio.
Dalili za kupatikana kwake zilionekana wakati wa uongozi wa Jakaya Kikwete akiwa Rais wa nchi, alipounda Tume ya Marekabisho yake iliyoongozwa na Jaji Warioba.
Maoni yalikusanywa mchakato ulifanyika, lakini ulikwamia katika hatua za kutamatisha, ambapo wabunge wa upinzani na CCM walitofautiana mitazamo na kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa anataka maslahi binafsi ndani ya jambo hilo.
Alipoingia Rais Samia Suluhu Hassan ilionekana kama unakwamuliwa, mengi yalizungumzwa na ikahitimishwa na msimamo wa Serikali kwamba, inataka itoe elimu kwa wananchi kwanza ndipo ianze mchakato.
Matukio ya utekaji nayo si jambo geni. Wengi wakiwemo maarufu wamepoteza uhai baada ya kutekwa na wengine haijulikani walipo akiwemo, mwanasiasa Ben Saanane na mwanahabari Azory Gwanda.
Kuhusu usimamizi wa rasilimali za nchi ni malalamiko ya kitambo ya mawakili na vyama vya upinzanio vikiituhumu Serikali kugawa rasilimali za nchi bila faida.
|
Uteuzi ni jambo moja, lakini kuitumikia nafasi uliyoteuliwa ni jambo lingine, hiki ndicho kinachowas
|
Uteuzi ni jambo moja, lakini kuitumikia nafasi uliyoteuliwa ni jambo lingine, hiki ndicho kinachowasubiri mawaziri wanne wapya katika wizara mbalimbali ambao tayari wameshateuliwa Julai 21, mwaka huu na kilichobaki ni kutumikia nyadhifa zao.
Ingawa uteuzi aghalabu ni faraja kwa mteuliwa, wadau wa sekta zitakazoongozwa na mawaziri hao wapya, wameonyesha shughuli pevu zinazowasubiri wateule hao.
Wateule hao wapya ni Deogratius Ndejembi aliyetoka Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulevamu) na kuteuliwa katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akimridhi Jerry Silaa.
Mwingine ni Ridhiwan Kikwete aliyetoka kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na sasa ni Waziri mteule wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulevamu), akimrithi Ndejembi.
Balozi Mahmoud Thabit Kombo naye ni miongoni mwa wateule hao, aliyepewa uwaziri katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akimrithi Januari Makamba aliyetenguliwa.
Kadhalika, kuna Jerry Silaa aliyeondolewa katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na sasa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, akimrithi Nape Nnauye ambaye pia uteuzi wake umetenguliwa.
Migogoro ya ardhi na ukiukwaji wa sheria ya ardhi ni machache kati ya mengi yaliyotajwa na wadau wa sekta ya ardhi kama kibarua kinachomsubiri Ndejembi katika wadhifa wake mpya.
Wakati Ndejembi akitarajia kibarua hicho, Kikwete naye anatakiwa kuwa tayari kuweka sawa suala la mikopo na mitaji kwa vijana, bila kutelekeza mpango wa uundaji wa baraza la vijana nchini.
Kibarua cha Balozi Kombo ndicho kilichotabiriwa kuwa chepesi kutokana na uzoefu wa mwanadiplomasia huyo, kwa mujibu wa wadau wa eneo hilo, huku wakimuandaa kuitafsiri diplomasia ya uchumi ambao ndiyo mwelekeo wa Serikali.
Ukistaajabu ya watatu hao, kinachomsubiri Silaa kitakushangaza, wadau wa sekta ya habari wamesema amepokea kijiti katika nyakati ambazo Serikali inachakata uboreshaji wa uchumi katika vyumba vya habari, hivyo hicho ndicho kibarua chake.
Kibarua cha Ndejembi
Kibarua kigumu zaidi kinachomsubiri Ndejembi katika wadhifa wake mpya ni migogoro ya ardhi changamoto ambayo imeonekana kuwasumbua mawaziri wengi waliopita katika wizara hiyo kama anavyofafanua, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Haki Ardhi, Cathbert Tomitho.
Kutokana na wingi wa migogoro hiyo, Tomitho alisema Silaa alijikuta anatumia muda mwingi kuisuluhisha, huku akiacha maeneo mengine yanayoihusu sekta hiyo ikiwemo umilikishwaji.
“Sio kwamba alikosa kipaumbele isipokuwa sekta ya ardhi ndivyo ilivyo,” alieleza.
Ukiachana na kibarua hicho kwa mujibu wa Tomitho, Ndejembi pia ajiandae kusimamia utekelezwaji wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 ambayo kwa sehemu kubwa imekuwa ikikiukwa na ndiyo chanzo cha migogoro.
“Alipokuwa Silaa, alitembelea Bunju na maeneo mengine, malalamiko mengi ni viwanja kumilikishwa zaidi ya mara moja, tujiulize kwa nini manispaa na wizara yenyewe inamilikisha ardhi kwa zaidi ya mara moja, maana yake sheria haifuatwi,” alisema.
Uwajibishaji wa watendaji wa ngazi mbalimbali ndani ya wizara, ni jambo lingine lililotajwa na Tomitho kama jukumu zito linalomkabili Ndejembi katika uwaziri wake wa ardhi.
“Kuna hati miliki feki za ardhi zinatoka na kuna watu ambao ni maofisa kwenye wizara wanahusishwa, nadhani waziri anapaswa kuangalia kwanza watendaji wake,” alieleza Tomitho.
Ndejembi huyo huyo kwa mujibu wa Mwanazuoni wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dk Emmanuel Mchome ajiandae kufanya utambuzi wa umiliki wa ardhi unaopaswa kufanyika wakati wa upimaji na ramani itakayopatikana ibandikwe kwenye ofisi ya Kijiji au Kitongoji kwa miezi mitatu.
Kwa mujibu wa Dk Mchome, ramani hiyo inapaswa kuwa na majina ya wamiliki wa kila ardhi na ukubwa wa eneo wanalolimiliki.
“Kwa kipindi cha miezi hiyo mitatu, kila mmoja atakwenda kuangalia jina lake na ardhi yake, kama atatokea Mwananchi mwenye pingamizi atasema na utawekwa utaratibu wa kusikiliza na kutatua,” alisema.
Alieleza hiyo itasaidia kujua wamiliki halali wa maeneo na hivyo kuepusha utapeli na uuzaji holela wa ardhi.
Ajira, mitaji kwa vijana ni kibarua cha Kikwete
Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Youth Coalition (TYC), Lenin Kazoba alisema mitaji na mikopo kwa vijana ni moja ya jukumu ambalo hatma yake inamsubiri Kikwete katika nafasi yake mpya.
Kwa kuwa upatikanaji wa ajira ni changamoto nchini, Kazoba alisema wizara hiyo inapaswa kuweka mwongozo na mazingira mazuri ya kuwawezesha vijana kupitia mikopo.
Ingawa tayari Serikali imeshazindua mwongozo wa utoaji wa mikopo hiyo kwa makundi manne likiwemo la vijana, Kazoba alisisitiza umuhimu wa usimamizi kuhakikisha kundi hilo linanufika.
“Kulikuwa na mikopo iliyokuwa inatolewa kupitia halmashauri, haikuwa na mwongozo, hatimaye haikuwanufaisha vijana, lakini Kikwete anapokwenda pale ahakikishe anaweka mazingira mazuri,” alieleza.
Ukamilishaji upatikanaji wa sera ya vijana ni jukumu lingine linalomsubiri Kikwete katika wadhifa wake huo mpya.
Kwa mujibu wa Kazoba, hadi hivi sasa sera hiyo haijaonekana katika ajenda za Serikali, pamoja na umuhimu wake hivyo matumaini ya vijana ni kuona Kikwete anakwenda kulifanikisha hilo.
Uanzishwaji wa baraza la vijana ni jambo lingine linalomubiri Kikwete katika wadhifa huo mpya kwa mujibu wa Kazoba.
“Uanzishwaji wa baraza la vijana ni jambo lingine. Kwenye hili changamoto imekuwa katika sheria ambayo hata vijana wenyewe hawaijui, kwa maana sheria ya baraza ya mwaka 2015,” alisema.
Kinachosababisha vijana wasiijue ni kile alichoeleza, mazingira ya kupitishwa kwake, yalifanyika bila kuwahusisha vijana.
Silaa na uchumi katika vyombo vya habari
Licha ya Jerry Silaa kuonekana rafiki wa vyombo vya habari katika nafasi zote za uongozi alizowahi kushika, anakabiliwa na kibarua cha kubadili urafiki huo na kuwa kichocheo cha uimara wa uchumi wa sekta kwa ujumla, kama inavyoelezwa na Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena.
Urafiki wa Silaa na vyombo vya habari ulithibitika kwa kile kilichoelezwa na Meena kuwa, katika majukumu mengi tangu mwanasiasa huyo alipokuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, amekuwa akishirikiana na wanataaluma hiyo.
Mwanahabari huyo Mwandamizi, amesema anachopaswa kukifanya Silaa kwa sasa ni kuubadili uafiki aliokuwa nao kwa vyombo vya habari na aufanye kwa namna ya kupambania maslahi yao na hatimaye kuimarisha uchumi wa sekta husika.
“Vema kwa sasa urafiki wake (Silaa) uingie kwenye kubadilisha uchumi katika vyombo vya habari,” amesema.
Hata hivyo, mwanahabari huyo amesema hata waziri aliyeondolewa (Nape) amefanya mengi kwa maslahi ya taaluma ya habari, kadhalika yapo ambayo hakuyafanya pia.
“Uhalisia Nape alikuwa waziri wa habari alifanya kazi yake aliyotakiwa kuifanya na tunashukuru kwa kile alichokifanya, lakini kuna mambo mengi pia yalimshinda,” amesema.
Kuhusu yaliyomshinda, amesema ni baadhi ya mambo aliyokuwa akijadiliana na kukubaliana na wadau wa sekta ya habari, ambayo utekelezwaji wake haukufanyika.
Lakini Nape huyo huyo, Meena amesema kuna wakati alifanya mambo yaliyowafurahisha wanataaluma ya habari, ikiwemo kusimamia mabadiliko ya sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016, ingawa hayajakamilika kama walivyotaka.
kwa ujumla, amesema yapo maeneo ambayo Nape alifanya vema, lakini yapo ambayo wakati mwingine hayakuwafurahisha wanahabari.
Hadhi maalumu, diplomasia ya uchumi
Kwa upande wa Mahmoud Thabiti Kombo aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anakabiliwa na kuhakikisha anakamilisha kile kilichoachwa na mtangulizi wake, January Makamba.
Kwa mujibu wa Balozi wa zamani wa mataifa mbalimbali ikiwemo Italy na Ujerumani, Ali Karume alisema sera ya mambo ya nje na diplomasia ya uchumi ndiyo mwelekeo wa Serikali kwa sasa.
Kwa sababu hiyo, alieleza Balozi Kombo anapaswa kuendeleza pale ambapo mtangulizi wake ameishia, huku asiache kufanikisha suala la utoaji wa hadhi maalumu kwa watanzania waishia nje ya nchi.
Sambamba na yote, Balozi Karume alimtaka Kombo kuhakikisha anakuwa mwadilifu kwa kuwa nafasi aliyopewa ni tafsiri halisi ya kuwa msemaji wa mkuu wa nchi kimataifa.
“Lakini kwa kuwa Kombo alishakuwa balozi ameshajua mambo ya nje yanategemea mabalozi, hili jukumu halitamshinda,” alisema.
Ubora zaidi wa Kombo kwa mujibu wa Balozi Karume, ni kutoonyesha kwake malengo ya kisiasa zaidi ya nafasi aliyopewa, hivyo anaamini atatumikia vema.
|
Matukio ya kinyama yametokea dhidi ya wanawake wawili katika Mtaa wa Chinyika jijini Dodoma, ambao m
|
Matukio ya kinyama yametokea dhidi ya wanawake wawili katika Mtaa wa Chinyika jijini Dodoma, ambao miili yao imeokotwa na mmoja ukionekana kujeruhiwa na kitu chanye ncha kali.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mwili huo unaodaiwa kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali, umekutwa ukiwa umefungwa katika nailoni, boksi na kiroba.
Akizungumzia tukio hilo jana, Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa huo, Aloyce Maswikwi alisema miili hiyo ilionekana kati ya juzi na jana na mmoja kati ya wanawake hao hajatambulika.
Ilivyoonekana
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, mwili mmoja ulionekana na mwanakijiji aliyekuwa katika shughuli za uchungaji mifugo ukiwa umefungwa mithiri ya zigo la nguo za mtumba.
Kwa namna ulivyofungwa, alisema ilikuwa vigumu kubaini kama kuna mtu na mwanakijiji huyo alipomwita mwenzake kwa ajili ya kuangalia kilichomo, walilazimika kuchana na ndipo walipoiona miguu.
“Alipokwenda wakasema ngoja tufungue kuna nini, hali iliyowafanya kuchana, kumbe walikokuwa wamechana kulikuwa na miguu,” alisema.
Mwenyekiti huyo alieleza wawili hao walichana kila kilichofungashwa na baada ya kubaini kulikuwa na mwili wa mwanamke mtu, walipiga kelele zilizosababisha mkusanyiko wa watu.
“Wakatukaribisha tuangalie kama tuna mfahamu. Tulipanga foleni wanawake kwa wanaume, tukamwangalia yule dada (ana umri wa miaka kama 20) kwa kweli hatukumtambua. Kwa hiyo askari wakamchukua,” alisema.
Kwa mujibu wa Maswikwi, tukio la pili lilitokea saa 12.00 asubuhi jana, alipopigiwa simu na askari wa Kata kuelezwa juu ya uwepo wa msiba katika moja ya familia za mwanakijiji.
“Nilipofika nikakuta kweli amelala katika mlango hapa, wamemfunika shuka watu wengi wanalia, nikauliza vipi, nikaambiwa kuwa wamemkuta wamemtupa hakuwa na nguo,” alisema.
Alipohojiwa mama wa marehemu, Mwenyekiti huyo alisema mwanamama huyo alijibu mwanawe alimtoroka muda kidogo na hakufahamu alipokwenda.
“Alinieleza alikoenda (marehemu) hajui na wala ndugu zake hawafahamu ila kuna rafiki yake anaitwa Mwache ambaye waliolewa wote Zuzu ndiye anayefahamu alipo kama kuolewa kaolewa na nani na ndiye anayetumiwa kuleta matumizi ya mtoto hapa,” alisema Mwenyekiti.
Pamoja na kuuawa, Maswikwi alisema mwili wa mwanamke huyo haukuwa na jeraha lolote na kwamba hadi sasa chanzo cha kifo chake hakijafahamika.
Alisema matukio yote mawili yanaonekana kufanywa na watu wa nje ya mtaa huo.
“Yule dada watakuwa wamemuua huko mbali, wakaona waje wamtupe hapa Chinyika. Inaonekana kama ina ukatili fulani lakini sio. Matukio haya ni mazito. Nitoe wito kwa polisi waongeze juhudi katika kazi yao. Na endapo hawa watu watabainika watoe adhabu zinazostahili,” alisema.
Mama wa Marehemu, Careen Ndondo alisema mwanawe aliondoka wiki nne zilizopita bila kumwaga anakoelekea lakini jana aliarifiwa na mjukuu wake kwamba ameonekana amelala na akiitwa haitiki.
“Tukainuka na kaka yake tukaenda pale na kumkuta kalala chali, tukasema msimshike mtafuteni mwenyekiti lakini alipokuja ndugu yake mwingine alimshika na kumtingisha. Hata hivyo alimkuta kakauka, nikasema huyu amekufa sio mzima,” alisema.
Tangu mwanawe alipondoka, alisema hawakuwa na mawasiliano yoyote.
“Sijui kama walikuwa na mahusiano, rafiki yake anaweza kueleza vizuri kwa nini achukue fedha awe anamwita. Na jana alimwita mtoto wake yeye anasoma darasa la sita. Kwa kuwa alikuwa anamwita mtoto wake na kuzungumza naye, hatukuwahi kumtafuta,” alisema.
Naye mtoto wa marehemu (anayesoma darasa la sita), ambaye ndugu hawakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema alipoondoka hakumwambia anakwenda wapi, isipokuwa rafiki wa marehemu alimwita mara kwa mara na kumpa fedha za matumizi na wakati mwingine kuzungumza naye.
“Fedha ilipoisha nikaenda kumwambia fedha imeisha akanitumia fedha nyingine. Tukaja kuongea siku nyingine na mama akaniambia kuwa anaumwa na kuwa alitaka kurudi lakini anaumwa.
“Juzi jioni saa 11 nikaongea na Willy (anayedaiwa alikuwa na mama yake) akaniambia mama yangu anaumwa na juzi alikuwa hana fedha na kuwa atanitumia leo (jana),” alisema.
Mtoto huyo alisema mwanaume huyo aliyemtaja kwa jina moja la Willy alimweleza kuwa alikuwa akimuwahisha hospitali mama yake.
“Mara ya mwisho kuongea na mama yangu ilikuwa juzi (Jumamosi) akinianiambia mwanangu mimi naumwa kikohozi,” alisema mtoto huyo.
Naye rafiki yake, Mwacheni Matonya alisema siku alipoondoka Alice, yeye alikuwa saluni na kumuomba namba ya simu kwa ajili ya kumtumia mtoto wake fedha za matumizi.
“Mara ya kwanza alinitumia Sh5,000 nikampatia mtoto lakini nikamuuliza mbona shoga yangu hurudi akasema nipo sokoni ninauza nyanya lakini baadaye nitakuja.
“Baada ya hapo nikawa napiga simu haipatikani. Hadi jana (juzi) anakuja mtoto aniuliza mama yangu umeongea naye nikamwambia simu yake haipatikani,” alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa hafahamu rafiki yake alipokuwa akiishi hadi jana alipoitwa kuwa amefariki dunia.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Samwel Magesa alithibitisha kupokea miili ya wanawake hao wawili kati ya juzi na jana.
Alisema juzi saa 11 jioni walipokea mwili wa mwanamke ambaye jina lake halikufahamika lakini ulikuwa na majeraha katika sehemu mbalimbali yaliyosababishwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
“Huyu wa juzi alikuwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili, ilionekana baadhi ya majeraha kidogo yalikuwa yameenda ndani. Sehemu za kichwa pia zilikuwa na majeraha,”alisema.
Pia Dk Magesa alisema saa 3.40 jana walipokea mwili wa mwanamke ambao haukuwa na jeraha lolote na hivyo walikuwa wanaendelea na uchunguzi ili kubaini nini hasa kimesababisha vifo hivyo.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya zinaendelea baada ya simu yake kutopokelewa mara kadhaa.
Julai 17 mwaka huu, mtoto Telesphore Mwakalinga aliuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kukutwa karibu na nyumbani kwao Nyumba 300, kata ya Nzuguni huku ukiwa umeondolewa sehemu za siri na mkono mmoja.
|
Pamoja na uhakika wa kufika haraka, kupenya kwenye msongamano na gharama nafuu za usafiri wa bodabod
|
Pamoja na uhakika wa kufika haraka, kupenya kwenye msongamano na gharama nafuu za usafiri wa bodaboda, unajua madhara ya kiafya yaliyojificha nyuma ya raha hizo?
Sikutishi uache kupanda au kuendesha bodaboda, muktadha wa andiko hili ni mtazamo wa wataalamu wa afya, wanaoeleza madhara ya kiafya yanayowakabili watumiaji na madereva wa usafiri huo hasa wasipotumia vifaa kinga ikiwemo kofia ngumu.
Kwa mujibu wa wataalamu hao, pengine hautayaona matokeo sasa, lakini kwa kadri siku zinavyokwenda ndivyo unavyokaribia kukabiliwa na madhara hayo ikiwemo upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume.
Msingi wa kauli za wataalamu hao ni kile kilicholalamikiwa na baadhi ya madereva wa bodaboda, kuhusu kukabiliwa na magonjwa ya vifua na mapafu mara kwa mara.
Sambamba na magonjwa hayo, madereva hao wa bodaboda wametaja kusumbuliwa pia na migongo na viuno, huku baadhi wakikumbwa na magonjwa ya ajabu yanayosababishwa na mitikisiko inayochochewa na ubovu wa barabara.
Walichokisema bodaboda
Maumivu ya kifua na mapafu kujaa maji ni miongoni mwa magonjwa yanayomsumbua Daniel William anayefanya shughuli za udereva wa bodaboda, Dar es Salaam.
"Kama huvai kofia ngumu, unahisi kabisa baridi inapita puani moja kwa moja kwa sababu upepo ni mkubwa, ugojwa wa macho pia tunapata hasa mtu asipovaa kofia ngumu yenye kioo,” anasema.
Magonjwa hayo kwa mtazamo wa William, yanasababishwa na vumbi na mchanga unaorushwa na gari au bodaboda zinazowatangulia barabarani.
“Wakati mwingine mnaona macho yanatoka machozi au yanakuwa n rangu nyekundu, pia tunaumwa sana kichwa kwa sababu unakuta muda wote macho yanatoka machozi," anasema.
Hashim Bariki anayefanya shughuli hiyo pia, anasema changamoto kubwa kwake ni maumivu ya mgongo na kiuno yanayosababishwa na mashimo yaliyopo katika baadhi ya barabara.
"Barabara mbovu mtu ukienda kulala mwili wote hauna hali hasa kwenye mgongo na kiuno tunapata maumivu sana, kutokana na kurushwa kwenye mashimo ya barabara,” anaeleza.
Kinachomkabili Hashim ni tofauti na Hamza Juma anayeendesha bodaboda katika Jiji hilo, anayesema kuwashwa mikono ndilo tatizo sugu kwake hasa nyakati za usiku.
"Yani kwa hizi njia zetu zenye mashimo, kila ikifika usiku nikiwa nimetulia nasikia viganja vya mikono vinawasha yani kama mtu ananichoma na sindano.
“Hii inanitokea kila siku hasa nikiendesha pikipiki kwenye njia mbovu, baada ya muda inatulia,” anasema.
Bodaboda na nguvu za kiume
Upo uhusiano wa matatizo ya afya ya uzazi kwa wanaume na uendeshaji wa bodaboda katika barabara mbovu, kama inavyoelezwa na mtaalamu wa mfumo wa uzazi kwa wanaume wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Deogratius Mahenda.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, uendeshaji wa bodaboda katika barabara hizo unasababisha maumivu ya mgongo na kiuno, viungo ambavyo ndiyo muhimu kwa nguvu hasa za kiume.
“Maumivu hayo yakitokea inaweza kusababisha athari kwenye viungo vya uzazi na pengine nguvu za kiume. Nguvu za kiume zinategemea mfumo wa fahamu na damu iende ya kutosha kwenye uume," alisema.
Hatari ya muziki
Kama ulidhani muziki wa sauti ya juu unaopigwa kwenye bodaboda ni starehe unakosea, kelele hizo zinahatarisha mfumo wako wa kusikia, kwa mujibu wa Mtaalamu wa Masikio, Pua na Koo, Dk Edwin Lyombo.
"Sauti ya kiwango cha juu bila ya kuwa na kitu cha kuzuia inapunguza usikivu. Athari hizo zinaenda taratibu hata akiendesha bodaboda leo, matatizo atayagundua baadaye, mwanzoni anaweza asione shida," anasema Dk Lyombo.
Kuna hatari ya kupata madhara ya muda mfupi na mrefu, iwapo utaendesha bodaboda bila kuzingatia matumizi ya mavazi maalumu, ikiwemo kofia ngumu, kama inavyofafanuliwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa yatokanayo na Kazi, Hussein Mwanga.
Dk Mwanga ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya ya Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), anayataja miongoni mwa madhara ya muda mfupi ni maambukizi ya kifua.
Kwa upande wa madhara ya muda mrefu, anasema ni athari katika mapafu inayosababishwa na vumbi, moshi na uchafu mwingine unaotokana na moshi.
"Hii inaweza kuleta madhara ya muda mrefu inaathiri zaidi mapafu kwa sababu tunavuta zaidi hewa na vimbi likifika kwenye mapafu linajibadilisha kama mtu aliyevuta sigara madhara yake ni kama ugonjwa wa COPD,” anasema.
Madhara mengine ya muda mrefu kwa mujibu wa Dk Mwanga, ni ugonjwa wa shambulio la pumu na magonjwa mengine ya kifua ambayo aghalabu ni hatari kwa binadamu.
Saratani na magonjwa ya moyo ni madhara mengine ya kudumu yanayoweza kumkabili mtu anayeendesha bodaboda bila kuvaa vifaa maalumu.
"Ukiachana na mapafu kuna magojwa mengine ambayo yanaonekana na uhusiano kama magojwa ya moyo hadi saratani ya mapafu.
“Wanaoathirika zaidi ni watoto na watu wazima inaathiri hadi ukuaji wa mapafu, kama watoto ni abiria wa mara kwa mara au wanaishi karibu na barabara mapafu yanaweza yasikue vizuri," anasema.
Ili kuepuka magonjwa hayo, Dk Mwanga anasema madereva bodaboda wanapaswa kuvaa vifaa vya kujikinga kama maski na uzingatiwaji wa hilo ufanywe nchi nzima.
"Ni vizuri hatua zikaanza kuchukuliwa juu kama nchi iamue kupunguza hilo, kila mtu apunguze uchafuzi wa hali ya hewa kama vile kupunguza magari na ndiyo maana kwenye nchi zilizoendelea zinatumika sana baiskeli.
“Tunapaswa kuwa na lami zitakazosafishwa kila wakati kwa ajili ya kupunguza vumbi," anaeleza.
|
Licha ya madai ya kukithiri kwa vitendo vya rushwa katika sekta ya usafiri hasa wa daladala, wadau w
|
Licha ya madai ya kukithiri kwa vitendo vya rushwa katika sekta ya usafiri hasa wa daladala, wadau wa sekta hiyo wameonyesha uwepo wa mazingira magumu ya udhibiti wa vitendo hivyo.
Mazingira hayo magumu ya udhibiti wa rushwa kwa mujibu wa wadau hao, yanatokana na kuwepo kwa mnyororo mrefu wa vitendo hivyo unaohusisha watu wazito ndani ya jeshi la polisi.
Kasoro za kisheria nazo, ni jambo lingine lililotajwa na wadau kama kikwazo cha udhibiti wa vitendo vya rushwa katika sekta ya usafiri na usafirishaji.
Ingawa wadau wanaibuka na hoja hizo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Ramadhan Ng’anzi anasema udhibiti wa rushwa katika sekta hiyo pamoja na mbinu nyingine unapaswa kuanza kwa wamiliki wa daladala kuhakikisha hawana makosa.
“Kama gari lako halina makosa, uko vizuri unatembea barabarani, askari atakusimamishaje, au unawezaje kutoa rushwa wakati unajua huna kosa. Wanaotoa rushwa ni wale wanaojua wana makosa kwa hiyo ili kukwepa faini wanakubali kutoa rushwa,” anasema Ng’anzi.
Tunagawana na wakubwa
Suala la rushwa kwa askari wa usalama barabarani haliishii kwa askari wanaopokea fedha hizo kutoka kwa madereva na kondakta pekee, kama inavyoelezwa na mmoja wa maofisa wa askari wa usalama barabarani aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina.
Kwa mujibu wa ofisa huyo ambaye kimsingi ni msimamizi wa sheria, baadhi ya askari hao wanawekewa viwango vya fedha wanazopokea kutoka kwa madereva na kondakta wa daladala kwa ajili ya kuwasilisha kwa wakubwa zao.
"Fedha hiyo hiyo inakwenda hadi inafika ngazi ya juu, kwa hiyo kwenye utekelezaji wa sheria kuna changamoto. Bosi wako wanakuwekea viwango kwamba kwa siku umtumie Sh20,000 unalazimika kupambana ili umtumie, kwa hiyo kuna mnyororo," anasema.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, kama ilivyo kwa madereva na kondakta wa daladala, askari nao huwekewa kima cha fedha zinazotokana na rushwa kwa ajili ya kuwasilisha kwa bosi kila siku.
Kutokana na mazingira hayo, anaeleza inakuwa vigumu hata ukiwa mwadilifu kukwepa kupokea rushwa kwa kile anachoeleza, “utalazimika utoe fedha yako ya mfukoni uipeleke.”
Ofisa huyo anakwenda mbali zaidi akieleza askari wengine pamoja na kiasi wanachotakiwa kuviwasilisha kwa bosi, watafanya juhudi kukusanya na cha kwao, hapo ndipo daladala zinapoumizwa.
Lakini mzizi wa yote hayo, anasema ni changamoto ya madereva kutojua sheria, hivyo wanalazimika kutoa rushwa badala ya kuepuka kwa kuhakikisha wanakidhi vigezo vya kuwa barabarani.
“Kama huna kosa utasimamishwa vipi uombe rushwa, wanasimamishwa kwa sababu wana makosa mtu anaogopa kutoa Sh30,000 anaona bora atoe Sh5,000,” anaeleza na kusisitiza sio mabosi wote wanaopokea rushwa wengine waadilifu.
Suala la mkono mrefu katika rushwa linaelezwa pia na mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa Latra (jina lake limehifadhiwa), anayesema inafika kwa mabosi.
Kwa sababu ya maslahi hayo, anaeleza ndiyo maana hadi sasa Polisi wanang’ang’ana kukaa barabarani kusimamia usalama ilhali si jukumu lao la kisheria.
Vivyo hivyo, anasema polisi wataendelea kufanya ukaguzi wa magari na kutoa leseni za udereva ilhali sheria haitambui jukumu hilo kwao.
Ofisa huyo anaeleza sheria ya Latra kuanzia kifungu cha 5(1) D na kuendelea, kinaitambua mamlaka hiyo kama mratibu wa shughuli zote za usalama barabarani na sio polisi.
“Kifungu kinasema Latra ndiyo itaajiri wafanyakazi wote wa sekta ya barabara na reli, yaani hadi makondakta na madereva,” anasema.
Kifungu hicho hicho F, anasema ndicho kinachoipa Latra mamlaka ya kufanya ukaguzi wa magari yote ya biashara badala ya polisi.
“Kifungu G kinasema Latra ndiye atakayekagua ubora wa treni zote, imeunganishwa namna hiyo, kwenye sheria ya Sumatra hivyo havikuwepo,” anasema.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, wakati sheria inapitishwa baadhi ya wabunge walisema baada ya miaka miwili inapaswa kurudishwa bungeni kwa ajili ya Kuongezwa vitu.
Vitu vilivyotajwa kutakiwa kuongezwa, anasema ni madereva wakaguliwe na Latra badala ya polisi.
Lakini, anasema hilo halikutekelezwa hadi sasa na aliyesababisha ni mtu mmoja katika Wizara ya Mambo ya Ndani (hakumtaja).
“Kuna mtu akasema tukisema sheria hii ifutwe tutakosa maslahi yetu ile rushwa unayoiona barabarani inafika kwa watu wakubwa sio wadogo tu, hili tatizo lina nguvu ya wakubwa,” anaeleza
Hata hivyo, anasema kuna changamoto katika sheria ya usalama barabarani, inayompa polisi mamlaka ya kutoa leseni lakini huyo huyo ndiye anayekagua.
“Unatoa leseni alafu wewe mwenyewe unakwenda kujikagua, anayetoa leseni ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi anayekwenda kukagua ni Koplo.
“Hivi Koplo anaweza kwenda kinyume na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi kwa nidhamu ya jeshi hilo?” anahoji.
Anaeleza hata ukaguzi wa magari utafanywa na maofisa hao wa ngazi ya juu wa polisi, lakini watakaozikagua barabarani ni askari wa chini.
“Hii ni mbinu iliyopitwa na wakati ya usimamizi wa usalama wa barabarani,” anaeleza.
Wakati wadau wakieleza hayo kuhusu sheria, Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Deus Sokoni anasema sheria ya usalama barabarani ndiyo msingi wa usimamizi wa shughuli zote za usalama barabarani na kwamba inapaswa kusimamiwa na polisi kama ilivyoelezwa ndani yake.
“Sheria ya usalama barabarani ndiyo inayomtambua askari polisi kusimamia usalama barabarani na sio mamlaka nyingine au mtu mwingine,” anasema.
Kwa mujibu wa Sokoni, majukumu na shughuli za Latra zimetajwa katika sheria ya kuanzishwa kwake, lakini sio kusimamia masuala ya usalama barabarani.
Anasisitiza sheria ya usalama barabarani, inasimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, kupitia Jeshi la Polisi na ndani yake jeshi hilo limetajwa.
Katika sheria hiyo, anasema Latra imetajwa ndani ya Kifungu cha 44 kama mamlaka ya udhibiti.
Suala hilo linawekewa mkazo na Mwanataaluma wa Usalama Barabarani, Henry Bantu anayesema changamoto zote zinazoikabili sekta hiyo zinasababishwa na kutotekelezwa sheria inavyopaswa.
Kwa mujibu wa Bantu, sheria ya usalama barabarani na nyingine zote zinazosimamia eneo hilo, hazina tatizo bali matatizo wanayo wanaopaswa kuzitekeleza.
“Tatizo la utekelezaji linaanza na uelewa, tuna changamoto kubwa ya uelewa wa sheria kwa wananchi, ndiyo sababu wanajikuta watumwa wa sheria na wanashindwa kuitekeleza,” anasema.
Kwa hali ilivyo, Bantu anasema kuna umuhimu wa kuhakikisha elimu inatolewa ili wananchi waijue sheria husika, kufanya hivyo kutawawezesha kutambua namna ya kuitekeleza.
Anasisitiza wanaoona kuna changamoto za kisheria, pengine hawajaelewa.
Polisi kuhuru rushwa
Kamanda Ng’anzi alikiri kusikia vitendo vya rushwa vinavyodaiwa kufanywa na askari hao na kwamba kila juhudi zinafanywa kuwakamata wanaohusika.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, askari atakayebainika atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
Pamoja na kauli yake hiyo, Ng’anzi anasisitiza umuhimu wa wamiliki wa magari kuhakikisha vyombo hivyo vya usafiri havina makosa ili kuepuka kujiweka katika mazingira ya kuombwa rushwa.
Alisema hakuna trafiki atakayekusimamisha iwapo huna kosa na hata mwenye gari hatatoa rushwa iwapo anajijua si mkosaji.
Kwanini daladala zina makosa
Gari nyingi hasa daladala zinakutwa na makosa kwa sababu hazifanyiwi matengenezo kama inavyoelezwa na Mkuu wa Idara ya Taaluma ya Usafirishaji na Biashara wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dk Prosper Nyaki.
Kwa mujibu wa mhadhiri huyo, kila aina ya gari lina maelekezo yake kutoka kwa mtengenezaji juu ya lini linapaswa kufanyiwa matengenezo.
Sambamba na maelekezo ya matengenezo, anasema wazalishaji wa gari hizo, wameelekeza zikitembea umbali gani zinahitaji kubadilisha vilainishi na tairi.
Changamoto iliyopo kwa wamiliki wa daladala, anasema wengi hawafuatilii maelekezo ya kitaalamu juu ya matengenezo madogo ya magari husika, hivyo mengi ni mabovu.
"Mengi yanatembea yakiwa na ubovu kwa sababu wanaoyatumia hawazingatii maelekezo ya kitaalamu kuhusu matengenezo, hali hii inasababisha ukikagua ulikute na kasoro," anasema.
Hata hivyo, anaeleza ubora wa gari linalopaswa kutembea barabarani haupimwi kwa macho pekee, bali ni kufungua baadhi ya vitu, mathalan kujua iwapo vilainishi vipo na vinapaswa kuendelea kutumika.
Katika mazingira ya kutozingatiwa kwa matengenezo ya daladala, Dk Nyaki anasema ndipo madereva na kondakta wanajikuta wanahofu kusimamishwa na trafiki wakijua watakutwa na
Kauli ya Latra
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), Salum Pazzy, anasema kazi ya ukaguzi wa ubovu wa magari ni jukumu la Polisi kupitia sheria ya hali ya ukaguzi.
“Polisi ndio wanaohusika kukagua uzima wa gari na sio Latra, kwani hata sisi gari ikiwa mbovu tunawahusisha wao kwa kuwa ndio wana utaalamu katika eneo hilo,” anasema Pazzy.
Baada ya Latra kutoa leseni ya gari kuingia barabarani, Pazzy anasema mmiliki anaandikiwa barua ya kuipeleka polisi kwa ajili ya kukaguliwa, kisha ndiyi ataruhusiwa kuanza safari.
Katika utoaji wa leseni hiyo, anasema kinachozingatiwa ni idadi ya viti vya gari kulingana na safari kwa upande wa daladala, huku mabasi makubwa wanazingatia madaraja.
|
Kutenguliwa ni jambo moja, lakini kutenguliwa ukiwa katikati ya shughuli za nafasi uliyotenguliwa kw
|
Kutenguliwa ni jambo moja, lakini kutenguliwa ukiwa katikati ya shughuli za nafasi uliyotenguliwa kwayo ni jambo lingine, hiki ndicho kilichomkuta aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ambaye si mara yake ya kwanza.
Taarifa ya kuondolewa kwa Nape katika wadhifa huo, ilitolewa akiwa katikati ya hotuba kwenye hafla ya utoaji tuzo za wanawake wa kidigitali ambazo yeye alikuwa mgeni rasmi Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya pili mwanasiasa huyo anakumbwa na utenguzi katika mazingira yanayofanana, aliwahi kuondolewa katika Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo akiwa katika harakati za kupokea ripoti ya kamati aliyoiunda ya kuchunguzi tukio la uvamizi wa kituo cha redio cha Clouds mwaka 2018.
Mazingira ya kutenguliwa kwa Nape yanakumbusha kilichomtokea Mwigulu Nchemba aliyewahi kuondolewa katika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Taarifa ya kuondolewa kwake ilitolewa akiwa ziarani na hivyo kulazimika kuacha gari la waziri na kutumia usafiri binafsi.
Safari ya Nape katika wadhifa wa uwaziri ilianza mwaka 2015 Rais wa wakati huo, John Magufuli alipomteuwa kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na miaka miwili baadaye alimuondoa.
Hakukuwa na sababu iliyowekwa wazi na mamlaka ya uteuzi juu ya kuondolewa kwake, isipokuwa wengi walihusisha na uamuzi wake wa kuunda kamati ya uchunguzi dhidi ya uvamizi wa kituo cha redio cha Clouds.
Nape aliondolewa siku ambayo ndiyo aliyokuwa anapokea ripoti ya kamati hiyo iliyomtuhumu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutumia vibaya mamlaka yake kwa kuvamia kituo hicho cha redio.
Kwa mara ya pili, aliteuliwa tena kushika wadhifa wa uwaziri mwaka 2022, wakati huu akiwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari chini ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kama ilivyokuwa mara ya kwanza, amedumu ndani ya wizara hiyo kwa miaka miwili pekee na Julai 2024 aliondolewa bila kuelezwa sababu yoyote.
Lakini kuondolewa kwake wakati huu kunahusishwa na kauli yake ya hivi karibuni iliyoibua mijadala katika mitandao ya kijamii, kuhusu ushindi wa uchaguzi nje ya boksi la kura.
“Unajua nyie sikilizeni, matokeo ya kura sio lazima yawe ya kwenye boksi, inategemea nani anahesabu na kutangaza. Na kuna mbinu nyingi kuna halali, nusu halali na kuna haramu na zote zinaweza kutumika ilimradi mkishamaliza, unamwambia Mwenyezi Mungu nisamehe,” alisema Nape Julai 15, 2024.
Pamoja na kupingwa mitandaoni, kauli hiyo ilipingwa pia na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla aliyesema si msimamo wa chama hicho.
“Kuna kiongozi nimemsikia huko mitandaoni anasema eti ushindi wa uchaguzi hautokani na kura za kwenye boksi, mimi nataka nimwambie hiyo kauli isitazamwe kuwa inatokana na CCM,” alijibu Makalla alipokuwa ziarani mkoani Dar es Salaam.
Mtazamo wa kisiasa
Akizungumzia uamuzi wa kuondolewa kwa Nape, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk Revocatus Kabobe amesema pengine kauli yake ya Julai 15 ndiyo iliyomponza.
“Yalikuwa makosa makubwa kwa kiongozi mwandamizi kama Nape kutoa kauli kama hizo zenye kukichafua chama (CCM) na serikali juu ya uchaguzi.
“Kauli yake inaweza kuwa imechukuliwa kama uthibitisho kwa wapinzani ambao mara zote wamekuwa wakilalamika kuibiwa kura,” ameeleza.
Dk Kabobe amehusisha kuondolewa kwa Nape na madai yaliyowahi kutolewa na mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akimtuhumu kwa hujuma za uchaguzi ndani ya CCM wakati wanapiga kura za kuwachagua wabunge wa Afrika Mashariki (EALA).
“Ukizingatia kuwa rais anatekeleza vizuri falsafa yake ya 4R, vitendo kama hivi vya kumrudisha nyuma lazima avikemee na kulinda chama na Serikali yake kwa wivu mkubwa. Nadhani hiki ndo alichokifanya,” amesema.
Kwa kuwa mwaka huu na ujao kuna chaguzi, Dk Kabobe amesema kauli kama hizo hazipaswi kufumbiwa macho na ndio maana mamlaka ya uteuzi imeonyesha njia na inastahili pongezi kwa hilo.
Hata hivyo, Kabobe ameeleza kuhusu mabadiliko mengine ykiwemo yanayomuhusisha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Yusuph Makamba akisema ni kawaida katika kuboresha utendaji wa kila siku wa shughuli za Serikali.
|
Mbunge wa kuteuliwa, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amemwandikia barua Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackso
|
Mbunge wa kuteuliwa, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amemwandikia barua Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ya kujiuzulu nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa barua aliyomwandikia Dk Tulia, Balozi Mbarouk amesema sababu ya uamuzi wake huo ni changamoto za kijamii zinazomkabili sasa.
“Ninalazimika kuchukua uamuzi wa kujiuzulu ili nipate nafasi ya kushughulikia changamoto hizo,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Bunge, ikinukuu barua ya Balozi Mbarouk.
Balozi Mbarouk ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki aliteliwa Aprili mwaka 2021 kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sambamba na uteuzi katika nafasi hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan siku hiyo hiyo, alimteuwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, nyadhifa ambazo amedumu nazo hadi sasa.
Akiwa Naibu Waziri na Mbunge wa kuteuliwa, Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwaka 2022 ilimteuwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Baadaye wadhifa huo ulirithiwa na Rabia Maulid, huku Balozi Mbarouk akiendelea kutumikia ubunge na unaibu waziri.
Kabla ya nafasi hizo za kisiasa, katika miaka ya 2013 hadi 2019, Balozi Mbarouk ameitumikia Serikali kwa nyadhifa za kidiplomasia, akiwa balozi wa nchi za Falme za Kiarabu.
Hatua yake ya kujiuzulu wadhifa huo, inamfanya moja kwa moja akose sifa ya kuendelea na nafasi ya Naibu Waziri ambao kwa mujibu wa Katiba inampasa mbunge kushika nafasi hiyo.
Si wa kwanza kujiuzulu ubunge
Balozi Mbarouk si mbunge wa kwanza kujiuzulu wadhifa huo, iliwahi kufanywa hivyo na aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum wa CCM, Bahati Ndingo Agosti mwaka 2023.
Tofauti na Balozi Mbarouk, Bahati yeye katika barua yake kwenda kwa Dk Tulia aliandika msingi wa uamuzi wake huo ni kutafuta namna nyingine ya kuwatumikia wananchi.
Siku chache mwanasiasa huyo alikwenda kuwania ubunge wa Mbarali mkoani Mbeya na kushinda, nafasi ambayo anahudumu hadi sasa.
Uamuzi kama huo ulifanywa pia na Sheha Faki aliyeshinda ubunge wa Konde visiwani Zanzibar Agosti mwaka 2021. Kilichostaajabisha kwa Faki, alijiuzulu kabla hata hajaapishwa na Spika.
Katani Katani naye alitangaza kung’atuka katika kiti cha ubunge wa Tandahimba kwa tiketi ya chama cha CUF, Februari mwaka 2020, lakini baadaye alihamia CCM.
Kama ilivyo kwa Katani, Marwa Ryoba alijiuzulu ubunge wa Serengeti kwa tiketi ya Chadema na hapo hapo alitangaza kuhamia CCM.
Uamuzi kama huo ulifanywa na Joseph Mkundi aliyekuwa mbunge wa Ukerewe aliyeukacha ubunge kwa tiketi ya Chadema na kuhamia CCM.
Lazaro Nyalandu naye Oktoba mwaka 2017, alitangaza kujiuzulu ubunge kwa tiketi ya CCM na sababu kuu ilikuwa ni nia yake ya kuhamia Chadema.
|
“Ukiwa dereva wa daladala Dar es Salaam unawatumikia mabosi wawili; kwanza mmiliki wa gari na pili,
|
“Ukiwa dereva wa daladala Dar es Salaam unawatumikia mabosi wawili; kwanza mmiliki wa gari na pili, trafiki.”
Ni kauli ya Bosco Joram (si jina halisi) dereva wa daladala linalofanya safari kati ya Buyuni Chanika na Ubungo Simu 2000.
Malalamiko ya Joram yanatolewa na idadi kubwa ya madereva na makondakta wa daladala wakidai kuombwa rushwa kwa maelezo ya fedha za kubrashia viatu.
Wanaeleza hulazimika kila siku kutenga fedha kwa ajili ya askari wa usalama barabarani maafuru trafiki ili kukwepa kutozwa faini ama kwa makosa ya usalama barabarani, yanayohusu vyombo wanavyoendesha au wakati mwingine pasipo kosa lolote.
Uchunguzi wa Mwananchi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam umebaini madereva huwasilisha kwa wenye magari hesabu ya kati ya Sh80,000 hadi Sh200,000 kwa siku kutegemea ukubwa wa gari na umbali wa safari.
Mbali ya hilo, hutenga fedha kwa ajili ya mafuta na kiasi kinachosalia hugawa fungu kwa ajili ya posho yao na ya trafiki ili kuwezesha siku kuisha vema.
Joram anasema hutenga kati ya Sh10,000 na Sh15,000 za kuwapa trafiki, akieleza maeneo ambayo hulazimika kuwa makini ni Vingunguti na Kipawa ambako mara nyingi trafiki husimama katika Barabara ya Nyerere. Iwapo akisimamishwa huacha Sh2,000 kwa trafiki aliyemkamata.
“Suala la kutoa hela haliwezi kwisha kwa kuwa usipofanya hivyo wanakuandikia faini. Sasa kama una kosa la kuandikiwa faini Sh30,000 halafu uone ubahili wa kutoa Sh2,000! Hiyo hapana," anasema Joram, mtazamo ambao pia wanao madereva wengine.
Saleh Kassim, dereva wa daladala kati ya Chanika-Gongo la Mboto anasema trafiki hukubali Sh2,000 kwa kosa lisilozidi faini ya Sh30,000, lakini ukiwa na zaidi ya moja wanakutaka kupeleka gari kituoni.
"Ukikamatwa ndiyo umetoka kuamka au umetoka gereji, unamwambia sina kitu nikirudi nitakucheki. Ukirudi unamalizana naye, ukijidai umesahau anakukamata," anasema akiainisha maeneo ambayo tafiki husimama kuwa ni Videte (Chanika), Magenge, Mapensheni na Shule ya Msingi Pugu.
Kwa wastani anasema hutumia Sh10,000 kwa ajili ya trafiki, kauli inayoungwa mkono na John Gabriel anayefanya kazi kati ya Stesheni na Mbande.
Miraji Kiboko, dereva wa daladala kati ya Homboza na Machinga Complex, anasema wanapokutana na askari kutoka makao makuu ya trafiki kiwango hupanda hadi Sh5,000.
"Kama ulishawahi kuona askari wanakuwa wengi kituoni, wakati mwingine wameegesha gari pembeni, ukikamatwa na hao ujue Sh5,000 itakuhusu, hawapokei Sh2,000," anasema.
Kondakta aliyejitambulisha kwa jina moja la Samson, anayefanya kazi katika daladala la Kigogo –Kivukoni akijibu swali ni kwa vipi askari atajua kwamba alishalipa fedha anasema:
“Wanajua magari yote ya njia wanayopangiwa, hivyo kama kituoni wapo watatu, ujue kabisa wanaambiana yule mimi tayari nishachukua, hivyo hawakukamati.”
Nassor Imran, dereva wa daladala kati ya Tegeta Nyuki na Mwenge anasema mapato kwa siku ni kati ya Sh130,000 na Sh180,000 ikitegemea idadi ya abiria na unafuu wa msongamano barabarani.
Anasema Sh100,000 huzipeleka kwa mmiliki wa gari kila siku bila kujali limefanya kazi au la, huku akitenga Sh14,000 kwa ajili ya trafiki barabarani.
Kutokana na mazingira hayo, anaeleza kuna wakati hushindwa kugawana posho na kondakta wake ingawa zipo siku hupata kiasi cha kuridhisha.
Baadhi ya madereva wanasema hubakiwa na wastani wa Sh40,000 ambazo hugawana na kondakta.
"Hii inategemea na biashara ilivyokuwa siku hiyo, ikiwa mbaya kati ya Sh25,000 hadi 20,000, hatukosi kwa siku kurudi nayo nyumbani," anasema mmoja wa madereva.
Nelson Manda, kondakta wa daladala katika njia hiyo anasema kuna wakati hulazimika kutoa fedha kwa trafiki hata kama hakuna kosa la usalama barabarani au kuhusu gari.
"Gari halina kosa, kama la kwangu ni jipya bosi kakamilisha taratibu zote, lakini kwa askari lazima utoe fedha," anasema.
Suala la rushwa kwa askari wa usalama barabarani, kwa mujibu wa mmoja wa madereva katika njia hiyo, lina mkono mrefu hivyo ni vigumu kudhibitiwa.
"Siku hizi tunawapa Sh2,000 hadharani hawajifichi, kwa nini hawajifichi ni kwamba mabosi zao wamehalalisha wanajua hakuna wa kuwafanya lolote," anaeleza.
Barabara ya Morogoro
Katika barabara ya Morogoro, baadhi ya madereva na makondakta wanaofanya safari kati ya Mbezi na Mlandizi wanasema ukiacha maeneo mengine kwenye barabara hiyo, vituo maalumu vya kuacha hela kwa trafiki ni Kibamba kwa Mangi na Magari Saba.
Wanaeleza kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa sita mchana katika vituo hivyo daladala husimama na kuacha Sh2,000 kwa trafiki wanaokuwapo hapo.
"Huo ndiyo utaratibu, hauwezi kuukwepa kama ni konda au dereva wa daladala, ukishatoa Sh2,000 basi unafanya kazi kwa amani siku nzima, labda itokee tu umefanya kosa," anasema dereva wa daladala, James Peter.
Mwandishi wa Mwananchi aliyepiga kambi kituo cha Kibamba kwa Mangi asubuhi ya Ijumaa Julai 19, 2024 kati ya saa 2.00 na saa 3.00 alishuhudia trafiki watatu wakichukua fedha kutoka kwa madereva na makondakta wa daladala zilizotokea Mlandizi kwenda Mbezi.
Baada ya kushusha abiria, kondakta aliyekunja fedha kwenye tiketi, alienda upande wa dereva na kumkabidhi trafiki ambaye wakati huo alikuwa akizungumza na dereva.
Kituo cha Magari Saba, siku hiyo ya Ijumaa, Julai 19, 2024 saa 4.00 asubuhi walikuwapo trafiki wawili, mmoja akiwa amevaa koti la bluu na suruari ya kaki.
Dereva wa daladala alipomuona kabla hajasimama alimweleza kondakta kuna ‘kimeo.’
"Huyu (akimaanisha askari aliyevaa koti la bluu) huwa hakubali kupokea Sh2,000 kama wengine,” anaeleza dereva huyo katika mazungumzo na kondakta.
Baadaye alisimamisha daladala lingine, Mwananchi ilishuhudia trafiki huyo akipokea Sh5,000.
Dereva aliyejitambulisha kwa jina moja la Rashid alilieleza Mwananchi kwamba trafiki huyo hulazimisha kupewa Sh5,000 hadi Sh10,000 na usipompatia siku hiyo huwezi kufanya kazi kwa raha.
"Tunatoa mara moja kwa siku, ingawa kuna askari wanalazimisha Sh5,000, lakini mara nyingi tunaacha Sh2,000 miaka minne iliyopita ilikuwa ni wajibu kuitoa na trafiki hawakuona aibu kuchukua, kidogo kipindi hiki wanachukua kisirisiri, lakini huwezi kupita asubuhi Magari Saba au Kwa Mangi bila kuacha pesa hiyo," anasema.
John Tarimo dereva wa daladala kati ya Gongo la Mboto na Kawe anasema ili abiria asione mara nyingi huenda nyuma ya gari na fedha hutolewa mkononi au hukunjwa kwenye tiketi. Trafiki humpa risiti kondakta ili kuonyesha kaandikiwa faini.
Dereva wa daladala zinazotoa huduma kati ya Buza na Mwenge, Said Rashid anasema fedha hizo trafiki husema ni kwa ajili ya kubrashi viatu.
“Ukianza safari Buza Kwalulenge kituo cha kwanza unasimamishwa na askari kwa Mama Kibonge, Temeke Usalama, halafu ukifika Tabata Mwananchi unawakuta, kisha utawakuta Ubungo River Side na Mpakani Mwenge. Kila kituo lazima uache Sh2,000,” anasema.
Jackson Masia, dereva wa daladala kati ya Mnazi Mmoja hadi Simu 2000 kupitia Buguruni anasema:
“Kuna wakati wanadiriki hata kunyang’anya ufunguo wa gari kisa wamenyimwa Sh2,000 na wanatutukana hadharani na abiria wanasikia wanapotoa maneno ya fedheha,” anasema.
“Nyakati za asubuhi abiria wanataka kuwahi kwenye majukumu yao lakini wanakusimamisha pembeni wanazunguka nyuma kama hujawafuata wanakuchukulia kuwa una kiburi hutaki ushirikiano,” anasema.
Kauli ya Darcoboa
Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Shifwaya Lema akizungumzia na Mwananchi amesema kama chama hawajawahi kupokea malalamiko kutoka kwa madereva.
“Hao ni madereva waliosema, inawezekana ni sahihi kwa sababu wao ndio wako kazini, lakini siwezi nikakubali wala kukataa kwa sababu hakuna anayesema moja kwa moja,” amesema.
Amesema licha ya chama hicho kusikiliza kero za madereva na makondakta, suala hilo halijawahi kufikishwa kwenye vikao kama hoja rasmi.
“Hoja ikiletwa huwa tunakaa tunaijadili kwa pamoja na kama kuna changamoto tunaitatua. Kwa bahati nzuri wakileta hoja zao, huwa kuna mfumo tunao kama ni Jeshi la Polisi tunaongea nao, lakini mpaka sasa hazijaletwa hoja na kwa kuwa hazijaja, siwezi kuvalia njuga hoja ambayo haijaja,” amesema.
Wasemavyo trafiki
Akizungumzia tuhuma hizo za rushwa, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Ramadhan Ng’anzi amekiri kusikia malalamiko ya madereva na makondakta kuhusu vitendo hivyo.
Amesema Jeshi hilo lipo makini kufanya uchunguzi kubaini askari yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa ili achukuliwe hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
Hata hivyo, amesema anatambua juu ya uwepo wa baadhi ya askari wasio waadilifu, hivyo wanajihusisha na vitendo vya rushwa licha ya kuzuiwa na kanuni na taratibu za kazi zao.
Amesema kuna ugumu wa kupambana na vitendo hivyo, unaosababishwa na kukosekana ushahidi wa moja kwa moja, ambao kimsingi ndiyo utakaomtia mtendaji hatiani.
“Inaonekana kama pande zote mbili zina masilahi kati ya mtoa rushwa na mpokeaji, kwa sababu wanajificha inakuwa ngumu kupata ushahidi,” amesema.
Wakati wowote atakapobainika askari anayejihusisha na vitendo hivyo kwa mujibu wa Ng’anzi, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Amesema hatua hiyo haitakuwa mara ya kwanza, kwani wapo askari kadhaa waliowahi kuadhibiwa ikiwemo kufukuzwa kazi kwa vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa fedha.
Alipoulizwa kuhusu vitendo hivyo kuhusishwa na viongozi wa Jeshi hilo, amesema jukumu lao ni kusimamia sheria na watahakikisha hilo linatekelezwa wakati wote.
Kamanda Ng’anzi amesisitiza yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo na ukapatikana ushahidi atachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria.
Takukuru yaonya
Akizungumza na Mwananchi Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni amewaonya madereva na makondakta akiwataka kuepuka kutoa rushwa kwa trafiki kwa sababu nao wanaingia mtegoni.
“Suala la rushwa lina sehemu mbili, lina mtoaji na mpokeaji, kama madereva wanatoa maana yake kuna makubaliano kati yao na wapokeaji.
“Nawashauri hao madereva wasitoe rushwa, badala yake wakiombwa au kushawishiwa, basi watoe taarifa kwa viongozi wa Jeshi la Polisi au Takukuru ili hatua zichukuliwe,” amesema.
Amesema wamekuwa wakifuatilia vitendo hivyo na kuchukua hatua pale wanapobaini makosa.
“Kuna hatua mbalimbali sisi kama taasisi tunachukua, kwa kuendelea kutoa elimu kwa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani juu ya madhara ya rushwa,” amesema na kuongeza:
“Pia tumetoa taarifa nyingi ambazo wamechukuliwa hatua, wamefukuzwa kazi na wengine pia mafaili yao yamefikishwa mahakamani,” amesema.
|
Licha ya Serikali kubadili mfumo wa utahini kwa masomo sita ya elimu ya msingi likiwemo hesabu, wada
|
Licha ya Serikali kubadili mfumo wa utahini kwa masomo sita ya elimu ya msingi likiwemo hesabu, wadau wa elimu wamesema juhudi hizo zifanywe pia katika kuwaandaa walimu wawe na umahiri wa kufundisha masomo hayo.
Ingawa kumekuwa na mapokezi chanya ya mabadiliko hayo, baadhi ya wadau wameonyesha upinzani hasa katika mtihani wa hesabu, wakisema unalazimu kumpima mwanafunzi kwa mtindo mmoja, ilhali uwezo na uelewa wao ni tofauti.
Wamekwenda mbali zaidi na kueleza, kulipaswa kuwepo na mitindo mbalimbali ya maswali ili isimchoshe mwanafunzi kujibu kwa namna moja.
Katika mabadiliko hayo, ule utaratibu wa mtihani wa hesabu kuwa na majibu ya kuchagua hautakuwepo tena, badala yake mwanafunzi atapaswa kukokotoa hesabu.
Taarifa kuhusu mabadiliko hayo ilitangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo jana Dk Said Mohamed, aliyesema mtihani wa somo la Hisabati utampasa mwanafunzi kukokotoa na kuandika majibu sahihi katika maswali yote.
“Lengo la maboresho haya ni kuimarisha utahini wa umahiri kuhakikisha wahitimu wanapata umahiri, weledi, uwezo wa kufikiri na maarifa na ujuzi utakaowawezesha kuwa na msingi imara wa elimu,” alieleza.
Kwa mujibu wa Dk Mohamed, sambamba na hisabati, katika mitihani mingine wanafunzi watapimwa kwa aina mbalimbali za utahini, ikiwemo maswali ya kuchagua, kuoanisha, majibu mafupi, kupanga maneno na sentensi na kutafsiri picha.
Hata hivyo, alieleza maboresho hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maoni ya wadau juu ya mbinu za kuboresha mbinu za utahini.
Katika maboresho hayo, maswali yatapungua kutoka 45 hadi sita au nane na vipengele kati ya 33 hadi 38
Walichokisema wadau
Akizungumza na Mwananchi jana, Mwanazuoni wa Nadharia na Vitendo katika Mitalaa wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (Duce), Dk Josta Nzilano alisema mabadiliko hayo yanaunda mtindo mmoja pekee wa kumpima mwanafunzi katika mtihani.
Lakini kiuhalisia kwa mujibu wa Dk Ndilano, kulipaswa kuwa na mitindo zaidi ya mmoja ya kuwapima wanafunzi katika mtihani hasa wa hesabu.
Katika mtihani mmoja, alieleza kunapaswa kuwa na mitindo mbalimbali ya kumpima mwanafunzi, akimaanisha aina mbalimbali ya maswali yanayopaswa kujibuwa kwa njia tofauti.
“Kuwa na maswali yenye mtindo tofauti ina maana sana kulingana na akili ya mtoto na uwezo wake. Kuna mwingine anapimwa zaidi kwenye maswali ya kukokotoa na wapo wale wenye uwezo wa kujua majibu lakini hawezi kujieleza, wote wanajua isipokuwa wanatofautiana uelewa,” alisema.
Kwa mujibu wa Dk Nzilano, kunatakiwa kuwa na maswali mengi ya mtindo tofauti na kipimo kiwe ni kwa kiasi gani mtahiniwa amejibu maswali ya aina gani zaidi.
“Mabadiliko haya pengine ni hofu ambayo wataalamu wameona kwamba pengine watoto watakuwa wakipata majibu kwa kuhisia, lakini si sawa,” alisema.
Kinachotakiwa, alisema wanaoandaa mtihani walipaswa kupewa mafunzo ya kutunga maswali thabiti yanayopima mwanafunzi uwezo wa kutenda.
“Wapewe mafunzo, sio suala la kuondoa maswali, hapo tunajenga tatizo lingine kwa sababu watoto hawana uwezo sawa, kuna mwingine ana uwezo sana wa kujieleza mwingine hana uwezo wa kujieleza,” alisema.
Kwa upande mwingine wanazuoni hao wameyaona mabadiliko hayo kama majibu ya kilio cha muda mrefu cha wadau wa elimu juu ya mfumo wa utahini, kama inavyoelezwa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St. John, Shadidu Ndosa.
“Maswali yanayotaka majibu ya kuchagua ni wazi yanapima kumbukumbu pekee, mtihani unapaswa kupima kumbukumbu, uwezo wa kufiki na kuchambua mambo. Kinachoenda kufanyika sasa kitakidhi sifa hizo za mtihani.
“Mfumo huu utatuwezesha kujua kwa usahihi viwango vya wanafunzi wetu wanaohitimu darasa la saba, uwezo wa mwanafunzi unaonekana pale anaposhughulisha akili yake kutafuta majibu sio kubahatisha kama ambavyo imeonekana kwa miaka ya karibuni,” alisema Ndosa.
Aina hiyo ya upimaji kwa mujibu wa Ndosa, itasaidia kupunguza uwezekano wa wizi au kuvujishwa kwa mitihani matukio ambayo yamekuwa yakibainika katika kila mitihani ya taifa inapofanyika.
Kwa mtazamo wa mhadhiri huyo, mfumo huo utazifanya shule kuja na mbinu thabiti za kuandaa wanafunzi kuelewa wanachofundishwa tofauti na ilivyokuwa awali ambapo nguvu kubwa iliwekwa kwenye kujibu mitihani.
Kwa upande wake mdau wa elimu, Ochola Wayoga alisema mabadiliko hayo ya mfumo wa utahini yalitakiwa kufanyika kwa muda mrefu kwa kuwa hakuna namna mwanafunzi angepimwa uwezo wake wa kufanya hesabu kwa maswali ya kuchagua.
“Hesabu ni lazima mtoto afundishwe kukokotoa ili kupata majibu, sasa huo utaratibu wa kuchagua uliwekwa ili kupunguza kelele za watu yalipokuwa yanatoka matokeo kwa kuwa ilionekana kuna wanafunzi wengi walifeli somo hili.
Kabla ya maswali ya kuchagua mtihani wa hesabu ulikuwa wa kukokotoa, ufaulu ulikuwa hauzidi asilimia 20 sasa ikatafutwa njia ya kukabiliana na hilo ndiyo yakaja maswali ya kuchagua ambayo kwa hakika haikuwa njia sahihi. Ni heri sasa tunarudi kwenye mstari.”
Hata hivyo Wayoga alisema mabadiliko ya mfumo wa mitihani pekee hayawezi kuwa na tija kama hautafanyika uwekezaji mkubwa kwenye kutengeneza walimu wenye umahiri katika kufundisha hesabu.
“Ili mwanafunzi aelewe ni lazima afundishwe na mwalimu mwenye umahiri katika somo husika, sasa je hao walimu tulionao wanaandaliwa vyema? Jibu ni hapana ndiyo maana kilio cha kufeli hesabu kimeendelea kuwa kikubwa”alisema Wayoga.
Hoja hiyo ya maandalizi ya walimu imeelezwa na Ndosa ambaye alisisitiza kuwa mfumo wa kuwaandaa walimu unapaswa kujengewa msingi mzuri tangu chini ili kuwapata watu wanaoweza kuhamisha maarifa kwa wengine.
“Suala la hesabu ni tatizo la muda mrefu, suluhu yake inapaswa kuanzia chini kabisa huko kwenye kuwaandaa wanaobeba jukumu la kufundisha somo hili” alisema Ndosa.
Majibu ya Serikali
Akijibu hayo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo alisema wakati wote walimu wameandaliwa kufundisha kwa mbinu za ukokotoaji hasa katika somo la hisabati.
Mbinu hizo hizo, alieleza ndizo zinazotumika na walimu kufundisha darasani na kwamba haikuanza sasa ni utaratibu wa muda mrefu.
“Hili la maandalizi ya walimu kufundisha kwa njia ya ukokotoaji sio jipya, ni muda mrefu sana wamekuwa wakiandaliwa kwa utaratibu huo na wanafundisha hivyo darasani. Hata wewe (mwandishi) bila shaka ulifundishwa hesabu kwa kukokotoa,” alisema.
Kwa mujibu wa Profesa Nombo, kuna wakati mfumo wa utahini ulibadilika na hivyo kukinzana na utaratibu wa ufundishaji, akiurejea utaratibu wa kuweka majibu ya kuchagua katika somo la hesabu.
Lakini, kinachofanywa sasa kwa mujibu wa Profesa Nombo, kinaendana na mfumo wa ufundishaji, kadhalika matakwa ya sera na mitalaa ya elimu.
Sambamba na hilo, mtendaji mkuu huyo wa wizara hiyo, alisema msingi wa uamuzi huo ni kuwajenga wahitimu wawe na fikra tunduizi.
“Kusema ukweli fikra tunduizi ni zao la hesabu hasa mtoto akijua kukokotoa anakuwa na fikra tunduizi na ndiyo sababu ya mabadiliko haya. Tunataka watoto wawe na uwezo wa kifikra,” alieleza Profesa Nombo.
|
Mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameonyesha mashaka juu ya kuzorota kwa hali
|
Mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameonyesha mashaka juu ya kuzorota kwa hali ya kibinadamu na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), huku akipendekeza muda wa kusitishwa mapigano usiwe na kikomo.
Mawaziri hao wanaoshughulikia Amani na Usalama na Mahusiano ya Nchi Wanachama wa jumuiya hiyo, wamependekeza umuhimu wa kuanzisha rasmi shughuli za usaidizi wa amani ndani ya EAC.
Wakizungumza katika mkutano uliowakutanisha mwanzoni mwa Julai visiwani Zanzibar, Mawaziri hao wamependekeza umuhimu wa kukamilisha haraka Mkataba wa Ulinzi wa Pamoja wa EAC na kuanzisha rasmi Baraza la Mawaziri la jumuiya hiyo kuhusu Amani na Usalama.
Baraza hilo, kwa mujibu wa mawaziri hao litatoa mwongozo wa wakati unaofaa kuhusu masuala ya amani na usalama.
Katika taarifa yao ya pamoja, viongozi hao wanaoziwakilisha nchi wanachama wa EAC, walibaini hali ya mahusiano kati ya nchi wanachama na athari zake mbaya kwa ajenda ya uunganishaji, wakihimiza nchi kutumia mifumo iliyopo kutatua migogoro.
“Waziri wa Rwanda na DRC walikubaliana kukutana haraka iwezekanavyo ndani ya mfumo wa Mchakato wa Luanda, wakati Waziri wa Rwanda na Burundi wamekubaliana kukutana Oktoba 31, 2024, kujadili masuala ya pande mbili yaliyo baki,” inasomeka sehemu ya majadiliano yaliyoandikwa kwenye Jarida la Wiki la EAC.
Katika mkutano huo, mawaziri wa jumuiya hiyo ya kikanda walijadili changamoto zinazohusiana na ufadhili wa jumuiya na madeni, wakipendekeza yalipwe haraka iwezekanavyo na nchi wanachama.
“Mawaziri walijadili mfumo endelevu wa ufadhili wa jumuiya na kupendekeza kuwa suala hilo liangaliwe katika mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Fedha, EAC, na Mambo ya Nje kuchunguza njia za ziada za ufadhili,” inasomeka sehemu nyingine ya taarifa hiyo.
Pia walikiri uharaka wa kukamilisha mchakato wa kurekebisha Mkataba wa Uanzishwaji wa EAC na kuripoti kwa Mkutano wa Viongozi ipasavyo, kadhalika kuharakisha marekebisho ya michakato ya maamuzi na kanuni.
Mkutano huo uliwakutanisha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa EAC kwa ajili ya kujadili masuala muhimu yanayoathiri ukanda huo.
Kuhusu hali ya DRC, Mkutano wa Mawaziri hao ulipongeza kusitishwa kwa mapigano yaliyojadiliwa na Serikali ya Marekani na kupendekeza muda wake uongezwe bila kikomo.
“Mawaziri walikiri kuwa amani na usalama endelevu Mashariki mwa DRC unahitaji mchakato wa kisiasa na kupendekeza kuitishwa kwa mkutano wa viongozi wa nchi za EAC ili kufufua Mchakato wa Nairobi unaoongozwa na EAC kwa ushirikiano na Mchakato wa Luanda,” imeeleza taarifa hiyo.
Katibu Mkuu wa EAC, Veronica Nduva, alisisitiza wakati jumuiya inaendelea kukabiliana na changamoto na fursa zinazoendelea, matokeo ya mkutano huo yataongoza mipango ya baadaye inayolenga kukuza maendeleo endelevu, ustawi wa pamoja, na utulivu katika kanda.
“Ninapenda kurudia ujumbe wangu kwenye Baraza la Kawaida la 45 lililoisha hivi karibuni kuhusu umuhimu wa amani na utulivu katika kukuza uunganishaji wa kijamii, kiuchumi na kisiasa wa kanda yetu,” alisema Nduva.
Alisema ni njia ya mazungumzo pekee ndiyo itakayoiwezesha jumuiya hiyo kumaliza changamoto zake, zikiwemo za amani na usalama.
Alizisisitiza nchi wanachama kushirikiana na kuimarisha mifumo ya usalama wa kanda, kukuza utatuzi wa migogoro na kuhamasisha utamaduni wa amani ndani ya jumuiya.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, January Makamba alisisitiza umuhimu wa umoja kati ya nchi wanachama, akisema ndiyo kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
“Uunganishaji unaweza kufanikiwa tu ikiwa amani, utulivu na usalama vimeanzishwa kote kanda,” alisema.
Alisema mkutano huo uliwaelekeza mawaziri kuwezesha utekelezaji wa nguzo nne za uunganishaji: umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa fedha na shirikisho la kisiasa.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Miundombinu, Sekta za Uzalishaji, Kijamii, na Kisiasa, Andrea Malueth; Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Forodha, Biashara, na Masuala ya Fedha, Annette Ssemuwemba; Mwanasheria wa Jumuiya, Dk Anthony Kafumbe; na wajumbe wengine kutoka nchi wanachama.
|
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeipinga kauli ya kiongozi wake wa zamani, Nape Nnauye aliyesesema ushi
|
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeipinga kauli ya kiongozi wake wa zamani, Nape Nnauye aliyesesema ushindi katika uchaguzi hautokani na wingi wa kura za kwenye boksi, bali unategema nani anayehesabu na kutangaza matokeo.
Nnauye aliyewahi kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, alitoa kauli hiyo jana usiku alipotembelea soko la Kashai mkoani Kagera na kuzungumza na wananchi.
Katika kuwahakikishia ushindi wa mbunge wa Bukoba Mjini, Stephen Byabato katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Nnauye ambaye kwa sasa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alitoa kauli hiyo.
“Unajua nyie sikilizeni, matokeo ya kura sio lazima yawe ya kwenye boksi, inategemea nani anahesabu na kutangaza. Na kuna mbinu nyingi kuna halali, nusu halali na kuna haramu na zote zinaweza kutumika ilimradi tu mkishamaliza unamwambia Mwenyezi Mungu nisamehe pale nilipokosea,” alisema.
Nape anakuja na kauli hiyo, katikati ya kipindi ambacho Rais Samia Suluhu Hassan anahimiza usawa na haki katika uchaguzi, akijinasibu katika uongozi wake chaguzi zitakuwa huru.
Katika kulithibitisha hilo, ametambulisha falsafa ya R4 zenye tafsiri ya maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga upya.
Kama hiyo haitoshi, mabadiliko ya sheria tatu ikiwemo ya uchaguzi yamefanyika na kulibadili jina la tume inayosimamia uchaguzi hadi kuitwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Lakini, kauli hiyo ya Nape inakuja katikati ya malalamiko ya vyama vya upinzani juu ya kukosekana haki na uhuru katika chaguzi mbalimbali nchini.
Katika malalamiko hayo, CCM inalalamikiwa kwa kile kinachodaiwa na wapinzani kuwa kinapanga matokeo na kuiba kura.
Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Nape kutoa kauli inayofanana na hiyo, akiwa Mwenezi wa chama hicho mwaka 2015 aliposema CCM itarudi Ikulu hata kwa “Bao la mkoani.”
Kauli hiyo iliibua mijadala mitandaoni, wengi wakiitumia kama ithibati ya ushindi wa chama hicho katika chaguzi mbalimbali unahusisha njia zisizo halali.
Majibu wa CCM
Kauli ya Nape ilijibiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla alipozungumza katika mkutano wake wa hadhara katika Uwanja wa Panga ikiwa mwendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kauli hiyo haitokani na msimamo wa chama hicho.
“Kuna kiongozi nimemsikia huko mitandaoni anasema eti ushindi wa uchaguzi hautokani na kura za kwenye boksi, mimi nataka nimwambia hiyo kauli isitazamwe kuwa inatokana na CCM,” alisema.
Alisisitiza kauli hiyo isitafsiriwe kuwa msimamo wa CCM, badala yake chama hicho kinaheshimu ushindi wa haki katika chaguzi.
Kwa mujibu wa Makalla, chama hicho kitaheshimu matokeo yoyote na uamuzi wowote wa wananchi kupitia sanduku la kura.
“CCM itaheshimu matokeo yoyote na uamuzi wowote wa wananchi kupitia sanduku la kura na yeyote atakayeshinda kwa haki ndiye atakayepewa ushindi,” alisema Makalla.
Chalamila aomba radhi kiaina
Katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ni kama alikiomba radhi kiaina chama hicho kuhusu kauli yake aliyowataka wafanyabiashara wa soko la Kariakoo kuacha kuandamana kwa kwenda katika chama hicho, badala yake waende katika ofisi yake.
Katika ufafanuzi wake juu ya hilo, Chalamila alisema dhamira ya kauli yake kwa wafanyabiashara hao ni kuwataka wangeandamana kwenda katika ofisi za chama hicho ngazi ya wilaya badala ya taifa kama walivyofanya.
Kwa mujibu wa Chalamila, kilichofanywa na wafanyabiashara hao Julai 11, mwaka huu ni kama kumchongea kwa viongozi wa juu wa CCM, akieleza asingependa kuikosa nafasi aliyonayo sasa.
Mzizi wa yote hayo ni kauli yake ya Julai 12, alipozungumza na wafanyabiashara wa soko la kariakoo, akiwaambia: “Mlichokifanya wafanyabiashara kwenda CCM jana ni sawa na mgonjwa wa malaria kwenda mtu asiyetibu malaria.
“Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ipo mlipaswa kuja hapa kwa kuwa ndiyo tunaolisimamia na sio huko mlikokwenda,” alisema Chalamila.
Kauli ya Chalamila inakuja ikiwa ni siku moja tangu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla aeleze wafanyabiashara hao walikuwa sahihi kwenda katika ofisi za chama hicho.
Katika kauli hiyo, Makalla alisema kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alishawaelekeza viongozi wa chama hicho na Serikali kupokea kero za wananchi, hakuna namna CCM inaweza kujitenga nao hicho walifanya sahihi kwenda katika chama hicho.
Chalamila ameyasema hayo leo, Julai 16, 2024 alipozungumza katika mkutano wa hadhara katika ziara ya Makalla ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
“Mheshimiwa Makalla, wafanyabiashara kwenda makao makuu ya CCM ni kupotea njia kwa sababu ni kama wamekwenda kunishitaki, nilimaanisha wangeenda hata ofisi ya wilaya, Mkoa na hata ngazi za chini kabla ya kafika makao makuu,” amesema.
Kwa kuwa wameamua kuvuka ngazi mbalimbali, amesema ameona ajitetee kwa kuwaeleza walipaswa kwenda katika ngazi za chini kabla ya kufika juu.
Hata hivyo, amesema msingi wa kuyafafanua hayo ni kuondoa kile alikiita minong'ono inayoendelea katika mitandao ya kijamii kwamba yeye sio mwana-CCM.
“Naomba niseme hapa Wazo (Kawe) mimi ni mwanachama wa CCM nisiyetiliwa shaka, nafahamu ofisi ndogo ya Lumumba ndipo anapopatikana Mwenyekiti wa CCM (Rais Samia).
“Hatua ya wafanyabiashara kwenda pale ni kama wanakwenda kunichongea na kwa sababu hii nafasi niliyonayo ninaipenda nisingependa kuipoteza,” ameeleza.
|
Baada ya muda mrefu wa kutoa huduma za kisheria bila taaluma, hatimaye usaidizi wa kisheria imetambu
|
Baada ya muda mrefu wa kutoa huduma za kisheria bila taaluma, hatimaye usaidizi wa kisheria imetambuliwa na kuwa taaluma rasmi.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST) kupewa jukumu la kutoa mafunzo ya taaluma hiyo kwa ngazi ya astashahada na stashahada.
Licha ya wasaidizi wa kisheria kuwa nguzo muhimu ya utoaji misaada ya kisheria kwa wananchi mbalimbali hasa vijijini, wengi wao walikumbwa na kejeli kuwa, kazi wanazofanya hazikuwa rasmi.
Hatua ya taaluma hiyo kufundishwa katika taasisi hiyo, imeelezwa leo, Ijumaa Julai 12, 2024 na Mratibu wa Mafunzo hayo wa LST, Dk Kevin Mandopi alipokuwa katika Maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Dk Mandopi, uamuzi wa utoaji mafunzo ya wasaidizi wa kisheria kwa ngazi ya astashahada na stashahada umefikiwa ukilenga kuiimarisha taaluma hiyo.
Msingi wa kuiimarisha taaluma hiyo ni kile alichoeleza, imekuwa muhimu na msaada kwa wananchi wengi hasa vijijini, ambao aghalabu hupoteza haki zao kwa kutojua taratibu za kisheria.
“Itakuwa taaluma rasmi na inayoheshimika, Serikali imetutaka tufanye hivi kwa kutambua umuhimu wa wasaidizi wa kisheria nchini. Kama inavyotambulika kwa sasa Rais Samia Suluhu Hassan ameanzisha usaidizi wa kisheria na watu wengi wanasaidiwa,” amesema.
Amesema hadi sasa tayari kuna wahitimu 15 wa ngazi ya astashahada ya taaluma hiyo na sasa dirisha limeshafunguliwa kwa ajili ya maombi ya ngazi ya astashahada na stashahada.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini alipofanya ziara katika taasisi hiyo, pamoja na mambo mengine, alisema Serikali ipo katika hatua za kuwatambua rasmi wasaidizi wa kisheria.
Kwa sababu hiyo, alisema ndiyo maana wameona umuhimu wa kuipa LST jukumu la utoaji elimu kwa ngazi hizo katika taaluma ya wasaidizi wa kisheria.
“Wasaidizi wa kisheria ndiyo walinzi wa haki za wananchi wengi vijijini, unakuta mtu anadhulumiwa lakini kwa sababu hajui taratibu za kisheria anapoteza haki yake, hawa wasaidizi wamesaidia sana na ndiyo mwelekeo wa Serikali.
“Sio sawa unaona viongozi wanapokwenda ziarani wanakimbiliwa kwa matatizo madogo madogo, kukiwa na wasaidizi wengi wa kisheria waliobobea watawasaidia wananchi huko waliko,” amesema.
|
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk Tulia Ackson ametia mguu katika kuongeza nguvu ya shiniki
|
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk Tulia Ackson ametia mguu katika kuongeza nguvu ya shinikizo la kupatikana suluhu ya mgogoro kati ya Urusi na Ukraine.
Mgogoro kati ya mataifa hayo umevuka mwaka sasa, huku juhuzi za jumuiya ya kimataifa na wapatanishi mbalimbali zikionekana kugonga mwamba.
Hatua ya mkuu huyo wa IPU kuisaka suluhu ya mgogoro huo ni wajibu wake wa kikatiba inayoutaka umoja huo kuhakikisha ustawi wa amani miongoni mwa wanachama wake.
Mabunge ya Ukraine na Urusi ni sehemu ya wanachama wa Umoja wa Mabunge Duniani.
Dk Tulia ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, ameanza harakati hizo leo, Ijumaa Julai 12, 2024 kwa kukutana na Rais wa Urusi, Vradmir Putin jijini St. Petersburg kwa mazungumzo.
“Kabla ya kuzungumza naye tayari tulishazungumza na Maspika wa nchi zote hizo mbili na sisi kama Umoja wa Mabunge Duniani tumezungumza naye kama Kiongozi wa nchi,” amesema.
Mazungumzo hayo kwa mujibu wa Dk Tulia, yamejikita katika sura ya kuziweka pamoja nchi hizo (Urusi na Ukraine) na hatimaye mabunge ya pande zote yajadili kuhusu amani.
“Tutarajie IPU itatengeneza fursa ya Mabunge ya pande zote yazungumzie amani katika maeneo yao ya utawala,” amesema.
Hii si mara ya kwanza kwa Dk Tulia kufanya majaribio kadhaa ya kuitafuta amani kwa nchi wanachama, aliwahi kufanya hivyo katika mgogoro wa Israel na Palestina, siku chache baada ya kuchaguliwa kuiongoza IPU.
Katika mgogoro huo, Novemba 30, 2023 jijini Tel Aviv, kiongozi huyo alifanya mazungumzo na viongozi wa Israel na mamlaka ya Palestina.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma, Dk Tulia ameagiza kamati ya amani na usalama ya IPU kuhakikisha amani na usalama vinapatikana kutokana na mgogoro unaoendelea kati ya nchi hizo.
“Nimekuja kutembelea maeneo ya Palestina na Israel ambao wote hawa mabunge yao ni wanachama wa IPU.
“Lakini muhimu zaidi kuwafahamisha kuwa tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu na kamati hiyo itakuwa hapa siku zijazo kutafuta uhalisia wa mgogoro na kuleta taarifa tutakayoijadili ili tuone huko mbele tunawezaje kuwa na amani na usalama kwa watu wote," amesema Dk Tulia.
Amesema miongoni mwa msingi ya IPU ni kuhakikisha uhai wa kila binadamu unalindwa na IPU itafanya kila linalowezekana ili dunia iwe sehemu salama na ya amani kwa binadamu wote bila kujali rangi, itikadi, imani na maeneo wanayotoka.
|
Maandamano mengine ya wafanyabiashara yameibuka katika Soko la Kariakoo, wakilalamikia majina yao ku
|
Maandamano mengine ya wafanyabiashara yameibuka katika Soko la Kariakoo, wakilalamikia majina yao kukatwa katika orodha ya wanaopaswa kurejeshwa sokoni humo.
Maandamano hayo yaliohusisha wafanyabiashara zaidi ya 800, yamelenga kuushinikiza uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo kuingiza majina yao ili nao wawe sehemu ya watakaopewa vizimba katika soko hilo, linalotarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni.
Hilo linatokea zikiwa zimepita wiki tatu tangu mgomo wa wafanyabiashara utokee sokoni hapo na hatimaye nchi nzima, wakiitaka Serikali ipunguze nguvu katika ukusanyaji wa kodi na iondoe vikosi kazi vya kudai kodi.
Wafanyabiashara hao waliondolewa sokoni hapo Julai mwaka 2021, baada ya kutokea ajali ya moto iliyounguza soko hilo na kuathiri shughuli kadhaa.
Baadaye Serikali ilitangaza ukarabati na ujenzi mpya wa soko hilo kwa gharama ya Sh28 bilioni, uliokamilika mwaka huu na kwamba juzi uongozi sokoni hapo ulitangaza majina ya wafanyabiashara watakaorudishwa sokoni.
Katika orodha hiyo uongozi wa soko hilo ulitoa orodha ya wafanyabiashara 891 kati ya 1,662 watakaorejea sokoni humo, huku wengine wakikosa vigezo vya kurejea.
Hata hivyo, uongozi huo ulishaweka wazi waliorejeshwa ni wale waliokuwa na mkataba na bodi ya uongozi huo, huku wale wasiokuwa nayo wanapaswa waombe kupitia mfumo rasmi.
Mgomo ulivyokuwa
Picha lilianza kwa wafanyabiashara hao kujikusanya katika Viwanja vya Mnazi Mmoja saa 5:30 asubuhi kwa ajili ya kujiandikisha kwa maofisa wa Shirika la Masoko la Kariakoo, shughuli iliyoanza tangu saa 3:00.
Kabla shughuli hiyo haijaisha, sauti za malalamiko ya wafanyabiashara wakionyesha kuchoshwa na utaratibu wa kuhakikiwa.
Baadaye, walikusanya viti na meza walizotumia maofisa hao na kuwafanya watumishi hao waondoke viwanjani hapo.
Wakati wmaofisa hao wanaondoka, wafanyabiashara nao walianza safari ya kuendelea zilipo ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba, waliandamana hadi eneo hilo.
Nyimbo za ‘tunataka haki yetu, Tunataka soko letu’ ndizo zilizokuwa zikisikika kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Dakika chache baadaye walifika katika ofisi hizo na kupokelewa na maofisa wa CCM, akiwemo Mkuu wa Utawala wa chama hicho, Marco Mbaga aliyewataka watulie kwa kuwa tayari uongozi wa Serikali Wilaya umeshaarifiwa.
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu naye alizungumza na wafanyabiashara hao akisisitiza msimamo wa Serikali ni kuhakikisha wote wanarejea sokoni.
Walichosema wafanyabiashara
Beatrice Mmari ni mmoja wa wafanyabiashara ambao jina lake halikuwepo katika orodha hiyo, alihoji Serikali imewaacha ili wakaibe.
Mfanyabiashara mwingine, Sudi Jongo alisema siku tatu zilizopangwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao kujiandikisha ni chache, lakini ni usumbufu kwa kuwa hii ni mara ya tatu wanaandikishwa.
"Mimi niombe hii kazi ifanywe wiki moja, siku tatu hazitoshi, maana walioachwa ni wengi, hii itasaidia kila mwenye haki kurudi sokoni," alisema.
Majina yaliyoorodheshwa yamekuwa mageni kwa Mariam Zuberi aliyefanya shughuli zake miaka 15 sokoni hapo, akitaka uchunguzi ufanywe.
“Wakati soko linaungua wengine tulitoka pale tukarudi kijijini kusubiria soko lijengwe, kwa muda tumekuwa tukiishi kwa kutegemea ndugu, leo hii majina yametoka mtu haupo, wanataka familia zetu zihudumiwe na nani,” alihoji.
Mfanyabiashara mwingine ambaye jina lake si sehemu ya yaliyoorodheshwa ni Respa Bernard aliyesema licha ya ukongwe wake sokoni hapo, ameenguliwa.
“Tuimeshahakikiwa zaidi ya mara tatu, moja wakati tukiwa tunatoka sokoni, mara ya pili na viongozi wetu, mara ya tatu ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ilala, leo majina yametoka unaambiwa hauna vigezo, ni vigezo gani wanavyotaka hawa watu,” alisema.
Orodha hiyo imemwacha hata Sultan Mkagile, aliyesema katika upande wao wauza ndizi wote hawakuorodheshwa.
Kabla ya mgomo huo, Julai 5, mwaka huu, Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Hawa Ghasia aliweka wazi watakaorejeshwa ni wale wenye mikataba na shirika pekee na wasiokuwa na nayo wanapaswa kuomba kupitia mfumo rasmi.
Katika taarifa ya orodha ya majina hayo, shirika hilo lilitoa siku tatu kuanzia jana kwa wenye hoja au maoni kuhusu majina yao kutoonekana kwenye orodha ya uhakiki kufika viwanja vya Mnazi Mmoja ambako maofisa wake watakuwa wanasikiliza madai hayo.
Mgomo ulivyozimwa
Baada ya kelele na vuguvugu la maandamano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo alifika katika ofisi hizo saa 6:00 mchana, akiahidi kuwakutanisha na Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila kesho.
"Niwahakikishie hakuna mtu atakayepoteza haki yake katika hili, kesho asubuhi saa mbili tukutane kwa kwa Mkuu wa Mkoa," alisema.
Kauli hiyo ndio uliokuwa mwisho wa maandamano hayo.
|
Reli ya Kisasa (SGR) imeonekana kuwavutia wasafiri wengi tangu ilipoanza kutumika nchini, ikisafiris
|
Reli ya Kisasa (SGR) imeonekana kuwavutia wasafiri wengi tangu ilipoanza kutumika nchini, ikisafirisha abiria zaidi ya abiria 4,000 kwa siku kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Idadi ya abiria wanaosafiri kwa treni hiyo kwa siku imefikia kiwango hicho katika kipindi ambacho, safari pekee zinazofanyika ni katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.
Kwa mujibu wa TRC, idadi ya abiria wanaosafiri kwa SGR kwa siku inatarajiwa kuongezeka mara mbili ya wanaotumia sasa, pindi zitakapozinduliwa safari za Dodoma mwishoni mwa mwezi huu.
Kwa kawaida, ingechukua zaidi ya mabasi 70 kusafirisha abiria 4,000, jambo linaloonyesha dalili ya mapinduzi katika sekta ya usafirishaji hasa utakapoanza ule wa mizigo.
"Matokeo yamekuwa makubwa sana. Tunavyoongea, tiketi zote za treni ya saa 10:00 jioni leo (Jumatatu) zimeuzwa, na pengine hata ile ya kesho asubuhi (Jumanne) nayo imeuzwa," alisema Masanja Kadogosa Mkurugenzi wa TRC.
Treni hizo zilianza kutoa huduma ya usafiri kwa njia ya Dar es Salaam hadi Morogoro Juni 14, mwaka huu, huku safari za Dar es Salaam kwenda Dodoma zikitarajiwa kuanza Julai 25.
Kwa mujibu wa Kadogosa, zitakapoanza safari za Dar es Salaam kwenda Dodoma, kutafanyika mabadiliko ya muda, akidokeza pengine treni itaanza safari kutoka Dar es Salaam saa 11:00 alfajiri badala ya saa 12:00 asubuhi.
Sambamba na hilo, alieleza shirika hilo itaanzisha treni itakayoondoka Dar es Salaam saa 2:30 asubuhi.
“Mtu anayekwenda kutembea lazima achague treni ya saa 2:30 asubuhi ili kutoa nafasi kwa abiria wanaosafiri kwa shughuli za kibiashara na za dharura kama vile mikutano, watapanda ya saa 11:00 alfajiri,” alisema.
Kadogosa alisema wameanzisha maegesho ya magari katika kituo cha Dar es Salaam yatakayoegesha magari 500 kwa wakati mmoja.
“Lengo ni kuwezesha teksi na ndugu wanaowasubiri abiria kuegesha magari yao wakati wakisubiri kuwasili kwa treni,” alisema.
Hata hivyo, alieleza kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) kilichopo nyuma ya kituo cha SGR cha Tanzanite karibu na Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, pia kitasaidia kufikisha abiria eneo hilo.
"Ili kuepuka msongamano, kabla ya treni kuwasili katika Kituo cha Dar es Salaam, wanapaswa kuanza kuomba teksi treni inapokaribia kufika," alisema.
Akielezea tofauti kati ya treni hizo na zile za kawaida, Kadogosa alisema zote ni treni za SGR lakini za kisasa zinakwenda moja kwa moja hadi Morogoro bila kusimama katika kituo chochote, wakati ya kawaida ina vituo kadhaa vya kusimama.
Alisema mkazi wa Pugu anaweza kuabiri treni ya haraka ikiwa atakuja kupanda katika kituo cha Dar es Salaam (kituo cha Tanzanite) na kinyume chake.
Kwa upande wa muda, treni ya haraka inaokoa kati ya dakika 20 hadi 30 katika safari ya Dar es Salaam-Morogoro na kwamba safari ya Dar es Salaam-Dodoma itakapoanza, muda halisi unaookolewa unaweza kuwa hadi saa moja.
Kadogosa alieleza reli ina maana inapoendesha au kusafiri zaidi ya kilomita 400 bila kusimama.
Unaposafiri kwa treni ya haraka kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ndipo unaweza kuona tofauti na kuchagua ni treni gani ya kupanda.
Alibainisha treni ya haraka ni kwa abiria wenye shughuli za dharura kama biashara, kazi, mikutano na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
"Treni ya haraka ikianza saa 11:00 alfajiri inafika saa 12:30, ikimaanisha kwamba mtu anayeishi Morogoro anaweza kufanya shughuli zake za kila siku akiwa Dar es Salaam," alisema.
Hii ni sawa na nchi zilizoendelea zenye treni za SGR.
Alisema treni hiyo inasimama katika vituo vinne kabla ya kufika Morogoro.
“Inapoanza kutoka Dar es Salaam inasimama Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere na mwisho Morogoro.
"Abiria anaweza kuomba tiketi ya kupanda treni katika kituo chochote kati ya vituo vilivyotajwa tofauti na treni za haraka ambapo abiria anaweza kupanda tu katika kituo cha mwanzo," alisema.
Mtu anahitaji Sh20,000 kwa tiketi ya daraja la kawaida kusafiri kwa treni ya haraka kati ya Dar es Salaam na Morogoro, wakati abiria wa daraja la biashara na kifalme wanalipa Sh35,000 na Sh45,000 mtawalia.
Kwa treni ya kawaida, tiketi ya Dar es Salaam-Morogoro inagharimu Sh13,000 na Sh21,000 kwa daraja la kawaida na biashara mtawalia.
|
Kubweteka kisera, mawazo na mfumo wa siasa ni miongoni mwa sababu zinazotajwa kuviweka baadhi ya vya
|
Kubweteka kisera, mawazo na mfumo wa siasa ni miongoni mwa sababu zinazotajwa kuviweka baadhi ya vyama tawala vya siasa, katika mstari mwembamba wa ushindi au kushindwa kabisa chaguzi zilizofanyika hivi karibuni.
Kwa mujibu wa wanazuoni wa sayansi ya siasa, matokeo mabaya katika chaguzi za hivi karibuni dhidi ya vyama tawala, yamechochewa na kujisahau kutimiza sababu za kuwa kwao madarakani.
Mitazamo ya wanazuoni hao, inarejea kilichotokea katika chaguzi zilizofanyika kwenye nchi kadhaa mwaka huu, ikiwemo Afrika Kusini, Senegal na Ufaransa.
Katika chaguzi hizo, zilizofanyika katika miezi tofauti mwaka huu, vyama vilivyokuwa madarakani vimekumbwa na msukosuko wa ushindi, lakini vingine vimeanguka kabisa.
Chama cha ANC kilichoongoza kwa miaka 30 nchini Afrika Kusini, kimejikuta katika mtihani wa kushindwa kufikia zaidi ya asilimia 50 ya kura, zitakazokiweka madarakani.
Licha ya kuwa na mfululizo wa matokeo chanya katika chaguzi za tangu mwaka 1994, mgombea wa chama hicho cha ukombozi wa taifa hilo, Cyril Ramaphosa katika uchaguzi wa mwaka huu ameshindwa kuendeleza historia.
Katika mazingira hayo, chama hicho kwa mara ya kwanza kimelazimika kutengeneza Serikali ya Umoja wa Kitaifa kati yake na mpinzani wake wa muda mrefu, chama cha DA.
Hali inayokaribiana na hiyo imekikabili chama tawala cha nchini Ufaransa cha National Rally (RN), ambacho pamoja na ushindi wake katika kiti cha urais, kwenye viti vya ubunge kimeanguka vibaya.
Katika uchaguzi wa duru ya pili wa nchi hiyo wa mwaka huu, Muungano wa Vyama vya mrengo wa kushoto vya New Popular Front (NPF), umepata viti 168 dhidi ya 143 vya RN.
Kutokana na mazingira hayo, Rais Emmanuel Macron analazimika kuunda Serikali ya Muungano, kwa maana ya kushirikiana na wanasiasa wa mrengo wa kushoto.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Gabriel Attal yupo mbioni kuwasilisha barua ya kujiuzulu, ingawa Macron hayupo tayari kwa hilo.
Iwapo Attal atajiuzulu, Waziri Mkuu katika taifa hilo atatokana na ushindani kutoka vyama vya siasa za mrengo wa kushoto na kulia na tayari kiongozi wa NPF, Jean-Luc Melenchon ameonyesha nia ya kukitaka cheo hicho.
Katika taifa la Senegal nako, chama tawala kimeshindwa kufua dafu dhidi ya mgombea wa upinzani, Bassirou Faye aliyepitia maswaibu ya kuwekwa gerezani kwa tuhuma za kuchochea uasi, akiwa kiongozi wa upinzani.
Faye alimshinda mgombea wa chama tawala, Amadou Ba, katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo, akipata asilimia 54 katika kura za duru ya kwanza.
Kutokana na mazinmgira hayo, Mwananchi limezungumza na wanazuoni mbalimbali wa Sayansi ya Siasa, walioeleza kwa undani kilichojificha nyuma ya matokeo hayo.
Watawala wamebweteka
Kubweteka kwa vyama vilivyopo madarakani, kunakovifanya visiwe na mbinu mbadala au mpya za kuwashawishi wananchi ni moja ya sababu za hali hiyo, kama inavyoelezwa na Mwanazuoni wa Sayansi ya Siasa, Profesa Ambrose Kessy.
Kwa mujibu wa Profesa Kessy, katika siasa za vyama vingi, huwa na ushindani na anayetawala lazima abuni mbinu mbadala.
“Inapotokea wakabweteka (chama tawala) wale washindani wanaweza wakapata ushindi,” anasema.
Hayo yote yanachochewa na kile alichoeleza, kuongezeka kwa uelewa wa wananchi, kadhalika urahisi wa upatikanaji wa taarifa za utendaji wa vyama.
“Upatikanaji wa taarifa umekuwa mwepesi na kila kinachofanyika na vyama vilivyopo madarakani vinahojiwa vikihusishwa na maana vyama hivyo kuwa madarakani. Ikitokea vyama hivyo vimekosa majibu sahihi vinajiweka hatarini, ndicho kinachotokea,” anasema.
Sambamba na hayo, Profesa Kessy anahusisha kilichovitokea vyama kadhaa na kukua kwa demokrasia kulikobadilisha upepo wa siasa duniani.
“Kwa sasa ni kama kuna upepo wa kubadilika kwa wale waliopo madarakani wanapaswa kujitathmini na kwa sababu wananchi wanaelewa haki zao kuna hatari ya kuviadhibu,” anasema.
Ni wito kwa vyama tawala
Profesa Kessy anasema kinachoendelea kutokea kinatoa wito kwa vyama vinavyotawala kuhakikisha vinatimiza wajibu wake, kabla havijakumbwa na adhabu kutoka kwa wananchi.
“Kwa kadri demokrasia inavyokuwa na ndivyo mbinu za wananchi kuwaadhibu watawala zinavyoongezeka. Kuna kuadhibu kupitia sanduku la kura, lakini kuna kuwaadhibu kupitia maandamano ingawa sio njia inayopendekezwa sana,” anaeleza.
Kiu ya mabadiliko
Kwa mtazamo wa Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Dk Sabatho Nyamsenda kuna mambo mawili yanayochochea misukosuko au anguko la vyama tawala madarakani.
Mwanazuoni huyo anataja sera za vyama husika kama moja ya sababu ya hali hiyo, akifafanua vingi vinatekeleza zile zinazowapa unafuu matajiri kwa maana ya sekta binafsi, huku zikiwaumiza masikini.
Ukiachana na sera hizo, Dk Nyamsenda anaitaja sababu nyingine za hali hiyo ni kushindwa kwa vyama hivyo kutekeleza yale vilivyoyaahidi kwa muda wote vilipokuwa madarakani.
“Baada ya watu kupiga kura wanajikuta wanapoteza nguvu ya maamuzi juu ya nchi yao, lakini vyama hivyo havileti mabadiliko yoyote na wao wanakuwa hawana nguvu ndiyo maana wanaviadhibu kwa kutafuta vyama vyenye na sera mbadala,” anasema.
Ingawa wananchi hawana uhakika iwapo uamuzi wa kuchagua vyama vingine utawapa tija wanayoitarajia, anasema wanaamua kufanya hivyo ilimradi waone mabadiliko.
Hata hivyo, anaeleza hatari ya yanayoendelea ni kufikia wakati ambao wananchi hawataamini kama sanduku la kura linaweza kusaidia kuleta mabadiliko.
Dk Nyamsenda anasema utakapofika wakati huo, wananchi hao hao watatafuta namna nyingine itakayoshinikiza mabadiliko, akirejea maandamano yanayoendelea nchini Kenya.
Hakuishia hapo, anasema ikishindikana kwa njia hiyo ya demokrasia, anaeleza kilichotokea Burkina Faso cha Jeshi kuongoza nchi, kinakuwa karibu kujitokeza.
“Bila shaka unaona Rais wa Burkina Faso pamoja na kwamba amepatikana kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi lakini ni miongoni mwa viongozi wanaoungwa mkono sana na wananchi.
“Hiyo inaonyesha kwamba, wananchi walichoshwa na watawala wa kidemokrasia wakaamua kutafuta mabadiliko kwa kila namna,” anaeleza.
Kutokana na hicho kinachoendelea kwa vyama vingine, Dk Nyamsenda anatoa wito kwa vyama vingine tawala duniani, kuchukulia yanayotokea kwa wenzao kama dalili mbaya kwao.
Mhadhiri mwingine wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk Revocatus Kabobe anasema vyama tawala vimekumbwa na changamoto ya kushindwa kusimama upande wa wananchi na kutatua kero zao hasa kupanda kwa gharama za maisha.
“Chama cha siasa lazima kiwe na utamaduni wa kubadilika kulingana na wakati hasa kusikiliza wananchi wanataka nini. Sifa kuu ya vyama vikongwe Afrika kama CCM vimeweza kusalia kuongoza dola, pamoja na sababu nyingine ambazo zinasemwa, moja kuu ni sifa yake ya kubadilika kulingana na wakati,” anasema.
Pasi na kuwa na mfumo wa kufanya mabadiliko ndani na nje ya chama kulingana na mahitaji ya wananchi, anaeleza uwezekano wa kushindwa huwa mkubwa.
“Chama pekee kitakachoweza kukaa madarakani kwa muda mrefu ni kile kinachojibu changamoto za watu wake na kutoa majibu ya kero za kila siku za watu wake,” anasema.
Kutokana na hayo, anasema vyama vinapaswa kujifunza kujenga ushawishi wa hiari kwa wananchi ili vikubalike na sera zao.
Kadhalika, anasema vikishika madaraka na kuunda Serikali, lazima vifanye kazi moja kuu ya kujibu hoja za wananchi kwa vitendo.
“Msingi wa chama cha siasa ni kushika dola na kutumia dola kuhudumia wananchi wake,” anaeleza Dk Kabobe.
Mwanazuoni mwingine wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Hussein Macheta anasema vyama hivyo vinapoteza ushindi pengine kwa sababu ya kuchokwa.
Kuchokwa kwa vyama hivyo, kunasababishwa na ama vimeshindwa kutimiza matarajio ya wananchi au vimetumia ukongwe wake kama msingi wa kusalia kwake madarakani.
“Wanapaswa wawe wabunifu, waangalie wapigakura wa wakati husika ni kundi gani na wahakikishe sera zao zinaendana na kundi husika,” anasema.
|
Kama ilikuwa kiu yako kuwa na ofisi au makazi katika ghorofa na gharama kubwa ya kodi ya pango ndiyo
|
Kama ilikuwa kiu yako kuwa na ofisi au makazi katika ghorofa na gharama kubwa ya kodi ya pango ndiyo iliyokuwa kikwazo, pengine huu ni wakati mzuri wa kutimiza ndoto yako.
Hiyo inatokana na kupungua kwa zaidi ya nusu ya bei ya pango katika majengo ya maghorofa kadhaa nchini, kwa mujibu wa ripoti ya uthabiti wa kifedha Tanzania ya mwaka 2023, iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Ripoti hiyo iliyohusisha majengo 13 ya biashara na makazi, inaonyesha kati ya hayo, saba bei ya pango lake ilishuka mwaka 2023, ikilinganishwa na mwaka 2022.
Lakini, hali ilikuwa tofauti kwa majengo matatu ya maghorofa, ambayo kwa mujibu wa ripoti hiyo, bei yake ya pango ilisalia bila kubadilika katika kipindi cha miaka hiyo na matatu mengine bei iliongezeka.
Kiasi cha bei ya pango kilichopungua katika maghorofa hayo ni sawa na asilimia 53.8 kwa kipindi cha mwaka mmoja kutoka Desemba 2022 hadi Desemba 2023 kwa mita ya mraba.
Mchanganuo wa mabadiliko ya bei hizo katika ripoti hiyo, unaonyesha mita moja ya mraba katika jengo la Golden Jubilee Desemba 2022 ilikuwa Sh36,000, lakini Desemba mwaka 2023 ilikuwa na kuwa Sh25,000.
Hali kama hiyo ilishuhudiwa katika jengo la Twin Towers, ambalo kodi ya mita moja ya mraba iliyokuwa Sh32,000 mwaka 2022 ilipungua hadi kufikia Sh25,000.
“Jengo la The International House Property kodi ilipungua kutoka Sh28,000 hadi Sh25,000 kwa mita ya mraba katika kipindi cha mwaka huo mmoja,” imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.
Mafao House nalo, kodi yake imeshuka kutoka Sh16,000 hadi Sh12,000, kama ilivyo kwa Samora Avenue lililopungua bei ya kodi kutoka Sh18,000 hadi Sh16,000 na PSSF Tower I ambayo mwaka 2023 mita ya mraba inapangishwa kwa Sh17,000 kutoka Sh18,000 ya mwaka 2022. Bei hizo ni kwa mita moja ya mraba.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, bei ilishuka hata katika jengo la Quality Plaza kutoka Sh22,000 hadi Sh21,000 kwa mita ya mraba.
Kwanini zishuke?
Ingawa kupungua kwa kodi hizo ni fursa kwa wapangaji, kwa wamiliki ni maumivu, lakini maendeleo ya teknolojia yaliyosababisha kazi nyingi kufanywa mtandaoni inatajwa kuwa moja ya sababu, kama inavyoelezwa na Mwanazuoni wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Aurelia Kamuzora.
Mhadhiri huyo alisema maendeleo ya sayansi na teknolojia yanasababisha kazi nyingi kufanyika mtandaoni na hivyo wateja wa ofisi za kupanga wanapungua.
“Wakati mwingine wateja wa kupanga katika majengo hayo wanapungua kwa sababu wengi wanaanzisha kampuni mtandaoni na wanaweza kufanya huko bila kuwa na ofisi,” alisema Profesa Kamuzora.
Kuongezeka kwa majengo hayo ni sababu nyingine, inayotajwa na mwanazuoni huyo kama chachu ya wamiliki kushusha bei, akifafanua wanalenga kuvuta wateja.
“Tumewahi kufanya utafiti unaofanana na huo, bei kushuka hii inamaanisha majengo yamekuwa mengi (supply), kama ‘supply’ ni kubwa itabidi kuwe na msawazo wa biashara ambapo inalazimu wamiliki kupunguza bei ili wateja waongezeke,” alisema.
Janga la Uviko-19 nalo lililosababisha kampuni nyingi kufunga ofisi zake, kwa mtazamo wa Mack Patrick mtaalamu wa uchumi, ni sababu nyingine ya kupungua kwa kodi hiyo.
“Uviko-19 ulivyoathiri sekta ya utalii ni sawasawa na kwenye sekta ya milki, kwasababu mzunguko wa biashara ulikuwa mdogo duniani kote na majengo hayo mara nyingi wapangaji wake ni sekta binafsi ambazo miaka mitatu nyuma ziliyumba.
“Wakati mwingine katika uchumi unapunguza bei ya bidhaa ili upate wateja wengi, ndio hicho kinachofanyika,” alisema.
Meneja wa Uwekezaji wa jengo la Johari Rotana Tanzania, Doris Zeng alionyesha mtazamo tofauti, akigusia mahali lilipojengo husika na bei ya kupangisha ni sababu za kukosa wateja.
“Naamini ni mambo mawili, moja ni eneo, ikiwa wateja wako watarajiwa wako Masaki, utapata ofisi Masaki, na hautachukua ofisi katikati ya jiji. Sababu nyingine ni bajeti, baadhi ya kampuni ndogo haziwezi kumudu pango na gharama katika jengo,” alisema Doris.
Mengine bei haijabadilika
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Kodi ya pango katika Jengo la Benjamini Mkapa ilisalia kuwa Sh20,000 kwa mita ya mraba, kadhalika jengo la Social Security House ikibaki kuwa Sh16,000 na hata Commercial Complex Sam Nujoma haikubadilika ilibaki kuwa Sh27,000.
Wakati bei za pango zikishuka katika majengo mengi, ripoti hiyo pia inaonyesha kwa miaka mitatu mfululizo wastani wa kiwango cha upangaji katika majengo kinazidi kuongezeka.
“Wastani wa kiwango cha upangaji katika majengo ya biashara mwaka 2020 kilikuwa asilimia 80, mwaka 2021 kiliongezeka hadi asilimia 81 na mwaka 2022 kilifika asilimia 85,” imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.
Kuhusu kuongezeka kwa idadi ya wapangaji katika majengo hayo, ripoti inasema kunasababishwa na mzunguko wa biashara kuongezeka baada ya athari za Uviko-19 kupungua.
“Sekta ya milki iliendelea kupata nafuu kutokana na janga la Uviko-19 huku kiwango cha umiliki wa mali za kibiashara kikiongezeka kwa wawekezaji wa sekta hiyo. Viwango vya umiliki kuongezeka vinahusishwa na uboreshaji wa mazingira ya biashara, miundombinu na mahitaji,” kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Yapo yaliyoongeza kodi
Wakati bei ikishuka na kusalia kama ilivyokuwa kwa baadhi ya majengo, mengine yamepandisha bei likiwemo Rita Tower kutoka Sh16,000 hadi Sh20,000 kwa mita ya mraba, kama ilivyoelezwa na ripoti hiyo.
Victoria House nalo lilipandisha bei kutoka Sh16,000 ya mwaka 2022 hadi Sh18,000, huku PSSSF Tower II ikiongeza kutoka Sh23,000 hadi Sh25,000 kwa mita ya mraba.
Hata hivyo, ripoti hiyo imetaja sababu za kuongezeka kwa bei katika majengo hayo ni; “Ongezeko la mapato ya kaya kadri hali ya uchumi inavyoimarika na msukumo wa mahitaji kutokana na ukuaji wa idadi ya watu na ukuaji wa miji.”
|
Uamuzi wa kukataa kusoma somo la Fizikia, unadaiwa kumsababishia mwanafunzi Finileth Augustine (18)
|
Uamuzi wa kukataa kusoma somo la Fizikia, unadaiwa kumsababishia mwanafunzi Finileth Augustine (18) wa Shule ya Sekondari Kiteme, kichapo kilichomlaza Hospitali kwa siku nne tangu Julai 4, mwaka huu.
Mwanafunzi huyo, inadaiwa alijikuta akila kichapo hicho cha fimbo kutoka kwa Mkuu wa Shule hiyo,…. baada ya uamuzi wake wa kukataa kusoma somo la fizikia ambalo ni hiari kwa elimu ya sekondari.
Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo anayesoma kidato cha tatu katika shule hiyo, alichapwa fimbo mgongoni, mabegani na makalioni kiasi cha kusababishiwa majeraha.
Akizungumzia tukio hilo leo, Jumatatu Julai 8, 2024, mwanafunzi huyo amesema mkasa ulianza baada ya mwalimu huyo kumtaka asome somo la fizikia naye akakataa kwa kile alichodai haliwezi.
"Mkuu wa shule aliniambia kuwa si nimewahi kuongea nawewe lakini kuhusu somo hilo? Nikamjibu ndiyo ila siliwezi akaniambia sasa nataka leo nikuchape mpaka unisimulie," amesema.
Baada ya mazungumzo yao hayo, Finileth amesema mwalimu huyo alimwagiza fimbo, kisha akamtaka apige magoti mbele ya wanafunzi.
Wakati yeye amepiga magoti, amesema mwalimu huyo alikuwa akiendelea na mazungumzo na wanafunzi wengine, kisha akaanza kumchapa.
Licha ya kuomba msamaha, mwanafunzi huyo amesema haikufua dafu, kwani kichapo kiliendelea huku mwalimu akimwambia atamchapa hadi afikie kumpeleka hospitali.
Baada ya kichapo hicho, Finileth anasimulia alipewa wiki moja na mwalimu wake ili aamua ama asome somo hilo au afukuzwe shule.
"Nilijitahidi kunyanyuka ili niende kwenye mdahalo wa shule nikafanikiwa kwa wakati huo na kwenda ila nilishindwa kukaa nikalala hadi ulipomalizika na kuruhusiwa kurudi nyumbani," amesema.
Kutoka shuleni kwenye umbali wa kilomita nne hadi nyumbani, Finileth amesema alitembea kwa kuchechemea na kufika saa moja jioni.
Wingi wa fimbo hizo, kwa mujibu wa Finileth, ndio uliomsababishia maumivu makali na hivyo kulazwa hospitali hadi sasa.
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Jesca Augustine (58) amesema alishangazwa kumwona mwanawe akitetemeka na mwili wake ukitokwa damu.
Kama huduma ya kwanza, amesema alikwenda kuchemsha maji ya moto kwa ajili ya kumkanda na kumwagia mwili wote, lakini shughuli ilikuwa kwenye kumvua nguo kwani zilishikana na vidonda.
"Niliangalia kwenye makalio fimbo zilizopita pale ukweli nililia sana nikachana ile siketi aliyokuwa amevaa nikamuosha na kumkanda kila eneo ila aliendelea kutetemeka na kulia huku akiugulia," amesema Jesca.
Alipoona hali inakuwa mbaya zaidi, aliwasiliana na dada yake Finileth, kisha baadhi ya walimu ambao simu zao ziliita bila kupokelewa.
Baadaye, amesema mmoja wa walimu katika shule hiyoalifika nyumbani akitaka kumpeleka hospitali, lakini alimgomea akitaka aliyefanya kitendo hicho ndiye anayepaswa kwenda.
Saa saba usiku, mwalimu aliyehusika na tukio hilo, amesema alikwenda nyumbani hapo na walishirikiana kumpeleka hospitali.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo cha Kimeya alikolazwa Finileth, Dk Erasto Mosha amethibitisha kumpokea mwanafunzi huyo akiwa na majeraha mbalimbali.
Baada ya uchunguzi wa kitaalamu, amesema alibaini mwanafunzi huyo ameshambuliwa maeneo tofauti ya mwili wake.
"Nikweli tulimpokea Mwqnafunzi huyo na mpaka sasa yuko hapa anaendelea na matibabu na uangalizi wa kina kujua afya yake ila nishauri jamii, walimu na wazazi tusiwe tunapiga watoto kiasi hiki tunawasababishia matatizo makubwa ya kiafya," amesema.
Mkuu wa shule ashikiliwa
Akizungumzia hilo, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dk Abel Nyamahanga alisema tayari mwalimu huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Muleba mkoani Kagera.
“Mtuhumiwa hadi sasa anashikiliwa na Polisi, kwa sababu mgonjwa bado hajaruhusiwa kutoka hospitali amelazwa, anamalizia sindano za mwisho.
“Kwa kadri madaktari watakavyoshauri kama atatolewa, basi itajulikana kama mwalimu naye atapewa dhamana au laa,” alisema.
Sambamba na hilo Dk Nyamahanga, alisema mwalimu huyo amesimamishwa kuwa mkuu wa shule, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.
Alieleza tayari kamati ya awali ya uchunguzi wa tukio hilo, iliyoundwa na Mkurugenzi wa Muleba, imeshafika shuleni na imeanza kufanya uchunguzi kujua nini kilitokea.
|
Huenda maisha ya ustaafu ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Lain Kamendu ya
|
Huenda maisha ya ustaafu ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Lain Kamendu yakaanza kwa msukosuko, baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza arudishwe kujibu tuhuma za ubadhirifu.
Kamendu aliyestaafu utumishi wa umma, Juni 22, mwaka huu anatuhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa Bwalo la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lugalo mkoani Iringa.
Pamoja naye, Mhandisi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Sigachuma amesimamishwa kazi, kupisha uchunguzi kuhusu ubadhirifu huo, huku Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ikitakiwa kuharakisha uchunguzi.
Hilo ni moja kati ya matukio mengi ya upigaji fedha yanayofanyika katika halmashauri na serikalini kwa ujumla na Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby aliwahi kueleza juu ya kukithiri kwa vitendo hivyo.
“Wapigaji ni wengi, wengine utasikia tu, mama anaupiga mwingi, sio anaupiga mwingi kwamba anamsifia kwenye moyo, anaupiga mwingi yeye anaiba fedha. Anatandika fedha alafu akija huku anajifanya anasifia,” alisema Juni 21, alipokuwa akichangia Bajeti ya Serikali na Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2024/25.
Kama hiyo haitoshi, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha unaoishia 2023, ilibainisha halmashauri nchini zimeshindwa kukusanya Sh61.15 bilioni kutoka vyanzo muhimu.
Majaliwa alitoa agizo hilo jana, alipozungumza na wananchi wa Kilolo mkoani Iringa, baada ya kukagua ujenzi wa shule hiyo, aliyosema hakufurahishwa na maendeleo yake.
Mzizi wa madai ya ubadhilifu huo ni kile kilichoelezwa na Majaliwa kuwa, bwalo hilo halijakamilika ilhali Serikali ilitoa Sh774 milioni na Sh341 milioni zimetumika huku nyingine Sh433 milioni hazijulikani zilipo.
“Taarifa za hapa hazijanifurahisha. Serikali tumeleta fedha zote Sh3 bilioni kwa ajili ya kujenga majengo yote yaliyo ainishwa kwenye ujenzi huu likiwemo jengo la utawala, mabweni , madarasa, chumba za huduma za afya, maabara na nyumba za walimu,” alisema.
Alisema ilitakiwa ujenzi huo usimamiwe na uende kwa wakati lakini haujakamilika ikiwamo bwalo hilo, jambo ambalo amedai hawawezi kuwaacha wale wakiwa wima.
Waziri Mkuu alisema kwenye jengo la utawala, fundi madirisha hajaweka nyavu, amemaliza kazi na kwamba tayari amelipwa fedha yote.
“Lazima leo atafutwe yule fundi aletwe hapa aweke nyavu kwenye lile jengo la utawala. Amemaliza kazi, amekabidhi na hajaweka nyavu, atakuja kuweka lini? Lazima aletwe hapa. Mkuu wa Wilaya simamia hili, mhandisi ambaye ameshindwa kusimamia haya nitaeleza baadae,” alisema.
Alisema amekagua ujenzi wa madarasa amefanya ujanja wa kuhamisha madawati mabovu na kuyaficha huku darasani yakibaki mazima.
“Madawati yale yaliyo chanika chanika, kiti mguu mmoja mfupi mmoja mrefu haikubaliki, hii ni fedha ya wananchi lazima thamani yake ionekane. Nimeagiza aitwe aliyetengeneza madawati na roli lake kwa gharama yake aende akatengeneze upya atuletee madawati yetu safi,” alisema Majaliwa.
Akizungumzia jengo la maabara, alisema kuna mifuniko inayopitisha maji, nyaya za umeme, bomba za gesi lakini badala ya kutengeneza vizuri, wamepachika tofari jambo ambalo litawafanya walimu kushindwa kufanya kazi yao.
“Mwalimu akigundua gesi inavuja mahali atatoaji lile tofari na nyie mmegandamiza hakuna hata mahali pa kuingiza kidole. Mtataka kumpa kazi nani? maana yake waje wabomoe, wafuatilie gesi inatoka wapi. Ondoa yale yote na tengeneza upya,” alisema.
Majaliwa aliagiza Mkurugenzi arudishwe kuja, Mhandisi kusimamishwa kazi ili wapelekwe mahakamani na kueleza Sh774 milioni zimetumikaje.
“Mhandisi akae pembeni hadi uchunguzi tujue nani ni nani na yeyote aliyeingia ndani tutamchukua popote alipo,” amesema.
Ameagiza wote waliohusika kusimamishwa kazi ili uchunguzi ufanyike.
“Tunapokuta haya madude dude lazima tuchukue hatua,” amesema Majaliwa.
Amesema ujenzi wa Chuo cha Biashara (CBE) lazima ujenzi huo usimamiwe ipasavyo.
Afisa elimu kwa sababu ye aliondolewa maana yake mlikuwa hamtaki aje kuona madude yeye atapata onyo kali na mjue anapaswa kusimamia miradi ya elimu.
“Takukuru Mkoa ingia kazini na nyie msichunguze kesi mwaka mzima na hawa nataka tujue kama wamehusika au lah. Wananchi nataka niwaambie tutaendelea kusimamia miradi yote ya Serikali na kuchukua hatua kwa wale ambao hawatekelezi matakwa ya nchi yetu,” amesema Majaliwa.
Ameagiza halmashauri ya Wiulaya ya Kilolo kutumia fedha za mapato ya ndani kujenga jengo la dharura kwa ajili ya eneo la kupata chakula.
Ujenzi wa CBE
Majaliwa amesema Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa Chuo cha Biashara CBE wilayani Kilolo ikiwa ni mkakati wake wa kuongeza vyuo vya biashara.
Amewaagiza wasimamizi wa ujenzi Wilayani Kilolo kuhakikisha wanasimamia
|
Katika hali isiyotabirika, mgomo na maandamano ya wafanyabiashara wadogo maarufu Machinga ulizuka kw
|
Katika hali isiyotabirika, mgomo na maandamano ya wafanyabiashara wadogo maarufu Machinga ulizuka kwa takriban saa tano katika Soko la Simu2000 jijini Dar es Salaam.
Mzizi wa mgomo huo, ni kuishinikiza Manispaa ya Ubungo ifute uamuzi wake wa kukabidhi eneo linalotumiwa na Machinga kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) kwa ajili ya kujenga karakana.
Manispaa hiyo ilitoa taarifa ya kufanya uamuzi huo, Julai 4, mwaka huu katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoeleza, tayari baraza hilo na manispaa zimeridhia ombi hilo la Dart, baada ya vikao mbalimbali ikiwemo wakala huo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko.
“Baada ya majadiliano hayo na baada ya madiwani kuonyeshwa mchoro mzima wa mradi huo na wao kutafakari na kuona wafanyabiashara waliopo pale watakwenda wapi, hivyo basi leo hii (Julai 4), baraza limeamua rasmi kwamba eneo litolewe kwa Dart,” alisema Meya wa Manispaa hiyo, Jaffar Nyaigesha.
Kutokana na taarifa hiyo iliyochapishwa katika mitandao ya kijamii ukiwemo ukurasa wa Instagram wa Manispaa ya Ubungo, wafanyabiashara katika soko hilo wamesema kilichofanyika ni kama kuwafukuza katika eneo waliloaminishwa watakuwepo wakati wote.
“Tuliaminishwa eneo hili ndilo yatakuwa makazi rasmi ya biashara zetu baada ya kuhamishwa hamishwa kutoka barabarani na maeneo mengine mengi ndani ya Manispaa hii, leo hii tunasikia habari za kuja Dart, wameamua kutufukuza,” alisema Mussa Ndile Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Maboresho ya Soko hilo ambaye pia ni mfanyabiashara sokoni hapo.
Saa tano zilivyokuwa
Mgomo na maandamano hayo yalianza saa 1 asubuhi wafanyabiashara wakijikusanya katika lango la kutokea kwenye Kituo cha Daladala cha Simu2000.
Kujikusanya kwao kuliambana na kuweka vizuizi katika malango yote la kuingilia na kutokea magari kwenye kituo hicho, huku kila duka na biashara sokoni hapo ikiwa imefungwa.
Si hivyo tu, vizuizi pia viliwekwa katika barabara ya Simu2000 kwenda Sinza na hivyo kuzuia shughuli za usafirishaji wa abiria zilizokuwa zinafanywa na daladala.
Nyimbo za 'hatutaki karakana tunataka soko letu' ndizo zilizokuwa zikisikika zikiimbwa na waandamanaji katika eneo hilo, huku mabango yaliyoandikwa jumbe mbalimbali ikiwemo 'hatutaki karakana Simu2000, Mama Samia njoo ututetee.'
DC Ubungo afukuzwa
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vilianza kuingia katika eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara, bila mafanikio na saa 3 asubuhi alifika Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko.
Wafanyabiashara walimtaka Bomboko aondoke katika eneo hilo kwa kile walichodai, walishamwita kwa takriban mara tatu, lakini aliwapuuza.
Kutokana na mabishano yaliyokuwepo kati ya wafanyabiashara na vikosi vya ulinzi na usalama, ilibidi Bomboko asogee kwa umbali na mita kadhaa kutoka eneo walilokuwepo wafanyabiashara, bila kufanikiwa kuzungumza nao chochote.
Shangwe na hali ya kuzomewa ilizuka kutoka kwa wafanyabiashara hao wakifurahia kusogea kwa kiongozi huyo.
Baada ya kusogea pembeni, Bomboko alizungumza na vyombo vya habari akihoji ni kiongozi gani aliyetangaza eneo hilo limebadilika matumizi na kwenda kwa Dart kwa ajili ya kujenga karakana.
“Taarifa hizi mmepata wapi, tusaidiane hapa ili tuone, sisi tumekuja kusikiliza baada ya kupata taarifa wafanyabiashara wenye maduka na bodaboda wanazuia daladala zisiingie ndani mawasiliano,” alisema.
Alieleza ujio wake katika eneo hilo ni kujiridhisha na uhalisia wa taarifa alizosikia kuhusu kusitishwa kwa usafiri wa daladala, kadhalika taarifa inayodai soko limeuzwa kwa wachina.
“Hii ni taarifa ninayosikia kutoka kwa wafanyabiashara ni Mchina gani aliyenunua soko, lakini kiongozi gani aliyetangaza kwamba hili eneo linakwenda kubadilishwa matumizi,” alisema.
Kwa mujibu wa Bomboko, kuna siasa katika eneo hilo akisema ni vuguvugu lililoanza katika maeneo mengi zikilenga kuifanya Serikali iache kuendelea na mambo ya msingi.
“Ombi langu ni kwamba tuache wafanyabiashara wengine walio tayari kufanya biashara waachwe waendelee lakini wale ambao wana mashinikizo yao, Serikali ipo tayari kuwasikiliza,” alisema.
Ahadi ya Chalamila
Saa 4 asubuhi mgomo na maandamano hayo yalisababisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila afunge safari hadi sokoni hapo.
Haikuwa kama kwa Bomboko, wafanyabiashara hao walimpongea kwa shangwe Chalamila huku nyimbo za kumsifu na kuonyesha tumaini kutokana na ujio wake zikiimbwa.
Katika mazungumzo yake, Chalamila aliahidi kukutana na wafanyabiashara hao Julai 13, mwaka huu akiwa na mamlaka zote zinazolalamikiwa.
Kwa mujibu wa Chalamila, kukutana kwake na wafanyabiashara hao itakuwa baada ya kuzisikiliza mamlaka zote kisha atataka kuzisikiliza mbele ya Machinga hao.
Hata hivyo, alikiri kuwepo kwa mpango wa Dart kupewa sehemu ya eneo hilo, ingawa amedai alielekeza Manispaa ya Ubungo izungumze na wakala huo kisha iliwasilishe jambo kwake.
"Hili linalosemwa kwa asilimia 100 lipo, lisemwalo lipo ndugu zangu, lakini bado halikuwa limefika ofisini kwangu, lakini mlipaswa kushirikishwa," alisema.
Aliwataka wafanyabiashara wafungue biashara na kuendelea na shughuli zao, akisisitiza Julai watasikia kutoka kwa Serikali uhalisia wa jambo wanalogomea.
Lakini, Mkuu huyo wa Mkoa alisema kabla ya uamuzi wowote ilikuwa muhimu wafanyabiashara kushirikishwa, akisisitiza “imetosha kuendelea kuwanyanyasa wafanyabiashara.”
"Leo ni Jumatatu naomba mundelee na kazi zenu hadi Jumamosi nitakuja nataka kumsikiliza mtu wa Dart na wengine wote, kisha kwa kuwa sio siri nikija jumamosi nitakuwa nao ili wanieleze mbele yenu," alisema.
Awali, kabla ya kuzungumza, Chalamika alitoa nafasi kwa wafanyabiashara waeleze sababu ya kugoma kwao, Ndile alikuwa miongoni mwa wazungumzaji.
Katika maelezo yake, Ndile alionyesha hofu ya wafanyabiashara kuhamishwa katika eneo hilo kutokana na Manispaa ya Ubungo kuvunja ahadi yake ya kuwaacha waendelee kulitumia, badala yake inawakabidhi Dart.
Alieleza licha ya Serikali kutumia takriban Sh300 milioni kwa ajili ya maboresho hayo, inaonekana Manispaa hiyo haioni umuhimu wake, ndiyo maana inaamua kulikabidhi kwa wakala huo.
Alikwenda mbali zaidi akieleza pamoja na uwekezaji uliofanywa na Serikali, wafanyabiashara nao wamewekeza fedha zao kuboresha vibanda hivyo.
“Tulikubali kuhamishwa barabarani na katika maeneo mengine ya barabara na tuliambiwa hapa ndiyo yatakuwa makazi yetu ya kudumu iweje leo anapewa Dart,” alisema.
Historia ya soko
Meya mstaafu wa Ubungo (Chadema), Boniface Jacob alichapisha katika ukurasa wake wa X (zamani Twitter), akisema atawarudisha wafanyabiashara hao barabarani.
Chapisho lake hilo, linatokana na kile alichoeleza, ni yeye akiwa Diwani wa Kinondoni mwaka 2010-2015 halmashauri hiyo ilinunua ekari tano za eneo hilo kutoka kwa Shirika la Posta lililokuwa linalimiliki.
Baada ya kununua, alisema liligawiwa kwa ajili ya matumizi ya Stendi ya daladala, choo cha umma na soko la mazao na biashaara ndogondogo mwaka 2013.
Baadaye mwaka 2016 alipokuwa Meya wa Kinondoni, alisema walizungumza na wafanyabiashara kuwaondoa katika maeneo ya barabara ikiwemo Ubungo Mataa na wote walikubali.
“November 2017 baada ya mgawanyo wa Halmashauri ya Kinondoni na Ubungo, sisi wa halmashauri mpya ya Ubungo tuliwaomba wenzetu watuachie Stendi ya Mawasiliano na soko hilo la Simu2000,” aliandika.
Hilo lilitekelezwa kwa makubaliano kuwa, Manispaa ya Ubungo itaiachia Kinondoni Stendi ya Makumbusho na soko la Makumbusho na kwamba anashangazwa na uamuzi wa Julai 4, mwaka huu wa baraza la madiwani.
Uwekezaji wa Dart
Katika mazungumzo yake na Mwananchi juzi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Aron Kagurumjuli alikiri kuwepo kwa mpango huo akifafanua hautaathiri uwepo wa wafanyabiashara wala kituo cha daladala.
Kwa mujibu wa Kagurumjuli, hakuna machinga atakayeondolewa katika eneo hilo kutokana na utekelezwaji wa mpango huo, zaidi ya kuboreshewa zaidi maeneo yao ya kufanyia shughuli zao.
“Kabla ya lolote wataboreshewa kwanza eneo la kufanyia biashara, likishakamilika kuboreshwa watapewa ni hapohapo wala si kwingine,” alisema.
Katika maboresho hayo, Mkurugenzi huyo alisema vibanda 989 vya machinga, fremu za maduka makubwa 186 na maeneo ya mama na babalishe yatajengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao.
Alisisitiza tathmini imeshafanyika na imebainika eneo litakalojengwa kwa ajili ya wafanyabiashara litawatosha waliopo na mengine yatabaki.
|
Hali ya hofu imezuka katika makaburi ya sabasaba jijini Mbeya, baada ya watu wasiojulikana kuyageuza
|
Hali ya hofu imezuka katika makaburi ya sabasaba jijini Mbeya, baada ya watu wasiojulikana kuyageuza makaburi hayo kuwa vitanda kwa ajili ya malazi.
Hofu zaidi inatokana na matukio ya kustaajabisha yanayofululiza katika eneo hilo, ikiwemo watu hao wanaolala juu ya makaburi hujifunika nguo nyeupe mithiri ya sanda.
Kwa mujibu wa wakazi wa maeneo hayo, si ajabu kukuta nazi zimevunjwa, vyungu na zaidi baadhi ya watu huogeshana hadharani katika njiapanda iliyopo karibu na makaburi hayo.
Gazeti hili, limefanya uchunguzi katika eneo hilo kwa takriban wiki tatu na kubaini uwepo wa vitu mbalimbali zikiwemo nguo, viatu karibu na makaburi hayo.
Wakati wananchi wakiwa na hofu hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) kutuma kikosi kazi kufanya doria kisha limpe mrejesho.
Mwananchi limezungumza na baadhi ya wakazi wa maeneo ya karibu na makaburi hayo, walioeleza kwa sehemu kubwa watu hao ni wahalifu na wanayatumia makaburi hayo kama sehemu ya kujificha.
Kutokana na mazingira hayo, walisema imekuwa vigumu kwa ndugu wa marehemu waliozikwa kwenye makaburi hayo kwenda kufanya usafi.
"Tunashuhudia mambo ya ajabu licha ya watu kuweka hifadhi wapo wengine wanakuja kufanya matambiko ya kishirikina kwa kufukia vichwa vibichi vya mbuzi na kuku wakiwa hai kwenye mabakuri yaliyojengewa pembeni na ambayo hayajajengewa kabisa,” alisema mmoja wa wananchi kwa sharti la kutotajwa jina.
Muda wa matukio
Mwananchi mwingine karibu na maeneo hayo, alieleza watu hao hulala makaburini hapo kuanzia saa 8 usiku na huamka saa 11.45 alfajiri na wakati mwingine saa 12, huku wale wanaovunja vyungu wakifanya mambo yao nyakati za usiku mnene.
"Ukiwa mtu wa wasiwasi huwezi kuvumilia mambo tunayoona, kama Polisi wanafanya doria muda huo ndio mzuri hawata kosa watu watumie mbinu za kiintelejensia kwani wapo wanajibanza uwezi kudhania kama kuna watu wamelala," alisema.
Kinachodaiwa kusababisha watu hao kugeuza makaburi hayo kuwa malazi yao, ni kile kilichoelezwa hawakubaliki katika jamii hivyo wameamua kuishi humo.
"Wapo kama wawili ni sugu wameishi ndani ya makaburi kwa zaidi ya miaka 25 niliwafukuza lakini waliendelea na kwa vificho, kuna wakati niliwategea niwakamate ili wachukuliwe hatua waliponiona walikimbia na kuacha vitu vya thamani kama nguo ambazo uwenda ziliibiwa nami nilizichoma moto," alisema mmoja wa wananchi.
Kwa upande wake, Kijana aliyelala kwenye makaburi hayo, Amani Agustino alisema analazimika kuishi eneo hilo kutokana na kukosa sehemu ya kulala kufuatia hali duni ya maisha na doria za mara kwa mara katika kituo kikuu cha mabasi ya mikoani.
"Mimi nimetokea Mkoa wa Rukwa nilikuja kusaka maisha awali nilikuwa nalala kituo kikuu cha mabasi ya mikoani lakini baada ya kujenga uzio na kuimarisha ulinzi nimekuja kuweka hifadhi hapa ingawa tupo wengi wengine ni kweli waharifu ambao ufika usiku wa manane na kutoka alfajiri sana," alisema.
Kauli za wananchi
Mkazi wa sabasaba anayejihusisha na shughuli za kukata majani ya mifugo, Alex Alex alisema idadi kubwa ya waliofanya makaburi kuwa hifadhi yao ni wahalifu.
"Hawa jamaa sio watu wa kawaida kwa sababu sehemu ya makaburi sio rahisi mtu unaenda kulala pasipo hofu yoyote na kama sio waharifu basi ni masuala ya imani za kishirikina," alisema.
Alisema ili kurejesha amani kwa jamii ni Jeshi la Polisi kuingilia kati kwa kufanya doria na watakaobainika wahojiwe kwa kuwa si wenyeji wa maeneo hayo.
Kisa mkasa
Sekela Joel mkazi wa Forest alisema amewahi kunusurika kubakwa majira ya alfaji akielekea Hospitali ya Rufaa Kanda kuona wagonjwa.
"Nilipita eneo la jirani na makaburi hayo lengo nipite sehemu kuna daraja linaunganisha na Kata ya Jakalanda na Mbalizi road ghafla nilikuta vijana wawili wameziba sura wakinifuata nyumba nililazimika kukimbia ndio kunusurika lakini walifanikiwa kuvuta kikapu kilicho kuwa na mahitaji ya mgonjwa," alisema.
Familia waliozika ndugu
Happy Fredy alisema mazingira ya eneo hilo kwa sasa sio salama kwani wanashindwa kuwahi alfajiri kusafisha makaburi kutokana na watu hao wanaolala makaburini.
"Kiuhalisia kama ujawahi kuona unaweza kukimbia kwani ni mithiri ya mtu aliyehifadhiwa kwenye sanda na ukiwaita wanaitika kwa sauti nzito kwa madai wako nyumbani kwao hawahitaji kelele," alisema.
Ombi
Aliiomba Serikali kuona umuhimu wa kujenga uzio katika makaburi ili kuepuka watu mbalimbali kulitumia eneo hilo kama maficho yao.
"Hapa sio kulala tu hata imani za kishirikina zinafanywa sana na jamii yenye imani haba kwa kuzika kuku wazima ardhini ambao zaidi ya mara mbili nimeshuhudia," alisema.
Kauli ya Viongozi
Akizungumza kwa masharti ya kutoandikwa jina gazetini mmoja wa kiongozi alisema matukio ya watu kulala yaliwahi kuripotiwa na hatua zilizochukuliwa ikiwemo kufanya doria na kuwabaini .
"Hayo yaliwahi kutokea tulifuatilia lakini tulio wabaini baada ya kuhoji walikuwa hawana sababu za msingi ,kimsingi suala hilo kama limejirudia tutalifanyia kazi," alisema.
Kauli ya Polisi
Akizungumza na Mwananchi kuhusiana na matukio hayo hususan vijana kuweka hifadhi makaburini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga alisema amelipokea suala hilo na kulifanyia kazi.
"Siwezi kujibu moja kwa moja kama nalielewa muda huu ,nitamuagiza Mkuu wa Upelekezi Wilaya(OCD)kupanga kikosi kazi kufanya doria kwenye maeneo ya makaburi ya sabasaba ili kuwabaini watu hao," alisema.
Kuzaga aliwataka viongozi wa ngazi za kata na vijiji, kuhamasisha doria za polisi jamii na ulinzi shirikishi ili kukabiliana na matukio ya uharifu katika maeneo yasiyo salama kwa jamii hususan kwenye makaburi.
|
Hofu imezuka kwa wafanyabiashara wadogo maarufu Machinga katika Soko la Simu2000, baada ya kuwepo mp
|
Hofu imezuka kwa wafanyabiashara wadogo maarufu Machinga katika Soko la Simu2000, baada ya kuwepo mpango wa sehemu ya eneo hilo kukabidhiwa kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao, Dart inapewa eneo hilo kwa ajili ya kujenga Karakana ya mabasi yake, mbadala wa ile iliyopo Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kinachozusha hofu miongoni mwao ni kile wanachoeleza, walikabidhiwa eneo hilo na kuahidiwa ndilo litakalokuwa rasmi kwa shughuli zao baada ya kuhamishwahamishwa kutoka maeneo mbalimbali, lakini inakuwaje linakabidhiwa kwa Dart.
Sambamba na hayo, machinga hao wanahofu uwepo wa Dart katika eneo hilo, utawanaondoa baadhi yao, kadhalika kukiondoa Kituo cha Daladala cha Simu2000, ambacho ndicho tegemeo lao la kupata wateja wanaofika hapo kusubiri usafiri wa kwenda maeneo mbalimbali.
Kutokana na mazingira hayo, Mwananchi linazo taarifa za maandalizi ya mgomo wa machinga katika soko hilo, unaotarajiwa kuanza leo, wakishinikiza Serikali iwasikilize na kubadili uamuzi wake.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo lilipo eneo hilo, Aron Kagurumjuli amesema pamoja na Dart kujenga karakana yake katika eneo hilo, hakuna mfanyabiashara atakayeathirika zaidi ya kuwekewa mazingira mazuri.
Madai ya wafanyabiashara
Akizungumza na Mwananchi jana, mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema kinachowapa hofu ni uamuzi wa makabidhiano ya eneo hilo kufanywa bila wafanyabiashara kushirikishwa.
Alieleza walipaswa kushirikishwa tangu Dart ilipowasilisha kusudio au ombi la kupewa eneo hilo, ili wajadili kwa pamoja kama inawezekana au vinginevyo.
“Hatukushirikishwa na tunashangaa juzi (Julai 4, mwaka huu) Manispaa inatangaza kuwa eneo hilo la Stand na Soko wamepewa Dart ili wajenge Karakana ya mabasi,” alisema.
Lakini hilo, alisema limefanyika wakati tayari wafanyabiashara hao walishakuwa na tetesi za Dart kupewa eneo hilo tangu Oktoba mwaka jana na hawakuwahi kuambiwa rasmi.
Katika tetesi za Oktoba mwaka jana, alisema wafanyabiashara waligoma na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba alikwenda na kuwaambia hakuna mpango wa Dart kupewa eneo hilo.
“Hata mwaka mmoja haujaisha tangu eneo hili liboreshwe na Serikali na wafanyabiashara kutumia fedha zao kukamilisha maboresho hayo Manispaa ya Ubungo inatangaza imewapa Dart,” alisema.
Mfanyabiashara mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Amos alisema kinachomuumiza ni uwekezaji wa kumalizia ujenzi wa banda la biashara alioufanya ambao hatimaye unakwenda kupotea.
“Nimetumia karibu Sh500,000 kuboresha banda langu, leo hii tunapoambiwa Dart wanakuja na tumezoea kuhamishwa hamishwa inatupa wakati mgumu. Kwa nini tusingeambiwa mapema ili tujadiliane,” alisema.
Uamuzi huo wa manispaa ya ubungo, umemkatisha tamaa ya biashara Neema Swai anayefanya biashara katika soko hilo.
Neema alisema alidhani Simu2000 ndiyo eneo la mwisho kuhamia kibiashara, lakini kwa dalili anazoziona muda si mrefu atahamishwa tena na Serikali.
“Kila nilipohamishwa nilipoteza mtaji, kuhama kunafilisi huku nako wametufuata kwanini wasingepewa maeneo mengine kwani Ubungo ina Simu2000 pekee,” alihoji.
Mwananchi linazo taarifa kuwa, eneo hilo lina jumla ya mita za mraba 36,000 na kati ya hizo, Manispaa imepanga kuipa Dart 30,000 na mita za mraba 6,000 ndizo zitumike na wafanyabiashara.
Katika soko hilo, kuna wafanyabiashara zaidi ya 1,000 na wanaeleza mita za mraba zitakazoachwa kwa ajili yao hazitatosha.
Hofu nyingine za wafanyabiashara kutokana na uamuzi huo wa Manispaa ni kuondoka kwa kituo cha daladala, wakisema kikiondolewa hakutakuwa na mzunguko wa biashara.
Kinachowashangaza, iweje viongozi wote waliopita, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Amos Makala wawaaminishe kuwa eneo litakuwa chini yao wakati wote na sasa kufanyike vinginevyo.
Baraza la madiwani laridhia
Katika taarifa ya kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ubungo ya Julai 4, mwaka huu, Meya wa Manispaa hiyo, Jaffar Nyaigesha alisema baraza hilo limeridhia kuipa Dart eneo hilo.
“Baada ya kutafakari maombi hayo (ya Dart), hatimaye Manispaa ya Ubungo imekubaliana na ombo hilo. Ombi hilo limeridhiwa baada ya kupitia vikao mbalimbali ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya na vikao vya wataalamu wa manispaa,” alisema.
Sambamba na vikao hivyo Nyaigesha alisema kamati ya fedha ya baraza la madiwani la manispaa nalo lilijadili kisha baraza la madiwani kwa ujumla wake limejadili.
“Baada ya majadiliano hayo na baada ya madiwani kuonyeshwa mchoro mzima wa mradi huo na wao kutafakari na kuona wafanyabiashara waliopo pale watakwenda wapi, hivyo basi leo hii (Julai 4), baraza limeamua rasmi kwamba eneo litolewe kwa Dart,” alisema.
‘Baraza limegawa kimagumashi’
Licha ya taarifa hiyo ya Nyaigesha, Mwananchi imearifiwa kuwa, kilichoelezwa na Meya huyo si msimamo wa baraza la madiwani.
Kadhalika, chanzo hicho ambacho ni sehemu ya wajumbe wa kikao cha baraza hilo, kimesema hawakuwahi kujadili kuhusu kukabidhi eneo hilo kwa Dart isipokuwa waliwahi kupewa elimu tu.
“Hata hicho kikao cha Julai 4, hakikuwa cha kujadili kuwapa Dart eneo, tuliitwa kwa ajili ya kupewa elimu ya namna Dart itakavyolitumia eneo, lakini tunashangaa baadaye inatoka taarifa kwamba tumeridhia, wamepewa kimagumashi,” alisema.
Chanzo hicho, kinadai kuna watu wamenunuliwa kuhakikisha suala hilo kuhakikisha baraza la madiwani linapitisha suala hilo haraka.
Manispaa ya Ubungo
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli alikiri kuwepo kwa mpango huo akifafanua hautaathiri uwepo wa wafanyabiashara wala kituo cha daladala.
Kwa mujibu wa Kagurumjuli, hakuna machinga atakayeondolewa katika eneo hilo kutokana na utekelezwaji wa mpango huo, zaidi ya kuboreshewa zaidi maeneo yao ya kufanyia shughuli zao.
“Kabla ya lolote wataboreshewa kwanza eneo la kufanyia biashara, likishakamilika kuboreshwa watapewa ni hapohapo wala si kwingine,” alisema.
Katika maboresho hayo, Mkurugenzi huyo alisema vibanda 989 vya machinga, fremu za maduka makubwa 186 na maeneo ya mama na babalishe yatajengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao.
Alisisitiza tathmini imeshafanyika na imebainika eneo litakalojengwa kwa ajili ya wafanyabiashara litawatosha waliopo na mengine yatabaki.
Baada ya hatua hiyo, alisema ndiyo utekelezaji wa ujenzi wa karakana ya Dart utaanza na kwamba hakutakuwa na muingiliano kati ya biashara za machinga na mradi huo.
Kuhusu kituo cha daladala, alisema hakitaathirika badala yake safari za usafiri huo kwenda eneo hilo zitaongezeka ili watu wakapande mabasi yaendayo haraka.
“Hakitaathirika litakuwa eneo bora zaidi kuliko maeneo mengine yote na litakuwa na biashara kubwa zaidi kuliko mengine yote, ukizingatia kitaunganishwa na kituo cha uwekezaji cha Ubungo,” alisema.
Kwa mujibu wa Kagurumjuli, mipango ya Serikali juu ya maendeleo ya wananchi inabadilika kila siku na aghalabu utekelezwaji wake unazingatia tija iliyopo.
“Hakuna mpango wa maendeleo unaopangwa na Serikali unaokuja kuwa shida baadaye kwa wananchi wake, hakuna mpango wa namna hiyo,” alisisitiza.
Alipoulizwa ni lini mradi huo utaanza, alisema kwa sasa wapo katika hatua ya kukamilisha michakato ya ndani kisha kwenda kuzungumza na wafanyabiashara kuwaelimisha kuhusu mpango wote ulivyo.
“Wasubiri waambiwe waangalie utekelezaji wa programu yenyewe ndiyo waseme changamoto,” alisema.
Historia ya machinga na eneo hilo
Chimbuko la biashara za machinga katika soko hilo ni agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la Septemba mwaka 2021 alipotaka wafanyabiashara hao wapangwe kutoka barabarani hadi katika maeneo rasmi.
Manispaa ya Ubungo chini ya Mkuu wa Wilaya wa wakati huo, Kheri James iliratibu jambo hilo na kuwahamisha machinga kutoka maeneo mengine yote na kuwapeleka Simu2000.
Hatua hiyo ilifuatiwa na maboresho ya soko hilo yaliyozinduliwa na Makala (alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam), June 2022 na Sh70 milioni zilitolewa kufanikisha hilo kwa awamu ya kwanza.
Baadaye Mei 2023 Manispaa ya Ubungo ilitoa Sh100 milioni kwa ajili ya maboresho zaidi yaliyohusisha ujenzi wa mabanda na kisha ilitoa Sh39 milioni na kufanya jumla ya vibanda vilivyojengwa vifikie 234.
Kati ya vibanda hivyo, 170 viligawiwa kwa wafanyabiashara Septemba mwaka jana na vingine41 viligawiwa baadaye.
|
Uamuzi wa Serikali kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu Machinga katika barabara na kuwapatia ma
|
Uamuzi wa Serikali kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu Machinga katika barabara na kuwapatia maeneo rasmi ya kufanyia shughuli zao, umeonekana kugonga mwamba.
Hiyo ni baada ya makundi ya wafanyabiashara hao, kushuhudiwa wakirejea kwa kasi barabarani, huku ugumu wa biashara katika maeneo waliyopangiwa, wakiitaja kuwa moja ya sababu.
Kwa mujibu wa machinga wenyewe, kupangwa kwao katika maeneo yaliyotajwa kuwa rasmi kwao, umefanyika bila kuzingatia miundombinu sahihi, hali iliyochochea uchache wa wateja na hivyo kudumaza biashara zao.
Kwa sababu hiyo, wafanyabiashara hao katika mikoa mbalimbali nchini, wameyahama maeneo waliyopangiwa na kurejea barabarani, wanakodai kuna idadi kubwa ya wateja.
Vuguvugu la kupangwa kwa wafanyabiashara hao, lilianza Septemba 13, 2021 na kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan, aliyewataka wakuu wa mikoa yote nchini kuratibu jambo hilo bila kutumia nguvu.
Sambamba na wakuu wa mikoa aliwataka wamachinga pia, kuhakikisha wanawasikiliza viongozi hao na wanafuata sheria na kanuni pale watakapopangiwa maeneo ya kufanyia shughuli zao.
Msingi wa maelekezo hayo ni kuhakikisha mikoa yote nchini inakuwa na mazingira safi.
Utekelezwaji wa maelekezo hayo ulianza mara moja, kwa wakuu wa mikoa na Wilaya mbalimbali nchini kutenga maeneo ya biashara kwa ajili ya machinga.
Kwa upande wa Mkoa wa Dar es Salaam, masoko ya Machinga Complex, Kisutu, Ilala, Kijichi, Kisemvule, Kamchea na Toa Ngoma, yalipangwa kwa ajili ya Machinga.
Masoko mengine yaliyopangwa kutumiwa na wafanyabiashara hayo kwa upande wa Jiji hilo ni Mtambani, Mwenge Cocacola, Kigogo Sambusa, Mawasiliano, Big Brother na Mbezi Shule.
Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya, machinga walipangiwa kwenda kufanya shughuli zao katika soko la Old Airport.
Kama ilivyofanyika katika mikoa hiyo, maeneo mengine ya Tanzania wafanyabiashara hao walipangiwa maeneo rasmi ya kufanya shughuli zao, lakini sasa wameyakacha na hatimaye kurejea barabarani.
Kwanini wanarudi
Mazingira magumu ya biashara katika maeneo ambayo Serikali iliwapeleka ndizo sababu za kurejea kwa Machinga barabarani kama inavyoelezwa na Selina Joram anayefanya biashara zake Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam.
Mazoea nayo ni sababu nyingine iliyotajwa na Haule anayefanya biashara zake katika soko la Kariakoo tangu mwaka 2008, akisema hana mbinu za kupata wateja nje ya soko hilo.
“Haya ni maisha wengine tumeshayozoea na kwa kuwa ndio ajira yetu tunavumilia, mie nipo hapa kitambo najua kuna msimu wanapoa na maisha yanaendelea,” alisema.
Alihusisha kuondoshwa kwao na masuala ya kisiasa, akisema kwa nyakati kama hizi unapoelekea Uchaguzi, hakuna anayewasumbua.
“Mfano sasa hivi kuelekea uchaguzi, hakuna mtu anatushika hapa, wanajua tutakuja kuwaadhibu kwenye kura, ila ukiisha tu watu tujipange kwani kila ikifika kipindi hiki ndivyo inavyokuwaga hivi,” alisema Haule.
Wingi wa machinga barabarani kwa mujibu wa Masi Yussuf anayefanya biashara Kariakoo, unasababishwa na ongezeko la vijana wanaofanya shughuli hizo baada ya kuhitimu ngazi mbalimbali za elimu bila kupata ajira.
“Wapo waliomaliza darasa la saba mwaka jana, kidato cha nne na wale wa kidato cha sita ambao wameshindwa kuendelea na shule kutokana na sababu mbalimbali, hawa tupo nao huku mtaani,” alisema.
Ugumu wa biashara katika maeneo waliyopelekwa uliibuliwa pia na Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Yusufu Namoto aliyesema miundombinu ya maeneo hayo ni changamoto.
Alisema changamoto nyingine ni kubombolewa kwa baadhi ya masoko makubwa na yanapokalmilika wafanyabishara hao wanaachwa kando na kuchukuliwa wengine hali inayosbabisha wakimbilie mtaani.
Mbali ya stendi hiyo, alitaja soko la Mbagala, stendi ya Magufuli na soko la Kariakoo, akisema maeneo rasmi hupewa watu wenye uwezo mkubwa kifedha, huku wenye uwezo wa chini wakibai bila maeneo.
James Samwel anayefanya shughuli za umachinga mkoani Mbeya, alisema mitaji midogo waliyonayo haikidhi kuwaweka katika maeneo rasmi, wanalazimika kuzurura barabarani.
“Tunaamua kurejea mjini kutokana na sehemu tunazopangiwa kutokuwa safi kwa biashara, kule Old Airport hakuna mzunguko wowote wa biashara, tulienda njaa imanusura ituue”
“Kama wapo siliasi serikali kututengea eneo hilo waboreshe mazingira, vyoo hakuna, maji ni shida, barabara ni vumbi kali, hakuna mzunguko wa biashara” alisema Samwel.
Mfanyabiashara mwingine, Hafidh Juma alisema sehemu ya machinga ndio imekuwa kimbilio la wahitimu wa elimu ya vyuo vikuu, vya kati, vidogo na kiwango chochote cha elimu kutokana na ukosefu wa ajira.
“Mimi ni mhitimu wa chuo tangu 2015 fakati ya Afisa Rasilimali watu (HR), nimeomba ajira muda mrefu sipati nimejikusanya nikapata mtaji mdogo naendesha maisha,” alisema Juma.
Kwa upande mwingine mfanyabiashara Bariki John alisema uwapo wa wamachinga katika eneo hilo wamekuwa kero kwani wanaziba maduka yao na wateja wengi huishia eneo la machinga na kuwafanya wao kukosa mapato.
Amesema bado wanaona kuwapo dalili za ‘watu wa juu’ kuwatumia machinga kujinufaisha na kuwafanya wenye maduka wanaolipa pango na kodi serikalini kuingia hasara.
“Sisi waliopanga maduka haswa maeneo ya ndani ya soko tunakosa wateja kwakuwa wengi wanaishia huko nje walipo machinga, nadhani kuwa walio juu wamewapa mitaji kutudumaza,” anasema John.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera alipotafutwa, alisema yuko safarini nchini China.
Akizungumza kwa niaba ya Homera, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa alisema kwa kutambua thamani ya machinga, Serikali mkoani humo ipo hatua za mwisho kukamilisha miundombinu ambayo ilionekana kutokuwa rafiki.
"Kwa maana haitatumika nguvu yoyote bali tutashirikisha mamlaka zote tupitie maeneo yote ikiwamo barabara, maji, vyoo na sehemu zote ili tujiridhishe kwa pamoja waweze kurudi sehemu yao," alisema Malisa.
Naye Ofisa biashara Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Furaha Mkonongo anasema licha ya wamachinga kuwapo wengi eneo la Kabwe, lakini wapo kwenye operesheni maalumu kuwaondoa.
Jijini Mwanza napo wafanyabiashara wamerudi maeneo waliyoondolewa, licha uongozi wa jijini hilo kuanzisha Kikosi kazi maalum kukabiliana na wafanyabiashara hao.
Kikosi kazi hicho kinachoundwa na askari wa Jeshi la Akiba yaani mgambo wenye gari aina ya Toyota Hilux, kwa nyakati tofauti kimeonekana kikipita katikati ya jiji hilo na kukwapua bidhaa za machinga wanaofanya biashara maeneo yaliyokatazwa.
Jiji hilo linakadiriwa kuwa na wamachinga zaidi ya 9,000.
Akizungumza katika mahojiano na Mwananchi, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba amesema uwepo wa wamachinga katikati ya jiji hilo siyo tu unaikosesha Serikali mapato (bila kutaja kiasi) na kuathiri biashara za walipa kodi wenye, pia unachangia uchafuzi wa mazingira ya jiji hilo huku akidokeza kuwa asilimia 25 ta taka zinazokusanywa katikati ya jiji hilo huzalishwa na machinga hao.
"Jiji la Mwanza linazalisha taka zaidi ya tani 350 na asilimia 25 ya taka hizo sawa na tani karibia 90, wakati huo wanaozalisha kiwango hicho cha taka hawalipi ushuru wa taka wala ushuru wa huduma," amesema Kibamba.
Kibamba amewataka machinga jijini humo kutokaidi maelezo aliyotoa ya kuwapeleka kufanya biashara zao kwenye masoko yaliyoelekezwa likiwemo Soko la Mchafukuoga, Buhongwa, Dampo wilayani Nyamagana na Soko la Bango la Zein, Kilimahewa na National (Nyasaka) wilayani Ilemela mkoani humo.
Akizungumza kwenye kikao na Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza Julai 6, 2024, Mkuu wa Mkoa, Said Mtanda amesisitiza kuwa msimamo wa Serikali ni kuona machinga wakifanya biashara katika maeneo yaliyoelekezwa na kuendelea kutekeleza agizo ya Rais Samia Suluhu Hassan la kuwapanga wafanyabiashara hao.
“Tuweke juhudi zetu wakati tunawapanga wa machinga, wakati tunafanya zoezi la wananchi kulipa kodi lakini tufanye pia iende samaba pia na uboreshawaji wa masoko yetu ili tunapogombana na hawa watu wae na maeneo ya kwenda,” amesema Mtanda.
Kauli ya wamachinga
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Muungano wa Wamachinga Mkoa wa Mwanza (MWM), Said Tembo, machinga ni mfanyabiashara anayemfuata mteja hivyo uamuzi wa kuwaondoa katikati ya jiji hilo unaondoa tafsiri ya neno 'Machinga'.
Tembo amesema hata katika masoko walikopelekwa hakuna miundombinu ya kuridhisha na inayoweza kuwafanya wafanyabiashara hao watulie kwa kile alichodai masoko hayo hayana wateja wa kutosha kwa ajili ya bidhaa zao.
"Machinga tunapenda maeneo yenye mikusanyiko ya kutosha ili hata tukiuza bidhaa zetu basi tupate hata fedha ya kuhudumia familia zetu na kulipia kodi ya pango huko tunakoishi sasa ukitupeleka eneo ambalo hakuna wateja lazima turudi tunapoona kuna wateja," amesema Tembo.
Kuhusu masoko yaliyojengwa, Tembo amesema uamuzi huo haukuwa shirikishi badala yake ulifanywa na wataalam wa Jiji hilo ambao walipendekeza machinga kuhamishiwa katika sehemu ambazo hawakuzipendekeza.
Jijini Arusha nako hali ni hiyo hiyo, ambapo sasa wamachinga wameiomba Serikali iwatengenezee mfumo rafiki ili waweze kutumia maeneo rasmi yaliyotengwa na Serikali.
Licha ya uongozi wa Jiji la Arusha kujenga masoko mawili kwa ajili ya wamachinga, wamekacha kuyatumia masoko hayo ambayo yamejengewa miundombinu ikiwemo ya vyoo na maji, huku ikiwa ni hasara kwa serikali.
Maeneo yaliyojengwa ni pamoja na Machame, Ulezi na Olmatejoo, ambayo kwa sasa wafanyabiashara wachache ndiyo wapo, wengiw akiwa wamerudi kandokando ya barabara ikiwemo ya Soko Kuu la Arusha na Kilombero.
Wamachinga waliozungumza na Mwananchi, wamelalamikia mazingira mabovu ya kufanya biashara na kwamba hayana mzunguko wa biashara.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Wilaya ya Arusha, Paulo Sanga, anasema wanaomba Serikali itengeneze mfumo rafiki ikiwemo pale wanapotekeleza mradi ambao unagusa kundi hilo, wawape nafasi ya kutoa Mawazo yao kama walengwa.
“Tunaomba Serikali itutengenezee mfumo rafiki, mfano inapoleta mradi ambao unagusa kundi la machinga watupe nafasi ya kutoa Mawazo sisi kama walengwa, waweke mazingira yanakofikika, kupitia Mawazo yetu wakifanya tafiti wataamua jambo ambalo ni rafiki kwetu sote,” anasema
Arafa Idd, ambaye ni mmachinga nje ya soko kuu la Arusha, anasema eneo la Machame walilopangiwa awali lilikuwa halina wateja hivyo kushindwa kuendelea kufanya biashara na kuamua kurejea barabarani kama ilivyokuwa awali kabla hawajatengewa maeneo.
“Tulikaa kule kwa muda ila tatizo hakuna mzunguko wa wateja, tukajikuta tumetaka tamaa kwani tuna mikopo hivyo kila wiki tunadaiwa marejesho, tunashindwa kukaa mahali ambapo hakuna wateja ndiyo maana nimerudi huku barabarani, na ninauza kweli,” amesema.
Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za jamii jiji la Arusha, Isaya Doita, anakiri wamachinga kuwa mfupa mgumu na kudai miongoni mwa sababu ni pamoja na watendaji waliopendekeza masoko hayo kujengwa katika maeneo ambayo hayana mzunguko wa watu.
“Tukubaliane waliofanya maamuzi ikiwemo sisi madiwani hatukufanya utafiti wa kutosha ila mbaya zaidi machinga hawakushirikishwa ni wapi wao wanadhani wangefanya biashara ili waweze kujipatia kipato chao cha kila siku,” amesema.
Juhudi za kumpata Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda kuzungumzia hatua wanazochukua kudhibiti wamachinga zilikwama kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa na alipofuatwa ofisini kwake hakuwepo.
Hata hivyo, Meya wa Jiji la Arusha, Maxmilian Iranghe, amesema mkakati wa jiji hilo ni kutokuwa na wamachinga katikati ya mji na kuwa kwa sasa wanajenga masoko makubwa ya kisasa kwa ajili ya wamachinga katika maeneo ya Kilombero na Kwa Morombo ambayo yana watu wengi.
Jijini Dodoma, baadhi ya wafanyabiashara wadogo wamekanbusha kukwepa kodi, wakisema pamoja na shughuli hizo, wanalipia ushuru na tozo za Halmashauri ya Jiji kwa mujibu wa sheria.
Wakizungumza na Mwananchi wafanyabiashara hao wamesema awali walikuwa hawatoi tozo wala ushuru wowote kwa sababu walikuwa hawana maeneo rasmi ya kufanyia biashara zao lakini baada ya serikali kuwaweka kwenye maeneo rasmi wanatoa ushuru uliopangwa na Jiji.
Mwenyekiti wa soko la Machinga Complex Jijini Dodoma Athumani Ally amesema siyo kweli kwamba wao wanakwepa kulipa kodi kwani kulingana na aina ya biashara wanazofanya ndani ya soko hilo wanajulikana kuwa ni wafanyabiashara wadogo ambao wanalipa ushuru wa Jiji.
Naye mfanyabiashara mwingine kutoka soko la Sabasaba Privas Kulaya amesema hakuna mmachinga anayekwepa kulipa kodi bali wanalipa ushuru kutokana na ukubwa wa biashara wanazofanya.
“Hivi sasa serikali imeweka utaratibu mzuri wa wamachinga kufanya biashara lengo ni kuwainua na wao wawe wafanyabiashara wakubwa ili waingie kwenye mfumo wa kulipa kodi hivyo si kweli kwamba wanakwepa kulipa kodi kwa sababu hata kipato chao hakitoshi kuingia kwenye walipa kodi wakubwa,” amesema Kulaya.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipoulizwa suala hilo juzi, alisema hawezi kuzungumzia kwa wakati huo kwa kuwa alikuwa uwanja wa ndege akiajiandaa na safari.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amesema jiji hilo limefanikiwa kuwaondoa wamachinga waliokuwa wanafanya biashara zao kwenye maeneo yasiyo rasmi kwa asilimia 95 kwa kuwapeleka kwenye soko la Machinga Complex ambalo limebeba wafanya biashara wadogo takribani 3,500 wa kila aina.
Lakini amesema wamebaki wachache ambao huwa wanarudi kwenye maeneo waliyoondolewa kwa kuvizia lakini huwa wanakabiliana nao kwa kutumia mgambo wa Jiji na kuendelea kutoa elimu zaidi ili waondoke kwenye maeneo hayo na kwenda kwenye maeneo rasmi yaliyotengwa kwa ajili yao.
Pamoja na hatua hiyo, wamachinga wameendelea kurudi kwenye maeneo waliyohamishwa, huku uchafu wa mazingira ukikithiri.
Maeneo ambayo yamekithiri kwa wafanyabiashara hao ni pamoja na Karikaoo, Mbagala Rangi Tatu, GongolaMboto, Mwenge na Mbezi, Kivukoni Kigamboni.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila alipoulizwa Julai 5, 2024, alisema, “suala hilo la wamachinga ndugu mwandishi naomba tuwasiliane baadaye tafadhali."
Julai 4, 2024 alipoulizwa suala hilo alimtaka mwandishi kumtumia ujumbe na hata alipotumiwa, hakujibu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya, amekiri kurejea kwa wafanyabiashara hao na kueleza ni kutakana na ufinyu wa maeneo yanayoendana na mazingira yao ya kufanyia kazi.
"Tunaliona hili la wafanyabiazhara na tayari tumeliwekea mpango ambapo soko la Tandale na lile la Tandika tumeyatengea Sh6 bilioni kila moja kuwatengeneza mazingira mazuri ya kufanyia shughulinzao kazi ambayo itaanza wakato wowote kuanzia sasa,” amesema Mabelya.
Wataalamu
Mtaalamu wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Abel Kinyondo amesema kuwapo kwa mfumo unaobebesha watu mzigo wa kodi, kunasababisha ukwepaji wa kodi.
“Au kuwafanya Kutumia karakana kuuza bidhaa au kupitisha bandari bubu ni mambo ambayo yanasababishwa na baadhi ya watu kutolipa kodi.
“Nikiona kuna mtu anaweza kuleta biashara hiyo hiyo kama yangu akauza bila kodi unaanza kunifundisha wizi ndiyo hapo wengine watauzia dukani na kuuza bei tofauti ya risiti na isiyokuwa ya risiti, unawafanya watu wakosee kwa sababu mfumo wako hauna haki,” amesema.
Amesema ikiwa watu wengi wanalipa kodi inapunguza mzigo wa kodi huku akitolea mfano kuwa kama wanalipa asilimia 18 watu millioni 1 wakiongezeka kuwa milioni 14 kwanini walisilipe asilimia 7.
Kuhusu ukosefu wa ajira, amesema katika tafsiri machinga ni ajira kwa sababu ni amuingizia mtu kipato lakini ikiwa mtu anafanya kazi hiyo kutokana na kukosekana kwa kitu kingine cha kufanya ni tatizo.
“Tujiulize kuwa watu wangapi wakipewa kazi nyingine tofauti na machinga wataendelea na kazi hiyo, Wanaichagua kwa sababu hana njia nyingine ya kujiingizia kipato,” ammesema.
Kwa upande wake mchambuzi wa Uchumi na Biashara, Oscar Mkude amesema kwa kipindi kirefu sasa, ajira katika sekta iliyo rasmi zimekosekana jambo linalofanya Wanao fikia umri wa kuanza kazi.
Amesema vijana wa miaka 21 na kuendelea ni wengi, lakini nafasi za ajira ni chache sana Hivyo wengi wanasubiri kwa muda mrefu kupata ajira rasmi.
Hivyo ukosefu wa ajira rasmi vinahusiana moja kwa moja na arija zisizo rasmi ikiwemo umachinga.
“Machinga ni moja ya njia ya kuishi kwa walio wengi, ni sehemu waliojiegesha ni wakitegemea mambo yatakaa sawa na wataweza kupata kazi au shughuli nyingine za kuwapatia vipato,” amesema Mkude.
Kuhusu kodi, Mkude amesema machinga pia ni namna ya kukwepa ugumu wa kurasimishwa kwa maana ya kuanza kulipa kodi, ushuru na mambo kama hayo.
|
Baada ya kushika kasi bungeni, mjadala wa sukari hatimaye umehamia nje ya muhimili huo, huku Bodi ya
|
Baada ya kushika kasi bungeni, mjadala wa sukari hatimaye umehamia nje ya muhimili huo, huku Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), ikipingana na hoja za Chama cha Wazalishaji wa Sukari Tanzania (TSPA).
Miongoni mwa hoja za wazalishaji zilizopingwa na SBT ni ile inayodai bodi hiyo ilizipa kampuni zilizoitwa za vocha mamlaka ya kuagiza sukari, ilhali hazina vigezo vya kisheria.
Kadhalika, SBT imepinga madai ya kuchelewa kutoa vibali kwa wazalishaji, ikisema iliwapa taarifa mapema, isipokuwa walichelewa kufuata vibali hivyo.
Msingi wa majibu wa bodi hiyo ni hoja zilizoibuliwa Julai 1, 2024 na TSPA kupitia Mwenyekiti wake, Balozi Ammi Mpungwe aliyesema kuchelewa kwao kuingiza sukari nchini, kulisababishwa na SBT kuchelewesha vibali.
Katika maelezo hayo, Balozi Mpungwe alieleza kwa kutambua hali mbaya ya upatikanaji wa sukari, Kampuni ya Kilombero Sugar iliamua kuchepusha meli iliyokuwa na tani 4,500 za sukari kwenda nchi nyingine, iletwe nchini kisha masuala ya vibali yaanze kushughulikiwa.
Kutokana na hoja hizo, Mkurugenzi wa SBT, Profesa Kenneth Bengesi leo, Ijumaa Julai 5, 2024 amewaambia waandishi wa habari kuwa, kilichoelezwa na wazalishaji si sahihi.
Akijibu kuhusu kuchelewa kutoa vibali, amesema Mchi 20, mwaka jana, bodi hiyo iliwaalika wazalishaji kwenda kuchukua vibali vya kuingiza sukari.
Pamoja na mwaliko huo, amesema Kilombero Sugar ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufuata kibali hicho Mchi 30, 2023, huku Kagera Sugar na Mtibwa Sugar zilichukua Aprili 14.
“Kampuni ya TPC ilichukua kibali chake Mei 3, 2023 na Bagamoyo Sugar haikuchua kabisa kibali chake,” amesema.
Pamoja na kampuni hizo nne kuchukua vibali, amesema ni Kilombero pekee ndiye aliyeagiza sukari kwa msimu huo kiasi cha tani 2,380, huku vingine vikiwa havikuagiza.
Kwa mujibu wa Profesa Bengesi, hali hiyo ilisababisha kutokuwa na sukari ya ziada kwenye mzunguko wa soko na hivyo bei ilipanda hadi kufikia wastani wa Sh4,000 kwa kilo Juni mwaka 2023.
Hali hiyo hiyo, kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, ndiyo iliyochangia kuharibu utengemao wa soko la msimu wa mwaka 2023/24.
Kuhusu madai ya Kilombero Sugar kuchepusha meli ya tani 4,500 kabla ya kupewa kibali, Profesa Bengesi alilipinga hilo kwa hoja kuwa, kampuni hiyo ilileta sukari nchini kwa awamu tano na kati ya hizo hakuna ya kiwango hicho.
“Kama Kilombero ilichepusha meli yenye tani 4,500 kwanini sukari ya kilombero iliyoingia ya kwanza ilikuwa ni tani 265 na kwa nini mwezi Januari na Februari kiasi kilichoingia kilikuwa chini ya hizo tani 4,500,” alihoji.
Katika maelezo yake, alionyesha mchanganuo wa sukari iliyoingizwa na kampuni hiyo akisema Januari 29, 2024 iliingiza tani 265, Februari 2 tani 1,272, Februari 9 tani 238.5, Februari 23 tani 662.5 na Februari 27 iliingiza tani 662.5.
Kuhusu kampuni zinazodaiwa za wauza vocha, amesema kila kampuni iliyopewa kibali ilikuwa na leseni halali za biashara ya chakula na hivyo hoja ya jina la kampuni haina msingi na imelenga kuichafua Serikali.
“Kampuni hizo ambazo zimebezwa na zinaitwa kuwa ni za vocha ndizo zilizoingiza sukari na kutuvusha katika kipindi hiki kigumu na sasa sukari kuuzwa kutoka Sh6,500 kwa wastani hadi Sh2,800,” amesema.
Pia, ameeleza changamoto nyingine ni baadhi ya wazalishaji kuwa na wasambazaji wachache wanaotoa ugavi wa sukari katika eneo kubwa hali inayosababisha kuhodhi bidhaa hiyo na kusababisha upungufu kwa baadhi ya maeneo hivyo bei kupanda.
“Suala hili limefanyiwa kazi kwa Serikali kuchukua hatua ya kufanya mabadiliko ya Sheria ya Tasnia ya Sukari kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2024 ili iwatambue na kuwasajili wasambazaji wa sukari nchini na kuongeza uwazi katika mfumo wa usambazaji,” amesema.
Hata hivyo, ameeleza msingi wa mabadiliko ya sheria ya sukari ni kutengeneza mazingira wezeshi kwa wadau wakiwemo wazalishaji, wasambazaji, wakulima na mlaji wa mwisho.
Mabadiliko hayo, amesema yamelenda kubaini gharama halisi za uzalishaji wa sukari nchini na hivyo kuwezesha kujulikana kwa bei ya bidhaa hiyo.
Kadhalika, amesema ni kuweka utaratibu wa upimaji wa ufanisi wa viwanda vya sukari kwa kuzingatia mipango ya maendeleo iliyopo katika sekta ya sukari.
Dhamira nyingine amesema ni kKuhakikisha kunakuwa na uwazi katika mfumo wa usambazaji wa sukari na wakati wowote nchi iwe na hifadhi ya sukari kwa ajili ya dharura.
Lakini dhamira nyingine, amesema ni kuondoa changamoto zilizopo katika uagizaji wa sukari ya kuziba pengo kwa kuiwezesha Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuagiza, kuhifadhi na kusambaza kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa kisheria.
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.